Mbowe sasa avuka mipaka, afanya matumizi ya gari la serikali kwa shughuli za CHADEMA

Hawa CHADEMA hawapaswi hata kufananishwa na UVCCM, maana UVCCM ina ofisi zake yenyewe na pia ina miradi yake ya kuweza kuendesha jumuiya hiyo (ukiachana na michango ya uanachama), lakini CHADEMA kwanza jengo mpaka leo wamepanga (ni nyumba ya shemeji yake Mbowe hivyo unajua kwanini hataki kutoka) lakini pili chama hakina miradi halali, mradi wa CDM ndio huo M4C wanaufanya kwa siri nzito.

Obsessional and autism dissorders on track
 
Bodyguard wa rais analipwa na nani? Mbona hadi kwenye vikao vya 'mashetani' wa kijani yumo? Vikao vya 'kishetani' vya CCM kufanyika ikulu vipi? Polisisiemu na agenda yao ya kuwa tawi la CCM vipi? Stop uttering nonsense out of ignorance
 
HAMY- D. Mtu akisoma hoja yako pembeni ya msitari anaweza kudhani wewe ni mzalendo;lakini ukweli ni kwamba wewe sio mzalendo ila ni M-CCM. Mambo yako wazi yakionyesha Viongozi wa CCM Wanatumia Polisi wa Serikali, Jeshi la Serikali[JWTZ] ukiachilia mbali idadi kubwa ya magari na ndege za serikali kila siku kwa shughuli za chama chao.

Hebu ona hii, tarehe 20,jan 2013 Magari yafuatayo yalikuwa katika msafara wa Makamu mwenyekiti wa CCM Taifa [Bw Philip Mangula] na baadae kwenye mkutano wa hadhara uwanja wa Nyamagana, Mwanza:-
STK 3643, STJ 9522,STK 3831, STK 3791, NW UJ, RC MWANZA,SM 4416, STJ 2901. Hili ni kwa Mwanza Mjini Peke yake. Sasa kabla ya kututaka tujadili hoja ya Mbowe hebu tuongoze kujadili matumizi ya CCM na CUF halafu tutamalizia kwa Mbowe na kutoa azimio.
 
Hivi ni lazima mimi ndio niseme ya Kikwete? wewe kama una ushahidi na hayo uliyo yasema na umeona kuna haja ya kuyawasilisha hapa jamvini, basi jenga hoja yako na uilete hapa.

Si jukumu lako ILA hujawahi kutuambia uhuru wako wa kuyaona na hayo ulinyanganywa na nani?!
Kuna uwezekano wa fikra zanazoelekea sehemu moja?
Tatizo lako ni kulazimisha fikrazo kuwa na mapengo!
Said Mwema ni IGP na ni shemeji ya mwenyekiti wako, ni sifa ipi ilimpa cheo cha IGP?
Ni wapi utaweka mipaka kwa mwenyekiti wa CCM mkoa kutaka taaarifa ya utekelezaji wa ilani kutoka kwa watumishi wa umma wakati serikali ipo?
Ni mipaka ipi tuiweke kuhakikisha kwamba Rais wa nchi haendi na BODYGUARD tunayemlipa kwa kodi yetu kwenye mikutano ya chama?Kwa hiyo umejilazimisha kuamini kwamba CCM ndo ina viongozi wenye uzoefu?
Akina Sitta au Mwakyembe na MALIPO ya DOWANS...
Tehe!
Majembe yenu hayo...!
 
chadema kimejaa viongozi limbukeni yasiyojua hata maana ya uongozi uongozi katibu mkuu anazoazoa wanawake tu mbowe kazi kuuwa watu tu na ujambazi.
Kama yote uyasemayo ni makosa ILA serikali haijayapa uzito, huoni unamdhalilisha mwenyekiti wako kwamba hana uwezo wa kushughulikia uhalifu?
Kumbe na wewe unaona kwamba serikali chini ya chamam chenu inanyamazia uhalifu?
Hilo halijaanza leo ndg!
Hata wauza dawa za kulevya walipewa muda kujirekebisha......
 
We jamaa kila nikiangalia uzi wako lazima uongelee CDM au Mbowe.
We gamba au? Daaaah.....
 
HAMY-D

Poor minded,wewe kila kukicha una muwaza Mbowe na CHADEMA,asubuhi chadema,mchana chadema,usiku chadema,Mawazo yako ni chadema,chadema,chadema,chadema,na wakati chama chetu kina poromoka,unadhani watu waliopo Jf wana ufinyu wa mawazo kama unavyodhani wewe? Unadhani hawajui kufanya judgement kati ya viongozi wa chama chetu na chadema ni wepi wana fuja mali za serikali?
 
Hawa CHADEMA hawapaswi hata kufananishwa na UVCCM, maana UVCCM ina ofisi zake yenyewe na pia ina miradi yake ya kuweza kuendesha jumuiya hiyo (ukiachana na michango ya uanachama), lakini CHADEMA kwanza jengo mpaka leo wamepanga (ni nyumba ya shemeji yake Mbowe hivyo unajua kwanini hataki kutoka) lakini pili chama hakina miradi halali, mradi wa CDM ndio huo M4C wanaufanya kwa siri nzito.

Na ulivyo hamnazo unajifanya kuikejeli CDM wakati kila dakika ndicho unachowaza?
 
HAMY-D
Kaka punguza mapenzi yaliyopitiliza kujificha nyuma ya uzalendo. Mbowe atakuwa na makosa kwa kutumia rasilimali za umma katika shughuli za chama ama binafsi lakini sijawahi kuona habari yako humu jamvini ikimkemea Kikwete, Salma Kikwete, Mawaziri, MaRCs na MaDCs kutumia magari ya serikali katika shughuli za CCM. Kumbuka hata kipindi cha kampeini za chaguzi mbali mbali mawaziri wamekuwa wakitumia rasilimali za umma ktk shughuli za chama. Mfano hai ni Steven Wasira na Magufuli IGUNGA na ARUMERU MASHARIKI. Try to reduce subjectivity in your arguments
 
Last edited by a moderator:
Ukiambiwa utoe ushahidi wa haya unaweza?Kwanini unapenda kufanya hisia na wamiliki wa JF?Unatokea upande wa Wilson Mkama au Nape?

Niko tayari kuweka ushahidi wa maneno na massage ninazopokea toka kwa Admns ikitokea mchango wako uko kinyume na Pro -CDM's.
Viongozi wa Serikali naCCM wanatukanwa na hata kufananishwa na wanyama, lakini ukimgusa kiongozi wa cdm utaishiwa kupata onyo,matusi na ban.
NB. nimepokea onyo hilo hivi majuzi.
 
Pia familia ya panya iko ccm kuanzia babu hadi kilembwe wote ni wezi, hii ndio sifa ya kupata uongozi ccm

unavyotafuta viongozi wa hovyo hovyo huna haja ya kubabaika sana, just move on to CCM you will find alot there.
 
mbona mashangingi ya mawaziri na wakurugenzi yanashinda huko mvuti na maeneo mengine kwenye mashamba ya wakubwa lakini huoni kama ni matumizi mabaya ya mali zetu. hasa siku za week end
:)
 
Gari alilopewa mbowe ni la kuendea bungeni tu na akialikwa ikulu? Hata ufafanue vp mi sitakuelewa, mawaziri wanakaz,wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenz wanazo kazi za kufanya kwa serikal je mbowe anakaz ipi ndan ya serikal ya ccm? Kuwa kiongoz wa upinzan unapewa jukumu gan la kufanya kwa gari analopewa? Kama mama salma alitumia helkopta ya polis hamkusema leo sijui utaelewekaje.
 
HAMY-D bwana kwel ww ni wa kuhurumiwa.
Hiv uliwaza kwanza kabla ya kuja na hii habar yako?
Kwel kuwa ccm inabid uwe na akil za mait.
 
Unasema rasilimali za taifa ni gari 1 la mbowe???...... umefirisika kwenye hoja. Kwamba hujui Tanzanite ni mali ya south Africa, migodi yetu, wanyama wetu, dowans, epa, makampuni ya simu kulipa 1m $ pekee.......hizi ndo baadhi ya rasilimali zetu zilizo liwa na maficcm. Usisahau Bil 300 za uswis.....meremeta....
 
HAMY-D

Mkuu ni kweli kutumia mali za uma kwa shughuli zako binafsi ni kosa. Kama wote tukielewa hivi na kuheshimu basi kweli tutakuwa tunatimiza haki na wajibu wa utawala wa sheria.

Lakini cha kustaajabisha hapa ni kwa nini tuangalie kosa likifanywa na upinzani ndio linakuwa kosa lakini likitendwa na chama tawala linajengewa hoja lionekane sio kosa? Kufanya hivi ni kuonyesha udhaifu mkubwa sana kwani ni vyema tukaona na kulikemea jambo baya kwa mtazamo mmoja tu bila kujali upande upi umefanya.

Natumaini kama mh Mbowe ni kiongozi makini basi ataliona hili na kulifanyia kazi. Na je vipi kwa hawa wa chama tawala, je wataona hayo makosa na kujirekebisha?

Mwisho namalizia kuwa kama kweli tunahitaji mabadiliko ya kweli basi tuweke unafiki na ushabiki wa kiitikadi pembeni ili tuijenge nchi yetu. Hapa umetoa hoja nzuri sana lakini unashindwa kueleweka kwa kuwa mara nyingi unatoa hoja zako kwa unafiki na ushabiki wa kiitikadi. Binafsi mimi ni mwanachama halali na hai wa chama cha mapinduzi lakini huwa nashangaa sana badala ya kukisaidia chama che kwa kukosoa yale mabaya eti ndio kwanza tunashabikia ujinga. Hivyo ni kukiua chama na kuvipa nguvu na kuviaminisha vyama vya upinzani kwa wananchi.

Mkuu badilika tujenge chama chetu kwani mtanzania wa sasa si yule wa karne zile za kutishwa na propaganda za kisiasa. Tukemee panapohitaji kukemewa na pia tutetee panapohitaji kutetea. Hii nchi ni yetu sote hivyo jukumu la kuijenga ni letu sote. Tukosoane na kusahihishana kwa hoja zenye mashiko na wala sio ushabiki wa kiitikadi ambao hauna faida kwa nchi yetu.
 
Last edited by a moderator:
Mbona mwenyekiti wenu anatumia ikulu kufanya mikutano ya chama chenu mbona kuna waziri anatumia gari la serikali kupeleka maji kwa hawara yake kinondoni!!!acha ubwege wewe hamy d sijui hamu D
 
Back
Top Bottom