Mbowe: Nipo tayari kuondoka CHADEMA...

Mbowe: Nipo tayari kuondoka CHADEMA...

Kwani CDM ni Baba yake au Mama yake? Sioni cha ajabu katika kauli hii.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema nipo tayari kuondoka CHADEMA ikiwa wanainchi hawatapata haki zao.

Source: Gazeti la Majira.

Kwa hakika hii ni kauli njema sana kwa kuwa hivi sasa CHADEMA inaonekaana dhahiri kujiridhisha mifumo na taratiz za CCM kwa mfano viongozi wa kuu wa Chama kuwa viongozi wa kuu wa Serikali. Hivi sasa Mbowe ni Mwenyekiti wa Chama na pia ndio Kiongozi wa Kambi Rasim ya Upinzani bungeni (kwa upinzani nafasi hii ni sawa na urais) Kwa maneo mengine Mbowe anaongoza Serikali ya Upinzani na pia anaongoza vikoa vya chama vinavyopaswa kufanya tathmini ya utendaji wake. Hapa hakuna "Checks and Balances" za kutosha na ndio maana katika siku za karibuni CHADEMA imeanza kudorora.

Kwa maoni yangu Mbowe anapaswa kuchagua nafasi moja katia ya Uenyekiti wa Chama na Uongozi wa Kamabi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Hii pia ni kwa wabunge wote wa CHADEMA kuachaia nafasi zote ndani ya chama ikiwemo Kamati Kuu na na Halmashauri Kuu ili wakawatumikie wapiga kura wao la sivyo CHADEMA ijitayarishe kupoteza majimbo mengi 2015. Ikiwa wabunge wa CHADEMA akina Zitto, Mnyika na wengineo wenye nyadhifa ndani ya chama watashindwa kuziachia ili vijana wengiwe waweze kuchomoza na kujulikaan kwa wapiga kura mapema kama ilivyokuwa kwa wao watatuthibitishia kuwa wan tamaa ya madaraka kama wenzao wa CCM.
 
"Chadema si Baba yangu wala si Mama yangu! Hata tukipata ridhaa ya kuongoza nchi hii lakini nikaona mambo yanaenda kinyume na matarajio ya Watanzania nitaondoka" - Mhe.Freeman Mbowe (Hotuba yake kwa watanzania waishio Washington DC)

Acheni kupotosha!
Kauli kama hii iliwahi kusemwa na Hayati Mwl. Nyerere kuwa "CCM si baba yangu wala Mama Yangu,.........."
 
Mkuu habari si mbaya ila Kichwa cha Habari hakishabihiani na habari!

Naona Richard Nyaulawa aliondoka na Majira!

Kimbunga,
Ni kweli.Ila mkuu umepotea sana.Imekua zamu yako sasa kupotea
 
Hakika kati ya viongozi ninao wa heshimu ndani ya chadema huyu mkuu anaongoza.Ila yule anayedondokaga bafuni namchukia bora angevunjika mkono kabisa
 
Kauli tata

Haina utata wowote, wenye utata ni ubongo wa aliyeileta hapa jamvini.

Hivi unaamini Majira wanaweza kuandika sentensi moja kama hiyo aliyoandika huyo Katibu wa Chuki Ugomvi na Fujo (CUF) wa hapa JF?

Mh.Mbowe alisema kama CDM itaja kuwa kandamizi kwa haki za wananchi kama ilivyo CCM basi yeye ataihama. Ni sawa na ile ya Baba wa Taifa kuwa CCM sio baba wala mama yake, anaweza kuhama.

Ukitaka kuona kauli tata zama hapa
 
Huo ndio uthubutu wa kisiasa unavyotakiwa, kwani mtu unaweza kujipima mwenyewe na ukaona kuwa hapa ngoja nipumzike ili tupate changamoto mpya! Japo si wakati muafa kwa sasa ila, kung'atuka ni utamaduni alituanzishia Mwalimu Nyerere. Mbona mpinzani wa Uganda naye ametangaza kung'atuka, ajabu iko wapo?
Poa Kamanda, ila kwa sasa bado tunakuhitaji.
 
josephine mushumbushi na slaa wanataka kufanya chama kama kampuni yao hili haliwezekani kabisa.
 
Kwani ajabu akisema hivyo, maneno kama hayo hayawezi tamkwa na wenyeviti wa ccm na CUF kwa sababu hawajiamini na wakitamka tu ndo ntolee kwa sababu wamechokwa

Siyo mara ya kwanza mbowe kusema hivyo, huwa anasema hiyo kauli mara kwa mara, msisitizo huwa uko kwenye misingi ambayo CHADEMA inaisimamia, siku CHADEMA ikiacha misingi yake yuko tayari kuondoka CHADEMA kuliko kuendelea kuwa kwenye chama ambacho kimepotoka na kuancha misingi yake! Hii ndo maana na background ya hiyo sentence.
 
Hii ni kauli inayoonyesha commitment ya kiongozi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Yupo kwa ajili ya wananchi na si chama pekeyake.
 
Safi sana BADO MMOJA.W.slaa..hatuwezi ongozwa na mtu mwenye degree za gospel.
 
Kwa hakika hii ni kauli njema sana kwa kuwa hivi sasa CHADEMA inaonekaana dhahiri kujiridhisha mifumo na taratiz za CCM kwa mfano viongozi wa kuu wa Chama kuwa viongozi wa kuu wa Serikali. Hivi sasa Mbowe ni Mwenyekiti wa Chama na pia ndio Kiongozi wa Kambi Rasim ya Upinzani bungeni (kwa upinzani nafasi hii ni sawa na urais) Kwa maneo mengine Mbowe anaongoza Serikali ya Upinzani na pia anaongoza vikoa vya chama vinavyopaswa kufanya tathmini ya utendaji wake. Hapa hakuna "Checks and Balances" za kutosha na ndio maana katika siku za karibuni CHADEMA imeanza kudorora.

Kwa maoni yangu Mbowe anapaswa kuchagua nafasi moja katia ya Uenyekiti wa Chama na Uongozi wa Kamabi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Hii pia ni kwa wabunge wote wa CHADEMA kuachaia nafasi zote ndani ya chama ikiwemo Kamati Kuu na na Halmashauri Kuu ili wakawatumikie wapiga kura wao la sivyo CHADEMA ijitayarishe kupoteza majimbo mengi 2015. Ikiwa wabunge wa CHADEMA akina Zitto, Mnyika na wengineo wenye nyadhifa ndani ya chama watashindwa kuziachia ili vijana wengiwe waweze kuchomoza na kujulikaan kwa wapiga kura mapema kama ilivyokuwa kwa wao watatuthibitishia kuwa wan tamaa ya madaraka kama wenzao wa CCM.

Humtendei haki Mbowe hata kidogo.Mbowe ni kiongozi ambaye amesababisha CDM iwe kama ilivyo.Ni mawazo hasi sana kusema Mbowe aachie chama wengine.
 
Back
Top Bottom