Mbowe: Mwulizeni zitto niliko mtoa

chaboo

Member
Dec 11, 2013
78
0
MWENYETI wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) Freeman
Mbowe, amewataka wanachama wa
chama hicho wamuulize Mbunge Kigoma
Kaskazini Zitto Kabwe wapi alikomtoa
hadi kufikia ngazi na hadhi aliyonayo
sasa katika medani ya siasa nchini.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana katika
kongamano la miaka 52 ya Uhuru wa
Tanzania Bara, lililoandaliwa na Umoja
wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Chaso)
kwa kushirikiana na Baraza la Vijana la
Chama hicho (BAVICHA)
Katika kongamano hilo lililofanyika
katika Hoteli ya Land Mark, Mbowe
ambaye alianza kwa kutaja historia yake
kama mwasisi kijana wa CHADEMA na
mwenyekiti wa kwanza, alisema mwaka
2003 akiwa katika harakati za kukijenga
chama, alipita katika vyuo mbalimbali ili
kupata vijana wasomi wajiunge na
CHADEMA na ndipo alipompata Zitto,
akiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
“Nikiwa katika harakati zangu za
kukijenga chama, nilipita Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam …nilibahatika kuwapata
kina John Mrema, Halima Mdee, Zitto
Kabwe, John Mnyika wakiwa viongozi
ambao walipenda siasa ya mabadiliko,
nami nikaondoka nao bila ya kusita,”
alisema.
Alisema nia ya kuwachukua vijana hao ni
kujenga chama kama taasisi ili kisonge
mbele tofauti na ilivyo sasa na siyo
kujenga jina la mtu kama watu
wanavyotaka iwe au wanavyodhani.
Mbowe alisema akiwa na vijana hao
pamoja na viongozi wengine, walifanya
kazi kama timu ili kuhakikisha
wanakiingiza chama hicho Ikulu,
akiamini kuwa asingeliweza peke yake
kukipeleka mbele chama hicho.
Aliwataja viongozi aliowachukua kutoka
katika vyama vingine vya siasa kuwa ni
pamoja na Mkurugezi wa Fedha wa
chama hicho, Antony Komu, Tundu
Lissu, Mabere Marando ambao walitoka
NCCR – Mageuzi.
Wengine ni Godbless Lema, Saidi Arfi na
Mchungaji Peter Msigwa ambao
walikuwa TLP na Ezekia Wenje aliyetoka
Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwa
mwenyekiti wa tawi moja la chama hicho
huku Mwanza.
Alisema safari ya kukijenga chama sio
lelemama kwani ni sawa na treni
inayotoka Dar es Salaam kuelekekea
Kigoma huku akiamini wote watafiki,
lakini imekuwa tofauti kwani wapo
walioshuka njiani.
“Safari yetu ya Kigoma toka Dar es
Salaam ilikuwa ndefu sana … wapo
walioshuka katika kituo cha kwanza tu
Pugu, wengine Morogogo na vituo
vingine vilivyofuata na kupata vilevile
lakini tutafika tu,” alisema.
Akitoa historia fupi ya maisha yake
katika siasa, Mbowe alisema aliingia
akiwa kijana mdogo muasisi ambaye
alipata nafasi ya kukiongoza chama kama
mwenyekiti wa kwanza wa vijana,
baadaye kupata nafasi mbalimbali
ikiwamo uenyekiti.
Alisema aliingia katika chama hicho na
kuchanguliwa kuwa kiongozi, lengo
likiwa kufanya mabadiliko kwa vitendo
na si kwenda kupata faida kama watu
wengine wanavyofikiria.
“Lakini nilifanya kazi yangu ya kuijenga
CHADEMA hatua kwa hatua kwa maana
nyingine nimefanya kazi ya chama kwa
miaka 23 sasa bila kulipwa mshahara
wowote kwa sababu mimi ni
mfanyabiashara,” alisema.
Alisema chama akitatoa maamuzi ya
kumwonea mtu yeyote bali
kitamhukumu mtu kutokana na makosa
yake.
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,153
1,250
As if yeye kadondoka toka mbinguni!!!!
Yeye kalelewa na nani??!!!
Role models hana??!!!
Kazaliwa anajua siasa sio??!!!


Ni aina gani ya kiongozi sasa anayetaka historia ziwe sehemu ya maamuzi???!!!!Why now kutoa hiyo taarifa???!!!Uswahilini tunaita kusimanga huku!!!!
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
91,295
2,000
As if yeye kadondoka toka mbinguni!!!!
Yeye kalelewa na nani??!!!
Role models hana??!!!
Kazaliwa anajua siasa sio??!!!


Ni aina gani ya kiongozi sasa anayetaka historia ziwe sehemu ya maamuzi???!!!!Why now kutoa hiyo taarifa???!!!Uswahilini tunaita kusimanga huku!!!!

kamanda mapovu ya nini tena , si kuna wanaojidai chama kina damu yao ? Ufafanuzi ndiyo huo , kumbe aliokotwa njiani tu !
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
12,759
2,000
WASIONE VYAELEA VILIUNDWA VIKAPANGWA VIKAPANGIKA,WENGI TUNAKUFAHAMU KAMANDA MBOWE KWA KUKAZA BUTI,SONGA MBELE KAMANDA,ILA MTOTO AKiNYEA MKONO WAKO UTAUKATA?
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,891
2,000
As if yeye kadondoka toka mbinguni!!!!
Yeye kalelewa na nani??!!!
Role models hana??!!!
Kazaliwa anajua siasa sio??!!!


Ni aina gani ya kiongozi sasa anayetaka historia ziwe sehemu ya maamuzi???!!!!Why now kutoa hiyo taarifa???!!!Uswahilini tunaita kusimanga huku!!!!
Sana mkuu. Ni vema angejieleza yeye kalelewa na nani na nani kamfanya awe mwenyekiti wa chadema
 

Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,403
2,000
Nimependa sana mfano wa train, ni kweli wengi watashuka wa wengi watapanda. Mpaka ifikie Kigoma train imejaa.
 

Character X

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
331
500
Good job Mr. Chairman, uongozi ni jukumu gumu sana, uongozi wowote!!.

Siwengi wanaoweza kuelewa hili. They say it takes a leader to understand one!

Lakini hekima ikuongoze pia., mimi naamini unaumia yanapotokea haya yanayotokea, lakini huenda unadhani hakuna namna inabidi yaende hivyo. Well, binafsi nadhani kwanafasi yako unaweza kuisimamia HAKI. Na kwamba, sio tu haki itendeke katika hili, laki haki IONEKANE ikitendeka katika hili,
Mh. Mwenyekiti bado upo umuhimu wakuhakikisha maamuzi yanafanyika juu ya taarifa zilizothibitishwa pasipo shaka kabisa lakini pia kwanidhamu na heshima ya utu na nafasi ya anaye kabiliwa na shutuma hizi, ikifika wakati sahihi taratibu sahihi zifuatwe kutoa adhabu yenye lengo la kufundisha na si kukomoa.

Katika hili mh. Mwenyekiti unayo nafasi kubwa! Na hapa ndipo uwezo Wako kiuongozi unapo onekana na wengi.,
Nafasi yako inaweza kuwa nafasi pekee ya kimbilio kwa wote wanaohisi ama kutendewa isivyo haki, ama kuadhibiwa kwa haki kabisa ila wakatafuta huruma ilikupunguza adhabu ambayo pengine ni kali sana.,

wewe ndio nafasi hiyo ya hekima na huruma.

Mheshimiwa,
Mungu akutangulie.
 

majebere

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
4,786
2,000
Mzee slaa alisha sema mjadala umefungwa lakini naona wao wenyewe wanauendeleza. Zitto ametulia kimya bila kumsema mtu vibaya,na yeye akifunguka si itakua mvurugano.hawa jamaa hekima imewapita kushoto kabisa.
 

Njilembera

JF-Expert Member
May 10, 2008
1,496
2,000
Miaka 23 ya kula hela za chama halafu anasema hajalipwa mshahara,hili jamaa jizi kweli

Majebebere: 'kama nimesema kweli kwa nini unanipiga, kama nimesema uongo weka ushuhuda wako mbele..." lau tu kama tungeweza kutumia kauli yako hii tukakushtaki au akakkustaki - ungefilisiwa sijui mkubwa/mdogo wangu.... kwa nini unafikiri mfanyabiashara ni mweizi. tukishaanza hivi nchi haitaendelea, nchi itaendelezwa tu na wanaoweza kukutanisha walaji na wazalishaji na hawa ni wafanyabiashara penda usipende. Na hatuwezi wote kuwa wanabiashara na wala wazalishaji ila wote ni walaji!
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,153
1,250
kamanda mapovu ya nini tena , si kuna wanaojidai chama kina damu yao ? Ufafanuzi ndiyo huo , kumbe aliokotwa njiani tu !
Kama povu mwaga chooni mkuu usipoteze nalo muda!!!!

Maisha ni kuelekezana,kukosoana,kusaidiana na kama hayo " nurturing and mentoring" kama ni historia haiwezi kuanza na yeye kwenda chuo! !!!!!!

Yeye kaanzia wapi mkuu! !!??
 

magohe

JF-Expert Member
May 21, 2011
728
195
nilishasema tangu zamani fadhira mpe mbuzi ,mswahili anakaraha zake.

jitu wamelitoa sigimbi leo hii anavimbisha makalio kwa kudhania yeye ni bora kumbe wapo zaidi yake.

Haya yananikumbusha Dr. aman warid kabouru alitoka zake marekani na suspender tu kapuku asokuwa na mbele wala nyuma kaja kapata ujira na umaarufu kupitia cdm kajiona mjanja.

ilifikia hatua hata wakathubutu kumuomba akiwakilishe chama ktk ngazi ya urais -2005 akatoka mbio bila kugeuka nyuma bila sababu za msingi.

siku zote ukifanya kazi na mswahili muangalie kwa macho yote mawili.

si watu hawa bali ni kinyaa tupu.

mbowe hekima tu ndo itakufanya uweze kuishi na hawa kunguru .

hawafugiki kaka hata uweke upendo wa namna gani.

hekima tu ikuongoze uweze kufikia malengo ndani ya chama kwa ajili ya taifa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom