Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,503
- 51,098
Hebu fikirieni hili suala:
Umma wa Tanzania umeanza kuamka, unakataa udalali wa rasilimali zao, unaanza polepole kukataa chapa waliyopigwa kwa muda mrefu kimkakati ya uoga, unaanza kuchukua hatua ya kupeleka Struggle katika hatua ya pili ya matendo badala ya maneno. Cha kusikitisha anatokea kiongozi mmoja wa Taasisi muhimu ya wananchi, ambaye kwa nafasi yake, na mizizi ya taasisi yake angeweza kusaidia pakubwa kuwatoa wananchi kutoka katika kongwa hili la kutochukua hatua yoyote ya kuiadabisha serikali yao kutokana na madudu makubwa inayofanya yeye anarudi nyuma, na matokeo yake kuisaidia CCM kuzima cheche ambazo zingesaidia kutengeneza moto mkubwa wa mabadiliko huko mbele. Ni ajabu sana!
1. Mbowe na siasa zake za ki "Uncle Tom"
Kipindi cha utumwa huko Marekani na Jim Crow, walikuwepo wamarekani weusi ambao kwa kuwa wao walikuwa na vijinafasinafasi katika mfumo wa Marekani, walikuwa wakipenda kujitapa kwa kauli za "I am the only negro working as an engineer here", "I am the first black clerk in here". Leo hii Huwezi kushangaa kumsikia Mbowe akijitapa na kauli yake maarufu ya siasa za nchi hii ni ya Farasi wawili, CCM na Chadema. Na hii Mentality ndiyo inayomsukuma kutaka alambwe miguu pale wananchi wanapotaka kusogeza struggle kwenda next level, Ili kuitia kibano serikali ya CCM katika suala la bandari na katiba mpya. Ndiyo maana Juzi huko Zanzibar, huku akisimama kwa kujitapa mbele ya wazee wa chama anahoji eti Chadema haikushirikishwa katika maandalizi ya mikutano na maandamano ya kuibana serikali ya CCM katika suala la katiba mpya na Bandari. Yaani anataka apigiwe magoti na wananchi kwenye struggle za kuitia kibano serikali, yeye nani, na kwa nini?!.
2. Mbowe amesaliti struggle za Watanzania kupeleka struggle next level
Sijui kama Mbowe na chawa wake ndani ya Chadema wanatambua athari za walichokifanya dhidi ya struggle za Watanzania katika kujikomboa kutoka katika minyororo ya Siasa chafu na uongozi mbovu wa CCM. Badala ya kuweka ego ya Kiuenyekiti, na ego ya uchama mbele, Mbowe alipaswa aangalie picha pana ya movement ya wananchi ya kutaka kuitia kibano Serikali ya CCM zaidi katika suala la bandari. Infact struggle hii inacompliment kabisa jitihada za chama cha Chadema za kudai katiba mpya. Badala ya Mbowe kuwapiga Rungu Sauti ya Watanzania, kama kweli angekuwa anahitaji mabadiliko ya kweli nchini, alipaswa aweke ego yake pembeni na kuwasaidia kadri inavyowezekana. Hii ingesolidify movement ya mabadiliko kutoka pande zote za kijamii na kisiasa za kuleta mabadiliko nchini. Lakini cha ajabu at the critical hour, Mwenyekiti kama kawaida yake ANABADILI GIA angani.
3. Jeuri ya Nyomi mikutanoni na kudhani Chadema haihitaji Sauti za mitandaoni
Inavyoelekea, wingi wa watu katika mikutano ya Chadema umeanza kuwapa kiburi viongozi wa Chadema na kudhani kuwa nyomi hilo linamaanisha kushinda chaguzi na labda eti hiyo ndiyo force pekee inayoweza kuipeleka Chadema mbele. Nataka nimwambie Mwenyekiti Mbowe na Chawa wake ndani ya Chama kuwa kudhani hivyo ni very naive, Maana hata kama hilo nyomi lote litaichagua Chadema, kama hakuna katiba mpya, tume huru ya uchaguzi ni kazi bure. Ndiyo maana ni ujinga mtupu kubeza cheche za struggle ambazo zitazaa moto wa mabadiliko ya kisiasa na kijamii nchini yatakayoisaidia hata Chadema yenyewe. Na mtu yeyote anayedharau kundi la wananchi ambalo liko "Enlightened" basi huyo hajielewi.
Na labda tu nimwambie Mbowe, kuwa pengine Nyomi la mikutano linamtia kiburi na kuamini kuwa Hakuna haja ya kuwaengage Watanzania wa mitandaoni. Asubiri aone kama CCM nao watapita katika kata hizohizo anazopita leo watu walewale waliojitokeza kumsikiliza kama hawatakwenda kuwasikiliza CCM pia. Ni Ujinga kudharau movement ya kundi dogo wenye uelewa ktk society
4. Akili za kuwaza ubunge, wingi wa ruzuku na kuendelea kuwa Mwenyekiti
Siyo siri, viongozi wengi ndani ya Chadema ya leo wanawaza ubunge tu mwaka 2025. Ni wachache sana miongoni mwao wanaowaza beyond ubunge. Na hii sauti ya waota ubunge ndani ya chama ni kubwa zaidi kuliko wale ambao Genuinely kabisa wanawaza mabadiliko ya kweli ya kimfumo nchini. Ukisikiliza kauli za viongozi wengi wa Chadema wako more worried na uchaguzi mkuu ujao, na ndiyo maana sasa wanazungumza habari za mabadiliko ya katiba kuelekea uchaguzi. Hoja zilezile ambazo miaka mitatu iliyopita walikuwa wakiwatukana ACT kwazo, ndiyo hizohizo leo wanazileta kwetu kama eti ni maono ya hekima ya chama. Kama hekima zinapatika ndani ya miaka mitatu, basi maana yake huko nyuma hakuwa na hekima anyway.
5. Mbowe kama Gatekeeper
It seems Mbowe, hayuko tayari kwa massive action nchini. Yaani anadhani kuwa CCM itatuleta mabadiliko kwa kuombwa, kwa kujitungia sheria za kujidhibiti yenyewe, kwa kuombwa kuleta katiba ya kujimaliza yenyewe. Na CCM kwa kutambua udhaifu wa Mwenyekiti katika mambo makuu matatu, Mosi anautaka uenyekiti tena, Pili ni muoga wa kupush hard na Tatu ana maslahi nchini ambayo wanaweza kumblackmail nayo basi wako Comfortable kuwa Mwamba ataruka na chopa, ataongea rousy speeches lakini itakapokuja muda ambao Watu wanataka kuraise up, basi Mwenyekiti atatumia machinery ya chama chake kujiweka pembeni na kuwaacha wanaotaka kuraise wakiwa marginalized. Ni jukumu la Wanachadema kukifanyia review chama chao waone kuwa The same Old Mwenyekiti ana kipya au sasa ni time ya Change ili kupush mabadiliko ya kweli nchini.
6. Mwisho
Hapa nataka nitoe tahadhari kwa viongozi wa Chadema ambao wameanza kuwa arrogant kwa kudhani Chadema is too big, na hawahitaji kuchangamana na watanzania wengine hasa wa mitandaoni.
Iko hivi, ni sisi wananchi wa Mitandaoni tuliopiga presha mpaka Mbowe akaachiwa. Ni sisi wananchi wengine wengi tu tusio na vyama lakini tuliokuwa tukiichangia Chadema katika operesheni zake. Ni sisi ambao tumeipa moral support, kwa kauli na matendo Na infact ni sisi ndiyo tunaolipa kodi ambayo leo hii Chadema wanapata ruzuku. Hii arrogance ya kijinga ambayo kwa bahati mbaya naona mnayo kuwa Walioko mitandaoni hawana dili, itakuja kuwatokea puani pale sentiment zitakapoanza kuwa negative kwenu na chama chenu. Kama mnabisha kaiulizeni ACT kwa nini haitoboi Tanganyika. Kawaulizeni negative content inawaathiri vipi!. Sasa msitufikishe huko.
Kama kweli Chadema ni chama cha wananchi, basi hiyo Taasisi ifanye kazi ya wananchi. Tungeshukuru sana kama Ingeshirikiana na Sauti ya Watanzani kuibana CCM zaidi, Kuitia kibano zaidi CCM kwenye suala la bandari na katiba. Kinyume cha hapo ni kuipa life support CCM na huo ni usaliti.
Nawasilisha!