Mbowe: SMG bastola zilitumika Arusha

Mbowe: SMG bastola zilitumika Arusha

[h=2]Monday, June 17, 2013[/h] [h=3][/h]

MWENYEKITI wa CHADEMA Freeman Mbowe, amevituhumu vyombo vya dola kuwa vinawafahamu watu walioshiriki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa chama hicho.


996186_10152909639290247_1473666877_n.jpg

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman

Mbowe, alisema tukio hilo ni la kupangwa na wamegundua risasi za bunduki aina ya SMG na bastola zilitumika mara baada ya mlipuko huo jambo linalozusha hofu na kudidimiza demokrasia ya vyama vingi.BONYEZA KUONA PICHA ZA MATOKEO mkutano wa chadema arusha - Google Search


Wakati Mbowe akitoa tuhuma hizo kwa vyombo vya dola, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema ameunda timu itakayoongozwa na makamishna wawili (Paul Chagonja na Isaya Mungulu), kwenda mkoani Arusha kuongeza nguvu ya uchunguzi.


Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani hapa, Mbowe alisema uchunguzi wa awali walioufanya wamebaini tukio hilo ni la kisiasa na lilipangwa.


Alisema ni vema serikali ikatangaza kuachana na mfumo wa vyama vingi kuliko kuruhusu mauaji na vurugu katika mikutano ya vyama vya upinzani vinavyoonekana kutoa wakati mgumu kwa watawala.


Aliongeza kuwa uchunguzi wa awali katika eneo la tukio umebaini bomu lililolipuliwa ni la kiwandani na si la kutengenezwa.


Alisema katika eneo la tukio maganda ya risasi kutoka katika bunduki ya SMG na bastola yalikutwa hali inayowafanya waamini kuna watu waliamua kufanya tukio hilo kwa kupanga.


Mbowe alisema risasi hizo pia ni miongoni mwa zilizopigwa kwenye tanki la mafuta la gari la matangazo la CHADEMA ambapo zililitoboa.


Alibainisha kuwa inavyoonekana wahusika walitaka kuzalisha mlipuko mwingine mkubwa na kuleta maafa makubwa katika mkutano huo.


“Haihitaji uchunguzi wa kwenda mwezini katika suala hili, ni wazi walipanga kutuua lakini wakaua watu wasiohusika. Waliouawa hawakuwa katika mpango wao na wamekuwa wahanga kwa niaba yetu.


“Hata kama utaamua kumuua Mbowe au (Godbless) Lema, huwezi kuiua CHADEMA kwani chama kitabaki, na wanachama wengine wataendeleza harakati za chama kama kawaida,” alisema.


Wabunge kutohudhuria Bunge


Mbowe alisema kutokana na tukio hilo ambalo limeua watu zaidi ya watatu, CHADEMA imeamua kulifanya ni la kitaifa na wabunge wake watashiriki kwenye maombolezo.


Alisema kuanzia leo wabunge wote wa CHADEMA hawatahudhuria vikao vya Bunge na watajumuika mkoani Arusha hadi misiba yote itakapomalizika.


Alisema wanatarajia kufunga mahema katika eneo la tukio na marehemu wote wataagwa katika eneo hilo ambapo ibada zote za Kiislamu na Kikristu zitafanyikia hapo.


IGP aunda timu


Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwema ameunda timu ya kuongeza nguvu ya uchunguzi itakayoongozwa na makamishna wawili ambao ni Paul Chagonja kutoka idara ya operesheni na Isaya Mngulu kutoka ofisi ya upelelezi makao makuu.


IGP Mwema alisema baada ya tukio hilo, jeshi hilo lilituma makamishna wawili kutoka makao makuu kwa ajili ya kuongeza nguvu ya uchunguzi wa tukio hilo na kwamba wameshaanza kukusanya taarifa mbalimbali zitakazoweza kusaidia kuwabaini watu waliohusika.


Alisema wameunganisha nguvu na vyombo vingine vya ulinzi na watawasaka wahalifu hao pamoja na walio nyuma yao kwa kile alichoeleza tukio hilo linaashiria kushamiri kwa matendo ya kigaidi nchini.


Akizungumzia tuhuma zinazotolewa na wananchi juu ya Jeshi la Polisi kuwajeruhi watu kwa risasi za moto, IGP Mwema alisema kila taarifa inafanyiwa kazi kwa umakini na kwamba baada ya uchunguzi watatoa taarifa kamili kwa umma juu ya kilichotokea jijini Arusha.


