Mbowe kuiuza CHADEMA kwa mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe kuiuza CHADEMA kwa mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nickname, Mar 30, 2011.

 1. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Katika kupitia vichwa vya habari vya magazeti mbalimbali leo hii,nimejionea kichwa kimoja cha habari katika gazeti moja.

  Gazeti hilo linadadavua mpango wa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe(Mb) wa kuiuza CHADEMA kwa mafisadi nchini Tanzania na vikao vinaendelea mjini Arusha,Tanzania.(Source : SautiHuru)

  Update:

  Na Mwandishi wetu
  Mmoja kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi(jina tunalihifadhi kwa sasa )anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya siri na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe ili kuingia ubia na chama hicho.

  Inaelezwa kuwa ,lengo la kigogo huyo ni kukiziba mdomo chama hicho kisimrushie makombora ya ufisadi kama walivyowahi kumrushia siku za nyuma.

  Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa kigogo huyo wa CCM amekuwa na mawasiliano ya siri na ya karibu na Mbowe huku vikao vingi viifanyika ndani ya hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Arusha (jina tunalo)

  Imebainika kuwa ndoa hiyo ya siri ni ya wanasiasa hao wawili,lakini ikilenga uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kigogo huyo wa CCM amemuahidi Mbowe kwamba wataunda "serikali ya umoja wa kitaifa" msaidia kwa kuacha kumuandama kwa tuhuma za endapo Mbowe atasaidia kuacha kumuandama kwa tuhuma za ufisadi na kuwadhibiti viongozi wengine wa chama chake,kutofanya hivyo kwenye maandamano na mikutano yao ya hadhara,pamoja na kwenye mahojiano na vyombo vya habari.

  Uchunguzi zaidi umebaini kuwa tayari kigogo huyo amempa mwenyekiti huyo wa CHADEMA kiasi kikubwa cha fedha ili chama hicho kinapoendelea na kampeni yake ya bomoa-bomoa mafisadi yeye asiguswe kabisa,kama hatua ya kumfikisha ndoto yake ya kutaka chama tawala kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya urais.Chanzo chetu cha uhakika kikiongea na Sauti Huru kwa sharti la kufichwa jina lake kimedai " huu ni mpango unafanywa kwa siri kubwa na ninajua hata mhusika (anamtaja) akijua habari hii imetoka atafadhaika sana"

  Habari zaidi zinadai kwamba kigogo huyo amefikia hatua hiyo baada ya kusoma alama za nyakati na kuona kwamba uwezekano wa mwenyekiti wa chama chake kumuunga mkono ni mdogo,hivyo hatoweza kupenya katika kinyang'anyiro cha uraisi 2015.

  " Huyu bwana amesoma alama za nyakati ,ameona kabisa uwezekano wa kuungwa mkono na mwenyekiti wake(wa CCM) ni mdogo sana hivyo ni lazima atafute njia nyingine hata kama njia hiyo itakuwa na madhara kwa chama chake", kilieleza chanzo hicho na kufafanua;
  "Si kwamba hajui mwenyekiti atalalia wapi,anajua lakini yuko tayari hata kukisaliti chama ili wote wakose.ivi ninavyoongea nanyi watu hawa wana mawasiliano ya kila mara juu ya suala hili ila Mbowe kaweka ngumu kuwa lazima waandikishiane ajue kabisa endapo (kigogo huyo atafanikiwa kuingia madarakani basi wataunda government of unity(serikali ya umoja wa kitaifa)".

  ...Aidha imefafanuliwa kwamba habari hizi zimeweza kumgusa hata Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe,lakini kwa namna ya pekee Zitto ameweza kudhoofisha mkakati huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni 'unafiki kwa Mbowe'
  "Mtakumbuka siku za hivi karibuni Zitto alishutumiwa na chama chake kwa madai ya kuwa na uhusiano wa mashaka na Idara ya Usalama wa Taifa.Chadema wamekuwa wakidai kwamba Zitto anatoa siri za chama chao nje na hata kumuundia kamati ya wazee kumshauri?" alihoji.
  Aliendelea :" Kilichotokea katika kamati hiyo siku walipokutana na Zitto ilikuwa tofauti kabisa,Zitto akawabadilishia mada pale alipowaambia wazee,'jamani ugomvi wangu na Mbowe ni pesa za chama,anatumia chama hiki hiki kupata fedha toka nje ya nchi na ndani ya nchi,lakini ninapojaribu kumkosoa kuwa tabia hiyo si nzuri kwa mwenyekiti wa chama ananijia juu,nyie mnajua kuwa amepokea fedha mamilioni kutoka kwa(anamtaja kigogo huyo) kwa ajili ya kutunyamazisha tusipige kelele za ufisadi dhidi yake?' "
  "Hivi hamjui tayari anafanya mazungumzo na mtu wa CCM kwa ajili ya power sharing ya mwaka 2015?"
  Kwa mujibu wa habari hiyo ni kwamba kigogo huyo atafanya kila liwezekanalo CCM kinamteua kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi;lakini anajua hilo litawezekana endapo kelele za ufisadi dhidi yake zitamalizika.
  " Huyu mtu ni mjanja sana na kwa sasa ana nguvu na mtandao mkubwa ndani ya CCMunaoweza kumfanya ateuliwe na chama kuwa mgombea, si hilo tu anajaribu hata kutafuta nguvu nje ya nchi ili endapo akikataliwa aweze kuwa na cha kuieleza jumuiya za kimataifa,"
  "Na kwa hatua aliyofikia ni kwamba endapo hatoteuliwa hasa kutokana na ufisadi wake,yuko tayari hata chama chake kipoteze nafasi ya uraisi kitu ambacho kinaonyesha kuwa hana sifa za kiuongozi isipokuwa ni tamaa ya utawala."

  My Take: Wale viongozi wa Chadema na wakereketwa waliopo humu JF watuthibitishie hii habari kama ni kweli.
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  yaani unachekesha sana ..... ukienda kwenye meza za wauza magazeti utakuta watu wamejaa wanasoma vichwa vya magazeti katika front page halafu wanatoka na kwenda kuhadisia .... lakini ndani ya gazeti kwenye habari yenyewe unakuta ni tofauti

  ndugu yangu kuwa makini na upende kununua gazeti na sio kutumbua macho kwenye meza za magazeti ....
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,518
  Likes Received: 5,652
  Trophy Points: 280
  sauti huru(source) ndio uthibitisho full stop! Na waulize wanauziwa nini,assets za cdm,wanachama wa cdm? Waambie bora wamesema TRA walambe kodi yao!
   
 4. R

  Rangi 2 Senior Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwani CHADEMA ni mali ya Mbowe? Acha kutuchefua.
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,518
  Likes Received: 5,652
  Trophy Points: 280
  waulize wakinunua lazima wauziwe na goodwill maana cdm inapendwa bwana! Lakini waambie kabla hatujaiuza cdm watoe maelezo watavyoitunza hiyo goodwill,tukiridhika na mipango tunaipiga bei tena kwa faida kubwa!
   
 6. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Umejibu hovyo kabisa,Usiniponde mimi mimi sijatunga hiyo habari,napenda kujua kama ni ya kichochezi au vp


  Katika My Take nataka kujua kuhusu habari hii,mtuambie nyie wanachama na viongozi wa Chama chenye nguvu kama hii habari ni ya kweli sio unaniponda mimi.
   
 7. H

  Haika JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Nadhani unajua fika vichwa vya habari siku hizi havikupi mwanga wa habari, ili upate jibu zuri la kueleweka, kutokana na swali lako, please scan, au retype hio habari hapa ndio wataalamu watakuambia kama kuna ukweli au ni yale mambo yetu ya kawaida.

  (kama usipoitoa watajua kwamba na wewe ni mmoja wao)
   
 8. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sauti Huru sio gazeti la kujadiliwa humu. Hili linamilikiwa na mmoja wa watuhumiwa wakubwa wa ufisadi Subhash Patel. Habari hiyo lazima itakuwa ni ya kutungwa.
   
 9. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Inawezekana kuwa kweli lakini hakuna logical flow. Mbowe auze Chadema ili apate nini? Huko kuuza anamuuzia nani? Of course ni vigumu kwa mkereketwa na mfuasi wa kawaida kujua hali ya mambo kwenye jambo kama hili ila kwa ujumla wake MANTIKI INAKATAA kuuona ukweli kwenye hili jambo.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Jamani... JF naona vichaa wanaongezeka kila siku, hivi ni ugumu wa maisha au ni ugumu wao wa kuelewa chanzo cha shida zilizowafanya warukwe na akili?
   
 11. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbowe familia bora. hana dhiki za kina mrema na cheyo za kuvizia minuso ikulu.
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  very low .... mbona hukununua hilo gazeti .....ubongo wako umejaa silicon
   
 13. m

  msosholisti Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ulikuwa hujui?, kaachiwa na mkwewe mtei. Pole sana.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yah kweli... kaachiwa aongoze chama ili kukomboa watu wenye mgando wa akili na mtindio wa mawazo kama wewe
   
 15. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kwa nini weye uliyesoma usitujuve?....mimi kama mwanachama nakwambia sio kweli
   
 16. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Bila kutaja CDM siku haijakamilika kwao..,na bora hata zingekuwa ishu za msingi..aaghr
   
 17. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuuu cdm mnatufanya kitu mbaya sana ndo maana tunataka tuwachanganye!
   
 18. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Mie nilikuwa najuwa ni mali ya ukoo na mbowe karithi kutoka kwa babamkewe! Au sivyo hivyo?
   
 19. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Na huyu babamkwewe aliirithi kwa nani?
   
 20. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Nickname, c'mon Great Thinker haishii kusoma vichwa vya habari vya magazeti yaliyo kwenye display table ya ventor bali hununua kupata undani wa heading!!! Umeidhalilisha JF na nashauri mod, ban mtu huyu!!! Kichwa cha habari usome wewe sijui kwa jirani yako kwenye daladala au wapi then maelezo utake JF!! %$$%^$%^ zako we!!
   
Loading...