Mbowe mtazame kwa umakini sana Lissu

Mbowe mtazame kwa umakini sana Lissu

Ibambasi wewe ni kada wa ccm chama marehemu,uchochezi wako mrudishie alokutuma.
 
Kwako Mwenyekiti wetu Mbowe, F.A. (MB-KUB)

Tunatambua wazi nguvu na jitihada na juhudi zako katika kuijenga CHADEMA licha ya msukosuko mkubwa wa mwaka 2015 pale Katibu Mkuu, Dr. W.P. Slaa alipojiondoa ndani ya chama kufuatia uamuzi wako wewe kumkaribisha ndani ya chama na kumpa nafasi ya ugombea urais, bila kushindanishwa, target yetu kuu dhidi ya vita ya ufisadi, Edward N. Lowassa. Yaliyotokea ni historia na hatuna haja ya kurejea tena. Licha ya UKUTA kuanguka vibaya sana pamoja na uimara wa Rais Magufuli katika kuiongoza nchi na chama chake (wahasimu wetu CCM), bado chini yako CHADEMA inasonga tu. Tunatambua kipindi kigumu ulichopitia cha kutoweka kwa msaidizi wako mkuu, Ben Saanane bila taarifa, lakini bado uko imara kabisa. Tunatambua uhsuishwaji wako na biashara ya mihadarati, ukwepaji kodi na kulipa mapango mpaka kuvunjwa kwa kitegauchumi chako hapo Bilcanas na madai ya kodi ya TRA. bado uko imara. Hiyo ni kwa uchache misukosuko unayopitia.

Sasa Ndugu Mwenyekiti kuna changamoto kubwa sisi makamanda tunaokijua chama, inakuja mbele yako. Nayo si nyingine bali ni uwepo wa Tundu A. Lissu. Tunatambua kuwa huyu ulimpatia nafasi ya kuja ndani ya chama na kuweza kugomeba ubunge wa Singida Mashariki mwaka 2010 nakuweza kuteteta tena mwaka 2015. Huyu jamaa si wa kumpuuza hata kidogo. Wote tu mashahidi jinsi alivyoweza kupata nafasiya kuwa Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika licha ya kupitia vikwazo na misukosuko mingi sana. Historia yake na yako zinafanana kwa kiasi fulani ingawa yake ina uzito zaidi hasa ukizingatia kiwango chake cha elimu, uwezo wake wa kujenga hoja na uimara wa misimamo yake. Ni kweli chama kimepata kuwa na kina wasomi wengi kama Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, Baregu, Safari, Vincent Mashinji na wengine wengi wasio na majina. Ila huyu Lissu, Mwenyekiti Mbowe kuwa naye makini sana.

Tunaona jinsi ambavyo ameweza kujijenga na kujipatia wafuasi wengi ndani na nje ya chama, hasa pale alpoweza kushinda nafasi ya urais wa TLS. Kwa sasa anafanya diplomasia ya kukutana na Rais Magufuli kupitia nafasi yake ya urais wa TLS. Ameshakutana na kaimu Jaji Mkuu, ana mpango wa kukutana na Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Sheria, n.k. Yote hayo ni kupitia nafasi ya urais wa TLS. Wewe Mwenyekiti huwezi kupata nafasi hiyo kutokana msimamo wa Rais Magufuli kutotaka siasa mpaka 2020. Nafasi pekee uliyo nayo ni ya ubunge na bahati mbaya sana hakuna tena mambo ya bunge "live". Nini maana yake? Nitafafanua.

Maana yake ni kwamba Tundu Lissu kwa sasa ana nafasi kubwa sana ya kusikika na kujitangaz an hivyo kujijenga, kupitia urais wa TLS. Ameshatoa na anaendelea kutoa matamko ambayo ndani ya chama yanamjengea ufuasi mkubwa sana na nje ya chama. Mwaka 2018 ni mwaka wa uchaguzi wa ndani. Tayari Lissu ameanza kupigiwa chapuona vijana wengi agombee uenyekiti (Lissu awe Mwenyekiti CHADEMA na Lema awe Katibu)

Pia mwenendo wa vijana wa CHADEMA mtandaoni unalekea kumjenga zaidi Lissu kuliko chama. Kwa uchache tazama mabandiko haya:

Nampongeza,kumtia moyo na kumuombea kwa Mungu Mh.Tundu Lissu

Ni Tundu Lissu na wala siyo Lowassa kushinda Urais 2020 kwa UKAWA

Je, Tundu Lissu aweza kuwa Mwanasheria bora wa Afrika?

Hayo ni mabandiko machache tu. Sasa Mwenyekiti Mbowe, tunajua kiwango chako cha elimu na ujenzi wako wa hoja. Swali la kujiuliza ni kwamba Lissu akigombea uenyekiti, unaweza kumshinda kweli? Nimewaza na kuona jinsi ulivyoweza kuwazuia Marehemu Chacha Wangwe licha kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama kipindi kile. Tunajua hakuwa na CV kama ya Lissu lakini alikuwa jasiri na mwenye ushawishi na kipndi hichi Lissu hakuwa ndani ya chama kivile. Akajaribu Zitto Kabwe. Huyu ana elimu kubwa na uwezo mkubwa kuliko wewe na kuliko Wange, pengine anashindana na Lissu.Lakini huyu ulimleta na kumkusa ndani ya chama

Kama wasemavyo waswahili, masikio hayazidi kichwa. Wote tuliona kilichompata alipojaribu kukupoka uenyekiti wako. Sasa yuko anahangaika na ACT yake. Tunajua ni kwa nini ni wewe tu lazima uendelee na uenyekiti wako. Chama unakijua vizuri sana. Wengine hawa kina Lissu, Zitto na wengineo hawajawahi hata kuweka senti kukijenga chama. Umetoa mengi kukjenga chama. Umezunguka nchi hii miaka mingi kukijenga chama.

Nakuuliza, je Mwenyekiti Mbowe, kwa kasi hii na uzito unaoongezeka wa Tundu Lissu, akisimama na kugombea uenyekiti, atakushinda?

Uko tayari kupambana naye? Una uwezo na sifa kama zake?

Je Lissue ana hela ya kukijenga chama?

Mwenyekiti Mbowe kuwa makini sana na Lissu.
Bashite weka Vyeti Mezani wacha kuhangaika na ya CHADEMA
 
Ha ha ha haaa. Inaonekana Mbowe anawastress sana CCM.

Na bado. Hebu mwambie JPM achague moja kwanza kati ya urais na uenyeketi, akikubali kuchagua moja rudi hapa tumzungumzie kamanda wa Anga, Freeman Aikaeli Mbowe.
 
Wewe ni mbweha mkubwa, unajaribu kujenga mfarakano ndani ya chama, hivi mbowe ni mwenyekiti wa kudumu?
Tuache ujinga demokrasia ianzie chamani.
Sina uhakika Lisu atataka awe mwenyekiti wa chama na tls
 
Ina maana akina Lizaboni siku hizi wameanza kuipenda Chadema? Naona wamekazana kushauri na kupanga safu ya uongozi. Akili za kitoto kweli eti lemgo lao kumkosanisha Lissu na Mbowe. Ovyo kabisa. Walianza hivyo hivyo wakampa kichwa Zitto na hatimaye akapotea. Leo ameanza kujipendekeza kwa Chadema na viongozi wake.
 
Uzuri wa Mbowe hana tamaa ya kulazimisha kugombea urais kama wenyeviti wengine .....so msitegemee kumgombanisha na wenzake kwa kigezo cha urais ....kama baba yake alivyojitoolea pesa TANU ikaleta uhuru akiwa na wafadhili wenzake yeye naye kajitoa kufanya kazi na kutumia uwezo wake kupata ukombozi wa kweli na ikiwa sio lazima yeye awe Rais
Hadi sasa chadema wana hazina ya vijana barubaru wasomi wenye uwezo wa kumwondoa Magufuli madarakani mwaka 2020 ....maana CCM wao watakuwa wamefungwa kamba hadi 2025 ....
CCM wataweza kuutetea kiti hiki kama wataweka mgombea tofauti!!,,..kama NAPE,JANURI au Mwigulu
 
Kitu ambacho wengi hamkijui kuhusu Mbowe, ni uwezo wake wa kufanya kazi na watu wasomi kuliko yeye. Mbowe ameelimika sana. Na wasomi waliomsaliti wote tumeona wanavyopotea kisiasa.
Mfano Dr. Amani Kaborou, alikuwa uingereza ni Mbowe aliyemtoa kule na kumleta nchini na kumuingiza kwenye siasa. Akamsaliti, kilichomkuta anajua mwenyewe, anaishi kwao kigoma siku hizi na sina uhakika kama atatoba katika CCM ya Magufuli, Akaja Wangwe, Mungu amlaze mahali pema peponi, akaja Zito Kabwe, umeongea vizuri kuwa anahangaika na ACT, akaja Dr. Slaa, amesikika kwenye mitandao kuwa ameshachoka kukaa kwenye baridi alikoenda baada ya kumsaliti Mbowe sasa anataka kurudi bongo. Akirudi bongo atakuwa anafanya kazi gani?
Umeongea vizuri sana kwamba wote hao ni Mbowe ndoo anawaingiza Chadema. Mbowe ameelimika sana, na anauzoefu mkubwa kama ulivyomwelezea. Demokrasia ya upinzani hailinganishwi na ya chama tawala, as long as chadema ni chama cha upinzani, I highly recommend Mbowe kuuendelea kuwa mwenyekiti. Ni mwenyekiti pekee ambaye yupo tayari kuacha watu wengine wawe marais. Na namalizia kwa kusema, Mbowe anajua sana kusoma upepo wa kisiasa kuliko unavyomdhania. 2020 akiona Lisu nyota yake inang'aa kuliko mwanachadema yeyote, atampa agombee urais.
Lissu hafai hata kuwa rais wa kijijini kwao,kutokana na tabia yake ya ukosefu wa busara !
 
Bandiko reeeefu halafu limejaa ujinga na upuuzi kwa kutumia akili za Lumumba.
 
Mleta mada bila shaka wewe ndiye muasisi wa lile group la whatsap kule Lumumba lililolenga kuwagombanisha Tundu Lissu na Mbowe Freeman lakini ikashindikana baada ya wenzio kutuhabarisha naona bado unashauku sana ya huo mpango wako ovu! Sasa kwa kuwa hautofanikiwa nakushauri uanzishe group jingine linaloshindanisha Mbowe Vs Konyola au Lissu Vs Konyola au Mkeo Vs Konyola huenda utafanikiwa bila hivyo kibarua cha buku saba kitaota nyasi na jiji litakushinda mwishowe utatuuzia msambwanda tukutifue magoya vinginevyo rudi kijijini kwa bibi yako DIBADUKE ukalime ngwara nyambaafu weye
 
Halafu nahisi CCM wameanza kunusa harufu ya maumivu uchaguzi wa 2020. Huku Lissu, kule Sumaye, pale Mbowe, kule Lijualikali, mbona tabu tu kwa CCM? Unajua uchaguzi wa 2015 CCM ilitembelea nyota ya Magu ambaye sasa hata wao wenyewe hawataki hata kumsikia. Nadhani atakatazwa hata kwenda kwenye kampeni maana kila anapopata nafasi ya kuongea na wananchi lazima atukwaze (mfano, serikali haina shamba, serikali haijengi nyumba za watu, mwafaaaaa! sishughuliki na kulisha wenye njaa, kwanza Tanzania hakuna njaa, mimi sikusaidiwa na mtu kushinda urais, najiamini, sipangiwi cha kufanya, n.k). Sasa makwazo wakati wa uchaguzi ni sumu ya ushindi. Natamani uchaguzi uwe kesho nimsikie Mzee anasemaje.
 
Hatutaki Lissu agombee uenyekiti wa CHADEMA. Tunachotaka ni kuona Lissu anapambana na Magufuli katika kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ifikapo 2020. Dikteta hana ujanja tena. Aanze kabisa kuandaa mashamba ya viazi vitamu kule Chato.
 
Back
Top Bottom