Mbowe in informal meeting with JK

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,578
0
Kama habari ya kuwashirikisha wapinzani katika serikali ni sahihi, basi hii itakuwa ni strategic move ambayo CCM wameiona ni njia pekee ya kutokea. Experiment ya Zanzibar imezaa matunda na wamefanyikiwa kuipa CCM uhai wa at least next two general elections kule visiwani.

CCM inaamini kabisa serikali yake imekuwa ni failure mbele ya wanachi, na wanaamini kabisa kuwa kwa sasa wana wakati mgumu sana kuendelea kutawala watu ambao hawakuwachagua wao wawe watawala. Na CCM inaamini fika kuwa Tanzania inaelekea pabaya kama wataendelea kulazimisha ushindi katika chaguzi zijazo. CCM inaamini kabisa kuwa njia pekee ya wao kuonekana bado wanafaa ni kuvisambaza virusi vya failures walivyo navyo kwenye vyama vyenye nguvu. Itakapofika wakati wananchi wakaamini kuwa si CCM wala si chama chochote kinachoweza kuwakomboa huo utakuwa ni ushindi mkubwa sana kwa CCM.

CDM wakikubali kushirikishwa katika serikali basi wajijue kuwa mwanzo wa mwisho wao unawadia Unless kwenye serikali hiyo wa-demand waziri wa mambo ya ndani na waziri kuu watoke CDM na wawe na nguvu zilezile walizonazo hawa waliopo madarakani kwa sasa. Hapo CDM inaweza ku-influence mabadiliko nchini. Ila wakikubali unaibu waziri au uwaziri wa jinsi na watoto wajue wamekwisha.
 
Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,545
1,250
Jumapili iliyopita (15 Jan 2015), Rais JK na Mbowe walikutana kwa siri, kilichojadiliwa pia kikawa ni siri. Gazeti la kiukweli la kimombo' The citizen' limetoa nyeti hizo ukurusa wa mbele bila chenga. Mbowe akaulizwa kwa simu, naye akikri kuwa ni kweli walikutana. Alipoulizwa mlijadili nini akapiga chenga, subiri msiba uishe. Gazeti lilipowauliza wasemaji wa ikulu nao wakatoa nje. Lilipomwuuliza Mnyika wa kueneza chama kuhusu sakata hilo naye akasema hana habari.

Maswali
Je, Dr Slaa na viongozi wakuu wa Chadema wanajua kikao hicho? Kama hapana kwanini? Kama siyo, Mbowe atujibu haraka.

Pili, kikao cha kwanza cha ikulu ilikuwa public kwanini hii ya mbowe aifanye siri peke yake?
Je, JK anamshawishi mbowe aikubali mchakato feki wa katiba?
Je, kati yao Jk anawasaliti ccm au Mbowe anasaliti Chadema?

tatizo la mbowe ni mfanyabiashara,wakati wenzake wanalia machozi ya msiba wa Regina yeye anatafuta namna ya kuhongwa na kuwa mke mdogo wa CCM bara,na kama mnabisha subirini muda si mrefu ,9yt clubs zake na hotel yake ya kule hai ishaanza kuchakaa anatafuta pesa za ukarabati wakati deni la NCCF bado hajalipa
 
FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,084
1,225
Sina tatizo kama Mbowe anakutana na kiongozi wa chama chochote, rais au hata katibu kata. Lakini ni muhimu kabisa (nasisitiza) kwa Mbowe kuwajulisha wananchi ameongea nini na huyo aliyekutana naye. Jambo lililofanya wananchi wakapoteza imani na ccm sio tu ni kwenye utendaji mbovu bali tabia ya 'usiri'. Watu wazima wanakaa kikao saa 1, 2, 3 au zaidi, wanaongea mambo yatakayogusa mustakabali wa nchi lakini wakitoka nje ya chumba cha mkutano wanakaa kimya?

CHADEMA wanatakiwa kukwepa huu ugonjwa wa kukaa kimya. Hilo ni tatizo la ccm nyie kama mnataka kuwa tofauti basi pa kuanzia ni hapo pa kuwa wawazi ziadi.
 
