Wakuu,
Leo na sasa hivi mzee wa anga na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe yupo Mjini Bukoba akiendesha operation ya kufungua matawi na kufunga bendera katika maeneo ambayo awali wenye kumiliki maeneo hayo walikuwa wana CUF.
Hadi sasa hivi nipo hapa kwenye cafe na nje pamefurika watu wakishuhudia Mbowe akivunja vijiwe vyote vya CUF na kusimika CHADEMA.
Anaongozana na mwanachma wake mpya Lwakatare.
Lakini kikubwa ninachokina hapa ni kuwa kuna maandamano pia ya wana CCM eti wanapokea Beno Malisa, yani hapa ni SIASA kwa mtindo mmoja jamani waombee wana Bukoba
Mbowe endelea kufungua matawi Mzee kuandaa viwanja vya 2010.Pia fuatilia kichwa kingine Hamad Rashid kutoka CUF(CCMb) ili kuimarisha timu yetu ya kuinyoa CCM 2010.
Wakuu leo mchana Mh. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, akiwa njiani kuelekea Biharamulo amefanya ziara ambayo haikutangazwa ili kufungua matawi mapya ya chadema hapa mjini Bukoba na kutoa kadi kwa wanachama wapya.
Amepita maeneo mengi kwa miguu akifanya zoezi hilo la kufungua matawi, akigawa kadi mpya za wanachama na kutoa hotuba ndogo kila mahali huku akikuta umati mkubwa wa watu ukimfuata.
Baada ya hapo ameondoka kuelekea Biharamulo kwa ajili ya kuungana na wana Dr Slaa ambao tayari wako katika kampeni ya uchaguzi wa jimbo la Biharamulo.
Wananchi wakimsikiliza Mbowe
Wananchi wakimfuata Mbowe katika safari za kwenda kufungua matawi.
Akipandisha Bendera ya Chadema kwenye tawi jipya
Hapa akipandisha bendera ya Chadema huku akishusha bendera ya chama kingine......😀😡🙁
Akitoa kadi kwa mwanachama mpya wa chadema
Akitoa kadi kwa mwanachama mpya wa chadema
Mbowe akihutubia katika moja ya hafla za kufungua matawi
Mbowe akihutubia katika moja ya hafla za kufungua matawi
Na kama anafungua matawi ya chadema, sawa lakini anajua kuwa Biharamulo wamejiandikisha wapiga kura wangapi na ni wangapi actually watakipigia kura chama chake ili kupata ushindi?
kwa maoni yangu ushindi wa Biharamulo ungewaboost kweli wana Chadema, lakini kama wataishia tu 'kuizika CUF' bila kuwa na mikakati ya ushindi, walau kwa jimbo hilo, basi wasitegemee maajabu 2010.
na mwaka lwakatare akihama chadema .......vijiwe vitabadilishwa kuelekea chama atakacho kwenda.
lwakatare hakupigia debe chama, hujipigia mwenyewe tu.........bora kuruhusiwe mgombea binafsi tujue moja
vyama vya siasa tanzania bado vina safari ndefu.
Hii inanikumbusha jambo!
Nani aliangalia kipindi maalum cha ITV jana usiku jinsi watu wanavyofukuzwa kwenye vijiji? Yaani vijiji vinafutwa just like that, kupisha ardhi itumiwe na wawekezaji. Nilidhani kipindi kitakuwa kifupi kama ilivyo kawaida, ila nilishangaa wanatueleza yanayotokea Moro, inafuata Mtwara, mara huku.... Duh!
Kama Kikwete alikuwa anaangalia hicho kipindi nadhani alifunga TV.
It is my hope that ITV would put these important footage on the Internet soon.