Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 297
Mimi nadhani, kwa kuwa Mh. Mbowe ni mfanya biashara wa kimataifa basi ataweza kuwaeleza tu ni nini alichokuwa anafanya na zile transfers kutoka Dubai kwenda Hong-Kong, kama ni za ukweli. Tusubiri matokeo ya uchunguzi.
Tusimsakame mleta mada au gazeti lenyewe kwa sababu wameeleza walichokipata toka Polisi - kama ni kweli.
Wasiwasi wangu ni kile kipengele cha kuwa CHADEMA ilipatiwa ruzuku kutoka kikundi cha Japan ya $300,000. Kwa kuwa CDM ni chama cha siasa kinachopata ruzuku kutoka serikalini basi accounts zake zote zinapaswa kukaguliwa na Mkaguzi mkuu wa serikali.
Katika huu ukaguzi kama ikionekana kuwa account za CDM hazikupata hizo pesa na badala yake waJapan wakisema waliziingiza kwanye account ya Mh. Mbowe ilioko Dubai basi itabidi Mh. Mbowe aeleze alizifanyia nini hizo hela za ruzuku (sidhani kama ni hivyo).
Kama ni kweli bado sio lazima kuwe na kosa. Inawezekana uongozi wa CDM ulikubaliana kuwekeza hizo hela nje ili zizaliane kidogo kabla ya kuzileta hapa Tanzania. Hapa CDM itabidi waoneshe huu mlolongo wa uwekezaji huko nje kiuwazi katika mahesabi yao.
Ni muhimu hili suala liwekwe wazi haraka sana ili liondoe haka kawingu kalikomzunguuka Mh. Mbowe. Nasema ni muhimu kiwingu kiondoke kwa sababu CDM ina safari ndefu sana kurudisha mvuto iliokuwa nao kabla ya Julai, 2015.
Mh. Mbowe ni mtu smart sana na hawezi kufanya upuuzi utakaomletea kashfa za money laundering. I hope hii habari haina mashiko. Tunahitaji waTanzania wanaojiamini kuwekeza nje kama huyu bwana. Kuna watu wa nnje chungu nzima wanawekeza hapa Tanzania, kwa nini na sisi tusiwekeze nje?
Wana CDM Kweli ni Mataahira, Hata Mbowe Akijinyea Wakamuona kwa Macho Yao, Wao Bado Watasema Kajamba tu.
Yanayosemwa Sio tena porojo za mitandaoni, ni gazeti lililosajiliwa limeyaandika, kwa nini Mbowe asiyakanushe au kwenda mahakamani kama sio ya kweli?