Elections 2010 Mbowe, Marando, Slaa, Zitto, Lissu, Mnyika

Dr asante sana kwa ufafanuzi mzuri, lakini tuhakikishie kuwa wabunge wetu hawatasusia vikao eti tu kwa vile JK anahutubia. CHADEMA ndio chama kikuu cha ushindani bungeni tunategemea serikali kivuli itaundwa na chadema kwa ushiriki wa vyama vingine. Kumsusia Rais wa NEC itamaanisha mmesusia serikali yake pia na hiyo itamaanisha wabunge wenu kukaa kimya kipindi chote watakapokuwa bungeni. maana wataihoji vipi serikali wasioitambua?

Kitu wananchi tunakisubiri kwa hamu ni CHADEMA kuthibitisha kuwa kweli ushindi wa JK sio halali kwa kutuonesha matokeo ya jimbo kwa jimbo kwa kulinganisha na yale NEC tujue uchakachuaji umetokea wapi na wapi.

Tunaisubiri hiyo BIG SURPRISE DR.
Luteni,
Thanks a lot. Napenda kukushukuru sana. Napenda tu nikuhakikishie kuwa Chadema is not just waiting for something to happen. i) Tulitangaza kutotambua matokeo na kutomtambua Rais aliyepatikana kwa kura kuchakachuliwa. ii) Chadema hatukuhudhuria Kutangazwa kwa matokeo na wala kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais. Maana yake tulikuwa tunapeleka ujumbe mzito kwa Rais aliyepatikana kwa mchakato usio halali na kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iliyokiri hadharani kuwa "ilifanya makosa mathalan waliponipa kura 3,789 iliyotangazwa na Judge Lewis Makame badala ya 22,021 iliyotangazwa na RO Geita. (Hatimaye walirekebisha). Maeneo mengi yalitangazwa kwa sura hiyo, japo hayakurekebishwa. Hali hii ni dhahiri iliashiria kuwa jumla ya kura za Dr. Slaa zilizokuwakitangazwa na Tume,ilikuwa au inabadilika au haifanani na Kura zilizotangazwa na RO katika Wilaya husika. Kasoro hizi baadhi zilirekebishwa wakati wa kujumlisha matokeo ya jumla, hivyo kasoro hii isiporekebishwa sura ya kura halisi ya nchi hii haiwezi kuwa sawa.iii) Tulilalamikia kubadilika badilika kwa idadi ya Waliojiandikisha kupiga kura mathalan kabla ya uchaguzi Tume ilitangaza idadi ya Wapiga kura 19,670,631 na siku ya matokeo ilitangaza idadi ya waliojiandikisha kuwa 20,137,303. Tumehoji tofauti hii hadharani. iv) Tumehoji idadi ndogo sana ya Wapiga kura 8,626,283 kati ya au 19 Millioni + au 20Millioni +) na kusababisha kiongozi wa nchi yenye watu zaidi ya 43 Millioni kuchaguliwa na idadi ndogo tu ya wapiga kura 5,276,822 kati ya wapiga kura halisi 8,398,394 tu. Hali hii inaashiria nini katika Governance? Hivyo kwa hoja hizi Chadema haikusubiri tu ...jambo literemke from heaven.
Hata hivyo katika mambo mazito kama haya, ambayo Tamko lolote linaweza kulifikisha nchi katika hatua ambayo haikutarajiwa, ni lazima Busara kubwa itumike, uvumilivu mkubwa na subira wakati Tafakuri ya kina inafanyika. Ndiyo hicho kinachofanyika Luteni.
Niseme tu subiri na Taifa lisubiri for a big surprise punde. Chadema ni chama kinachokwenda kwa mahesabu na hakikurupuki na wala hatakurupuka kamwe.
 
Dr. Slaa(PhD)

Kwanza nitoe shukurani zangu za dhati kabisa kwa kujitokeza ukumbini kwa mara nyingine tena ku share views na wana jamvi. Pili asante kwa majibu yako ambayo mbali ya kutoa dukuduku letu pia yanatia moyo kuwa kumbe mapambano bado yanaendelea hasa uliposema Taifa lisubiri for a big surprise.

Niliandika heading hii makusudi kabisa nikijua lazima kiongozi mmojawapo wa Chadema ataiona, na kwa kujibu kwako nafikiri ujumbe wangu umeshafika nilikokusudia sasa nitakunywa kwa raha. Ingawa umesema tusubiri for a surprise lakini nafikiri pia ndani ya hiyo surprise liwemo hili la ku boycott hotuba ya JK anayotarajia kuitoa kati ya J'nne na J'tano kama sikosei.

Kitendo hicho kitaleta impact kubwa sana kwa siasa za Tanzania sio kwake tu hata kwa mataifa marafiki zetu, hamtakuwa wa kwanza kufanya hivyo ni mabunge mengi yanashuhudia wapinzani wakifanya hivyo. Mfano ni CUF 2005 walivyosusia vikao na kutomtambua Karume hali ilivyopelekea kupigiwa kelele sana na mataifa ya nje na baadaye kuzaliwa kwa mwafaka no.2.

Najua Kikwete na CCM na Makamba hawataki hicho kitokee wanataka mhudhurie ili wawe na guts za kuutangazia umma na ulimwengu kuwa tayari mmeshayakubari matokeo kitu ambacho kitawakatisha tamaa waliowapigia kura nikiwepo mimi, mtaonyesha inconsistency kwenye maamuzi yenu. Mnaweza ku match-out wakati akianza na ku match-in akimaliza.

But all in all nawatakia vikao vyema vyenye busara ili mtoke na kitu kinatakacho konga nyoyo za wapiga kura wenu. Namalizia kwa kuwapongeza kwa kutoka na maamuzi ya busara kuhusu kambi ya upinzani bungeni, kwa akili ya kawaida tu huwezi kuungana na chama kilicho ndani ya serikali at the same time ukadai wewe ni mpinzani wa chama tawala.
 
What i expect CHADEMA MPs to do is to wait for Kikwete to walk in the Bunge chambers and while everyone is standing up, they(CHADEMA MPs) should just be seated and when JK is about to start his address, CHADEMA MPs should stand up and walk out in a show of defience. Once this mkwere is doen with his address, CHADEMA MPs can walk back in and take their rightful place as Official Opposition ikiwa ni pamoja na kujibu hotuba ya mkwere.
 
Hivi ni nani aliyewapa uhakika kuwa mnaebadilishana nae mawazo ni slaa wa kweli? au ni hiyo username?
 
Hata hivyo katika mambo mazito kama haya, ambayo Tamko lolote linaweza kulifikisha nchi katika hatua ambayo haikutarajiwa, ni lazima Busara kubwa itumike, uvumilivu mkubwa na subira wakati Tafakuri ya kina inafanyika. Ndiyo hicho kinachofanyika Luteni.
Niseme tu subiri na Taifa lisubiri for a big surprise punde. Chadema ni chama kinachokwenda kwa mahesabu na hakikurupuki na wala hatakurupuka kamwe.

Dr. Slaa, Peoples President! You said it all !!

Hii ni ahadi ambayo Watanzania wengi wanaisubiria. Mliitoa na mkairudia na sasa nashukuru kuwa unaitoa tena.

Tunaomba sana "Official Position na Statement" itolewe mtakapokuwa tayari. Watanzania tunaisubiri. Na hiyo statement iambatane na takwimu zitakazodhihirisha malalamiko ya CHADEMA ya kutokutambua matokeo ay Urais "beyond the reasonable doubt".

Hili likikubalika ni mtaji mkubwa sana wa 2015 ambapo inapaswa maandalizi yake yaanze sasa. CHADEMA may take all the time, but when you are ready, please come back with something very tangible, convincing and which both NEC and CCM cannot dispute, na hata kama wakidispute iwe ni katika propaganda tu.

Tuko pamoja Kamanda.

Amandla! Peoples . . . !
 
Hivi ni nani aliyewapa uhakika kuwa mnaebadilishana nae mawazo ni slaa wa kweli? au ni hiyo username?

Rainbow, wewe ni mgeni hapa JF?

Please take time hata kufanya research yako mwenyewe kwa posts za Dr. Slaa. A simple search can give u what u can believe.

Yes ni yeye. Wapo na wengine pia kama Freeman Mbowe, John Mnyika, Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo nk.
 
Nimeamua kuwataja nyie kwa vile naelewa mnaweza kunifikishia ujumbe wangu kwa viongozi na wana Chadema wote.

Kwanza nianze kwa kuwapongeza na kuwashukuru kwa kazi nzito mnayoifanya, pili ujumbe wangu ni mfupi tu kwa leo naomba kwa niaba ya kura zaidi ya milioni mbili za watanzania tulizowapa na zingine zikaibiwa muwe na msimamo wa pamoja.

Aliyekuwa mgombea urais Dr.Slaa(PhD) ameyakataa matokeo, nadhani wakati anaamua hivyo alikuwa na baraka zote za chama. Kama alikuwa na baraka za chama, pia chama kilikuwa na mikakati yake ya baadaye(plan-B). Sitaki kuamini kuwa mkakati wenu ulikuwa kutoyatambua matokeo tu basi baada ya hapo mkae kimya waiting for something to happen from heaven.

What I know you are still collecting data for evidence but whilst doing that please, DO NOT ATTEND THE INAUGRATION OF THE PRESIDENT'S SPEECH THIS WEEK. But if you decide otherwise you will have disappointed me and many of your supporters who voted you and Chadema on 31October 2010.

It is my plea.

Nimekuelewa vyema mkuu,

Nina la kuongezea ni kuwa CHADEMA sasa wangepanga pia mpango wa kwenda kutoa shukrani kwa wananchi walio wapigia kura na ndio jinsi ya kuendelea kuijenga ngome yao na kuchukua majimbo mengi mengi next 2015.

rainbow, wewe ni mgeni hapa jf?

Please take time hata kufanya research yako mwenyewe kwa posts za dr. Slaa. A simple search can give u what u can believe.

Yes ni yeye. Wapo na wengine pia kama freeman mbowe, john mnyika, zitto kabwe, kitila mkumbo nk.

kwa hiyo maana yako ni kuwa mbatia, lyatonga, maalim sef, lipumba, jk, rizwani, au makamba hawako hapa sio?
 
dr. Slaa(phd)
niliandika heading hii makusudi kabisa nikijua lazima kiongozi mmojawapo wa chadema ataiona, na kwa kujibu kwako nafikiri ujumbe wangu umeshafika nilikokusudia sasa nitakunywa kwa raha. Ingawa umesema tusubiri for a surprise lakini nafikiri pia ndani ya hiyo surprise liwemo hili la ku boycott hotuba ya jk anayotarajia kuitoa kati ya j'nne na j'tano kama sikosei.

Kitendo hicho kitaleta impact kubwa sana kwa siasa za tanzania sio kwake tu hata kwa mataifa marafiki zetu, hamtakuwa wa kwanza kufanya hivyo ni mabunge mengi yanashuhudia wapinzani wakifanya hivyo. Mfano ni cuf 2005 walivyosusia vikao na kutomtambua karume hali ilivyopelekea kupigiwa kelele sana na mataifa ya nje na baadaye kuzaliwa kwa mwafaka no.2.

Najua kikwete na ccm na makamba hawataki hicho kitokee wanataka mhudhurie ili wawe na guts za kuutangazia umma na ulimwengu kuwa tayari mmeshayakubari matokeo kitu ambacho kitawakatisha tamaa waliowapigia kura nikiwepo mimi, mtaonyesha inconsistency kwenye maamuzi yenu. Mnaweza ku match-out wakati akianza na ku match-in akimaliza.
.

tendo la kutoka nje na kurudi ndani ni kinyume na kanuni za maadili ya bunge na itasababisha wabunge wa chadema wasipewe posho zao za siku ambazo zinakaribia shilingi laki moja kwa siku KWA KILA MBUNGE MMOJA!!! na kwa jinsi walivyo wabunge wapya lengo lao la mwanzo ni kujipatia fedha ili kufidia gharama walizoingia kipindi cha uchaguzi!!!

kwa hali hiyo hakuna mbunge yeyote wa chadema atakae subutu kususia vikao vya bunge wakati jk anahutubia na habari nilizozipata sasa hivi zinasema kuwa jk anania ya kuanzisha utaratibu mpya wa kuhudhuria vikao vya bunge mara moja kwa wiki na hii itawafanya wabunge wa chadema washindwe kususia vikao kwa kuogopa ama kupoteza posho zao za siku, au mishahara yao minono, au adhabu ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa muda fulani na wakati huo huo itakuwa pigo kubwa kwa chadema kupoteza vyanzo vya mapato yake na matokeo yake ni kushindwa kulipa mishahara ya viongozi wake watendaji kama vile katibu wake mkuu na baya kuliko zote ni chadema kusambaratika na mungu apishe mbali hatungependa itokee!!!
 
Hata mimi nawategemea wafanye kama walivyofanya wajumbe wa baraza la wawakilishi kupitia CUF mwaka 2005, Karume alipoingia kuhutubia, wenyewe wali match out kuonyesha ulimwengu kuwa aliiba kura na si raisi halali. Wakifanya vinginevyo na ukimya uliopo sasa sisi wananchi tuliowaamini na kuwashabikia hatutawaelewa.
Hapo ndipo nitakapojua WATANGANYIKA TUMEBADILIKA NA KUWA WAKWELI NA WENYE KUMAANISHA :smile-big:
 
tendo la kutoka nje na kurudi ndani ni kinyume na kanuni za maadili ya bunge na itasababisha wabunge wa chadema wasipewe posho zao za siku ambazo zinakaribia shilingi laki moja kwa siku KWA KILA MBUNGE MMOJA!!! na kwa jinsi walivyo wabunge wapya lengo lao la mwanzo ni kujipatia fedha ili kufidia gharama walizoingia kipindi cha uchaguzi!!!

kwa hali hiyo hakuna mbunge yeyote wa chadema atakae subutu kususia vikao vya bunge wakati jk anahutubia na habari nilizozipata sasa hivi zinasema kuwa jk anania ya kuanzisha utaratibu mpya wa kuhudhuria vikao vya bunge mara moja kwa wiki na hii itawafanya wabunge wa chadema washindwe kususia vikao kwa kuogopa ama kupoteza posho zao za siku, au mishahara yao minono, au adhabu ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa muda fulani na wakati huo huo itakuwa pigo kubwa kwa chadema kupoteza vyanzo vya mapato yake na matokeo yake ni kushindwa kulipa mishahara ya viongozi wake watendaji kama vile katibu wake mkuu na baya kuliko zote ni chadema kusambaratika na mungu apishe mbali hatungependa itokee!!!
Hatuongelei ushabiki soma Kanuni za bunge zinasemaje si kusema Kikwete ana mpango wa kuhudhuria kila wiki hata kama kanuni hazimruhusu. Kuhusu posho hiyo si issue kubwa.
 
in this forum you seem majorit do not know how the government works. Non of you works with the government. Sheria nyingi hamjui. That is why mna shauti bila kujua mnafanya nini. You are all negative coz of your life style. Mnategemea
Changes kupitia net. Mje katika maisha halisi ya kwako binafsi. Unataka nini. What do you miss. Who is to help you. A politician or who.
 
hatuongelei ushabiki soma kanuni za bunge zinasemaje si kusema kikwete ana mpango wa kuhudhuria kila wiki hata kama kanuni hazimruhusu. Kuhusu posho hiyo si issue kubwa.

kama posho si issue kubwa kwa chadema, tunaomba ile ahadi ya elimu bure ianze sasa kwa michango ya wabunge wenu kusomesha angalau watoto mayatima ktk majimbo yao ndipo kauli ya posho sio issue iwe ni kweli!!!
 
Kaka acheni tu waendelee maana Zitto na wenzake hilo zoezi la kutoka hawatoliweza na hiyo italeta mpasuko tena. Najua akina Mnyika, Mdee, Mbowe, lema, n.k wataweza.
 
Hivi ni nani aliyewapa uhakika kuwa mnaebadilishana nae mawazo ni slaa wa kweli? au ni hiyo username?
Nikiona maelezo ya Makamba sihitaji kuwa na elimu ya mlimani kutambua kuwa alie andika/ongea ni Makamba...hivyo hivyo na shawishika kuamini hayo maelezo ni ya Dr W. Slaa rais wangu watanzania walio wengi
 
Luteni;

I have a different opinion. Wabunge wa CHADEMA wameshaapa kuitetea na kuilinda Katiba. Uzinduzi wa Bunge ni sehemu ya Matakwa ya Katiba. Wasipohudhuria wanaweza wakaleta mtafaruku wa kuanza kuleta mgawanyo kwa wanachama na mashabiki wa CHADEMA. Pia watakosa uhalali wa kuja kuchangia juu ya hiyo hotuba kikao kijacho.

CHADEMA sasa hivi ni official opposition party, lazima wawepo na waje wajibu hotuba hiyo officially.

However, naafiki kuwa Dr. Slaa kama anazo substantial evidence, asitambue matokeo kama haki yake yeye mgombea. Hii itaendelea kuwapa pyschological pressure CCM na JK. With time na kama Serikali itaendelea kufanya blunders, basi kuna uwezekano support kwa Dr. Slaa ikaongezeka.

Hahahaaa hoja yako kwa wansaikolojia tunaita so objective.. Yaani woga wa kimaendeleo... Unadhani itawakost kama wakisepa mkutano sio na JK... Lakini tutambue kuwa katiba ya nchi inamtambua raisi aliyechaguliwa na wananchi vinginevyo siye.... kwa hiyo CHADEMA wanaamini JK aliiba kwa hiyo kama wanataka kulinda katiba ni lazima watetee ukweli wa katiba na si vinginevyo!!!
 
Luteni,
Baada ya Tume ya Taifa kumtangaza JK kuwa ndiye mshindi, JK ndiye rais wa nchi, ukubali matokeo, usikubali matokeo, JK ndiye Rais wa nchi. Umtambue, usimtambue, haibadilishi kitu, JK bado ndie rais halali hata kama ameshinda kwenye uchaguzi ambao sio huru na wa haki, mshindi akishatangazwa ndio mshindi na wengine wote mnabwaga manyanga chini, mnasalimu amri na kuanza kujipanga upya kwa 2015.

Kitendo cha kukosa kusema chochote siku ya kutangazwa matokeo, was a mistake na missed opportunity kutoa duku duku lao la moyoni, sasa unanaka wakose na another opporturnity ya kutoa kauli yao kama kiongozi wa upinzani bungeni.

Usiwachuuze Chadema, afterall kususa ni tabia za kike, za kiume ni kupambana!.

Pasco;

Wakati wa matangazo ya Tume hakukuwa na room for negotiations, Dr Slaa alipeleka pingamizi uhesabuji usimamishwe; tume haikujali iliendelea; sio kama Chadema haikufanya kitu; Naungana na Luteni; Rais akiingia, akimaliza kusalimia, basi wabunge mmoja mmoja waanze kutoka nje, na tukio hilo liwe recorded na rais mwenyewe alione kama lilivyo maana kilichofanyika ni uhuni;

Nimegundua kilichofanyika; kura za JK zilikuwa zinabakizwa zilivyi ila kura za Dr Slaa zikawa zinapunguzwa kwa kiasi kikubwa ndio maana mmpaka ikawa hiyo 42% turnout. dangerous president, thief, sickness inauma sana hii
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom