Mbowe, mashambulizi dhidi ya Mwigulu Nchemba kwa memo hii kulikoni?

Jamani msishangae kutukanwa,kukejeliwa na kushambuliwa pale utakaposema ukweli kuhusu chadema na viongozi wake, wanaofanya kazi hiyo ni vijana wa chadema wasiojitambua wako pale makao makuu ni kikosi kazi kinaongozwa na Mnyika hawa vijana wanapewa Posho kwa kazi ya kuitetea chadema na kuisemea mazuri mitandaoni wakati huo huo wanaishambulia CCM na serikali yale lendo kuui kuidhoofisha kwa wananchi ili waichukie na kuja kuipa madaraka ya utawla chadema yani wanapandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya CCM na serikali yake usifikiri wako vijana wengi hapana ni vijana wachache wanejisajili kwa IDs tofauti tofauti hiyo ndiyo chadema yenye mikakati michafu ya kushika dola ukionganisha na ule mkakati wa kushawishi,kudhamini na kuchochea migomo na fujo zote hapa nchini kwa Madaktari,Wanafunzi vyuoni na walimu! SHAME ON U CHADEMA Kwa mbinu chafu zinazoumiza watanzania!

just one question bro,
mie sio mshabiki, mwanachama au kada wa chama chochote, ila nina maswali haya kwako:

1. Ni chama gani kinapaswa kusifiwa au kupondwa kutokana na hali ya nchi(kiuchumi) ilivyo sasa?
2. Je ni dhambi kuisema vibaya CCM hata kama yanayosemwa yana mantiki?

Ushauri, jaribu kuweka itikadi pembeni, halafu tathimini kidogo kama hali ya kila Mtanzania kimaisha inaridhisha.
 
Ndugu zangu,

Unaweza kukaa kimya kwa muda mrefu ukiangalia 'mpambano' hatimaye uzalendo ukakushinda na ukaona bora upaze sauti yako kufafanua mtafaruku.

Nimesoma sms za kifo cha Nchemba; nazinukuu,

1. 'Hivi wewe unajiamini nini? Kwa nini unatuzonga hivyo? Unadhani nchi hii ni ya ccm milele? Utajutia kimbelembele chako. Unadhani ni wewe tu unayejua sana? Ukabila kwenye chama chetu unakuhusu nini hata kama kweli kwa nini kututia aibu? Hata ufanyeje 2015 tunaingia ikulu na mjengoni tutajaa, Wangwe alijifanya kujua kama wewe leo yuko wapi?'

2. 'Bendera unayovaa kila siku shingoni itageuka sanda yako. Kila mtu ana haki ya kuvutia kwake lakini wewe umezidi. Hatuwezi kuitema keki tuliyokwishaionja'

3. 'Fahari yako itageuka kilio kwako. Utatutambua'

SOURCE: Tanzania Daima July 17, 2012.


Nitachambua sms zote kwa kadri ya mtazamo wangu.

Ujumbe wa kwanza hauna mantiki isipokuwa kukumbusha mambo yasiyofahamika hata leo. Unaposema 'unatuzonga' napata shida kuamini kwamba huo mi mzongo wa hoja maridhawa ama mzongo wa ubishi na hoja mfu, ilimradi makelele tu. Kwa mtu kujiamini hilo ni sawa, lakini kujiamini kwa mtu hakuwezi kumsababishia usumbufu wowote mtu mwingine kwa kuwa wote tunaendeshwa na akili zetu. Kuiacha hisia ifanye kazi bila kuwa na coordination baina ya ubongo na mdomo yaani coding unaweza kujikuta unaongea vituko sana mbele ya wenzio na ukaambulia kuvuna aibu.

Ukabila unaodaiwa kwenye sms ya 1 hauna uthibitisho kwa kuwa kwanza baadhi ya senior figures CDM sio wa kaskazini, lakini pia CDM imeandikishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kama Political Party na sio chama cha wachagga ama wanyamwezi. Kama kuna mwenye uhakika kwamba CDM ni chama cha Wanyamwezi basi awasilishe kwa Tendwa ili CDM kichukuliwe hatua stahili akiwemo Tendwa mwenyewe kwa kuruhusu ukabila utinge Bungeni. Hakuna hata kada mmoja wa CDM anayeweza kuandika akitetea ukabila hata kama kawehuka kiasi gani. Maneno ya vijiweni ni mengi, huwezi kuyaamini kirahisi. Na kama ni kweli imesemwa mitaani kwamba CDM ni chama cha ukabila basi ni aibu ipi CDM imevuna zaidi ya kuendelea kuungwa mkono kila kukicha na sote ni shahidi? Basi tuseme wana CDM wote Tanzania wajiandaa kubadili makabila yeo ili wote wageuke Wanyamwezi gurudumu lisonge.

Ujumbe, sms, wa pili ni mawazo finyu ambayo mwanafunzi wa kidato cha kwanza hawezi kuandika. Bendera ya Taifa kuvaliwa na Mwigulu kwangu sioni tatizo ikiwa humohumo bungeni inakanyagwa hovyo na viatu vichafu kila siku. Ni bendera hii hii ambayo inapepea kwenye mahoteli yaliyo na makasino, na ni bendera hii hii ambayo siku hizi hata ikifika saa 12 jioni wakati ishukapo watu hawana habari, wanatembea tu. Tundu Lissu (Mh Mb) aliwahi kuguswa na uvaaji wa skafu wa Mwigulu lakini sote tunajua Mh Simbachawene alivyotoa muongozo. Kama mwandishi ni mbumbumbu wa haya nashindwa kuamini kwamba Mh Mwingulu alishindwa vipi kumfafanulia. Labda niseme tu kwamba mwandishi hana busara na ni mchochezi. Suala la sanda sijui hata linahusiana vipi na kitambaa ambacho ukubwa wake hauzidi 1x1'.

SMS ya mwisho iko too general kwamba 'itageuka kilio kwako' pengine alikusudia kusema 'itageuka msiba kwako' maana ifike wakati tuyasome mawazo ya mwandishi. Mwigulu sidhani kama anafurahia akitafsiriwa kwamba ni 'fahari' katika medani za siasa ama jamii. Sidhani kama kuna politician yeyote anayependa kuwa fahari wakati nchi yake inamegwa bila huruma, na wakati wapiga kura wake kutwa kucha wanaomba hisani kwake. Siamini hilo. Pengine angesema 'kujulikana kwako' hapo angeeleweka. Mimi binafsi nimeshindwa kuamini kwamba mwandishi alikusudia nini kwa msg hii.

Mwisho niseme wazi kwa wazoefu wa kusoma hapa na pale, unaweza tu kugundua kwamba kwanza sms hizi zimeandikwa na mtu mmoja, zimeandikwa katika hali ya hasira na husuda, hazina ujumbe ulio wazi (zinaacha maswali mengi) na haziendani na hali halisi ya wimbi la upinzani nchini. Zimekosa uzito.

Lakini na tuwaachie maafande wetu wachunguze hili ili kubaini chanzo na makusudi hasa ya sms hizi tata.

Nawasilisha,

G Kassanga
Tabora.

Uchambuzi wako unaonyesha una akili timamu.
 
1. 'Hivi wewe unajiamini nini? Kwa nini unatuzonga hivyo? Unadhani nchi hii ni ya ccm milele? Utajutia kimbelembele chako. Unadhani ni wewe tu unayejua sana? Ukabila kwenye chama chetu unakuhusu nini hata kama kweli kwa nini kututia aibu? Hata ufanyeje 2015 tunaingia ikulu na mjengoni tutajaa, Wangwe alijifanya kujua kama wewe leo yuko wapi?'

Kila akiwa Jukwaani Mwiguklu ndio Propaganda zake, ambazo daima hazina mashiko... ukabila CHADEMA inapendwa na kukubalika sana katika miji yote mikubwa ambayo wanaishi wenyeji wengi mfano tu Mbeya,Iringa,Mwanza na kote kusini ukabila uko wap? Kuna mbunge wa chadema asiyelijua hilo? Ok Muuaji wa Kamanda Wange alishatiwa nguvuni na kuhukumiwa bado unatumia propaganda za kitoto kwa kujitumia SMS mwenyewe, shem on you Mwigulu. burn

 
Kweli utakuwa mwendawazimu kuandika msg za namna hii! Hakuna mtu anaweza kuacha ushahidi wa wazi namna hii. Hii ni Propaganda tupu!
 
Hivi tume ya mawasiliano TCRA wako wapi? Mbona hii ni kitu kidogo kujua original ya SMS hizo. Mantiki ya kusajili LINE yalikuwa nini?

All in all kama kuna Mbunge wa CDM ameandika hizo sms za kitoto na kipuuzi hii inaonyesha POLITICAL IMMATURITY ya hali ya juu.

Lakini kama ni Mwigulu amezi doctrine hizo SMS, pia ni UJINGA uliopitiliza sawa na hadithi ya Kova na yule Kichaa wa Kenya.

Lakini hii kitu haichukui hata dk 5 kama POLISI na TCRA wakitaka kujua UKWELI jambo hili.
 
hivi mnajua mchemba ni mwana JF mwenzetu???
kweli huyu jamaa ni kichwa tumesahau kabisaa bilion za uswisi tupo na msg za maji taka!
NCHI TUTAIBIWA HII MPAKA BASI!
 
Naona Analogue CCM inachanganikiwa kwenye ulimwengu wa Digitali. Haya wana CCM it time to migrate to the digital world! Kumbuka mwisho/deadline 2015 weraaaa....
 
CDM mmejiumbua wenyewe kwa hizi sms, na huo utetezi wako hata mtoto wa chekechea huwezi kumzuga, anzisha jukwaa lako uweke propaganda zako, JF ni jukwaa huru na kile ukiletacho huchambuliwa kwa kina.


Ingelikuwa ni heri huyo Mwigulu Mchimba angeliwaweka hadharani hao waliomtumia SMS hizo. Hata na Spika naye kwani amesema kuwa wanafahamika. Hivyo watutajia hao watu vinginevyo tutajua ni SMS za kutengenezwa tu. Mtu yeyote anaweza kununua Sim Card mpya na kujitumia SMS kwa kisingizio fulani.

profilepic 2012.JPG

TUWE WA KWELI ACHENI HIZOOOOOOOOOOOOO!!!!! NA TABIA YA KUJISHUKU!!!!!!



MIZAMBWA
NABII MTARAJWIA!!!
 
Wabunge wanapaopoteza muda wao kuattack personalties badala ya kusimamia maslahi ya taifa na wapiga kura wao wanastahili waambiwe nini zaidi ya hayo kwenye memo isemwayo imetoka kwa Mbowe. "Nini kifanyike kuondoa hali hii, i.e hali ya wabunge wenye kauli za wivu na fitna chungu kama mboga mbichi ya mchunga ????????"
 
CCM wamejitahidiii.. Hapo ndo mwisho wa uzushi wao?? Waambieni watoe hiyo namba iliyowatumia tuifanyie kazi within a second tutamtaja mwandikaji,,

1. Tutawaeleza namba imesajiliwa lini
2. Tutaonyesha location, mahali mtu aliyeandika alipokuwa
3. Tutaonyesha muda
4. Tutaonyesha kama hiyo namba imetumika kuwasiliana na watu wengine, calls, msgs etc.,
5. etc., etc.,
6. Mwisho mwigulu ataumbuka
 
hv jaman tuna spika kweli? upuuzi wa kina lusinde na mwigulu ndo spika akaacha mda wake na kufafanua ujinga huu kweli?huu ni utoto wa nchemba na lusinde ndo wameandka wenyewe
 
Usipate shida na ndio maana post zangu zote ziko waziwazi, ushahidi upo, ila unaweza kuanza na gazeti 'Tanzania Daima la leo'. Usipate shida nitafute mkuu. Ungekuwa na busara na mwenye nia njema na wewe ungeweza genuine info ili uwe verified but kwa kuwa uko gizani, timiza haja ya moyo wako.
Unajua wewe ni verified user sio anonymous tutakutafuta udhibitishe na useme umetoa wapi
 
Usipate shida na ndio maana post zangu zote ziko waziwazi, ushahidi upo, ila unaweza kuanza na gazeti 'Tanzania Daima la leo'. Usipate shida nitafute mkuu. Ungekuwa na busara na mwenye nia njema na wewe ungeweka genuine info ili uwe verified but kwa kuwa uko gizani, timiza haja ya moyo wako.
Unajua wewe ni verified user sio anonymous tutakutafuta udhibitishe na useme umetoa wapi
 
Hakuna kitu hapo ndgu watanzania ni kiini macho kinachofanywa na kikundi cha watu kwa manufaa yao binafsi na wala c ya kitaifa.

Tujiepushe nao. Hata maandiko matakatifu yaliwahi kusema kuwa palipo na wachafu bc tujitege nao.

Too falcious to be believed!!! Kwa nini kujitafutia umaarufu kwa kuzushia wengine uongo?
 
CDM mmejiumbua wenyewe kwa hizi sms, na huo utetezi wako hata mtoto wa chekechea huwezi kumzuga, anzisha jukwaa lako uweke propaganda zako, JF ni jukwaa huru na kile ukiletacho huchambuliwa kwa kina.


ujui usemalo,ipi hapo sms za kumtisha mtu aliyewai kutembea mguu peku akichunga ng'ombe na mbuzi nyikani?ivi sisi tuliowai kutishwa na polisi face to face tusemaje,mwisho kama kweli alitiswa si watu hao wangeshakamatwa au polisi wanasubiri mpaka yatokee kama ya Ndako licha ya kupewa habari mapema.
kunakuwa mwisho wa uonevu jamani tuvumiliane tu
 
Hizo msg kaandika Mwigulu,Chemba,kama hajaandika atupe hizo namba zilizomtumia hizo msg aone watu watakavyo kuja na data, ikiwemo location, imei na namba zinazotumika kwenye hiyo imei na watu ambao huwa anawasiliana nao.Aache ujinga wake.
 
leo hii ukiniuliza mwigulu sera zake ni zipi hata sijui..ninachojua kuhusu yeye ni kuleta vurugu bungeni...kuna mambo mengi yanayohusu taifa hili ya kujadiliana bungeni lakini huyu jamaa hayuko interested kabisa
 
Back
Top Bottom