Mbowe katika picha Bukoba

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Hizi ni picha za Mh Mbowe akiwa mjini Bukoba juzi. Inasemekana alihutubia mikutano kadhaa katika kata mbalimbali za mji wa Bukoba na kuvuna wanachama wengi waliokuwa wakinunua kadi kwa shilingi 500 tu. Na inasemekana anatembelea wilaya zote za mkoa wa Kagera. Kitu sijui je vijijini atafika? maana viongozi wa vyama vya siasa ikiwamo sisi m..... huishia mijini tu!

DSC_1595.jpg

DSC_1596.jpg

IMGP8689.jpg

IMGP8690.jpg

IMGP8691.jpg

IMGP8693.jpg

IMGP8692.jpg

IMGP8694.jpg
 
Wewe! huogopi watetea mafisaddi humu wakiziona hizi picha watakujia juu sana!

Good news ni kwamba Wahaya sio sawa na Wasukuma hawa wana msimamo bwana. Ingekuwa ni ndugu zetu wasukuma ningejua ni bure tu wakipewa tshirt tu wamekwisha
 
Hivi kuwa na MSIMAMO ni KUHUDHURIA MIKUTANO au...?

Kitu ninachokikubali ni kuwa hizi attempts za kuwatembelea wananchi ni nzuri za kuzungumza nao chochote kinajenga iman ya wananchi....ile sense ya kusema hawaji hadi uchaguzi inaondoka.....

Samahani Hivi Huyu Mkuu Shule "Special" aliyoandaliwa ameshamaliza au yupo ktk "Utafiti"
 
Inatia moyo sana kwamba watu wana hamu ya kusikia nuru mpya!

Jamani ufisadi wa CCM ulipo tufikisha yatosha, wakae pembeni kidogo warekebishe makosa yao.
 
Good news kwa wapenda mabadiliko kwa gharama yoyote maana maisha bora hayaji kwa imani potofu eti CCM ndio chama pekee kuongoza; pambana na wananchi mh mbowe usisumbuke na wanaopiga kelele mjini-2010 kuna kazi kubwa
 
Wewe! huogopi watetea mafisaddi humu wakiziona hizi picha watakujia juu sana!

Good news ni kwamba Wahaya sio sawa na Wasukuma hawa wana msimamo bwana. Ingekuwa ni ndugu zetu wasukuma ningejua ni bure tu wakipewa tshirt tu wamekwisha

Mzee tunatafutana ubaya eeehh...you have been warned!
 
Ohh sorry. Update nilizopata ni kwamba huyu jamaa kaamua kweli kweli maana anachanja mbuga mpaka vijijini. Si mchezo tena. Anawavuna wanachama na kujenga chama humo vijijini. Kwa mwendo huu tutafika tuendako.
 
Inatia moyo sana kwamba watu wana hamu ya kusikia nuru mpya!

Jamani ufisadi wa CCM ulipo tufikisha yatosha, wakae pembeni kidogo warekebishe makosa yao.

Nakuunga mkono ndugu yangu, kwa vyovyote vile MUNGU akinipa uzima kuwepo kwenye uchaguzi mwakani siipigii CCM kura, hata iweje. Enough is enough
 
Ohh sorry. Update nilizopata ni kwamba huyu jamaa kaamua kweli kweli maana anachanja mbuga mpaka vijijini. Si mchezo tena. Anawavuna wanachama na kujenga chama humo vijijini. Kwa mwendo huu tutafika tuendako.

That's good news man. I like that. Tanzania need to dare to elect Chadema or other part but not CCM
 
Jamani katika mikutano wingi wa mabendera nao unasisimua uwanja ,hapa nimetafuta bendera za Chadema sijaona hata moja.
 
Yes inatia moyo, CCM nao wameanza kuiga mtindo wa helicopiter. Hapo wananchi mjue jinsi CCM yenu wasivyo na mbinu yoyote ya ubunifu. Pamoja na mkutano huo na wingi wa watu kazi kubwa zaidi ni kushinikiza mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ajiuzuru maana inasemekana bado ana kadi ya CCM. Wanaomfahamu wanasema ni CCM damu.
 
Huyu hana jipya zaidi ya kuhangaikia maslahi yake...... Tanzania hatuna watu wenye nia na uchu wa ukombozi kwani kila anayejifanya kutafuta huo upenyo wa kujenga jamii mpya naishia kushibishwa hapo na kusahau alikotoka! huyu analinda maslahi ya biashara zake hana lolote jipya la usoni.....
 
Ni haki yako ya kidemokrasia,inaelekea umeshiba sana itikadi ya Katibu Mkuu Makamba na huo ni mtizamo wako.Hongera Kamanda Mbowe kwa kuwafuata wapiga kura na walipakodi wa vijijini endelea kueneza sera za CHADEMA ili wazipima na kutofaotisha na za vyama vingine.Nakutia moyo endelea wafuasi wako tupo na mimi naendeleza kueneza huku Kyela.
 
Huyu hana jipya zaidi ya kuhangaikia maslahi yake...... Tanzania hatuna watu wenye nia na uchu wa ukombozi kwani kila anayejifanya kutafuta huo upenyo wa kujenga jamii mpya naishia kushibishwa hapo na kusahau alikotoka! huyu analinda maslahi ya biashara zake hana lolote jipya la usoni.....

Nashangaa kwa karne hii duuu...??

Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa!

Bravo Mbowe bigup! Endelea kuamsha walio lala, nani ajuaye? huenda wewe ndiye mkombozi mpya wa kututoa katika makucha ya mkoloni mweusi CCM!
 
Back
Top Bottom