Nyie endeleeni kupiga porojo za akina Slaa, Mbowe na Lema au Lowassa. Msisahau kwamba hawa mnaopoteza muda kuwajadili hapa, hawabebi dhamana yoyote kwa watanzania. Chama chenu ambacho hamtaki hata kukikosoa kwa jambo lolote, ndicho kilichotoa ahadi na ndicho kitachoulizwa kimefanya nini baada ya miaka mitano. Mwaka 2020 watanzania hawatamwuliza Mbowe au Slaa au Lowassa kwa nini watoto wao hawakupata mikopo ya vyuo vikuu. Hawatawauliza watu hao viwanda viko wapi, na kama kama Tanzania ya wakati huo itakuwa ya viwanda. Hawatawauliza kama kila kijiji kimepatiwa milioni 50. Hawataulizwa kwa nini watanzania wengi bado wanakunywa maji ya tope na kutumia taa za vibatari huko vijijini. Narudia tena, akina Mbowe, Lissu, Slaa, Lowassa au Lema hawataulizwa chochote kati ya hayo. Msije kusema hatukuwaonya......