Aliwaomba wananchi wenye taarifa za kuweza kumtambua aliyerusha bomu pamoja na watu walio nyuma yake wajitokeze au wamtumie ujumbe kupitia simu yake ya mkononi namba 0754 78 55 57 na kwamba uhusika wao utafanywa kuwa siri.


IGP Mwema pia alisema watachunguza kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bara, Mwigulu Nchemba aliyowaambia wakazi wa Kimandolu kuwa wasipoichagua CCM katika uchaguzi wa madiwani wa Jiji la Arusha ulioahirishwa jana, watakufa.


Mwema alisema watachunguza kauli hiyo baada ya kuulizwa swali la hatua zilichochukuliwa kabla na baada ya mlipuko huo dhidi ya kauli ya Nchemba.


Juzi katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani kwa CHADEMA uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, kitu kinachodhaniwa ni bomu kilipuka na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa. BONYEZA VIDIO swahilivilla: Serikali yasema mlipuko uliotokea Arusha ni bomu la kutupwa kwa mkono


Chanzo: Tanzania Daima
 
Ccm hizi sio zama tena za ubabe na hujuma kwa wananchi, kwa hali hii kifo cha ccm hakiko mbali.
 
MWENYEKITI wa CHADEMA Freeman Mbowe, amevituhumu vyombo vya dola kuwa vinawafahamu watu walioshiriki kwenye mlipuko
wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa chama hicho. Mbowe, alisema tukio hilo ni la kupangwa na
wamegundua risasi za bunduki aina ya SMG na bastola zilitumika mara baada ya mlipuko huo jambo linalozusha hofu na kudidimiza demokrasia ya vyama vingi.

Wakati Mbowe akitoa tuhuma hizo kwa vyombo vya dola, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema ameunda timu itakayoongozwa na makamishna wawili (Paul Chagonja na Isaya Mungulu), kwenda mkoani Arusha kuongeza nguvu ya uchunguzi. Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani hapa, Mbowe alisema uchunguzi wa awali walioufanya wamebaini tukio hilo ni la kisiasa na
lilipangwa. Alisema ni vema serikali ikatangaza kuachana na mfumo wa vyama vingi kuliko kuruhusu mauaji na vurugu katika mikutano ya vyama vya upinzani vinavyoonekana kutoa wakati mgumu kwa watawala.

Aliongeza kuwa uchunguzi wa awali katika eneo la tukio umebaini bomu lililolipuliwa ni la kiwandani na si la kutengenezwa. Alisema katika eneo la tukio maganda ya risasi kutoka katika bunduki ya SMG na bastola yalikutwa hali inayowafanya waamini kuna watu waliamua kufanya tukio hilo kwa kupanga.

Mbowe alisema risasi hizo pia ni miongoni mwa zilizopigwa kwenye tanki la mafuta la gari la matangazo la CHADEMA ambapo zililitoboa. Alibainisha kuwa inavyoonekana wahusika walitaka kuzalisha mlipuko mwingine mkubwa na kuleta maafa makubwa katika mkutano huo. “Haihitaji uchunguzi wa kwenda mwezini katika suala hili, ni wazi walipanga kutuua lakini wakaua watu wasiohusika. Waliouawa hawakuwa katika mpango wao na wamekuwa wahanga kwa niaba yetu.

“Hata kama utaamua kumuua Mbowe au (Godbless) Lema, huwezi kuiua CHADEMA kwani chama kitabaki, na wanachama wengine
wataendeleza harakati za chama kama kawaida,” alisema. Wabunge kutohudhuria Bunge Mbowe alisema kutokana na tukio hilo ambalo limeua watu zaidi ya watatu, CHADEMA imeamua kulifanya ni la kitaifa na wabunge wake watashiriki kwenye maombolezo.

Alisema kuanzia leo wabunge wote wa CHADEMA hawatahudhuria vikao vya Bunge na watajumuika mkoani Arusha hadi misiba yote itakapomalizika. Alisema wanatarajia kufunga mahema katika eneo la tukio na marehemu wote wataagwa katika eneo hilo ambapo ibada zote za Kiislamu na Kikristu zitafanyikia hapo. IGP aunda timu Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwema ameunda timu ya kuongeza nguvu ya uchunguzi itakayoongozwa na makamishna wawili ambao ni Paul Chagonja kutoka idara ya operesheni na Isaya Mngulu kutoka ofisi ya upelelezi makao makuu.

IGP Mwema alisema baada ya tukio hilo, jeshi hilo lilituma makamishna wawili kutoka makao makuu kwa ajili ya kuongeza nguvu ya uchunguzi wa tukio hilo na kwamba wameshaanza kukusanya taarifa mbalimbali zitakazoweza kusaidia kuwabaini watu waliohusika. Alisema wameunganisha nguvu na vyombo vingine vya ulinzi na watawasaka wahalifu hao pamoja na walio nyuma yao kwa kile alichoeleza tukio hilo linaashiria kushamiri kwa matendo ya kigaidi nchini.

Akizungumzia tuhuma zinazotolewa na wananchi juu ya Jeshi la Polisi kuwajeruhi watu kwa risasi za moto, IGP Mwema alisema kila taarifa inafanyiwa kazi kwa umakini na kwamba baada ya uchunguzi watatoa taarifa kamili kwa umma juu ya kilichotokea jijini Arusha. Aliwaomba wananchi wenye taarifa za kuweza kumtambua aliyerusha bomu pamoja na watu walio nyuma yake wajitokeze au wamtumie ujumbe kupitia simu yake ya mkononi namba 0754 78 55 57 na kwamba uhusika wao utafanywa kuwa siri.

IGP Mwema pia alisema watachunguza kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bara, Mwigulu Nchemba liyowaambia wakazi wa Kimandolu kuwa wasipoichagua CCM katika uchaguzi wa madiwani wa Jiji la Arusha ulioahirishwa jana, watakufa. Mwema alisema watachunguza kauli hiyo baada ya kuulizwa swali la hatua zilichochukuliwa kabla na baada ya mlipuko huo dhidi ya kauli ya Nchemba .
Juzi katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani kwa CHADEMA uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, kitu kinachodhaniwa ni bomu kilipuka na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.

Ewe Mwigulu, tazama vilio na damu za watu hawo wanakulilia.Na tazama 2015 sioni wapi utakuwa. Mangula wewe ni Mzee wetu tunakuheshimu wambie vijana kama Mwigulu hao wanao wadhuru ni wa Tanzania wenzake. kwa nini anatoa kauli kama hizo? na siwelewi kwa nini polisi mnamwazha huyu mtu
 
Poleni CHADEMA na WanaArusha naona kuna watu wamepandikizwa kuwafanyia hivi kila mnapokutana ili Wapinzani wenu Kisiasa waweze kuhalalalisha Kauli zao kuwa mikutano ya CDM imejaa Vurugu na watu Wanauwawa. Lakini kama kweli mtu anaamua kuua wasio na hatia kwa ushabiki tu wa Kisiasa Damu ya hao watu ITANENA. Kila mtanzania ana haki na uhuru wa kujiunga na Chama cha Siasa apendacho pasipo tishio la kupotezewa maisha wala kujeruhiwa. Haya matukio hayapendezi na yanavuruga Nchi na kuigawa Vipande Vipande. Kwani CDM kama chama cha Upinzani kikapata Viongozi kwenye kata, mashina na Wilaya kunaharibika nini jamani hadi tufikie hatua hii ya Kurushiana MABOMU NA RISASI? Aibu na walaaniwe wanaofanya vitendo hivi vya Kuua wasio na hatia kwa USHABIKI WA CHUKI WA KISIASA. Ninaomba Mungu awape Subira na Hekima Wana CHADEMA katika kukabiliana na Msiba huu. Pumzika kwa Amani Marehemu wote na Poleni wafiwa.
 
Ukiona mpaka CHAGONJA anapelekwa ujue hakuna kesi. Wanatafuta tu namna ya kumnasua mwana CCM MWENZAO!... Kesi ya mwana-CCM kama NCHEMBA inabaraka za wakubwa zake atalindwa tu kama KAMUHANDA alivyoagiza MWANGOSI AULIWE!...

Kila analolifanya Mwigulu kwa wapinzani kwa manufaa ya CCM lina baraka za Rais Jakaya Mrisho Kikwete! Hiyo siyo siri kwani Kikwete alitamka wazi kuwa Mwigulu ndiye kiboko ya CHADEMA.
 
Broda,
Uko sahihi sana mkuu, na umetuliza kichwa.

Kimsingi ilibidi mhimili wa Bunge ambao ni mhimili ma wananchi utambue hilo na walipaswa kuahirisha shughuli zote za leo ili kuungana na Watanzania kuomboleza.

Mkuu,hawawezi kufanya hivyo kwani wao ndo walipanga na kutekeleza walipo wanashangilia kimya kimya,Mkuu wa Nchi nae anakula Bata nchi za nje, angekuwa amekufa Msanii ungesikia Salamu za Lambilambi siku hiyohiyo kutoka kwa Rais
 
wanachunguza.... hii ndio polisi jamii sio... mwema jibu haya
1. yuko wapi alimuua padre kule zenji???
2. yuko wapi aliemchinja padre kule sengerema???
3. yuko wapi aliemtesa dokta ulimboka???
4. yuko wapi aliyemuua mwandishi mwangosi kule iringa???
5. yuko wapi aliyemtesa abslom kibanda???
6. yuko wapi aliyesupply bomu na kuplan issue nzima ya bomu lililorushwa kanisani arusha????
7. yuko wapi aliyechoma makanisa zenji???
8. yuko wapi aliyemwagia tindikali saeed kubenea???
9. yuko wapi aliyempiga rungu mbunge wa arumeru aliyepigwa rungu jana makuyun wakat anasimamia uchaguzi???

hii ndo technic ya polisi kila siku ili kufanya danganya toto???? nadhan kikijitokeza kikundi cha kuingia msitun kitapata wafuasi wengi sana.... so much injustice!!!

Wako wapi waliowateka na kuwatesa Wabunge Ilemela na Ukerewe (Kiwia na Machemli)? Leo bila aibu Kikwete na Membe anapata wapi jeuri ya kumwambia Kagame apatane na waasi? Nashukuru wanyarwanda walimweleza JK kuwa hana jeuri ya kuwaambia hayo wakati nyumba yake mwenyewe imemshinda!!!!
 
huyu siasa zimemshinda, bora arudi kwenye kazi ya udj, wewe kama kiongozi wa chama unakuja ya hadithi kama hizi? Hizo risasi na bomu vyote visimpate yeye na lema? Labda hiyo smg alipewa kipofu.

Si alipewa mama yako, au umesahau??
 
wadau namba ya simu ya IGP SAID MWEMA naiweka vizuri muione ni hii: 0754 78 55 57
kwa wanaowajua wahusika wajaribu kumtumia IGP message, kisha tuone ujasiri wa polisi wa kuwashughulikia wahusika wa unyama huu.

Hakuna cha kumtafuta mchawi, mtuhumiwa namba moja ni Mwigulu Nchemba, huyu kijana hana hata adabu kwa Watanzania. Mwigulu Nchemba ndio anayetakiwa awekwe ndani na kama Mwema akishindwa basi Mwigulu Nchemba asubirie hukumu yake pindi nchi itakapokuwa chini ya Wananchi ndipo atakapo lipa dhambi zote alizozifanya za kuua, utekaji na kumwagia tindikali.

Mwigulu Nchemba kaa ukaavyo lakini jua una damu za Watanzania mikononi mwako na ipo siku utazilipa kwa gharama utakayokuja kuijutia

Huyu Mwema naye aache usani wake, anatumika na inawezekana alikuwa anajua kitakachotokea

Mtuhumiwa yupo na ni Mwigulu Nchemba sio mwengine na huyu Mwigulu Nchemba ndio atakayetaja genge lake la kigaidi

 
Hakuna cha kumtafuta mchawi, mtuhumiwa namba moja ni Mwigulu Nchemba, huyu kijana hana hata adabu kwa Watanzania. Mwigulu Nchemba ndio anayetakiwa awekwe ndani na kama Mwema akishindwa basi Mwigulu Nchemba asubirie hukumu yake pindi nchi itakapokuwa chini ya Wananchi ndipo atakapo lipa dhambi zote alizozifanya za kuua, utekaji na kumwagia tindikali.

Mwigulu Nchemba kaa ukaavyo lakini jua una damu za Watanzania mikononi mwako na ipo siku utazilipa kwa gharama utakayokuja kuijutia

Huyu Mwema naye aache usani wake, anatumika na inawezekana alikuwa anajua kitakachotokea

Mtuhumiwa yupo na ni Mwigulu Nchemba sio mwengine na huyu Mwigulu Nchemba ndio atakayetaja genge lake la kigaidi


ni kweli kabisa, kwasababu alishatajwa kumtumia pesa kwa njia ya M PESA Ludovick Rwezahura.
 
mbowe anachezea akili za watu amekosa huruma kwa watu kwa kupanga na kutekeleza uharifu.
 
uyo mwigulu anarigharimu sana taifa hili na sijui kuna kitu gani kipo nyuma yake kimlindacho mana uchochezi kaanza muda mrefu ila wanamwangalia ila mwisho wa ubaya ni aibu! poleni wanaarusha
 
kukososlewa unakokuongelea sijajua ni kupi...
walikosolewa sana na NCCR MAGEUZI chini ya mrema, wamekosolea sana na CUF chini ya lipumba na bado huu ujinga tunaoushuhudia leo KUANZIA BUNGENI HADI MTAANI HAUKUPATA KUTOKEA..
Ujinga huu ni swala jipya kabisa ambalo limekuja na CHADEMA kuwa upinzani rasmi.
na kuhusu mauaji!!!!! hutaniondoa katika imani yangu kuwa CDM is behind every blood drop. hizi humu ni tuhuma na uzushi tu toka kwa wachambuzi uchwara wanaoshabikiwa na watu wenye akili fupi kama maisha ya funza.
baada ya dhana dhaifu ya ufisadi kuota kutu sasa mmeamua mauaji ya watu iwe ndio kamba ya kuwaokoa. ni nani asiyejua kuwa mauaji yoyote yakitokea hapa nchini ni rahisi lawama kupelekwa kwa CCM na serikali yake!!!!!!!! hivyo basi yeyote mwenye kutaka kuichonganisha serikali na wananchi wake atajaribu kupanga mauaji ya watu ili mwishowe aipe lawama serikali. TAFAKARIII
Ndugu notradamme,ufisadi bado unapigiwa kelele.Wanyama wetu wanasafirishwa hai kwa ndege kwenda ughaibuni mf twiga!tembo wanakwisha,mikataba ya siri raslimali zetu mf gesi,fedha chafu nje ya nchi nk.Mchezo wa Arusha ni kama waliofanyiwa NCCR. Unakumbuka NCCR 1995(sijui umri wako),CCM ilipokabwa koo majimbo ya Dar,NEC wakaahirisha uchaguzi wa Dar,kisa karatasi za kura hazijafika!!Yaliyofuata baadaye ni historia.Tar 30/6/2013 tutakuwa tunajiandaa kupokea ugeni mkubwa,USA President,B Obama.Uwezekano wa uchaguzi ni mdogo, kisa Umeya wa jiji la Arusha.
CUF walizushiwa sana ugaidi.IGP(Ret) O.Mahita,alikwenda kwenye media akiwa na visu vyenye mipini rangi ya bendera ya CUF,eti kuna kontena zima la vile visu vya CUF.Hadi leo hatujui viko wapi.
Hayo mauaji na mateso ambayo vyama vya siasa/ Chadema wanahusika ni yapi?Nani alimwua D Mwangosi?Padre Zenji aliuawa na nani?Aliyemjeruhi kwa risasi padre Zenji ni nani?Nani alimteka na kumtesa Dr Ulimboka, Kibanda?Nani aliyemwagia tindikali katibu wa Mufti Zenji, Said Kubenea?
 
Tuhuma hizi zinanifanya niamini usemi usemao KIKULACHO KI-NGUONI MWAKO. Ikiwa itathibitika kuwa mauaji haya yametokana na chuki za kisiasa kama alivyonukuliwa Mwigulu Nchemba akitoa kauli hatari inayotishia demokrasia na uhai wa raia wema, na kama kuna wanasiasa watakaobainika kuhusika kwa namna moja au nyingine wachukuliwe hatua kali ikiwa ni pamoja na kuondolewa nyadhifa zao na kutoruhusiwa kuendesha shughuli zozote za kisiasa nchini. Kwa kawaida polisi hukamata kwanza na baadaye uchunguzi unafuata. Kwa nini asikamatwe awekwe rumande wakati uchunguzi ukiendelea? Haya, na mimi yangu macho na masikio, zaidi ya hapo namwomba Mwenyezi Mungu atufunulie yote na kuilinda nchi yetu dhidi ya watu wasiyoitakia mema Tanzania.:embarassed2:
 
Ndugu notradamme,ufisadi bado unapigiwa kelele.Wanyama wetu wanasafirishwa hai kwa ndege kwenda ughaibuni mf twiga!tembo wanakwisha,mikataba ya siri raslimali zetu mf gesi,fedha chafu nje ya nchi nk.Mchezo wa Arusha ni kama waliofanyiwa NCCR. Unakumbuka NCCR 1995(sijui umri wako),CCM ilipokabwa koo majimbo ya Dar,NEC wakaahirisha uchaguzi wa Dar,kisa karatasi za kura hazijafika!!Yaliyofuata baadaye ni historia.Tar 30/6/2013 tutakuwa tunajiandaa kupokea ugeni mkubwa,USA President,B Obama.Uwezekano wa uchaguzi ni mdogo, kisa Umeya wa jiji la Arusha.
CUF walizushiwa sana ugaidi.IGP(Ret) O.Mahita,alikwenda kwenye media akiwa na visu vyenye mipini rangi ya bendera ya CUF,eti kuna kontena zima la vile visu vya CUF.Hadi leo hatujui viko wapi.
Hayo mauaji na mateso ambayo vyama vya siasa/ Chadema wanahusika ni yapi?Nani alimwua D Mwangosi?Padre Zenji aliuawa na nani?Aliyemjeruhi kwa risasi padre Zenji ni nani?Nani alimteka na kumtesa Dr Ulimboka, Kibanda?Nani aliyemwagia tindikali katibu wa Mufti Zenji, Said Kubenea?

Hivi huyo sijui nota-demu atakuelewa kweli kwa vile naona kichwa chake kimejaa FUNZA!!
 
Chagonja na Mngulu walisema watatoa ripoti ya kuvamiwa kwa Absalom Kibanda kabla ya 17.04.2013 lakini mpaka leo hakuna taarifa zozote mpaka sasa.Tusitegemee uchunguzi wowote wa maana!
 
Hatuna imani na jeshi la polisi tena waendelee tu kuua.Sisi tunaongozwa na Mungu lazima mtaondoka madarakani nguvu ya umma inajipanga .Na nchi itarudi kwa wananchi sio wezi wachache ccm.mungu tuongeze nguvu.hatuogopi risasi wala bomu tena tafuteni kingine.
 
kukososlewa unakokuongelea sijajua ni kupi...
walikosolewa sana na NCCR MAGEUZI chini ya mrema, wamekosolea sana na CUF chini ya lipumba na bado huu ujinga tunaoushuhudia leo KUANZIA BUNGENI HADI MTAANI HAUKUPATA KUTOKEA..
Ujinga huu ni swala jipya kabisa ambalo limekuja na CHADEMA kuwa upinzani rasmi.
na kuhusu mauaji!!!!! hutaniondoa katika imani yangu kuwa CDM is behind every blood drop. hizi humu ni tuhuma na uzushi tu toka kwa wachambuzi uchwara wanaoshabikiwa na watu wenye akili fupi kama maisha ya funza.
baada ya dhana dhaifu ya ufisadi kuota kutu sasa mmeamua mauaji ya watu iwe ndio kamba ya kuwaokoa. ni nani asiyejua kuwa mauaji yoyote yakitokea hapa nchini ni rahisi lawama kupelekwa kwa CCM na serikali yake!!!!!!!! hivyo basi yeyote mwenye kutaka kuichonganisha serikali na wananchi wake atajaribu kupanga mauaji ya watu ili mwishowe aipe lawama serikali. TAFAKARIII

Hii ni theory mojawapo inayoweza kukokotoa kile kinachojiri ila haimaanishi wazo lingine kwamba CCM wanahusika halina uzito. CCM na CDM ni vyama vyenye haki sawa kisheria ila kimoja kipo madarakani kingine ni cha upinzani. Mimi binafsi sipendezwi na mauaji yoyte yanayotokea dhidi ya mtanzania yeyote awa mwana CCM au mwana chadema. Pili ni wajibu wa chama tawala na serikali yake kulinda raia wote bila kujali ni wana ccm au la, hivyo yeyote anayetoa kejeli kuhusiana na kilichotokea arusha ni mwendawazimu. Tatu huwa tunakimbilia kufanya makosa ya jinai kuwa ya kisiasa. Yeyote anayetenda haya ametenda jinai na anasitahili kuchukuliwa hatua za kisheria bila kujali tukio ni la kisiasa au laa. Serikali yetu imekuwa ni ya kulalamika na imejisahau kuwa yenyewe ndio yenye mamlaka na viongozi wakuu wamekuwa wepesi kupiga siasa hata kwenye matukio makubwa ya makosa ya jina kama haya. Haya mambo ni ya kuyathimini kwa umakini na kuchukua hatua stahiki.
 
Back
Top Bottom