CERDIC

Member
Oct 3, 2011
16
0
Mh. Mbowe as soon as we complete mourning activities let the public know what transpiried on your talks with president, otherwise I smell reputation risk and luck of trustworth,we are waiting hatutadanganya kama scandal za politicians wengine zilivyopotea kutokana na kikombe chbabu samunge
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
0
Kama habari ya kuwashirikisha wapinzani katika serikali ni sahihi, basi hii itakuwa ni strategic move ambayo CCM wameiona ni njia pekee ya kutokea. Experiment ya Zanzibar imezaa matunda na wamefanyikiwa kuipa CCM uhai wa at least next two general elections kule visiwani.

CCM inaamini kabisa serikali yake imekuwa ni failure mbele ya wanachi, na wanaamini kabisa kuwa kwa sasa wana wakati mgumu sana kuendelea kutawala watu ambao hawakuwachagua wao wawe watawala. Na CCM inaamini fika kuwa Tanzania inaelekea pabaya kama wataendelea kulazimisha ushindi katika chaguzi zijazo. CCM inaamini kabisa kuwa njia pekee ya wao kuonekana bado wanafaa ni kuvisambaza virusi vya failures walivyo navyo kwenye vyama vyenye nguvu. Itakapofika wakati wananchi wakaamini kuwa si CCM wala si chama chochote kinachoweza kuwakomboa huo utakuwa ni ushindi mkubwa sana kwa CCM.

CDM wakikubali kushirikishwa katika serikali basi wajijue kuwa mwanzo wa mwisho wao unawadia Unless kwenye serikali hiyo wa-demand waziri wa mambo ya ndani na waziri kuu watoke CDM na wawe na nguvu zilezile walizonazo hawa waliopo madarakani kwa sasa. Hapo CDM inaweza ku-influence mabadiliko nchini. Ila wakikubali unaibu waziri au uwaziri wa jinsi na watoto wajue wamekwisha.

CUF has seen this long time ago, now is your time to copy and paste
 
sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,536
2,000
muda si mrefu tunategemea kusikia mapya yaliyojiri toka kwenye maongezi ya faragha.Hatudanganyika kama kweli kuna usiri basi ni bora uvue magwanda utukabidhi,hatutaki serikali ya kinafiki ya mseto tunachotaka magamba wakae bench wengine nao waingie
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,525
2,000
Hivi, Nyerere alipokutana na Idi Amin pale Mwanza, na kwenye kikao cha OAU ilikuwa na maana kuwa Nyerere amelegeza msimamo wake kuhusu Idi Amin? Sote tunajua kichapo alichokipata Amin baadaye. Namwaminia sana Freeman. Tuwe na subira na tuwe great thinkers for once.
 
Nyerereism @work, hadi mtakapoamu kufikiri bila kutegemea mtu aliyefail kila kitu ndio mtaweza kujiongoza kwenye haki..

Besides, soon chadema watapewa zawadi ndogo, watafurahi kama walivyo furahi siku ile ya juice na picha; halafu mistari miwili ya maelewano..period
 
Bei Mbaya

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
2,263
1,250
Chadema namwamini Dr. Slaa na Lema baasi

mmoja hanunuliki, mwingine ni msema ukweli
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,525
2,000
Nyerereism @work, hadi mtakapoamu kufikiri bila kutegemea mtu aliyefail kila kitu ndio mtaweza kujiongoza kwenye haki..

Besides, soon chadema watapewa zawadi ndogo, watafurahi kama walivyo furahi siku ile ya juice na picha; halafu mistari miwili ya maelewano..period
Hata Marekani mpaka leo wanatumia adidu za rejea za founding fathers wao. Ni wapumbavu tu ambao wanajidai kusahau au kufuta misingi ya kule walikotoka na matokeo yake tunayaona leo. Nchi yenye dhahabu na almasi lakini rais wake kila kukicha ni kagulu ku njia na bakuli la ombaomba. Eti wawekezaji watatuletea neema.
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
0
Hata Marekani mpaka leo wanatumia adidu za rejea za founding fathers wao. Ni wapumbavu tu ambao wanajidai kusahau au kufuta misingi ya kule walikotoka na matokeo yake tunayaona leo. Nchi yenye dhahabu na almasi lakini rais wake kila kukicha ni kagulu ku njia na bakuli la ombaomba. Eti wawekezaji watatuletea neema.

Afadhali hao wa merakani waliacha misingi ya maana kwa nchi zao, sasa nyerere kaacha nini? kunyang'anya mali za watu, kutaifisha mali na nyumba za watu, kuendekeza udini etc..hatuwezi kufikiria kama nyerere kwasababu legacy yake ni worse sasa unahangaika aye wa nini..jaribu kuangalia namna nyingine zaidi ya mawazo mgando na ya kale ya nyerere..

