Mbowe: Lowassa ni dhaifu, ni bubu

Status
Not open for further replies.
List of shame ilitangazwa September 2007 huyo unayemtaja yumo au hayumo?

 
Lowasa anaitwa fisadi ,mimi sikatai ila shida ni wale wanaomwita fisadi ,wao ni akina nani kama yeye ni fisadi.
Naomba mtu mmoja mwenye kumbukumbu nzuri aorodheshe matukio ya ufisadi ya kutisha baada ya Lowasa kujiuzulu na tuone ni nani hakuwa ndani ya serikali au bunge anaegombea uraisi.
Na kama alikuepo alifanya nini kuonyesha jamii kuwa hakupendezwa na hayo.
 
Nani alijitoa kwenye serikali na kwenda kwenye media na kusema mimi najiuzulu nafasi yangu ndani ya serikali hii kwani siwezi kuwa sehemu yake kwa ufisad huu.
Aidha wa escrow au wowote ili sasa aje nasi tujue huyu si sehemu ya uchafu
 
Kama nimemwelewa Mbowe vizuri haimaanishi anataka achaguliwe yeye badala ya EL.
 
Dj Clay F akiwa katika ubora wake. Dj asidanganye watu, Lowassa ilikuwa tumaini la UKAWA, baada ya kutoa msimamo kuwa hawezi kuhama CCM, ndipo Dj Clay F anakuja na huu utumbo.
 

Ndio maana wenye Akili tunasema mwisho wa ccm ni october
 
Chama cha mapinduzi kimejaa wahuni,mwaka 2005 ni Lowassa na jk walitembea nchi nzima wakisema " Maisha bora kwa kila mtanzania"
Mwaka 2010 wakaja na Ari mpya,nguvu,mpya na kasi mpya walimu waliokuwa hawana nyumba za kukaa hafi leo shida ni ileilel
Uhuni uleule wa watu walewale,wanaanza nangojera za " safari ya matumaini"


Watanzania hatuhitaji kutiwa matumaini,kwani nchi inakila kitu,

Wakati watoto walikuwa wanashinda njaa shuleni Lowassa alikuwa waziri,

Wakati watoto wa shule wakikosa vitabu,madarasa na madawati Lowassa alikuwepo,

Wakati umeme wa mgawo na wakutegemea mvua Lowassa aliluwa waziri,

Wakati ajira za watanzania zikizamishwa kwa kuuzwa viwanda vyetu vya nguo,viatu,ngozi,sukari Lowassa alikuwepo,

Wakati nchi ikiendelea kukumbwa na rushwa,Lowassa alikuwepo,

Wakati Azimio la Arusha likivunjwa zanzibar ambalo ndilo liliwadhibiti wezi wa ccm Lowassa alikuwepo,

Wakati ccm ikishindwa kukusanya kodi,na kuendelea kukopa,Lowassa alikuwepo na kwa kujua mwelekeo wa Lowassa,juzi amesema" tunaweza kutumia geai kukopa fedha ulaya"


Huyu anaanza kuwaza kukopa,watanzania tutegemee nini,kwa rais aliyemiongoni mwa waovu na anaunga mkono kukopa huku deni la Taufa likiongezeka?
 

Mkuu hapo si nchi itauzwa kwa matajiri na wahindi.
 
"Ikulu ya watanzania inahitaji maskini mwemzao,si mtu anayetaka kuwa rais ili aongeze utajiri kutoka ng'ombe 1000 hadi 10,000!


Akiwa anajua kuwa magonjwa ni chanzo kikubwa cha umaskini,akiwa waziri wa maji,yako wapi mahi Lindi,mtwara,Dar es salaam,morogoro,Tanga,kigoma,Tabora,Mwanza,Mbeya,Magu,shinyanga Lowassa yako wapi majisafi na salama? Au visima ambavyo kila mtu anachimba ndio maji uliyoleta?


Magu tu na Bunda iliyokaribu na ziwa viktoria ilikushinda sembuse Ikulu?

Hatuhitaji dalali wa ikulu
 
Asema lowasa ni dhaifuuu!!!! Jamani siyo Mimi kamuulizeni Mbowe.
 
Mh.Mbowe amenukuliwa na Tanzania Daima akimchana Mh.Lowasa kuwa ni mgombea dhaifu na bubu wa kukemea ufisadi.

Amesema UKAWA hawawezi kuwa nae,hivyo asiwatishe CCM kuwa ana nafasi UKAWA.

Source:Tanzania Daima page no.5

Eti chanzo cha habari ni gazeti la Tanzania daima....!! Kwi kwi kwi kwi kwi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…