Mbowe na wenzake waomba shauri lao kuhamia Mahakama Kuu. Mh. Ester Bulaya ameunganishwa katika kesi yao

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
mboe+pic.gif

Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA), Ester Bulaya ameunganishwa katika kesi inayowakabili viongozi wengine wanane wa chama hicho, huku mawakili wa utetezi wakiomba kuhamishia shauri hilo Mahakama Kuu.

Baada ya kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka kwa kumuongeza Bulaya ambaye ni mshtakiwa wa tisa na kuongezwa mashtaka kutoka 10 hadi 12, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliwasomea upya mashtaka washtakiwa.

Baada ya kukamilisha hilo wakili huyo aliomba kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali, lakini wakili wa utetezi, Peter Kibatala aliomba shauri hilo kuhamishiwa Mahakama Kuu.

Kibatala alisema washtakiwa takriban wote ni wabunge na kwamba, shtaka la pili linakiuka haki yao ya msingi ya kufanya shughuli za kisiasa za chama wanachotoka cha CHADEMA.Kutokana na hilo, aliomba kulipeleka shauri hilo Mahakama Kuu ili itoe tafsiri iwapo ni halali kwa washtakiwa kushtakiwa kijinai.

Kwa shtaka la nne hadi la tisa, Kibatala anaomba mahakama iridhie wapeleke shauri Mahakama Kuu kwa sababu yanahusu masuala ya kikatiba juu ya uhuru wa kutoa maoni na hakuna mahali katika hati ya mashtaka inapoelezwa kwamba yaliyotamkwa na washtakiwa ni uongo au ni ya kutungwa.

Wakili wa Serikali Mkuu, Nchimbi alidai kilichowasilishwa na upande wa utetezi kisheria hakina mashiko, hivyo kuomba kujibu hoja hizo leo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anayesikiliza shauri hilo namba 112 la mwaka 2018 aliliahirisha hadi leo.

Bulaya na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama wakidaiwa kati ya Februari Mosi 2018 na Februari 16, 2018 wakiwa Kinondoni, Dar es Salaam walikula njama na kutenda kosa la jinai na kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na uchochezi.

Pia, wanakabiliwa na shtaka la kufanya mkusanyiko usio halali kinyume na sheria Februari 16, katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam; kutotekeleza agizo la polisi lililowataka kutawanyika na kusababisha kifo cha Akwilina Akwilini, aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kujeruhiwa askari wawili. Bulaya ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na shtaka la peke yake akidaiwa kushawishi kutendeka kosa la jinai.

Washtakiwa wengine ni mwenyekiti wa CHADEMA na mbunge wa Hai, Freeman Mbowe; Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa; naibu katibu mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu; naibu katibu mkuu (Bara) na mbunge wa Kibamba, John Mnyika; mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko; katibu mkuu wa CHADEMA, Dk Vincent Mashinji; mbunge wa Kawe, Halima Mdee; na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Chanzo: Mwananchi

Soma: Mbowe na viongozi 6 wa CHADEMA wafikishwa Mahakamani Kisutu, wasomewa mashitaka 8, wanyimwa dhamana hadi Machi 29

Soma:KISUTU, DAR: Mahakama yawapa dhamana Viongozi 6 wa CHADEMA bila kuwepo mahakamani. Kutoka gerezani Aprili 3, 2018...

Hakuna kesi ya kikatiba hapo, kibatara analengo la Kucherewesha kesi, maana issue ni kufanya mkusanyiko usio harari!! Km ulikuwa harari cwangethibitisha hapo hapo mahakamani? Au km hawakutoa rugha zakuchochea napo siwathibitishe? Jera inawanukia
 
Wabunge wa Chadema, wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, wameshawasili katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi saa 2.

Wabunge hao wanafika mahakamani kama walivyoamriwa na mahakama kutokana na mashtaka yanayowakabili, ikiwano ya kuhamasisha maandamano na uchochezi.

Miongoni mwa waliofika mahakamani ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Esther Bulaya wa Bunda, Halima Mdee (Kawe), Esther Matiko(Tarime Mjini), Naibu Katibu Mkuu bara, John Mnyika na Naibu Katibu Mkuu visiwani, Salum Mwalimu .

Mbowe, wenzake waomba kuhamia Mahakama Kuu
Wamefika mahakamai hapo kutokana na kesi inayowakabili namba 112 ya mwaka huu
Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri ataongoza kesi hiyo huku Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi akijibu hoja zilizowasilishwa jana na Wakili wa utetezi Peter Kibatala.
 
Hakuna kesi ya kikatiba hapo, kibatara analengo la Kucherewesha kesi, maana issue ni kufanya mkusanyiko usio harari!! Km ulikuwa harari cwangethibitisha hapo hapo mahakamani? Au km hawakutoa rugha zakuchochea napo siwathibitishe? Jera inawanukia
Mtu ambaye hata kuandika hujui unawezaje kuchambua masuala ya kisheria? Rudi shule kwanza kajifunze kuandika..masuala ya kisheria kwa uwezo wako ni ardhi na mbingu!
 
Hakuna kesi ya kikatiba hapo, kibatara analengo la Kucherewesha kesi, maana issue ni kufanya mkusanyiko usio harari!! Km ulikuwa harari cwangethibitisha hapo hapo mahakamani? Au km hawakutoa rugha zakuchochea napo siwathibitishe? Jera inawanukia
Jamani mnatuharibia Kiswahili!
 
Hakuna kesi ya kikatiba hapo, kibatara analengo la Kucherewesha kesi, maana issue ni kufanya mkusanyiko usio harari!! Km ulikuwa harari cwangethibitisha hapo hapo mahakamani? Au km hawakutoa rugha zakuchochea napo siwathibitishe? Jera inawanukia
Take your time kujifunza kiswahili badala ya kukurupuka na "harari "...
 
Hakuna kesi ya kikatiba hapo, kibatara analengo la Kucherewesha kesi, maana issue ni kufanya mkusanyiko usio harari!! Km ulikuwa harari cwangethibitisha hapo hapo mahakamani? Au km hawakutoa rugha zakuchochea napo siwathibitishe? Jera inawanukia

Ungejifunza kuandika vizuri kwanza.
 
Hakuna kesi ya kikatiba hapo, kibatara analengo la Kucherewesha kesi, maana issue ni kufanya mkusanyiko usio harari!! Km ulikuwa harari cwangethibitisha hapo hapo mahakamani? Au km hawakutoa rugha zakuchochea napo siwathibitishe? Jera inawanukia

Kwahiyo kufanya mkusanyiko usio halali ni JINAI ?

au hujaelewa kwanini anataka kwenda mahakama kuu/
Labda nikusaidie tu, anataka kwenda kuhoji hayo kuwa je ni halali kuita mashtaka kama hayo JINAI ?
 
Hakuna kesi ya kikatiba hapo, kibatara analengo la Kucherewesha kesi, maana issue ni kufanya mkusanyiko usio harari!! Km ulikuwa harari cwangethibitisha hapo hapo mahakamani? Au km hawakutoa rugha zakuchochea napo siwathibitishe? Jera inawanukia
Ndio furaha ya wapumbavu, wanavyotetewa hugeuka vichaa kushabikia watetezi wao wanavyosulubiwa. Pole sana, na wewe nenda ukawe upande wa Nchimbi!!
 
mh!hii picha siipendi,inadharirisha taasis ya Uraisi!
Mwenzako anafurahi sana, tatizo anajua sasa yeye ni tajiri namba 1 Africa. Nimewaona wakina Odinga na utajili wao binafsi hawajawahi toa hela hadharani hivyo. Huyu jamaa kweli zwazwa!!
 
Hakuna kesi ya kikatiba hapo, kibatara analengo la Kucherewesha kesi, maana issue ni kufanya mkusanyiko usio harari!! Km ulikuwa harari cwangethibitisha hapo hapo mahakamani? Au km hawakutoa rugha zakuchochea napo siwathibitishe? Jera inawanukia
Hebu peleka vyeti vya kuzaliwa uhamiaji. Vyako, baba na babu.
 
Back
Top Bottom