Kweli. Chadema si ajabu kikawa ni chama kizuri ila wengine tukimuangalia Mbowe, au Lema tuna conclude ni genge la wahuni illiterate.
Ni kweli, a new chairman is needed. Angalizo... Asiwe Mchaga wala mwenye undugu na Mtei, Mbowe.
Twende taratibu kijana. Umewahi kuisoma katiba ya ccm pamoja na ilani ya ccm? Matendo yanayofanywa na baadhi ya wanaccm ni kinyume kabisa cha katiba ya Chama pamoja na ilani.ccm katika katiba yao inaweka utu mbele pamoja na uzalendo wa nchi.naamini hata katiba ya chadema inaelekeza mambo mazuri.watu ndio wanafanya mambo mabaya.nimekueleza haya ili utambuwe kuwa mtu msafi hana Chama.kama ana nia nzuri atatekeleza uongozi wake kupitia Chama chochote. Chadema walifanya makosa makubwa kumchukua mtu ambaye wote tunajuwa Si muadilifu na hakuwa msafi.ndo maana nikasema hufai kujihusisha na vyama vya kisiasa kwani mawazo yako yanakutuma kua anayegombea uraisi kwa chama fulani ndio anashika na kuitawala katiba ya chama. CCM haina sera za kunishawishi nipo ndani ya Chadema kwa zaidi ya miaka 12 sipo kwa ajili ya lowassa..
Awepo au asiwepo bado nitaendelea kua part of Movement for Change kabla ya lowassa kuwepo tumehubiri mabadiliko na itabaki kua hivyo
Upinzani utashamiri tu ikiwa katiba mpya itapatikana yenye kuondoa umungu mtu na tume huru ya uchaguzi na muungano ufumuliwe na kusukwa upya ikiwa bado twauhitaji anyway. Dola iongezewe watu wenye fahamu kwa kufanya intake zao zipate watu wenye pass za hali ya juu na siyo failures. Hapo ndiyo ubabe utakoma na uchaguzi utakuwa huru na haki..
Hapana Mkuu, ACT unayoisema inapata wapi ongezeko la wanachama ilhali ina Mbunge mmoja tu !! Mbowe kafanya mengi katika kikijenga chama, katika uchaguzi huu amefanikiwa kviweka pamoja vyama vinne vyenye itikadi tofauti na wote tumeshuhudia kilichoendelea na idadi ya wabunge wa upinzani walipatikana pamoja na mazingira yasiyo sawa ambayo wamekabiliana nayo.
Hata kama CDM haijashinda Urais, lakini kuna chembe ya mbegu imepandwa kwa Watanzani na itaendele akuchipuka taratibu miyoni mwao ili mradi tu wabunge wa UKAWA waisimamie Serikali ipasavyo. Pamoja na mazuri aliyofanya Mhe. Mbowe bado kuna umuhimu wa kufanya Uongozi wa Chama uwe wa Kitaifa ambao wananchi wa Tanzania wanajiona kama sehemu ya chama kupitia viongozi kutoka maeneo yao.
Kwa mfano chama kama ccm Mwenyekiti anatoka Pwani, Makamu - Iringa, Itikadi na Uenezi - Mtwara; Katibu Mkuu - Arusha; Meneja Kampeni - Mara. Unaona kabisa kuwa chama kina utaifa na hao watu wanaisadia kuoneza hicho chama katika maeneo hayo. Bulembo akismama kuongea, watu wa Mara wanaona kuwa wanawakilishwa katika hicho chama.
Sasa bila kumumunya maneno angali nyumba ya pili (CHADEMA) ambayo wanategewa kuwatoa kimasomaso husasan Uongozi wakati wa kampeni ulikuwaje: Mwenyekiti - Arusha; Mgombea - Jirani; Meneja Kampeni- Jirani; Mkurugenzi wa Fedha - Jirani; Mwenyekiti Mwenza aliyekuwa anaongea sana na vyomba vya habari-Jirani.
Katika hali kama hiyo mwananchi. Katika hali kama hii, chama kinawezaje kushika nchi ? Hebu fanyeni chama kuwa cha Kitaifa acha kulalamika ilihali mnajidhoofisha wenyewe.
Mnategemea kweli mwananchi wa kawaida kutoka kijijini akiambiwa kuwa hiki chama ni cha Kikanda atashindwaje kuamini kama kipewa mifano hiyo !!!
Binafsi nilikuwa fan wa CHADEMA O.G ila baada ya Mbowe kuleta upuuzi wa gia angani sikuona jipya zaidi ya kubaki CCM O.G
Mwaka 2010 cdm ilipata kura 2 million, mwaka huu 6 million +. Gia ya angani imeleta kura 4 million + na kashkash kubwa kwa ccm. Kama watu hawaoni hili pamoja na ujumlishaji wa kura usiokuwa na hata chembe ya credibility, basi tumekwisha