Twende mbele tufikiri wenyewe..period, new ideas and new ways, kama unaona wawekezaji hawafai sema wewe unataka tufanyeje siyo kujaza server na nyerere..nenda kaimbe huko kanisani kwenu lakini kwenye mambo ya kitaifa ni failure..damn
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,355
2,000
Kote huko walianza kubadilisha katiba zao ili ziruhusu serikali ya mseto.Halafu kunywa chai ikulu si hoja, hoja walifuata nini? si ulisikia jinsi jk alivyokuwa anawashangaa mawaziri wake, lakini aliogopa kuenguliwa kwenye chama.
Mkuu katiba ya nchi hii haikatazi. Katiba inasema waziri lazoma awe mbunge:wakuchaguliwa, viti maalum ama wa kuteuliwa. Katiba iko strict kidogo kwa waziri mkuu ambaye anatakiwa awe wa kuchaguliwa na atokane na chama chenye wabunge wengi ama ambaye ataonekana kuungwa mkono na wabunge wengi! Kwa hiyo kwa waziri wa kawaida Rais anaweza kumteua mbunge yeyote kuwa waziri/naibu waziri ila kwa waziri mkuu Rais anatakiwa ateue mbunge wa kuchaguliwa na ambaye anatokana na chama chenye wabunge wengi lakini pia Rais AKIHISI kuwa unaungwa/utaungwa mkono na wabunge wengi basi ana uhuru wa kuteua mbunge wa kuchaguliwa toka chama chochote na kupeleka jina lake bungeni kwa ajili ya kuidhinishwa. Inakuwa ni kawaida kuteua waziri mkuu toka chama chenye wabunge wengi ili kuepuka Waziri mkuu mteule asijekataliwa na wabunge. Hivyo basi hata waziri mkuu kivuli anaweza kuukwaa uwaziri mkuu!
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,355
2,000
You have very narrow picture about politics, no permanent eneminity
Ni kweli mkuu. Nani aliamini kuwa Raila Odinga na Mwai Kibaki watakaa pamoja na kuwatawala Wakenya kwa raha zao? Hamkumbuki watu walivyokuwa wakikimbia na mikuki imesimama utosini na wengine kutahiriwa wakiwa wazee na kufariki kwa kupoteza damu nyingi kwa ajili ya kuwapigania Raila na Kibaki. Lakini sasa Kibaki na Raila wanakula bata na soseji kwa raha zao. Waliokufa walikufa. Mwishoni wanaambiwa eti walikufa kishujaa! Hao ndio wanaoitwa wanasiasa. Wengi ni vinyonga. Wao wanachotaka ni kutawala kwa hiyo ikija nafasi ya kutawala kwa njia yoyote ile basi wao ni halali yao!
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,525
2,000
Afadhali hao wa merakani waliacha misingi ya maana kwa nchi zao, sasa nyerere kaacha nini? kunyang'anya mali za watu, kutaifisha mali na nyumba za watu, kuendekeza udini etc..hatuwezi kufikiria kama nyerere kwasababu legacy yake ni worse sasa unahangaika aye wa nini..jaribu kuangalia namna nyingine zaidi ya mawazo mgando na ya kale ya nyerere..

Twende mbele tufikiri wenyewe..period, new ideas and new ways, kama unaona wawekezaji hawafai sema wewe unataka tufanyeje siyo kujaza server na nyerere..nenda kaimbe huko kanisani kwenu lakini kwenye mambo ya kitaifa ni failure..damn
Tuendeleze kutembeza bakuli huku madini yetu yakichukuliwa mchana kweupe. That is not damn failure.
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,587
2,000
tatizo la mbowe ni mfanyabiashara,wakati wenzake wanalia machozi ya msiba wa Regina yeye anatafuta namna ya kuhongwa na kuwa mke mdogo wa CCM bara,na kama mnabisha subirini muda si mrefu ,9yt clubs zake na hotel yake ya kule hai ishaanza kuchakaa anatafuta pesa za ukarabati wakati deni la NCCF bado hajalipa
Teh teh teh...Habari za hapo Mwanza Kalungine?
 
trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,742
2,000
Maalim Seif alifanya hivyo na Julius Nyerere.. Na hakudisclose waliyoyaongea hadi leo... Siasa bana..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom