Mbowe na Wenzake wanayo nafasi ya kuomba fidia kwa madhira waliosababishiwa?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,214
42,087
Wasalaam!

Jambo ambalo nimekuwa nikijiuliza baada ya serikali kuweka wazi kuwa haito endelea na case ya Mbowe na wenzake ambo walikuwa na tuhuma za ugaidi. Mbowe na wenzake wanayo haki ya kudai fidia au kudai fidia ya gharama za case hiyo iliyochukua siku zaidi ya miambili!

Mh Mbowe amenukuliwa akisema alitamani kuona case hii inaendelea hadi mwisho ili dunia ijue ukweli kuliko ilivyofutwa!

Mbowe na Wenzake wana haki ya kusamehe kama walivyofanya!

Lakini najiuliza ikiwa wakiamua kudai fidia ya gharama za case na muda waliopotezewa bila kusahau madhira waliopata wanayo haki kisheria kudai fidia kwa case iliyoondolewa na wanao shitaki?
 
Wachambuzi wa mambo na wanaojitolea kurejesha kwa jamii kama akina P. Tafadhali popote mlipo mfanye kama mnajikunatuwaone🤔.
 
mwenyewe ameomba ARUHUSIWE ANYAMAZE
Kitendo Cha kudai adai fidia mtamfanya aanze kuongea .
Mbowe ni mtu mzima.
Aliweza kunyamaza bila kuomba.
Ila mpaka ameamua kuomba UJUE KUNA JAMBO.muacheni apumzike
 
Kiukweli ingeleta maana hata kwa hao walioshiriki kukandamiza haki za watu. Maana italeta uelewa hata kwenye kesi zingine kabla ya kushitakiwa au kushitaki wahusika wajue Kuna faini mbele iwapo itagundulika hi kesi ya uongo. Kila mpenda haki ajitokeze kutujuza hasa wanasheria.
 
Kwa sheria zetu hizi za kikoloni ni ngumu sana kufanya hivyo na kufanikiwa!!la muhimu ni Kumshukuru Mungu tu, kwa kurudishiwa uhuru wako!!kwani si ajabu ukaanza mchakato huo ukasikia tena wamerudisha mashitaka yako tena!

Mtu ameshinda kesi mahakamani baada ya kukaaa miaka 10, gerezani na kuonekana hana hatia, lakini hawezi kuishitaki serikali sembuse , mtu aliyeachiwa kwa mamlaka ya DPP?
sheria zetu bado sana, yaani binadamu anakuwa nusu MUNGU.
 
Sheria haziruhusu?
 
Mbowe na wenzake wanajua kisheria DPP ana uwezo wa kuitisha tena kesi yoyote ile aliyofuta
 
Hawana nafasi kama kesi haijatolewa hukumu ni kama ukamatwe na polisi bila sababu sana sana utaishiwa kuachiwa tu
 
Kiukweli ingeleta maana hata kwa hao walioshiriki kukandamiza haki za watu. Maana italeta uelewa hata kwenye kesi zingine kabla ya kushitakiwa au kushitaki wahusika wajue Kuna faini mbele iwapo itagundulika hi kesi ya uongo. Kila mpenda haki ajitokeze kutujuza hasa wanasheria.
Sheria za Tz ni za hovyo sn DPP amepewa mamlaka ya kimungu
 
hawa CCM ilitakiwa tuyashinde kwenye mahakama ya rufaa, kwa kuifuta kesi SSH keisha tutengua kiuno, kwa sasa hakuna ujanjaa
 
Ule wito wa nyumba nyeupe bila shaka ulimaliza yote na ndo sababu ya kuitwa mle kabla hata hajafika kwake.

Yawezekana ndo maana uchungu ulimzidi kanisani hadi akalia.
 
Mimi natamani wafungue kesi ya madi ya gharama za kusi, kuchafuliwa jina na muda waliomzuia gerezani bila hatia
 
Wasalaam!

Jambo ambalo nimekuwa nikijiuliza baada ya serikali kuweka wazi kuwa haito endelea na case ya Mbowe na wenzake ambo walikuwa na tuhuma za ugaidi. Mbowe na wenzake wanayo haki ya kudai fidia au kudai fidia ya gharama za case hiyo iliyochukua siku zaidi ya miambili!

Mh Mbowe amenukuliwa akisema alitamani kuona case hii inaendelea hadi mwisho ili dunia ijue ukweli kuliko ilivyofutwa!

Mbowe na Wenzake wana haki ya kusamehe kama walivyofanya!

Lakini najiuliza ikiwa wakiamua kudai fidia ya gharama za case na muda waliopotezewa bila kusahau madhira waliopata wanayo haki kisheria kudai fidia kwa case iliyoondolewa na wanao shitaki?
Hakuna kiti kama hicho duniani. Kwani alifungwa kimakosa? Hajapewa kifungo chochote. Yeyte atulie tu na shida zake.
 
Mimi natamani wafungue kesi ya madi ya gharama za kusi, kuchafuliwa jina na muda waliomzuia gerezani bila hatia
Jisomeeni jamani, ili mjue mfumo wa haki ktk nchi! Mahabusu siyo adhabu. Angeomba fidia kama angekuwa amefungwa kimakosa na baadaye kuachiwa.
 
Wasalaam!

Jambo ambalo nimekuwa nikijiuliza baada ya serikali kuweka wazi kuwa haito endelea na case ya Mbowe na wenzake ambo walikuwa na tuhuma za ugaidi. Mbowe na wenzake wanayo haki ya kudai fidia au kudai fidia ya gharama za case hiyo iliyochukua siku zaidi ya miambili!

Mh Mbowe amenukuliwa akisema alitamani kuona case hii inaendelea hadi mwisho ili dunia ijue ukweli kuliko ilivyofutwa!

Mbowe na Wenzake wana haki ya kusamehe kama walivyofanya!

Lakini najiuliza ikiwa wakiamua kudai fidia ya gharama za case na muda waliopotezewa bila kusahau madhira waliopata wanayo haki kisheria kudai fidia kwa case iliyoondolewa na wanao shitaki?
Jibu la swali lako ni kwamba watuhumiwa walioachiwa huru hawana fursa kama hiyo. Mahakama ilitamka kwamba watuhumiwa wana kesi ya kujibu. Hiyo inamaanisha kwamba polisi walipowashika na kuwaweka mahabusu walikuwa na sababu ya kuridhisha kwamba njama za uhalifu zilikuwepo kweli. Hivyo huwezi kuilaumu Serikali kwa kumshika mtuhumiwa baada ya kujiridhisha kwamba kuna uhalifu unaobuniwa kufanywa. Kwamba DPP ameamua kutoendelea na kesi ni jambo jingine kabisa.
Hata kama kesi ingeendelea na watuhumiwa wakashinda, haiwezekani kuishitaki Serikali. Labda kama kutatolewa ushahidi wa kuridhisha kwamba watuhumiwa walishikwa kwa kuonewa tu na mtu mwenye njama au nia mbaya dhidi yao.
 
Back
Top Bottom