Mbowe: Jk aungwe mkono na kila chama

Mbowe: Jk aungwe mkono na kila chama

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,573
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, FREEMAN AIKAELI MBOWE ameviomba vyama vyote vya siasa kuunga mkono Hotuba ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ya kuvitaka vyama hivyo kutanguliza maslahi ya Taifa badala ya maslahi ya vyama vyao wakati wa Bunge la Katiba ambalo wajumbe wake watatangazwa na mh.Rais leo tarehe 07/02/2014 na kuanza rasmi vikao vyake tarehe 18/02/2014 mjini Dodoma.
 
Mbowe ni mnafiki akiwa kwenye majukwaa anazungumza uchochezi lakini akikutana na viongozi wenzake anajifanya mwema hafai kanisani wala msikitini.
 
Mbowe ameanza kukua sasa.
Mkuu kukua huyu jamaa ni bure kabisa siku zote akiwa kwa jk anajifanya mwema akiwa kwenye majukwaa ya kisiasa analeta uchochezi ili apate sifa za kijinga.
 
Mbowe ni mnafiki akiwa kwenye majukwaa anazungumza uchochezi lakini akikutana na viongozi wenzake anajifanya mwema hafai kanisani wala msikitini.
Simiyu Yetu
===>Tatizo Baba Riz anachozungumza sicho anachokitenda,subiri asikie Nepi au Mamvi kapayuka tofauti na alivyosema uone kama kesho tu hajabadilika,
===>Kifupi hawezi kusimamia anachokisema!
 
Last edited by a moderator:
Sijawahi kuona Rais aliyekosa msimamo binafsi kama huyu!
 
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, FREEMAN AIKAELI MBOWE ameviomba vyama vyote vya siasa kuunga mkono Hotuba ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ya kuvitaka vyama hivyo kutanguliza maslahi ya Taifa badala ya maslahi ya vyama vyao wakati wa Bunge la Katiba ambalo wajumbe wake watatangazwa na mh.Rais leo tarehe 07/02/2014 na kuanza rasmi vikao vyake tarehe 18/02/2014 mjini Dodoma.

Sisi tunataka muundo wa serikali mbili, na huo ndio msimamo wa CCM, "Raisi J M Kikwete 2/2/2014: Mbeya"
 
kila mtanzania anaipenda nchi hii atataka serikali mbili, hao wa serikali tatu wana lao jambo.
 
Mbowe ni mnafiki akiwa kwenye majukwaa anazungumza uchochezi lakini akikutana na viongozi wenzake anajifanya mwema hafai kanisani wala msikitini.

Mkuu unajuwa ikulu kuna juisi na mambo kama hayo, sasa huku majukwaani njaa kali inabidi atokwe povu ili wananchi watoe sadaka!
 
Back
Top Bottom