Mbowe na Zitto Kabwe wapimwe kwa hoja zao

Mbowe na Zitto Kabwe wapimwe kwa hoja zao

Tanzania sasa imechupa mbali na inazidi kupokea mabadiliko makubwa sana haswa ya kifikra. Kilasiku tunaona mikutano ya hadhara ya wanasiasa ikifanyika kuna inayotia moyo kwa wanasiasa wanaotumia muda wao kuandaa hoja za msingi na kuongelea mambo yanayowagusa wananchi moja kwa moja, wapo wengine wanaoandaa viloja vya kwenda kutajataja majina ya watu na pumba ambazo hazina mantiki yeyote kwa wananchi. Na hii ni dharau kubwa sana kwa wananchi kuwapotezea muda wao kuja kwenye mikutanoa na hakuna wanachokipata.

Hapa nasema lazima tuwapime wanasiasa wetu kwa hoja wanazoongea je kile anachokiongea kina tija kwa wananchi, pia wanasiasa wetu lazima wabadilike zile siasa za viloja mwisho ilikuwa 2010.Watanzania wa leo hawatakubali kuuziwa Mbuzi kwenye gunia watataka kumuona anafananaje na ana ubora gani.

Wachambuzi wa masuala ya siasa tusaidieni watanzania muwe mnajitahidi kuchambua yale ambayo yamezungumzwa na wanasiasa hao katika majukwaa yao, waanikieni viloja na hoja za wanasiasa wetu. Rai kwa wanachama na washabiki tuanze sasa kutoka vifua mbele kwa hoja anazozitoa mwanasiasa tunayempenda tusiangalie tu ujazaji watu tu jukwaani hii nchi imevimba changamoto ni nyingi sana.

Wakati huu ni kuwapima wanasiasa hawa wawili kwa hoja zao wakiwepo kwenye mikutano na nje ya mikutano.

Dr. Maji marefu umeharisha hapa.....
 
Ombs radhi mkuu umma wa wananchi wanyonge kwa kufanya comparison ya makosa kati ya mpigania uhuru na huyo msaliti.
 
Zitto alisaliti kitu gani? Mbowe alimsaliti mke wake kwa kuzaa nje ya ndoa.
Wewe ni Dr. Aina ya wale walionyang'anywa leseni za uganga na serikali au, maana hoja zako ni kama prof.Maji Marefu.
 
Ondoa huu uchafu bro . You cannot even leave some space kweli unataka tusome nini ? Shule za Lowasa hizi na madhara yake ya kusomea chini na majumba hayana madirisha

Uchafu huondolewa kwa usafi unaonaje ukiweka usafi kwa kujibu hoja hizi ili na wengine wawe makamanda?
 
Tatizo kubwa la Zitto ni usaliti Kwa watanzania, chama chake cha zamani, nafsi yake na wafuasi wake. Zitto was mwaka 2007 na Zitto wa Leo 2015 ni watu wawili tofauti ijapokuwa wanatumia sura ileile ya 2007.
Kimsingi, Leo Zitto anawafuasi wengi wa CCM kuliko chama kingine chochote cha siasa.Hii ni kutokana Zitto kutenda mapenzi ya CCM kuliko watanzania. Wao CCM wanatumia kichwa na Sura ya Zitto kufanikisha malengo yao.

Ndiyo maana,Zitto akiambiwa yeye msaliti anasema huo no ugomvi wake na Mbowe.Kwa MTU Kama Zitto tungetarajia kuona akibadilika kimatendo, mwenendo na kukemea wanaomwangamiza mitandaoni ambao Kwa kiasi kikubwa wanna chon vanisha na Umma. Mfano, kitendo cha yeye kusifiwa na CCM na yeye kuona ni sifa njema kinamwangamiza zaidi kisiasa kuliko kumjenga.Hili hataweza kuliona kwasababu ya jitihada za CCM. Baada ya Muda atakuja kujua kuwa adui take hakuwa Mbowe wala Chadema bali no CCM na yeye mwenyewe kutojitambua na kuamini kwamba angeweza kurevert his lost trust mbele ya jamii.

Kwa halo ilivyo, kuendelea kumtaja mbowe kwenye siasa za Zitto no kumpoteza Zitto na Kama hatashituka na kuwakea watu wa aina yako basi siasa zake zinaenda kubaya na atapoteza kuaminika kabisa kuliko anavyodhania.

Usaliti wa kina kafulila,Mbatia na wengine ambao kwa sasa ndio mashujaa wa ukawa uliisha lini mbona hamtaki kujibu hoja ?
 
ulichoandika ni huzuni kwa taifa...km haya ndio matumizi ya technologia ni mbaya kuliko kupoteza muda ktk pornographia ya internet.Kwa Tz na duniani kote mwanasiasa ni km neno Mswahili...Mwanaharakati=Mwokozi,mpigania haki.....mwanasiasa hana course...

Hata kama kwa mtazamo wako huo, tunamshauri mbowe aende shule ili aachane na siasa za kiuanaharakati.
Afanye siasa kama kiongozi aliyejiandaa kushika dola.
 
we mleta mada umekosa la kuleta hapa au ulitaka kupima maji kutaka kujua kama msaliti amepata mashabiki humu, ondoa upuuzi wako hapa
 
hakuna mwenye nafasi kumsikiliza msaliti.haiwezekani watu wote kwenye chama wakuchukie wewe mtu mmoja tuu, haiwezekani, na bahati mbaya wanatoa data za ukweli kuhusika na jambo linalowafanya wakuchukie, sasa hata kama unazo hoja vipi nani ana muda nazo. Wee unaye mtaka mpigie simu akuelezee.

mbowe anaweza kumzidi zitto kwa pesa tu basi
 
Zzk ni mwizi na mh Mbowe ni kiongozi na mtumishi wa watu.

Tumia akili japo kidogo,utudadavulie huo wizi wa zito
kuliko kuandika jumla namna hiyo
Inakuonyesha jinsi gani una uwezo wako mdogo wa kuchammbua mambo.
Zito ni mwanasiasa lulu ktk nchi hii.
 
Tatizo kubwa la Zitto ni usaliti Kwa watanzania, chama chake cha zamani, nafsi yake na wafuasi wake. Zitto was mwaka 2007 na Zitto wa Leo 2015 ni watu wawili tofauti ijapokuwa wanatumia sura ileile ya 2007.
Kimsingi, Leo Zitto anawafuasi wengi wa CCM kuliko chama kingine chochote cha siasa.Hii ni kutokana Zitto kutenda mapenzi ya CCM kuliko watanzania. Wao CCM wanatumia kichwa na Sura ya Zitto kufanikisha malengo yao.

Ndiyo maana,Zitto akiambiwa yeye msaliti anasema huo no ugomvi wake na Mbowe.Kwa MTU Kama Zitto tungetarajia kuona akibadilika kimatendo, mwenendo na kukemea wanaomwangamiza mitandaoni ambao Kwa kiasi kikubwa wanna chon vanisha na Umma. Mfano, kitendo cha yeye kusifiwa na CCM na yeye kuona ni sifa njema kinamwangamiza zaidi kisiasa kuliko kumjenga.Hili hataweza kuliona kwasababu ya jitihada za CCM. Baada ya Muda atakuja kujua kuwa adui take hakuwa Mbowe wala Chadema bali no CCM na yeye mwenyewe kutojitambua na kuamini kwamba angeweza kurevert his lost trust mbele ya jamii.

Kwa halo ilivyo, kuendelea kumtaja mbowe kwenye siasa za Zitto no kumpoteza Zitto na Kama hatashituka na kuwakea watu wa aina yako basi siasa zake zinaenda kubaya na atapoteza kuaminika kabisa kuliko anavyodhania.

Kwa habari ya kupotea kwa zito kisiasa.
hizi ni ndoto tena nzuri sana endelea kuota. Maana kwa mtazamo wako ungetamani awe ameshapotea lakini ndio anazidi kushamiri.
 
"UKAWA ni Wasaka tonge" kisha "Namshangaa Mbowe na kauli yake ya kutotaka ACT WASALITI wajiunge na UKAWA" ni usaliti na unafiki wa hali ya juu kutoa kauli mbili zinazopingana kisha kujibaraguza ati anamshangaa Mbowe! Badala ya kujishangaa yeye na kauli zake fyongo.

Hakuna mwenye nafasi kumsikiliza msaliti.haiwezekani watu wote kwenye chama wakuchukie wewe mtu mmoja tuu, haiwezekani, na bahati mbaya wanatoa data za ukweli kuhusika na jambo linalowafanya wakuchukie, sasa hata kama unazo hoja vipi nani ana muda nazo. wee unaye mtaka mpigie simu akuelezee.
 
Zitto Kabwe
Yaliyojificha kuporomoka kwa shilingi dhidi ya
Dola ya Marekani
Shilingi inahujumiwa na Mabenki? – Zitto Kabwe
Katika ukurasa wangu wa facebook mnamo
tarehe 25 Aprili 2015 niliandika kuhusu sababu za
shilingi kuporomoka thamani na majawabu ya
namna ya kurejesha thamani halisi ya sarafu
yetu. Nilieleza “Shilingi kuporomoka dhidi ya dola
na kuvuka 1$/2000TS kunasababishwa na sababu
kadhaa 1) Woga wa uchaguzi na hivyo Dola
nyingi kutoingia nchini (FDI etc) kusikilizia
Serikali ijayo inaundwaje 2) Woga wa uchaguzi
na hivyo matajiri kununua dola kwa kasi (too
many Tshs chasing too few $) ili kuzificha
(hoard) nje 3) kutouza mazao nje na kuagiza
bidhaa nyingi kutoka nje ( current account
deficit) 4) Benki Kuu kutoachia $ nyingi kwenye
soko kutokana na akiba ya fedha za kigeni
kupungua 5) Kuongezeka kwa huduma ya Deni la
Taifa ambapo malipo ni kwa fedha za kigeni kwa
madeni yaliyo wiva.
Niliendelea kushauri majawabu “Suluhisho 1)
Benki Kuu kuachia $ za kutosha kwenye soko
katika muda mfupi na wa kati (Mwezi Februari
BoT ilifanya hivi na kuongeza $64 milioni kwneye
soko bila mafanikio 2) Kuongeza mauzo nje hasa
ukizingatia kwa sasa 'our exports becomes
cheaper vis a vis foreign exchange) 3) Malipo ya
kodi ya Ongezeko la Mtaji kutoka BG (Shell
transaction ) na Ophir (Pavilion transaction),
malipo haya kwa fedha za kigeni 4) Punguza
kununua vitu vya anasa kutoka nje 5) Unafuu wa
huduma kwa Deni la Taifa ( Debt relief ) 6)
Punguza ujazo wa fedha nchini (mop tshs out)”.
Mjadala mkali umeendelea kuhusu suala hili
katika majukwaa mbali mbali. Ni dhahiri
kuporomoka kwa shilingi kunaathiri sana
Watanzania wa ngazi ya kati hasa
wafanyabiashara wa kati wenye kununua huduma
na bidhaa kutoka nje. Wenye viwanda
wanaotegemea malighafi kutoka nje gharama zao
za uzalishaji zimeongezeka zaidi na hivyo
kuhatarisha uzalishaji mali nchini. Licha ya
kwamba kuporomoka kwa shilingi kunafanya
bidhaa zetu za kuuza nje kuwa rahisi, lakini
huchukua muda kuzalisha bidhaa hizo na hasa
kilimo kuweza kufaidika hali hiyo. Kwa hiyo ni
faida kwa nchi kwa sasa kuwa na sarafu
stahmilivu ( stable) iliyojengwa kwenye misingi
imara ya Uchumi. Hata hivyo, inaonekana kuwa
sarafu ya Tanzania inahujumiwa. Kuporomoka
kwa Shilingi katika wiki za hivi karibuni sio
matokeo ya nguvu za soko bali ni matokeo ya
hujuma ( currency manipulations).
Mabenki makubwa ya kigeni nchini, inasemekana,
katika miezi ya karibuni yamefanya currency
manipulations na kupelekea dola chache
kukimbizwa na shilingi nyingi na hivyo bei ya dola
kupanda bei. Hii inatokana na ukweli kwamba
Benki zetu kubwa tatu zinazoongoza
zinaendeshwa na wageni. Inasemekana biashara
hii hufanyika kati ya matawi ya Benki za kigeni
hapa nchini na makao makuu yao. Kuporomoka
kwa shilingi kunakotokea hivi sasa hakuendani na
kuporomoka kwa miaka ya nyuma kipindi kama
hiki (ambacho ki kawaida ni miezi shilingi
hushuka thamani kwa sababu ya watalii kuwa
wachache na mauzo ya bidhaa nje kuwa madogo
sana). Wastani wa miaka 10 iliyopita inaonyesha
kuwa kipindi hiki shilingi hushuka kwa kati ya 8%
mpaka 13% na sio kuporomoka kwa zaidi ya 20%
kulikotokea hivi sasa. Kwa mfano mwaka 2011
miezi kama hii ( Februari – Mei) Shilingi
iliporomoka kutoka shs 1,380 kwa dola 1 mpaka
shs 1,570 sawa na mporomoko wa 12%. Hata
hivyo kuanzia mwaka huo mpaka mwaka 2014
shilingi imekuwa ikishuka thamani kwa kiwango
kidogo sana. Mwaka 2013 thamani ya shilingi
ilishuka kwa wastani wa asilimia 1.7 tu.
Uchambuzi huu wa thamani ya sarafu yetu
unaonyesha kuwa kuna zaidi ya nguvu ya soko
kunakotokana na mauzo yetu nje kuwa
machache. Vile vile kupanda kwa thamani ya
dola ya marekani duniani hakutoshi kuelezea
mporomoko huu wa kasi wa shilingi kuanzia
mwezi Disemba mwaka 2014 mpaka sasa.
Tuhuma za mabenki kuwa yanahujumu shilingi
(currency manipulations) zaweza kuwa na
ukweli.
Vile vile, inasemekana kumekuwa na utoroshaji
mkubwa wa dola kutoka nchini kwenda nje ya
nchi. Utoroshaji huu unafanyika kupitia wasafiri
wanaopita ukumbi wa VIP uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Dar es Salaam. Utoroshwaji huu
unatokana na hofu isiyo ya msingi kwamba
uchaguzi utakuwa na vurugu. Utoroshwaji wa
fedha ni kinyume sheria zetu. Sheria zetu za
fedha za kigeni zinazuia mtu kubeba zaidi ya
dola 10,000 za kimarekani zikiwa taslimu, kuingia
nazo nchini au kutoka nazo nchini. Tafiti za
haraka zinaonyesha kuwa huu umekuwa ni
utaratibu wa kawaida kila mwaka wa uchaguzi
tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Benki Kuu ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua
zifuatazo;
1. Kufanya uchunguzi wa kushtukiza mara moja
dhidi ya benki zote za kigeni zilizopo hapa nchini.
Uchunguzi huu utazame biashara ya fedha za
kigeni ya benki hizi kwa lengo la kuzuia ‘
currency manipulations’ na kuchukua hatua
madhubuti dhidi ya Benki yeyote itakayokutwa
imehujumu biashara ya fedha za kigeni kwa
lengo la kushusha thamani ya shilingi dhidi ya
dola za kimarekani.
2. Jeshi la Polisi na kitengo cha kuzuia utoroshaji
wa fedha ( anti money laundering unit) kufanya
ukaguzi wa lazima wa watu wote wanaosafiri
kwenda nje ikiwemo wanaopita sehemu ya watu
mashuhuri (VIP Lounge) ili kudhibiti utoroshaji
wa fedha za kigeni kwenda ughaibuni.
3. Watanzania tufikirie upya nafasi ya Mabenki
katika uchumi wa nchi na kufanya maamuzi
magumu ya kurejesha baadhi ya Benki katika
umiliki mpana zaidi wa Watanzania. Kwa
malengo ya muda wa kati, Benki kubwa 3 nchini
ilazimu kuwa na umiliki unaozidi 51% wa
Watanzania. Bila ya kushika mabenki nchi
itachezewa sana.
4. Suluhiho la kudumu la sarafu stahmilivu ni
kuongeza uzalishaji wa bidhaa za kuuza nje ya
nchi na kupunguza manunuzi ya bidhaa kutoka
nje. Urari wa Biashara wa Tanzania umepanuka
kutoka $1bn mwaka 2004 mpaka $6bn mwaka
2013 (BOT 2013) kutokana manunuzi yetu nje
kukua kwa kasi kutoka $2.5bn mpaka $11bn
wakati mauzo yetu nje yakikua kwa kasi ndogo
kutoka $1.4bn mpaka $5bn katika kipindi hicho.
Isingekuwa uimara katika urari katika uwekezaji
na uhamisho wa mitaji, Tanzania ingekuwa na
sarafu yenye thamani sawa na takataka. Serikali
ihimize uzalishaji mali mashambani na viwandani
na kuuza nje biadhaa zilizoongezwa thamani.
Zama za kutegemea dhahabu zimekwisha na sio
endelevu. Turudi kwenye misingi: Bidhaa za
Kilimo na Viwanda.
Tutaendelea kufuatilia thamani ya shilingi mpaka
ifikapo mwezi Julai ambapo ndipo kipindi kigumu
kwa shilingi huwa kihistoria. Hatua zilizoainishwa
zisipotazamwa na mamlaka tajwa thamani ya
shilingi dhidi ya dola ya Marekani yaweza kufikia
tshs 3000!
 
Vitu hivyo ndio unaanza kuona tofauti kati ya Zitto na Mbowe.
 
Msaliti ni Mbowe aliyezaa nje ya ndoa yake,kwani amechepuka kwa mke wake.
Aisey kumbe hii nayo ni hoja? Basi Ngoja tukupime wewe kwa hoja. Ulivyotoa mada ilihakisi mtu mwenye hekima ambaye anataka kujadili issues na siyo personalities. Lakini mtihani wa kwanza tu umerejea katika uhalisia wako!
 
Back
Top Bottom