Mbowe na ruzuku ya CHADEMA

Mbowe na ruzuku ya CHADEMA

Hahahaaa huu utafiti kiboko hako ka ofisi hapo ndio kana wafanyakazi 60 hadi 70?? Kwa kazi zipi?? Na wanajibanza wapi hapo au kule uwani maana vyumba vya hiyo guest sidhani kama vina accommodate watu wote hao...halafu ma.signatories wenu hapo si wawili wanaruhusiwa yan Mugabe taifa na katibu mkuu..sasa hapo kuna swali?? Halafu taja ofisi zenu zinazopokea ruzuku za kuendeshea ofisi hapa zitaje....hahahaa yajayo yanafurahisha
Mkuu safi sana. Hawa jamaa wanadhani kila mtu ni mjinga. Kwa kuongezea tu, hivi utafiti gani usio na hata mchanganuo? Kwanza watuambie hao wafanyakazi 70 wanalipwa kiasi gani kila mmoja (ingawa hana uhakika kama ni 60 au 70) ili tujue gharama kwa ujumla. Ofisi za kanda zinapewa kiasi gani. Hizo chaguzi anazozipigia mahesabu zinafanyikaga kila mwezi? Kwanini wanazihesabia kama vile ni matumizi ya kila mwezi. Mwisho, yaani hata CAG aliekagua mahesabu yao akakuta kuna ubadhirifu nae ni mjinga pia.

Yaani badala ya kumtetea Mwenyekiti wake, kaja kumdhalilisha na kumvua nguo kabisaa.
 
Hivi inakuwaje hujaelewa kamanda...hivi unataka nirudie maelezo yoooote...hahahah..naomba kamuulize CAG yale mabilioni yaliyofisadiwa aliyatoa wapi...mueleze pamoja na utaratibu wako wa ruzuku huu unaousema
mabilion gani wewe? Hivi katika ukaguzi uliopita cag si kaonyesha ccm ndio imepiga zaidi tena ni zaidi ya bil 11, hebu niambie ni chama kipi kimeifikia ccm ?
 
Nisingependamaneno hayo yatoke lumumba kwani ni kama kuitukana serekali yetu kuwa hawana vyombo vya kichunguzi miaka yote anapokula hizo ruzuku ambazo ni kodi zetu.
CAG naye hajui kitu hadi lumumba wamshitaki Mbowe?? Poleni. Nadhani tutafute tuhuma zingine zenye mashiko sio hizi
Hivi wewe hujasoma ripoti ya CAG au? Ndo maana wenzio wanang'ang'ana na ile 1.5 trillion ili madudu yao yasiongelewe. Lakini CAG kafichua kila kitu. Ufisadi mkubwa CDM kwenye fedha za ruzuku.
 
Kwenye management kujua mtu mwizi ofisini ni rahisi njia moja kumjua ni kungangania ofisi.Haendi hata likizo ili mwingine ashike Na mchoyo kufundisha wengine kazi aliyonayo ili aendelee kuonekana yeye ndie anajua!! Mbowe ana dalili zote za mwizi yeye ndie star chadema hataki kuondoka anataka kuatamia madudu yake anajua akija mwingine atayafukunua Na yeye aweza ishia jela.Miaka 20 Na zaidi aliyokaa yatosha chadema mfungasheni virago aingie mwingine Ruzuku hata Mimi pesa yangu ya Kodi imo kwenye ruzuku ya chadema ndio maana Nina hoji napendab kuwaambia chadema Mbowe apishe mtu mwingine.Wezi wa Ruzuku Na Mbowe wanataka kuendelea kuatamia madudu yao ya ulaji wa ruzuku Na fedha za wafadhili.Anataka kuatamia madudu yeye Na genge lake.Chadema nawashauri ipigeni chini kamati kuu yote wekeni wapya Na kurugenzi zote za chadema wekeni wapya
 
Last edited:
Nenda

Kaulize ikulu ina wafanyakazi wangapi ndio utajua kama wengine wananing'inia kwenye mapangaboi au kwenye swichi za umeme
Ofisini za raisi ziko Kila mkoa Na ikulu ndogo ziko Kila mkoa.Ofisi za makao makuu chadema ziko Kila mkoa?
 
Kwenye management kujua mtu mwizi ofisini ni rahisi njia moja kumjua ni kungangania ofisi.Haendi hata likizo ili mwingine ashike Na mchoyo kufundisha wengine kazi aliyonayo ili aendelee kuonekana yeye ndie anajua!! Mbowe ana dalili zote za mwizi yeye ndie star chadema hataki kuondoka anataka kuatamia madudu yake anajua akija mwingine atayafukunua Na yeye aweza ishia jela.Miaka 20 Na zaidi aliyokaa yatosha chadema mfungasheni virago aingie mwingine Ruzuku hata Mimi pesa yangu ya Kodi imo kwenye ruzuku ya chadema ndio maana Nina hoji napendab kuwaambia chadema Mbowe apishe mtu mwingine.Wezi wa Ruzuku Na Mbowe wanataka kuendelea kuatamia madudu yao ya ulaji wa ruzuku Na fedha za wafadhili.Anataka kuatamia madudu yeye Na genge lake.Chadema nawashauri ipigeni chini kamati kuu yote wekeni wapya Na kurugenzi zote za chadema wekeni wapya
Hapa kamanda unapigia mbuzi gitaa..hivi unawezaje kumtenganisha Mbowe na chadema..chama cha baba mkwe...??? Mtei mwenye chama amesisitiza mkwe wake aendelee kusimamia chama vizuri asisikilize maneno ya watu..aendelee kupigania demokrasia..hahahaha...chama kinaonekana kama kitega uchumi cha Mtei eti...nahisi tu..na wengine wanafuatia kwa nyuma..sasa utawapigaje chini
 
Hivi wewe hujasoma ripoti ya CAG au? Ndo maana wenzio wanang'ang'ana na ile 1.5 trillion ili madudu yao yasiongelewe. Lakini CAG kafichua kila kitu. Ufisadi mkubwa CDM kwenye fedha za ruzuku.

Kwa hiyo ni CDM pekee ndo walionekana wabovu?? Nauliza tu kwani sitaki kumsikia mtu anamuona mkuu hana akili. Ninavyomjua asingelikubali waendelee kula kodi zetu
 
Mbowe ni mbabe wenu.ni sawa na kuchapiwa mkeo na mwanamme anaekuchapia mkeo unamjua halafu huwez kumfanya lolote. Utabaki kulialia tu. Km wengi mlivojitoa ufahamu kupiga porojo zilezile kila siku, ruzuku ruzuku mbowe mbowe.
 
Hahahaha ubwabwa mtupu..wewe umetuandikia utaratibu wa kawaida wa kifedha ambao kila chama kuwa kinatakiwa kiufuate kisheria...kwani unadhani sehemu zote ambazo ulaji unatokea huwa hakuna utaratibu wa kifedha..? Je umeshaona kuna sehemu yoyote ambayo mlaji anawekewa hela mijakwamoja kwenye akaunti...???? Usitudanganye kamanda hapa...pesa inaliwaga kwa kutumia taratibu hizo hizo unazosema..kunakuwa na aidha malipo hewa ambayo hayana ushahidi, ama kuongeza bei katika huduma mbalimbali zinazotolewa kwa chama, kuobgeza bei kwenye manunuzi mbalimbali na hapa ndipo pesa inapigwa sana..na ndio maana msema kweli anakuwa CAG..Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambaye ana vigezo vya kuweza kugundua pesa kiasi gani ambayo imepigwa..na ndio maana CAG alugundua ufisadi mkubwa ndani ya chama wa mabilioni...hivi unadhani hili alikaa na kubuni mahesabu au...????????be careful usidanganye umma kamanda..kuwa mzalendo
Wambea mna mahangaiko yasiyokoma.mmekuwa waganga wapiga ramli.
 
Haya tukubali wananchi wanatuhumu...lakini hata CAG naye anatuhumu kamanda....?????? Hata wale wabunge wanotoka chadema nao unawaweka kundi lipi ...la CAG au la wale wanaotuhumu tuu...?

Hii ndio raha ya demokrasia ila huwa mnaharibu mnapotumia na jeshi la polisi kujibu hizi hoja.

Sasa twende pamoja, ni kweli CAG yeye hatumuhumu kwani ana uwezo wa kuchunguza, cdm hapa wamejitahidi kufanunua kwa kiwango chao wangalau kwa sasa. Kwa mujibu wa CAG ccm ina 12b ya matumizi ya mashaka na hakuna mchanganuo wowote mpaka sasa.

Kuna 1.5t matumizi ya mashaka ya serekali mpaka sasa. Serekali ilijaribu kutolea ufafanuzi aibu ndio ikawa kubwa zaidi. Na sasa wameamua kukaa kimya na kujitahidi kutangaza za cdm ili kuitumia kama kinga.

Twende kwenye hawa wanaohama cdm, wengine wanasema vyeo vinatolewa kwa rushwa ya ngono. Kuna taasisi yoyote inayoongozwa na muafrika isiyo na tuhuma za ngono? Nenda jeshini, nenda kwa wahadhiri wa vyuo, nenda kwa viongozi wa dini nk. Kuna kundi lenye sifa ya kunyooshea yoyote kidole kwenye hili?. Muafrika na ngono ni kama uji na mgonjwa.

Wengine wanaohama cdm wanasema kuna ubadhirifu na hakuna ruhusa ya kuhoji ruzuku na wanahamia ccm ambapo ni safi! Je ripoti ya ccm ya ubadhirifu wa mali za umma kuna hatua yoyote ya msingi zaidi ya mwenyekiti wa kamati kuzawadia ukatibu mkuu? Ile mikwara ambayo katibu mkuu wa ccm alisema atachukua amefikia wapi? Kuna mahali popote wanaccm wamehoji hizo 12b zilivyotumika? Mnapocheza siasa chafu za kutumia vyombo vya dola huwa mnadhani mmejificha sana na wananchi ni wajinga hawajui lolote bali wanategemea propaganda zenu kujua ukweli ni upi na uongo ni upi?
 
Mleta mada mwongo kwanza hajui idadi ya wafanyakazi wa makao makuu anasema wako kati ya 60 au 70!!!!! halafu wote tunajua ofisi ya makao makuu ya chadema pale waweza kaa ofisini watu 60 au 70 kwenye kale kajumba ? Uongo mtupu.Aweke majina ya hao wafanyakazi Na kazi zao.Kile kiofisi huwezi weka wafanyakazi 60 au 70.uongo.Wezi wa ruzuku nyie.M Mbowe akiondoka madudu mengi yatagundulika
ulishawahi ona simba ikichagulia kocha yanga!? punga wewe! madudu yapo kwenye ripoti ya Bashir mbona huzungumzii? bwabwa kabisa wewe! kutwa kucha mbowe akakuoe basi
 
Mkiambiwa hiyo ni saccos mnabisha
Mwenyekiti kajiweka kwenye list ya signatories
Hakuna muhasibu mkuu wa chama?
Ukiangalia walivyojipanga utajua kabisa ni genge la mafisadi
Mbowe~Mwenyekiti
Mashinji~Katibu
Mnyika~NK mkuu
Mrema~Kibaraka wa mbowe
Hapo kuna nani anaeweza kukataa amri ya mbowe.
Unaposema pesa inatumika kwa idhini ya kamati kuu unashangaza!
Ni kikao kipi kiliamua Mbowe alipwe kwa kukiuzia chama fuso mbili chakavu kwa milioni 400?
Ni kikao kipi kiliamua mbowe alipwe bilioni mbili alizozikopesha kwa chama?(hii ni query kutoka kwa CAG,mbowe kajilipa Bilioni mbili bila ya maandishi yoyote)
Sasa hivi vijana wa Mbowe,mnatumika kumuokoa bosi wenu,bila kujali hiyo ruzuku anayotafuna inachangiwa na wengi
 
Kumekuwa na maneno mengi na tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe kuwa anatafuna pesa za Ruzuku za chama,

Tuhuma hizo zimekuwa zikiendelea kila mara na sasa zikichagizwa zaidi na wanaohama kutoka Chadema kwenda kwenye vyama vingine hususani Ccm,

Yafuatayo ni matokeo ya Utafiti;

*NAMNA FEDHA INAVYOTOKA SERIKALINI MPAKA KUFIKA KWENYE AKAUNTI YA CHADEMA*

Serikali hutoa ruzuku kwa Chadema kila mwezi,

Fedha ikitoka Hazina (Serikalini) hupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa,

Msajili huiingiza pesa hiyo kwenye Akaunti ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (Board of Trustee Bank Account),

Bodi ya Wadhamini wa Chadema ndio hupeleka pesa hiyo kwenye Akaunti ya Chama tayari kwa matumizi. Pesa haiingizwi kwenye Akaunti binafsi ya kiongozi yeyote wa Chadema wala mwanachama wa Chadema. Huingizwa kwenye akaunti ya chama,

*NAMNA PESA INAVYOTOKA KWENYE AKAUNTI YA CHADEMA*

Wapo Watia Saini Wanne (4 Signatories) kwenye Akaunti ya Chadema Taifa. Ambapo watu wawili kati ya hao Wanne wanaruhusiwa kusaini Hundi (cheque) kwa ajili ya kufanya Malipo,

Watu hao kwa nafasi zao ni;
i) Mwenyekiti wa Chadema Taifa
ii) Katibu Mkuu wa Chadema Taifa
iii) Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara
iv) Mkurugenzi wa Fedha

Pesa yoyote haiwezi kutoka kwenye Akaunti ya Chadema mpaka Wawili kati ya hao wanne Watie Saini,

*WAKATI GANI PESA INATOKA KWENYE AKAUNTI*

Pesa yeyote ya Chadema haiwezi kutoka kwenye akaunti kama haijathibitishwa na Kamati Kuu,

Kamati Kuu ya Chadema tayari ilishaidhinisha matumizi ya kila mwezi ya chama (Normal Operation expenditures),

Lakini kama kuna matumizi mengine ya ziada ama dharura (mfano Uchaguzi wa marudio, kesi, matibabu), lazima Kamati Kuu ya Chadema ikae, ipime umuhimu wa kufanya matumizi ndio iidhinishe au ikatae matumizi hayo,

Sio Mbowe aidhinishe, sio Mashinji aidhinishe wala yeyote yule. Ni Kamati Kuu.

*CHADEMA INAPELEKA WAPI FEDHA YA RUZUKU WANAZOPATA KILA MWEZI*

i) Zipo fedha ambazo hutumika Makao Makuu kulipa Mishahara na Posho,

Chadema inao wafanyakazi kati ya 60 hadi 70 ambao wapo Makao Makuu ama hulipwa moja kwa moja toka Makao Makuu kuanzia nafasi za Wahudumu wa ofisi, Walinzi mpaka Mwenyekiti wa Taifa,

Mwenyekiti wa Taifa na wafanyakazi wengine walioko Makao Makuu ambao ni wanufaika wa Serikali (yaani wanaolipwa mishahara kutoka Serikalini), hawalipwi mishahara na Chadema,

Freeman Mbowe _(Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Mbunge wa Hai)_, John Mnyika _(Naibu Katibu Mkuu - Bara na Mbunge wa Kibamba)_, hawa wawili ni mfano wa wasiolipwa mishahara kwa sababu ni wanufaika wa Serikali. Badala yake hulipwa posho pale wanapotumwa na chama kwenda kufanya shughuli maalum mikoani au nje ya nchi,

ii) Fedha nyingine hupelekwa kwenye Ofisi 10 za Kanda (Kanda Mbili zipo Tanzania Visiwani na Kanda 8 zipo Tanzania Bara)

Fedha hizo kwenye Kanda hutumika kulipa Mishahara ya Wafanyakazi, Posho na Ruzuku kwenye Majimbo yote 264 ya Uchaguzi,

iii) Kuna fedha hutumika kushughulikia kesi mbalimbali za Viongozi na Wanachama wa Chadema. Fedha hizo hutumika kuwasafirisha Mawakili na kuwalipa Posho.

iv) Matumizi ya dharura ambayo hayaepukiki. Mfano Chaguzi za Marudio za Ubunge (ambazo hugharimu kati ya Milioni 100 hadi 120), chaguzi za Madiwani, gharama za Matibabu na Vifaa vya Uenezi wa Chama.

Kwa kuangali mchanganuo huo hapo juu, utaona kabisa Ruzuku ya Milioni 236 wanayopata Chadema kwa mwezi, haitoshi kwa matumizi yote ya Chama kwa mwezi.

Kitendo cha kumtuhumu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe ama kiongozi mwingine yeyote kuwa anakula fedha za Ruzuku, itabaki kuwa ni propaganda za kisiasa ambazo hazina ukweli wowote,

Na ikumbukwe, hakuna kiongozi yeyote anayeweza kutoa pesa ya ruzuku kutoka kwenye akaunti ya chama mpaka watia saini wawili wasaini hundi ndipo pesa itoke,

Mbowe anakulaje fedha ya ruzuku ya chama???

*Utafiti hupingwa kwa Utafiti. Nasubiri utafiti utakaoupinga utafiti huu.*

Asanteni
OK! HIyo ni nadhalia ya matuizi. Tuelezee uhalisia wake uko vipi? Mashtaka ya hao jamaa wanaohama kila kuchao, ilikuwa ni uhalisia wa matumizi, siyo nadhalia hii uliyoweka hapa. Hebu sikiliza tena clip hii:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom