Mbowe na ruzuku ya CHADEMA

Mbowe na ruzuku ya CHADEMA

Nisingependamaneno hayo yatoke lumumba kwani ni kama kuitukana serekali yetu kuwa hawana vyombo vya kichunguzi miaka yote anapokula hizo ruzuku ambazo ni kodi zetu.
CAG naye hajui kitu hadi lumumba wamshitaki Mbowe?? Poleni. Nadhani tutafute tuhuma zingine zenye mashiko sio hizi
 
Mleta mada mwongo kwanza hajui idadi ya wafanyakazi wa makao makuu anasema wako kati ya 60 au 70!!!!! halafu wote tunajua ofisi ya makao makuu ya chadema pale waweza kaa ofisini watu 60 au 70 kwenye kale kajumba ? Uongo mtupu.Aweke majina ya hao wafanyakazi Na kazi zao.Kile kiofisi huwezi weka wafanyakazi 60 au 70.uongo.Wezi wa ruzuku nyie.M Mbowe akiondoka madudu mengi yatagundulika
Naunga mkonohoja yako..vile vichumba vitatu viwe na wafanyakazi sabini..duuuuu...wanakaa chini labda wotebila meza wala kiti...hivi ndivyo ambavyo wanaanzaga kuiba mahela...kwa kutoa data za uongo......hahahahah
 
Tuwwkeeni hapa mchanganuo wote wa matumizi ya ruzuku kila mwezi tujiridhishe kama kweli pesa zimetumika vizuri ........
Peleka ombi hili chama cha kijani. Wakikupa, njoo nikuoneshe mchanganuo wa CDM
 
Hapa kuna amchanganuo gani umeuelewa...kweli mmezoea kudanganya watanzania..this time inakula kwenu..angaliajinsi watu wanavyotimkia ccm...hivi unadhani wote hawana akili...hahahahaha wajinga ndio waliwaooooo
mkuu.. basi tuache hayo weka na wewe kwenye chama chako cha ccm tujue mwanzo hadi mwisho zinavyotumika!
 
Ni siasa rahisi sana Kumtuhumu Mbowe kwamba anahujumu ruzuku ya CHADEMA, wajinga tu (ambao wengi ni CCM) ndo hutumia siasa ya namna hii wakiamini ndo itaimaliza CHADEMA na kufanya CCM ionekane bora,

Cha kushangaza zaidi unakuta anaesimamia hiyo hoja ni kijana anaedai kwamba ana elimu ya shahada na kuendelea, wengine ni wazee kabisa mfano POLEPOLE.
Haya tukubali wananchi wanatuhumu...lakini hata CAG naye anatuhumu kamanda....?????? Hata wale wabunge wanotoka chadema nao unawaweka kundi lipi ...la CAG au la wale wanaotuhumu tuu...?
 
YAANI SIGNATORIES NI MEMBERS WA KAMATI KUU TU?
 
Nenda
Naunga mkonohoja yako..vile vichumba vitatu viwe na wafanyakazi sabini..duuuuu...wanakaa chini labda wotebila meza wala kiti...hivi ndivyo ambavyo wanaanzaga kuiba mahela...kwa kutoa data za uongo......hahahahah
Kaulize ikulu ina wafanyakazi wangapi ndio utajua kama wengine wananing'inia kwenye mapangaboi au kwenye swichi za umeme
 
Kumekuwa na maneno mengi na tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe kuwa anatafuna pesa za Ruzuku za chama,

Tuhuma hizo zimekuwa zikiendelea kila mara na sasa zikichagizwa zaidi na wanaohama kutoka Chadema kwenda kwenye vyama vingine hususani Ccm,

Yafuatayo ni matokeo ya Utafiti;

*NAMNA FEDHA INAVYOTOKA SERIKALINI MPAKA KUFIKA KWENYE AKAUNTI YA CHADEMA*

Serikali hutoa ruzuku kwa Chadema kila mwezi,

Fedha ikitoka Hazina (Serikalini) hupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa,

Msajili huiingiza pesa hiyo kwenye Akaunti ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (Board of Trustee Bank Account),

Bodi ya Wadhamini wa Chadema ndio hupeleka pesa hiyo kwenye Akaunti ya Chama tayari kwa matumizi. Pesa haiingizwi kwenye Akaunti binafsi ya kiongozi yeyote wa Chadema wala mwanachama wa Chadema. Huingizwa kwenye akaunti ya chama,

*NAMNA PESA INAVYOTOKA KWENYE AKAUNTI YA CHADEMA*

Wapo Watia Saini Wanne (4 Signatories) kwenye Akaunti ya Chadema Taifa. Ambapo watu wawili kati ya hao Wanne wanaruhusiwa kusaini Hundi (cheque) kwa ajili ya kufanya Malipo,

Watu hao kwa nafasi zao ni;
i) Mwenyekiti wa Chadema Taifa
ii) Katibu Mkuu wa Chadema Taifa
iii) Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara
iv) Mkurugenzi wa Fedha

Pesa yoyote haiwezi kutoka kwenye Akaunti ya Chadema mpaka Wawili kati ya hao wanne Watie Saini,

*WAKATI GANI PESA INATOKA KWENYE AKAUNTI*

Pesa yeyote ya Chadema haiwezi kutoka kwenye akaunti kama haijathibitishwa na Kamati Kuu,

Kamati Kuu ya Chadema tayari ilishaidhinisha matumizi ya kila mwezi ya chama (Normal Operation expenditures),

Lakini kama kuna matumizi mengine ya ziada ama dharura (mfano Uchaguzi wa marudio, kesi, matibabu), lazima Kamati Kuu ya Chadema ikae, ipime umuhimu wa kufanya matumizi ndio iidhinishe au ikatae matumizi hayo,

Sio Mbowe aidhinishe, sio Mashinji aidhinishe wala yeyote yule. Ni Kamati Kuu.

*CHADEMA INAPELEKA WAPI FEDHA YA RUZUKU WANAZOPATA KILA MWEZI*

i) Zipo fedha ambazo hutumika Makao Makuu kulipa Mishahara na Posho,

Chadema inao wafanyakazi kati ya 60 hadi 70 ambao wapo Makao Makuu ama hulipwa moja kwa moja toka Makao Makuu kuanzia nafasi za Wahudumu wa ofisi, Walinzi mpaka Mwenyekiti wa Taifa,

Mwenyekiti wa Taifa na wafanyakazi wengine walioko Makao Makuu ambao ni wanufaika wa Serikali (yaani wanaolipwa mishahara kutoka Serikalini), hawalipwi mishahara na Chadema,

Freeman Mbowe _(Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Mbunge wa Hai)_, John Mnyika _(Naibu Katibu Mkuu - Bara na Mbunge wa Kibamba)_, hawa wawili ni mfano wa wasiolipwa mishahara kwa sababu ni wanufaika wa Serikali. Badala yake hulipwa posho pale wanapotumwa na chama kwenda kufanya shughuli maalum mikoani au nje ya nchi,

ii) Fedha nyingine hupelekwa kwenye Ofisi 10 za Kanda (Kanda Mbili zipo Tanzania Visiwani na Kanda 8 zipo Tanzania Bara)

Fedha hizo kwenye Kanda hutumika kulipa Mishahara ya Wafanyakazi, Posho na Ruzuku kwenye Majimbo yote 264 ya Uchaguzi,

iii) Kuna fedha hutumika kushughulikia kesi mbalimbali za Viongozi na Wanachama wa Chadema. Fedha hizo hutumika kuwasafirisha Mawakili na kuwalipa Posho.

iv) Matumizi ya dharura ambayo hayaepukiki. Mfano Chaguzi za Marudio za Ubunge (ambazo hugharimu kati ya Milioni 100 hadi 120), chaguzi za Madiwani, gharama za Matibabu na Vifaa vya Uenezi wa Chama.

Kwa kuangali mchanganuo huo hapo juu, utaona kabisa Ruzuku ya Milioni 236 wanayopata Chadema kwa mwezi, haitoshi kwa matumizi yote ya Chama kwa mwezi.

Kitendo cha kumtuhumu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe ama kiongozi mwingine yeyote kuwa anakula fedha za Ruzuku, itabaki kuwa ni propaganda za kisiasa ambazo hazina ukweli wowote,

Na ikumbukwe, hakuna kiongozi yeyote anayeweza kutoa pesa ya ruzuku kutoka kwenye akaunti ya chama mpaka watia saini wawili wasaini hundi ndipo pesa itoke,

Mbowe anakulaje fedha ya ruzuku ya chama???

*Utafiti hupingwa kwa Utafiti. Nasubiri utafiti utakaoupinga utafiti huu.*

Asanteni
Tumia jina lako halisi kama unaamini unayoyazungumza. Wewe ndio nyoka wake katika ulaji huu. Acha usanii
 
mkuu.. basi tuache hayo weka na wewe kwenye chama chako cha ccm tujue mwanzo hadi mwisho zinavyotumika!
Nakwambia utaratibu wa kifedha upo kila sehemu...hata nyumbani kwako..tatizo watu wanatumia taratibu hizohizo kupiga mafweza..wewe..ndio maana kuna wataalam wa kukagua matumizi ya fedha..CAG.umeelewa..kama hujaelewa tena uliza swali..
 
Tumia jina lako halisi kama unaamini unayoyazungumza. Wewe ndio nyoka wake katika ulaji huu. Acha usanii
Hahahaha wapashe hao.....jamaa kapewa buku saba kuja kuleta maelezo ya kitoto hapa..anadhani watu ni wajinga
 
Nakwambia utaratibu wa kifedha upo kila sehemu...hata nyumbani kwako..tatizo watu wanatumia taratibu hizohizo kupiga mafweza..wewe..ndio maana kuna wataalam wa kukagua matumizi ya fedha..CAG.umeelewa..kama hujaelewa tena uliza swali..
mbona hujaweka? Umekuja na porojo zilezile, yaana unataka kuniaminisha utaratibu wa matumizi ya ruzuku unafanana!? Mfano matumizi yangu na yako yanafanana!?
 
mbona hujaweka? Umekuja na porojo zilezile, yaana unataka kuniaminisha utaratibu wa matumizi ya ruzuku unafanana!? Mfano matumizi yangu na yako yanafanana!?
Hivi inakuwaje hujaelewa kamanda...hivi unataka nirudie maelezo yoooote...hahahah..naomba kamuulize CAG yale mabilioni yaliyofisadiwa aliyatoa wapi...mueleze pamoja na utaratibu wako wa ruzuku huu unaousema
 
Hivi Chadema ni Mbowe tu.hakuna wafuasi na wanachama nchi nzima?.
 
Nenda

Kaulize ikulu ina wafanyakazi wangapi ndio utajua kama wengine wananing'inia kwenye mapangaboi au kwenye swichi za umeme
Hahahaha pale ufipa ndio ikulu sio...haya majibu ndio yanatufanya hatupigi hatua za maendeo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom