Mwigulu, tuzungumze kizalendo kidogo! Bajeti na Janja ya CCECC

Apr 24, 2011
29
542
Mwigulu, tuzungumze kizalendo kidogo!

Bajeti kuu ya serikali, hotuba yako, ukurasa wa 44, unasema serikali imeanza mchakato wa kutafuta mkandarasi wa kujenga kipande cha SGR (Tabora-Kigoma) 514km kwa US$2.1 bilioni (Sh4.89 trillioni). Wakati tunajua umewapa kandarasi CCECC.

Katika mfumo wa TANePS (Tanzanian National e-Procurement System), Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa zabuni hiyo kwa Sh6.69 trilioni. Tofauti ya anachosema Mwigulu na TANePS ni Shs. 1.85 trilioni. Hii ni hatari. Hizi ni fedha zetu unachezea.

Mwigulu, umeamua kutudanganya hadharani kwa kuwa unajua hakuna kitu utafanywa. Mwigulu unasema “serikali imeanza mchakato” wakati ukweli ni kwamba Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa zabuni tangu 04.04.2022 kwa utaratibu wa ‘single source’

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) alipewa hii zabuni kwa utaratibu wa (single source’ ambayo ilidumu TANePS kwa dakika 30, yenye BID ID 421346 ambayo ipo secured? Opening na Closing date yake ni 10:00 hadi 10:30, 04/04/2022

Opened BID DETAILS;
Title; PA/154/HQ/2021-22/W/02 LOT 1
Status; (Evaluation)
Closing Date; 04/04/2022 10:00
Opening Date; 04/04/2022 10:30
Envelope; Single
Suplier Name; China Civil Engineering construction corporation
BID ID; 421346
Financial Value; 6,698,935,255,040.00
BID security provided; TRUE
BID security Value; 103932450000.00
FDR; 0.00
FDR Terms; —

Hii ndiyo zabuni mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) ameshinda kama ilivyoonekana katika mifumo rasmi ya serikali, TANePS. Mwigulu, hotuba yako inasema ni US$2.1 bilioni (Sh. 4.85 trillioni). Sasa hizi Sh1.85 trilioni mnataka kuzipeleka wapi? Kwanini mnacheza na pesa za umma kwa kiwango hiki? Kwanini?

Bunge limeshindwa kuona hilo na kujadili. Baraza la mawaziri ambalo Rais ndiye mwenyekiti wa kikao chake pia limeshindwa kubaini ‘upigaji’ huu na kuruhusu bajeti kuu ya serikali kwenda kupitishwa kwa shangwe, chereko na nderemo? Kweli mnawapenda watanzania hawa maskini?

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) aliyepewa zabuni hiyo kwa utaratibu wa ‘single source’ ana zaidi ya 38% ya kiasi ambacho Mwigulu (waziri wa fedha) amekitaja katika hotuba yake ya bajeti. Gharama za ujenzi ni US$4.8M (Sh11.19bn) kwa kila 1 km

Hii ziada ya Sh1.85 trilioni ambayo wanaitolea macho, ni mara 30 ya pesa waliotumia USA kushambulia miji ya Homs na Damascus nchini Syria 14.4.2018. USA walitumia Nyambizi inayotumia umeme wa nyuklia, ndege ya kijeshi B-1 bomber na meli vita bajeti ikiwa US$26M (Sh60 bilioni)

Sh1.85 trilioni ni karibu nusu ya utajiri wa Bilionea Mohammed Dewji. Ni zaidi ya fedha zilizotumika kwenye uwekezaji wa kiwanda cha saruji cha Dangote (Sh1.3 trilion). Ni robo ya Utajiri wa Rais wa zamani wa USA, Bilionea Donald Trump (Sh6.99 trilioni)

Ikiwa noti moja ya elfu 10 ina uzito wa gram 1, maana yake kwenye Sh1.8 trilioni (noti milioni 180) zina uzito wa gram milioni 180 (180,000,000gm) au kilogram 180,000 sawa na uzito wa tani 180. Reli ya SGR inayojengwa inaweza kuhimili mzigo wa uzito wa Tani 35. Hii NI KUFURU.

Yaani hiyo ziada ambayo inabaki katika hiyo biashara ya Mwigulu na CCECC ni zaidi ya bajeti za wizara tatu katika mwaka wa fedha 2022/2023. Ni fedha nyingi. Ni zaidi ya fedha zote ambazo zilipigwa katika ufisadi wa ESCROW (Sh 306 bilioni) na EPA (Sh 133 bilioni) kwa pamoja.

Pia hata ukijumlisha MEREMETA (Sh205.9 bilioni), RADA (Sh73 bilioni), KAGODA (Sh40 bilioni), MABILIONI YA JK (Sh50 bilioni) bado hufiki hiyo tofauti ya kiasi cha waziri na CCECC (Sh 1.85 trilioni). Bunge lenye utimamu lingeomba ‘review’ ya ‘procurement and tendering’.

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa ujenzi wa lot Na. 5, Isaka – Mwanza (249 km). Miezi 16 amejenga 4.4% pekee na HAKUNA hata kipande kimoja cha reli ameweka katika miezi 17. Mwigulu anasema bungeni kwamba haukuwepo ufadhili wa kifedha. Ni MZAHA.

Utaratibu wa zabuni za ‘single source’ ni LAZIMA mkandarasi akidhi vigezo na uwezo. Huyu mkandarasi wa Mwigulu hana sifa hizo. Miezi 17 ameshindwa kupeleka hata ambulance, hakuna usalama kwa wafanyakazi, amefanya kazi kwa 4.4%. Mkandarasi huyu hajakidhi vigezo vya single source.

China Civil Engineering construction corporation (CCECC) kapewa ujenzi wa lot Na. 6 kutoka Tabora - Kigoma (514km). Hivyo kwa 514km mkandarasi atatumia US$2.1 bilioni (Sh4.89 trillioni). Kapewa zabuni bila ushindani. Zingatia; TANePS inaonyesha ni Shs. 6.69 trilioni

Phase 1 Dar es Salaam – Morogoro (300 km) kandarasi ni Yapi Merkezi na Mota Engil Africa. Phase 2 Morogoro- Makutupora (422 km) kandarasi ni Yapi Merkezi. Phase 3 Makutupora–Tabora (294 km) kandarasi ni Yapi Merkezi. Kumbuka, phase 3 imegharimu US$1.9 billion (Sh4.43 trillioni)

Mwigulu, Mkandarasi wako, China Civil Engineering construction corporation (CCECC), amekidhi wapi kupewa kandarasi ya US$2.1 bilioni (Sh4.89 trillioni) wakati miezi 17 amejenga lot Na. 5 kwa 4.4% pekee? Dar Es Salaam - Mwanza ujenzi wake jumla ni Sh14.9 trillion (US$6.4 billion).

China Civil Engineering construction corporation (CCECC) Tabora-Kigoma (411km) anachukua Sh6.69 trilioni. Zaidi ya nusu ya fedha zote ambazo zimetengwa kwa ujenzi wa Dar Es Salaam - Mwanza ujenzi wake jumla ni Sh14.9 trillion (US$6.4 billion). Ni UJAMBAZI hakuna shaka.

Utaratibu wa ununuzi katika kazi za ujenzi, ununuzi wa huduma na bidhaa kwa njia ya “single source” unasimamiwa na Kanuni ya 159, 160 na 161 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2013 kama zilivyofanyiwa marekebisho na Tangazo la Serikali Na. 333. la mwaka 2016.

Kwa utaratibu wa ununuzi wa ‘single source’, PPRA inatakiwa kuhakikisha wanapata wazabuni wenye sifa, uzoefu na uwezo wa kutekeleza mikataba hiyo kwa haraka na ndani ya muda wa mkataba na kuhakikisha Serikali inapata thamani ya fedha kwa manunuzi yote yatakayofanyika.

Athari za kutumia mzabuni mmoja kwa utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ ni kiini cha rushwa, uzembe, upendeleo, pamoja na uwezo mdogo wa mzabuni. Ndiyo sasa tunaona yanayotokea kati ya Mwigulu Nchemba na China Civil Engineering construction corporation.

RICHMOND; kampuni ilipewa zabuni ya kuzalisha umeme ikiwa haina fedha, wataalam wala ofisi. Ndiyo iliondoka na Edward Lowassa. Sasa China Civil Engineering construction corporation (CCECC) nao wamepewa zabuni katika mazingira kama hayo. Mwigulu anakiri kweli hawakuwa na fedha

Mfumo wa ushindani wa wazabuni wengi, ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi, huchukua takriban miezi mitatu au zaidi hadi kutangazwa mshindi. kutoa zabuni bila ushindani kunaleta upendeleo kwa baadhi ya wazabuni kwa gharama za watu wengine. Rushwa inaweza kutamalaki.

Kuna uwezekano mkubwa wa kutekeleza miradi chini ya kiwango. Gharama za mradi zinaweza zisiwe halisi. Kwamba zinaweza kuwa gharama kubwa zaidi, maana makubaliano ndio yanasimamia gharama za mradi. Tuwaonee huruma watu wetu. UMASKINI ni mkubwa.

MMM, Martin Maranja Masese
Mtikila!
 
Mwigulu, tuzungumze kizalendo kidogo!

Bajeti kuu ya serikali, hotuba yako, ukurasa wa 44, unasema serikali imeanza mchakato wa kutafuta mkandarasi wa kujenga kipande cha SGR (Tabora-Kigoma) 514km kwa US$2.1 bilioni (Sh4.89 trillioni). Wakati tunajua umewapa kandarasi
Kumekucha
 
Huwezi kuwaona UVCCM kwenye mada kama hizi. Wenyewe hupenda kutumia muda wao mwingi kusifia ujinga tu humu jukwaani.

Mama anaupiga mwingi! Sijui mama amejenga nini! Huku watu wanapiga hela kama hawana akili vile.
 
Mwigulu, tuzungumze kizalendo kidogo!

Bajeti kuu ya serikali, hotuba yako, ukurasa wa 44, unasema serikali imeanza mchakato wa kutafuta mkandarasi wa kujenga kipande cha SGR (Tabora-Kigoma) 514km kwa US$2.1 bilioni (Sh4.89 trillioni). Wakati tunajua umewapa kandarasi
Muwe mnawapa wabunge wanaoweza kuongea Bungeni hizi tips..

Ujue CCM huwa wanatumia hii miradi mikubwa kuiba pesa za Nchi..

Kwa staili hii,Katiba mpya inahitajika mapema Sana japo haitamaliza rushwa ila itapunguza.
 
Mwigulu, tuzungumze kizalendo kidogo!

Bajeti kuu ya serikali, hotuba yako, ukurasa wa 44, unasema serikali imeanza mchakato wa kutafuta mkandarasi wa kujenga kipande cha SGR (Tabora-Kigoma) 514km kwa US$2.1 bilioni (Sh4.89 trillioni). Wakati tunajua umewapa kandarasi
Hata taarifa ya mapato ya TRA aliyoitoa haiko sahihi kwa sababu Kuna sehemu inadai TRA hadi April wamekanya 17.2 Tln na sehemu nyingine wanaseama ni 19.4 Tln sasa kipi ni sahihi?
 
Ohoo kumekucha!

Uchambuzi ni sawa ila siwaelewagi mkishaanzaga kulinganisha linganisha... ili iweje sasa?
 
Back
Top Bottom