Mbowe mtazame kwa umakini sana Lissu

Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
9,284
4,688
Kwako Mwenyekiti wetu Mbowe, F.A. (MB-KUB)

Tunatambua wazi nguvu na jitihada na juhudi zako katika kuijenga CHADEMA licha ya msukosuko mkubwa wa mwaka 2015 pale Katibu Mkuu, Dr. W.P. Slaa alipojiondoa ndani ya chama kufuatia uamuzi wako wewe kumkaribisha ndani ya chama na kumpa nafasi ya ugombea urais, bila kushindanishwa, target yetu kuu dhidi ya vita ya ufisadi, Edward N. Lowassa. Yaliyotokea ni historia na hatuna haja ya kurejea tena. Licha ya UKUTA kuanguka vibaya sana pamoja na uimara wa Rais Magufuli katika kuiongoza nchi na chama chake (wahasimu wetu CCM), bado chini yako CHADEMA inasonga tu. Tunatambua kipindi kigumu ulichopitia cha kutoweka kwa msaidizi wako mkuu, Ben Saanane bila taarifa, lakini bado uko imara kabisa. Tunatambua uhsuishwaji wako na biashara ya mihadarati, ukwepaji kodi na kulipa mapango mpaka kuvunjwa kwa kitegauchumi chako hapo Bilcanas na madai ya kodi ya TRA. bado uko imara. Hiyo ni kwa uchache misukosuko unayopitia.

Sasa Ndugu Mwenyekiti kuna changamoto kubwa sisi makamanda tunaokijua chama, inakuja mbele yako. Nayo si nyingine bali ni uwepo wa Tundu A. Lissu. Tunatambua kuwa huyu ulimpatia nafasi ya kuja ndani ya chama na kuweza kugomeba ubunge wa Singida Mashariki mwaka 2010 nakuweza kuteteta tena mwaka 2015. Huyu jamaa si wa kumpuuza hata kidogo. Wote tu mashahidi jinsi alivyoweza kupata nafasiya kuwa Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika licha ya kupitia vikwazo na misukosuko mingi sana. Historia yake na yako zinafanana kwa kiasi fulani ingawa yake ina uzito zaidi hasa ukizingatia kiwango chake cha elimu, uwezo wake wa kujenga hoja na uimara wa misimamo yake. Ni kweli chama kimepata kuwa na kina wasomi wengi kama Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, Baregu, Safari, Vincent Mashinji na wengine wengi wasio na majina. Ila huyu Lissu, Mwenyekiti Mbowe kuwa naye makini sana.

Tunaona jinsi ambavyo ameweza kujijenga na kujipatia wafuasi wengi ndani na nje ya chama, hasa pale alpoweza kushinda nafasi ya urais wa TLS. Kwa sasa anafanya diplomasia ya kukutana na Rais Magufuli kupitia nafasi yake ya urais wa TLS. Ameshakutana na kaimu Jaji Mkuu, ana mpango wa kukutana na Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Sheria, n.k. Yote hayo ni kupitia nafasi ya urais wa TLS. Wewe Mwenyekiti huwezi kupata nafasi hiyo kutokana msimamo wa Rais Magufuli kutotaka siasa mpaka 2020. Nafasi pekee uliyo nayo ni ya ubunge na bahati mbaya sana hakuna tena mambo ya bunge "live". Nini maana yake? Nitafafanua.

Maana yake ni kwamba Tundu Lissu kwa sasa ana nafasi kubwa sana ya kusikika na kujitangaz an hivyo kujijenga, kupitia urais wa TLS. Ameshatoa na anaendelea kutoa matamko ambayo ndani ya chama yanamjengea ufuasi mkubwa sana na nje ya chama. Mwaka 2018 ni mwaka wa uchaguzi wa ndani. Tayari Lissu ameanza kupigiwa chapuona vijana wengi agombee uenyekiti (Lissu awe Mwenyekiti CHADEMA na Lema awe Katibu)

Pia mwenendo wa vijana wa CHADEMA mtandaoni unalekea kumjenga zaidi Lissu kuliko chama. Kwa uchache tazama mabandiko haya:

Nampongeza,kumtia moyo na kumuombea kwa Mungu Mh.Tundu Lissu

Ni Tundu Lissu na wala siyo Lowassa kushinda Urais 2020 kwa UKAWA

Je, Tundu Lissu aweza kuwa Mwanasheria bora wa Afrika?

Hayo ni mabandiko machache tu. Sasa Mwenyekiti Mbowe, tunajua kiwango chako cha elimu na ujenzi wako wa hoja. Swali la kujiuliza ni kwamba Lissu akigombea uenyekiti, unaweza kumshinda kweli? Nimewaza na kuona jinsi ulivyoweza kuwazuia Marehemu Chacha Wangwe licha kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama kipindi kile. Tunajua hakuwa na CV kama ya Lissu lakini alikuwa jasiri na mwenye ushawishi na kipndi hichi Lissu hakuwa ndani ya chama kivile. Akajaribu Zitto Kabwe. Huyu ana elimu kubwa na uwezo mkubwa kuliko wewe na kuliko Wange, pengine anashindana na Lissu.Lakini huyu ulimleta na kumkusa ndani ya chama

Kama wasemavyo waswahili, masikio hayazidi kichwa. Wote tuliona kilichompata alipojaribu kukupoka uenyekiti wako. Sasa yuko anahangaika na ACT yake. Tunajua ni kwa nini ni wewe tu lazima uendelee na uenyekiti wako. Chama unakijua vizuri sana. Wengine hawa kina Lissu, Zitto na wengineo hawajawahi hata kuweka senti kukijenga chama. Umetoa mengi kukjenga chama. Umezunguka nchi hii miaka mingi kukijenga chama.

Nakuuliza, je Mwenyekiti Mbowe, kwa kasi hii na uzito unaoongezeka wa Tundu Lissu, akisimama na kugombea uenyekiti, atakushinda?

Uko tayari kupambana naye? Una uwezo na sifa kama zake?

Je Lissue ana hela ya kukijenga chama?

Mwenyekiti Mbowe kuwa makini sana na Lissu.
 
Baada ya siri ya umoja wa vichaa wa chama cha mabashite (UVCCM) kuvuja kuhusu kuanzisha watsapp groups za kuwafarakanisha wanachama wa CDM kwa hoja ya Lissu vS Mbowe, sasa naona wamekuja JF kwa nguvu mpya. Mara Mbowe vs Lowasa, Mara Mbowe vs Lissu......
Yaani ni ubashite mtupu. CHADEMA wanagawana majukumu arifu wala sio vyeo kama nzi wa kijani wa Dodoma
 
Tundu Lissu .. Mwenyekiti chadema na John Mnyika katibu mkuu ....hapa ndio chadema itafufuka katika wafu... vinginevyo ni kuendelea kupoteza muelekeo tu....endeleeni na ayatollah mpoteze uelekeo ..mtakua mnadandia matukio ...mwisho wa nchi ya ahadi...
 
Kitu ambacho wengi hamkijui kuhusu Mbowe, ni uwezo wake wa kufanya kazi na watu wasomi kuliko yeye. Mbowe ameelimika sana. Na wasomi waliomsaliti wote tumeona wanavyopotea kisiasa.

Mfano Dr. Amani Kaborou, alikuwa uingereza ni Mbowe aliyemtoa kule na kumleta nchini na kumuingiza kwenye siasa. Akamsaliti, kilichomkuta anajua mwenyewe, anaishi kwao kigoma siku hizi na sina uhakika kama atatoba katika CCM ya Magufuli, Akaja Wangwe, Mungu amlaze mahali pema peponi, akaja Zito Kabwe, umeongea vizuri kuwa anahangaika na ACT, akaja Dr. Slaa, amesikika kwenye mitandao kuwa ameshachoka kukaa kwenye baridi alikoenda baada ya kumsaliti Mbowe sasa anataka kurudi bongo.

Akirudi bongo atakuwa anafanya kazi gani?
Umeongea vizuri sana kwamba wote hao ni Mbowe ndoo anawaingiza Chadema. Mbowe ameelimika sana, na anauzoefu mkubwa kama ulivyomwelezea. Demokrasia ya upinzani hailinganishwi na ya chama tawala, as long as chadema ni chama cha upinzani, I highly recommend Mbowe kuuendelea kuwa mwenyekiti. Ni mwenyekiti pekee ambaye yupo tayari kuacha watu wengine wawe marais.

Na namalizia kwa kusema, Mbowe anajua sana kusoma upepo wa kisiasa kuliko unavyomdhania. 2020 akiona Lisu nyota yake inang'aa kuliko mwanachadema yeyote, atampa agombee urais.
 
Tundu Lissu .. Mwenyekiti chadema na John Mnyika katibu mkuu ....hapa ndio chadema itafufuka katika wafu... vinginevyo ni kuendelea kupoteza muelekeo tu....endeleeni na ayatollah mpoteze uelekeo ..mtakua mnadandia matukio ...mwisho wa nchi ya ahadi...
mbona kipindi hiki hiki cha huyo unaemuita Ayatolah ccm mnabamizwa vibaya sana
 
Wewe wapi mbona lissu hata kabla hajawa rais wa TLS alikuwa anasikia hata kabla hajasema mambo ya dictator uchwara lissu alikuwa anawika na ataendelea kuwika

Urais sio bar au magazetini. Kama mnataka kumpima lissu kwa kiatu cha Uraisi. Kigezo cha kwanza. Kama mwanasiasa Mbunge amelifanyia nini Jimbo lake. Na tungependa tumsikie pia kama mbunge kwanza haya mengine ni nyie wenzetu wa anayepambana na mwalimu mkuu kwa kelele basi anakuwa kaka mkuu.
 
Back
Top Bottom