Mbowe, na sisi pia tumekuchoka pumzika acha udikteta ndani ya chama

Mimi ni mfuasi wa mageuzi ndani ya nchi hii ila niseme ukweli wa principle ya dictetor yeyeto, watu wanao mzunguka huwa hawamwambii ukweli na uwa wanamkimbia pale maji yakiwa shingoni hivyo natoa ushauri sio tu kwa Mbowe, Watu wote wenye mamlaka ya kiuongozi jaribuni kuwa mnatoka na kwenda kusikiliza Umma unataka nini juu ya uongozi wenu.

Ndicho kinachofanyika kwa Mbowe watu walio karibu yako wanakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ila ukweli wanaujua wewe umechoka hauna tena jipya ndani ya chama wao wanakushauri upuuzi ili waendelee kula ruzuku sasa subiri 2020 ruzuku ikipungua jinsi watakavyokubadilikia.

Mbowe Jiangalie Ondoka kwa heshima kama kweli CHADEMA ni taasisi ni hayo tu toka nenda mtaani sikiliza watu halisi sio wapambe.
Mbona ccm iliyokaa madarakani miaka 58 ikiamua hatima ya maisha yenu na watoto wenu hamuiambii mmeichoka? nadhani watanzania tunshida kubwa
 
Wewe hujitambui una matatizo makubwa ya akili na unahitaji uangalizi mkubwa sana wa Dr ,eti umemchoka Mbowe na unataka eti apumzike.
Mbowe ana impact gani na maisha yako na ndugu zako?
Unamchoka mwenyekiti wa Chama cha siasa kilichojaa misukosuko kibao ya kuandamwa na dola unaacha kumchoka Magufuli aliyesababisha vilio kwa mamilioni ya watanzania?
Wewe una roho ya kichawi kabisa,kama umemchoka nenda kapige kura ya kumkataa kuliko kuja na hoja za kichawi hapa.
Naunga mkono hoja
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mimi ni mfuasi wa mageuzi ndani ya nchi hii ila niseme ukweli wa principle ya dictetor yeyeto, watu wanao mzunguka huwa hawamwambii ukweli na uwa wanamkimbia pale maji yakiwa shingoni hivyo natoa ushauri sio tu kwa Mbowe, Watu wote wenye mamlaka ya kiuongozi jaribuni kuwa mnatoka na kwenda kusikiliza Umma unataka nini juu ya uongozi wenu.

Ndicho kinachofanyika kwa Mbowe watu walio karibu yako wanakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ila ukweli wanaujua wewe umechoka hauna tena jipya ndani ya chama wao wanakushauri upuuzi ili waendelee kula ruzuku sasa subiri 2020 ruzuku ikipungua jinsi watakavyokubadilikia.

Mbowe Jiangalie ondoka kwa heshima kama kweli CHADEMA ni taasisi toka nenda mtaani sikiliza watu halisi wapenda mabadiliko ya kweli sio wapambe.
Technically.

Umeongea ukweli Mtupu bila kujali itikadi ya chama ulichonacho. Safi Sana na hivi ndo mtu mwenye akili anatakiwa kushauri.
 
Ndio hapo tunapoona kuwa CCM ni chama kilichojichokea kuongoza. Haiwezekani chama makini kiwe na Rais asiye heshimu Sera na ilani yake kama Magu afanyavyo!
Chadema ingeweza kumdhibiti mgombea wake kufuata na kuheshimu sheria na katiba.

Nakubaliana na ww kabisa chakaza, kwanza mimi naamini kabisa ccm sio chama makini bali ni chama chenye nguvu za dola. Na suala la ccm kushindwa kuongoza nchi hilo liko wazi ndio maana wameweka mabavu ya vyombo vya dola mbele.

Napenda nikukatalie hapa hapa bila kuuma maneno kuhusu cdm kuwa na uwezo wa kumdhibiti Lowassa, kwanza kwa nguvu za kikatiba alizonazo rais cdm isingekuwa na uwezo wowote wa kumdhibiti. Kumbuka Lowassa alikuja cdm muda mfupi kabla ya uchaguzi, hivyo tabia rasmi ya Lowassa ilikuwa haifahamiki pindi akiwa na madaraka hasa ya urais. Cdm ingeweza vipi kumdhibiti mtu ambaye kabla hata hajawa rais aliweza kulazimisha watu aliotoka nao ccm wapewe nafasi za kugombea ubunge na udiwani, na kuna waliopewa ubunge kabisa kwa shinikizo lake? Sasa hata jambo dogo tu la yeye kukaa high table aliweza hata akiwa hana madaraka yoyote, ingemdhibiti vipi akiwa rais? Kama alikuwa anakaa high table huku akiwa hata kuvaa sare za chama hataki nani angemdhibiti? Tushukuru tu Lowassa hakuwa rais, japo sikubaliani kabisa na Magufuli kuwa rais wetu.
 
Ushauri mzuri!
Bora umenisaidia kusema. Ni kweli Mbowe kafanya mazuri na kakifikisha chama pazuri. Pia amekaa madarakani muda mrefu wa kutosha, ni vyema akipisha wengine wasogeze chama mbele. Uzoefu unaonyesha kiongozi mzuri huwa ni miaka 10 mwisho, ikizidi sana 15. Ikipita hapo, hata yale mazuri yake huanza kuyaharibu.

Tujenge utamaduni wa kupokezana vijiti ili kuleta mawazo na hamasa mpya kila wakati. Msimamo wangu huu ni dhabiti na ninaweza kuutetea bila kumhofia mtu yoyote. Huu sio muda wa Mbowe kuendelea tena kuwa mwenyekiti wa cdm kwa Utetezi wowote ule.
 
Ndugu usidhani kuongoza chama cha siasa kwenye hizi nchi zilizokosa ustaarabu wakisiasa ni kazi rahisi.Ata kama kuna wengine wanaoweza kuongoza ila sidhani kama nibusara kumweka mbowe pembeni kwasasa kulingana na hali halisi ilivyo, kwasababu Mbowe tayari anajulikana kuanzia busara zake hadi uvumilivu sasa usidhani ni jambo rahisi kumpata mwingine mwenye kaliba hiyo kwenye zama kama hizi.Kumbuka siasa isipochukuliwa kwa uangalifu inaweza kuleta majanga makubwa sana kwaiyo nivyema kua na kiongozi anayeweza kudhibiti hisia zake,ujinga wake, hasira zake na wafuasi wanaunga mkono chama ili chama kiendelee kua na utulivu.Tofauti na hapo mambo yanaweza kubadilika.
 
Waafrika tuna shida gani? Mabingwa wa kuona matatizo ya wenzetu huku ya kwetu tunafumbia macho
 
Mimi naomba mbowe aendelee mpaka muda wa magufuli uishe maana huyu jamaa kwa kupanda dau sidhani kama kuna mtu ata resist zaidi ya mbowe kisha onyesha hana bei
 
mwaka 1995 kura ya NCCR Mageuzi
mwaka 2000 CHADEMA
Mwaka 2005 Chadema
2010 chadema
2015 Nilipigia kura yangu ya kwanza kwa MAGUFULI
NAJIPONGEZA SANA KUMPA MTU SAHIHI KURA YANGU. Mabadiliko ni ya muhimu mahali popote pale.
Mbona umetumia ID mpya?
 
Ni kipi ambacho Mbowe anazuia sasa hivi akiwa mwenyekiti? Kama ni uhanga yeye ni muhanga namba moja wa udictator wa Magufuli. Miradi yake mingi imehujumiwa tena kwa sababu zilizo wazi za kisiasa. Kesi anazo za kubambikiwa na huenda akafungwa, alikaa ndani siku 90 tena kwa amri toka juu na hakuna chochote alichofanya.

Kama ni haiba ya chama inazidi kuharibiwa huku yeye akiwa mwenyekiti, viongozi mbalimbali wanahongwa na kuhamia ccm, mikutano na kazi za kisiasa zilizopo kisheria Magufuli kazizuia na Mbowe katii bila hata kwenda mahakamani kupata uamuzi wa kisheria. Kampokea Lowassa na kumpa cheo adhimu cha kugombea urais, hivi leo karudi ccm baada ya kuitumia cdm kama kondomu, mwenyekiti madhubuti hawezi kuokoteza mgombea urais kwa njia ya mwendo kasi. Sasa kwa mazingira hayo na muda aliokaa madarakani aendelee kuwa mwenyekiti ili iwe nini kwa mfano?
Mkuu kama yote hayo amepitia na bado anapambana tuambie nani huko anafaa ambaye akipitia katika tanuru hilo hata hamia huku mtaa wa 2.?

Msije kuwa mnafanya uchaguzi kila mwaka wa mwenyekiti.
 
Huu ni msimamo wa watu wote wenye akili timamu, achana na wale ccm njaa.
Ni heshima kubwa Mbowe akikaa pembeni sasa, Chadema ina watu wenye uwezo mkubwa wa kukiongoza chama katika zama hizi za kibabe.

Kama John Heche aliiongoza Bàvicha kwa mafanikio ni kwa nini hili kundi LA vijana wa hovyo lisimchukulie fomu John Heche?
Kuna uzi hapa uliwekwa kuwa Heche anaenda kuwa katibu wa chama. Nadhani huko kutakuwa kutamu zaidi kuliko yeye kuwa mwenyekiti.
 
Mkuu kama yote hayo amepitia na bado anapambana tuambie nani huko anafaa ambaye akipitia katika tanuru hilo hata hamia huku mtaa wa 2.?

Msije kuwa mnafanya uchaguzi kila mwaka wa mwenyekiti.

Kwani ni yeye tu anaweza kupitia hayo? Ni lazima anayekuja na yeye apitie mazingira yake? Mbona wako wapinzani wengi tu wanapitia hayo, au yeye ni special? Kaondoka Slaa na cdm bado ni hai, tujenge cdm imara kama taasisi, na sio viongozi ving'an'ganizi wa madaraka eti ni watu imara. Kama amekuwa mwenyekiti kwa miaka 15 bila kujenga taasisi imara bali kujigeuza yeye ndio imara, basi hicho sio chama bali kundi la marafiki walioko kwenye siasa. Cdm tujitahidi kuepuka siasa za mtu bali tujenge chama imara, kwani Mbowe anaweza kufa hata leo, je ikitokea hivyo ndio chama kitakufa, acheni mambo ya utetezi wa aibu.
 
Mimi naomba mbowe aendelee mpaka muda wa magufuli uishe maana huyu jamaa kwa kupanda dau sidhani kama kuna mtu ata resist zaidi ya mbowe kisha onyesha hana bei

Hana bei, unajua ilikuwaje akampokea Lowassa? Tema mate chini.
 
Wewe hujitambui una matatizo makubwa ya akili na unahitaji uangalizi mkubwa sana wa Dr ,eti umemchoka Mbowe na unataka eti apumzike.
Mbowe ana impact gani na maisha yako na ndugu zako?
Unamchoka mwenyekiti wa Chama cha siasa kilichojaa misukosuko kibao ya kuandamwa na dola unaacha kumchoka Magufuli aliyesababisha vilio kwa mamilioni ya watanzania?
Wewe una roho ya kichawi kabisa,kama umemchoka nenda kapige kura ya kumkataa kuliko kuja na hoja za kichawi hapa.
Rungu kichwani komredi kipepe
 
Kwani ni yeye tu anaweza kupitia hayo? Ni lazima anayekuja na yeye apitie mazingira yake? Mbona wako wapinzani wengi tu wanapitia hayo, au yeye ni special? Kaondoka Slaa na cdm bado ni hai, tujenge cdm imara kama taasisi, na sio viongozi ving'an'ganizi wa madaraka eti ni watu imara. Kama amekuwa mwenyekiti kwa miaka 15 bila kujenga taasisi imara bali kujigeuza yeye ndio imara, basi hicho sio chama bali kundi la marafiki walioko kwenye siasa. Cdm tujitahidi kuepuka siasa za mtu bali tujenge chama imara, kwani Mbowe anaweza kufa hata leo, je ikitokea hivyo ndio chama kitakufa, acheni mambo ya utetezi wa aibu.
Kila heri huko. Sie tupo na mchakato wa kumsimika wetu adumu zaidi ya 2025.
 
Leo nakuunga kidole boss.

Mimi ni CCM ambaye naamini kwenye upinzani wa kweli na nachukia upinzani wa kitaarabu uliopp sasa JF na kwingine.

Kwa nguvu zozote za serikali na CCM Mbowe lazima awe mwenyekiti wa Chadema kwakuwa Mbowe ana busara sana na mstahimilivu wa shida. Mbowe sio mtu wa vita ila mtu wa Diplomasia ya juu.

Chadema ingenivutia nijiunge kama ingepata mtu kama John Heche nk ambao sio waoga na huweka busara pembeni inapobidi.

Kwa Mbowe. serikali na CCM itakuwa itakuwa na furaha sana kwakuwa wanamjua. mtoto aliyekuzwa na mzazi ambaye ni mtumishi wa ngazi za juu serikalini.

Tukiweka vyama pembeni na tuangalie utaifa Mbowe atabaki sio challenge kwa CCM.

Back
Top Bottom