Nani alikudanganya kuwa maendeleo au mabadiliko huletwa na sera? Umekaririshwa?
Sera za elimu, afya, shughuli za kiuchumi, kwa vyama vingi katika mataifa mengi zinafanana. Kama ingekuwa ni sera ndiyo huleta maendeleo, basi viwango vya maendeleo katika mataifa yote vingekaribiana. Lakini ukweli ni kuwa pamoja na mfanano mkubwa sera, tofauti ya kiwango cha maendeleo kati ya mataifa ni tofauti sana.
Tatizo la CCM siyo sera bali ni udhaifu wa usimamizi, upungufu wa ubunifu, ukosefu wa uzalendo, na uwezo mdogo wa viongozi. Katikati ya yote ipo RUSHWA na UFISADI. Lakini wizi, ufisadi na rushwa vinasababishwa na udhaifu wa uongozi. Kama Kikwete angekuwa ni Rais imara na jasiri angeweza kuondosha rushwa, ubadhirifu na wizi. Maana huhitaji watu wengi kuondoa rushwa, unahitaji Rais imara na mzalendo tu. Nchi zote Duniani zilizokuwa zimekithiri kwa rushwa halafu ikaondolewa au kupunguzwa sana, ukichunguza ni Rais tu aliyeweza kuleta tofauti. Mfano mdogo nenda tu hapo Rwanda.
Hapa kwetu hatuna kiongozi wa kusimamia vita dhidi ya rushwa. Ukiona kiongozi anasema nileteeni ushahidi wa wala rushwa, ujue huyo ni kiongozi dhaifu na wala hana dhamira ya kuipiga vita, anatafuta kisingizio cha kutokushughulikia rushwa.