Mbowe mtazame kwa umakini sana Lissu

Mbowe mtazame kwa umakini sana Lissu

Kama kuna wakati ambao UVCCM imekosa muelekeo kiasi cha viongizi kukosa kujiamini basi ni enzi hii ya Magu.
 
mbona kipindi hiki hiki cha huyo unaemuita Ayatolah ccm mnabamizwa vibaya sana
kwahiyo kila anayepinga humu ccm...kazi unao,kwahiyo zidumu fikra za mwenyekiti ...ukweli ni kwamba chadema kinahitaji REFORM ya uongozi ..kukirejesha...mahala pake kamaa mpinzani mkuu wa ccm ..kwani kuna dhambi gani wengine kugombea uenyekiti na uraisi ndani ya chadema... unaelewa vizuri maana ya demokrasia wewe..???
 
Mawazo mufilisi kabisa!
Kamwe tundulissu hawezi kurubuniwa na bwana yule!
Kuomba kukutana ni trick tu kwasababu anajua bwana yule alivyona na chuki hawezi kukubali
Jikite kwenye theme ya mleta post ambayo imeainishwa wazi kabisa juu political & leadership potentials kati ya Lissu na M/kiti Mbowe ndani Chadema, swali je Mbowe atahimili vishindo vya Lissu endapo atatangaza nia na huenda ama anayotayari ama baadhi ya wanachama wameanza kumpigia chapuo kama alivyotuthibitishia mleta post kwa mifano.
 
Thread ndefu
Sijawahi kuona mawazo mufilisi kama ya kwako mleta mada..

Mungu akusamehe kwa dhamira yako mbaya ya kujenga chuki kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu.

Adui ya hawa unaotaka wagombane ni CCM halafu akili yako ilivyo unawafitinisha..
 
Very good thoughts and they can become a reality, Lissu is definetly more popular than mbowe, and he has a chance to carry the flag of Chadema, and that is only possible if chadema is well united.

Lissuu ajue kuwa Uraisi wa TLS pia unaweza kuwa ni mtego kwake, akifeli hapo kwa mikurupuko yake kama hii ya kuomba kuonana na Raisi ambaye anamtukana kila siku na kutetea waovu kama wakwepa kodi bandarini na mashirika ya kigeni yanayo hudumu uchumi wetu, yanaweza kumweka pabaya, na CDM ikamtelekeza.

In politics people like Lissu are a great liability to their own leaders like mbowe. He needs to careful and smart.
 
Kwako Mwenyekiti wetu Mbowe, F.A. (MB-KUB)

Tunatambua wazi nguvu na jitihada na juhudi zako katika kuijenga CHADEMA licha ya msukosuko mkubwa wa mwaka 2015 pale Katibu Mkuu, Dr. W.P. Slaa alipojiondoa ndani ya chama kufuatia uamuzi wako wewe kumkaribisha ndani ya chama na kumpa nafasi ya ugombea urais, bila kushindanishwa, target yetu kuu dhidi ya vita ya ufisadi, Edward N. Lowassa. Yaliyotokea ni historia na hatuna haja ya kurejea tena. Licha ya UKUTA kuanguka vibaya sana pamoja na uimara wa Rais Magufuli katika kuiongoza nchi na chama chake (wahasimu wetu CCM), bado chini yako CHADEMA inasonga tu. Tunatambua kipindi kigumu ulichopitia cha kutoweka kwa msaidizi wako mkuu, Ben Saanane bila taarifa, lakini bado uko imara kabisa. Tunatambua uhsuishwaji wako na biashara ya mihadarati, ukwepaji kodi na kulipa mapango mpaka kuvunjwa kwa kitegauchumi chako hapo Bilcanas na madai ya kodi ya TRA. bado uko imara. Hiyo ni kwa uchache misukosuko unayopitia.

Sasa Ndugu Mwenyekiti kuna changamoto kubwa sisi makamanda tunaokijua chama, inakuja mbele yako. Nayo si nyingine bali ni uwepo wa Tundu A. Lissu. Tunatambua kuwa huyu ulimpatia nafasi ya kuja ndani ya chama na kuweza kugomeba ubunge wa Singida Mashariki mwaka 2010 nakuweza kuteteta tena mwaka 2015. Huyu jamaa si wa kumpuuza hata kidogo. Wote tu mashahidi jinsi alivyoweza kupata nafasiya kuwa Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika licha ya kupitia vikwazo na misukosuko mingi sana. Historia yake na yako zinafanana kwa kiasi fulani ingawa yake ina uzito zaidi hasa ukizingatia kiwango chake cha elimu, uwezo wake wa kujenga hoja na uimara wa misimamo yake. Ni kweli chama kimepata kuwa na kina wasomi wengi kama Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, Baregu, Safari, Vincent Mashinji na wengine wengi wasio na majina. Ila huyu Lissu, Mwenyekiti Mbowe kuwa naye makini sana.

Tunaona jinsi ambavyo ameweza kujijenga na kujipatia wafuasi wengi ndani na nje ya chama, hasa pale alpoweza kushinda nafasi ya urais wa TLS. Kwa sasa anafanya diplomasia ya kukutana na Rais Magufuli kupitia nafasi yake ya urais wa TLS. Ameshakutana na kaimu Jaji Mkuu, ana mpango wa kukutana na Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Sheria, n.k. Yote hayo ni kupitia nafasi ya urais wa TLS. Wewe Mwenyekiti huwezi kupata nafasi hiyo kutokana msimamo wa Rais Magufuli kutotaka siasa mpaka 2020. Nafasi pekee uliyo nayo ni ya ubunge na bahati mbaya sana hakuna tena mambo ya bunge "live". Nini maana yake? Nitafafanua.

Maana yake ni kwamba Tundu Lissu kwa sasa ana nafasi kubwa sana ya kusikika na kujitangaz an hivyo kujijenga, kupitia urais wa TLS. Ameshatoa na anaendelea kutoa matamko ambayo ndani ya chama yanamjengea ufuasi mkubwa sana na nje ya chama. Mwaka 2018 ni mwaka wa uchaguzi wa ndani. Tayari Lissu ameanza kupigiwa chapuona vijana wengi agombee uenyekiti (Lissu awe Mwenyekiti CHADEMA na Lema awe Katibu)

Pia mwenendo wa vijana wa CHADEMA mtandaoni unalekea kumjenga zaidi Lissu kuliko chama. Kwa uchache tazama mabandiko haya:

Nampongeza,kumtia moyo na kumuombea kwa Mungu Mh.Tundu Lissu

Ni Tundu Lissu na wala siyo Lowassa kushinda Urais 2020 kwa UKAWA

Je, Tundu Lissu aweza kuwa Mwanasheria bora wa Afrika?

Hayo ni mabandiko machache tu. Sasa Mwenyekiti Mbowe, tunajua kiwango chako cha elimu na ujenzi wako wa hoja. Swali la kujiuliza ni kwamba Lissu akigombea uenyekiti, unaweza kumshinda kweli? Nimewaza na kuona jinsi ulivyoweza kuwazuia Marehemu Chacha Wangwe licha kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama kipindi kile. Tunajua hakuwa na CV kama ya Lissu lakini alikuwa jasiri na mwenye ushawishi na kipndi hichi Lissu hakuwa ndani ya chama kivile. Akajaribu Zitto Kabwe. Huyu ana elimu kubwa na uwezo mkubwa kuliko wewe na kuliko Wange, pengine anashindana na Lissu.Lakini huyu ulimleta na kumkusa ndani ya chama

Kama wasemavyo waswahili, masikio hayazidi kichwa. Wote tuliona kilichompata alipojaribu kukupoka uenyekiti wako. Sasa yuko anahangaika na ACT yake. Tunajua ni kwa nini ni wewe tu lazima uendelee na uenyekiti wako. Chama unakijua vizuri sana. Wengine hawa kina Lissu, Zitto na wengineo hawajawahi hata kuweka senti kukijenga chama. Umetoa mengi kukjenga chama. Umezunguka nchi hii miaka mingi kukijenga chama.

Nakuuliza, je Mwenyekiti Mbowe, kwa kasi hii na uzito unaoongezeka wa Tundu Lissu, akisimama na kugombea uenyekiti, atakushinda?

Uko tayari kupambana naye? Una uwezo na sifa kama zake?

Je Lissue ana hela ya kukijenga chama?

Mwenyekiti Mbowe kuwa makini sana na Lissu.
acha kutuchonganisha. Kila mmoja ana uwezo wake na wote ni viongozi wetu.

Nani kakwambia elimu/akili/maarifa mpaka uwe na cheti. Kwa taharifa yako Mbowe ni bonge la kiongozi (maarifa, akili, hekima, busara, ujasiri na uadilifu).
 
Kitu ambacho wengi hamkijui kuhusu Mbowe, ni uwezo wake wa kufanya kazi na watu wasomi kuliko yeye. Mbowe ameelimika sana. Na wasomi waliomsaliti wote tumeona wanavyopotea kisiasa.
Mfano Dr. Amani Kaborou, alikuwa uingereza ni Mbowe aliyemtoa kule na kumleta nchini na kumuingiza kwenye siasa. Akamsaliti, kilichomkuta anajua mwenyewe, anaishi kwao kigoma siku hizi na sina uhakika kama atatoba katika CCM ya Magufuli, Akaja Wangwe, Mungu amlaze mahali pema peponi, akaja Zito Kabwe, umeongea vizuri kuwa anahangaika na ACT, akaja Dr. Slaa, amesikika kwenye mitandao kuwa ameshachoka kukaa kwenye baridi alikoenda baada ya kumsaliti Mbowe sasa anataka kurudi bongo. Akirudi bongo atakuwa anafanya kazi gani?
Umeongea vizuri sana kwamba wote hao ni Mbowe ndoo anawaingiza Chadema. Mbowe ameelimika sana, na anauzoefu mkubwa kama ulivyomwelezea. Demokrasia ya upinzani hailinganishwi na ya chama tawala, as long as chadema ni chama cha upinzani, I highly recommend Mbowe kuuendelea kuwa mwenyekiti. Ni mwenyekiti pekee ambaye yupo tayari kuacha watu wengine wawe marais. Na namalizia kwa kusema, Mbowe anajua sana kusoma upepo wa kisiasa kuliko unavyomdhania. 2020 akiona Lisu nyota yake inang'aa kuliko mwanachadema yeyote, atampa agombee urais.
Wewe mbeba ngada za mwenyekiti kwa jinsi Mbowe alivyotusaliti na kuuza chama kwa mafisadi,

Kwa zambi hii Mbowe must go
 
Mtazamo wako ni mzuri,lakini kwenye ulingo wa siasa Mbowe ana upeo wa hali ya juu,ukibisha muulize Lowasa, prof Lipumba na dr slaa.Kwenye elimu hajawahi kufoji cheti lakini hakufanya vizuri akiwa kidato cha sita si kwa sababu ya ukilaza bali sababu za yeye kuchanganya mambo mengi kiasi cha kukosa concentration katika kusoma.Kiufupi kwa upeo wa Mbowe ktk siasa naamini yeye mwenyewe ataamua kutogombea umwenyekiti kwa awamu nyingine kwani kwa sasa anao makamanda wa kutosha kukiendeleza chama mbele na si sababu ya kumwogopa au kumwaza Lissu.Kwani pamoja na yeye kustaafu bado nafasi ya mwenyekiti yaweza kwenda kwa kamanda mwingine tofauti na Lissu.Kwa mtazamo wangu Lissu ni mtendaji mpambanaji hivyo anafaa zaidi kuwa katibu mkuu chadema kisha Lema anafaa zaidi kuwa katibu wa itikadi na uenezi.
 
Mbowe ametusaliti na kuuza chama kwa mafisadi.

Mbowe must Go
 
Tundu Lissu .. Mwenyekiti chadema na John Mnyika katibu mkuu ....hapa ndio chadema itafufuka katika wafu... vinginevyo ni kuendelea kupoteza muelekeo tu....endeleeni na ayatollah mpoteze uelekeo ..mtakua mnadandia matukio ...mwisho wa nchi ya ahadi...
Bashite atawafaa sana ukatibu CCM.
 
Kwako Mwenyekiti wetu Mbowe, F.A. (MB-KUB)

Tunatambua wazi nguvu na jitihada na juhudi zako katika kuijenga CHADEMA licha ya msukosuko mkubwa wa mwaka 2015 pale Katibu Mkuu, Dr. W.P. Slaa alipojiondoa ndani ya chama kufuatia uamuzi wako wewe kumkaribisha ndani ya chama na kumpa nafasi ya ugombea urais, bila kushindanishwa, target yetu kuu dhidi ya vita ya ufisadi, Edward N. Lowassa. Yaliyotokea ni historia na hatuna haja ya kurejea tena. Licha ya UKUTA kuanguka vibaya sana pamoja na uimara wa Rais Magufuli katika kuiongoza nchi na chama chake (wahasimu wetu CCM), bado chini yako CHADEMA inasonga tu. Tunatambua kipindi kigumu ulichopitia cha kutoweka kwa msaidizi wako mkuu, Ben Saanane bila taarifa, lakini bado uko imara kabisa. Tunatambua uhsuishwaji wako na biashara ya mihadarati, ukwepaji kodi na kulipa mapango mpaka kuvunjwa kwa kitegauchumi chako hapo Bilcanas na madai ya kodi ya TRA. bado uko imara. Hiyo ni kwa uchache misukosuko unayopitia.

Sasa Ndugu Mwenyekiti kuna changamoto kubwa sisi makamanda tunaokijua chama, inakuja mbele yako. Nayo si nyingine bali ni uwepo wa Tundu A. Lissu. Tunatambua kuwa huyu ulimpatia nafasi ya kuja ndani ya chama na kuweza kugomeba ubunge wa Singida Mashariki mwaka 2010 nakuweza kuteteta tena mwaka 2015. Huyu jamaa si wa kumpuuza hata kidogo. Wote tu mashahidi jinsi alivyoweza kupata nafasiya kuwa Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika licha ya kupitia vikwazo na misukosuko mingi sana. Historia yake na yako zinafanana kwa kiasi fulani ingawa yake ina uzito zaidi hasa ukizingatia kiwango chake cha elimu, uwezo wake wa kujenga hoja na uimara wa misimamo yake. Ni kweli chama kimepata kuwa na kina wasomi wengi kama Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, Baregu, Safari, Vincent Mashinji na wengine wengi wasio na majina. Ila huyu Lissu, Mwenyekiti Mbowe kuwa naye makini sana.

Tunaona jinsi ambavyo ameweza kujijenga na kujipatia wafuasi wengi ndani na nje ya chama, hasa pale alpoweza kushinda nafasi ya urais wa TLS. Kwa sasa anafanya diplomasia ya kukutana na Rais Magufuli kupitia nafasi yake ya urais wa TLS. Ameshakutana na kaimu Jaji Mkuu, ana mpango wa kukutana na Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Sheria, n.k. Yote hayo ni kupitia nafasi ya urais wa TLS. Wewe Mwenyekiti huwezi kupata nafasi hiyo kutokana msimamo wa Rais Magufuli kutotaka siasa mpaka 2020. Nafasi pekee uliyo nayo ni ya ubunge na bahati mbaya sana hakuna tena mambo ya bunge "live". Nini maana yake? Nitafafanua.

Maana yake ni kwamba Tundu Lissu kwa sasa ana nafasi kubwa sana ya kusikika na kujitangaz an hivyo kujijenga, kupitia urais wa TLS. Ameshatoa na anaendelea kutoa matamko ambayo ndani ya chama yanamjengea ufuasi mkubwa sana na nje ya chama. Mwaka 2018 ni mwaka wa uchaguzi wa ndani. Tayari Lissu ameanza kupigiwa chapuona vijana wengi agombee uenyekiti (Lissu awe Mwenyekiti CHADEMA na Lema awe Katibu)

Pia mwenendo wa vijana wa CHADEMA mtandaoni unalekea kumjenga zaidi Lissu kuliko chama. Kwa uchache tazama mabandiko haya:

Nampongeza,kumtia moyo na kumuombea kwa Mungu Mh.Tundu Lissu

Ni Tundu Lissu na wala siyo Lowassa kushinda Urais 2020 kwa UKAWA

Je, Tundu Lissu aweza kuwa Mwanasheria bora wa Afrika?

Hayo ni mabandiko machache tu. Sasa Mwenyekiti Mbowe, tunajua kiwango chako cha elimu na ujenzi wako wa hoja. Swali la kujiuliza ni kwamba Lissu akigombea uenyekiti, unaweza kumshinda kweli? Nimewaza na kuona jinsi ulivyoweza kuwazuia Marehemu Chacha Wangwe licha kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama kipindi kile. Tunajua hakuwa na CV kama ya Lissu lakini alikuwa jasiri na mwenye ushawishi na kipndi hichi Lissu hakuwa ndani ya chama kivile. Akajaribu Zitto Kabwe. Huyu ana elimu kubwa na uwezo mkubwa kuliko wewe na kuliko Wange, pengine anashindana na Lissu.Lakini huyu ulimleta na kumkusa ndani ya chama

Kama wasemavyo waswahili, masikio hayazidi kichwa. Wote tuliona kilichompata alipojaribu kukupoka uenyekiti wako. Sasa yuko anahangaika na ACT yake. Tunajua ni kwa nini ni wewe tu lazima uendelee na uenyekiti wako. Chama unakijua vizuri sana. Wengine hawa kina Lissu, Zitto na wengineo hawajawahi hata kuweka senti kukijenga chama. Umetoa mengi kukjenga chama. Umezunguka nchi hii miaka mingi kukijenga chama.

Nakuuliza, je Mwenyekiti Mbowe, kwa kasi hii na uzito unaoongezeka wa Tundu Lissu, akisimama na kugombea uenyekiti, atakushinda?

Uko tayari kupambana naye? Una uwezo na sifa kama zake?

Je Lissue ana hela ya kukijenga chama?

Mwenyekiti Mbowe kuwa makini sana na Lissu.
Yaaani Lumumba hawalali sababu ya Tundu lissu daa haya kachukue buku 3 siku hizi maisha magumu dau limeshuka sio buku 7 tena
 
Mbowe must Go. Tundu Lissu in

Ha ha ha ha ha lol.. Wakati mwingine muwe mnaona aibu lol.. Hii id imeshafungua nyuzi nyingi za kumpinga na kumdharau Lissu.. Leo imeingia hapa inajifanya kuonyesha Lissu kichwa..

Hii id ingeachia zile ids nyingine ndo ziendelee na propaganda ili at least muingize siku huko Lumumba..
 
Back
Top Bottom