Mbowe hukumsikiliza Dkt. Slaa, sasa umeizika CHADEMA!.

Mbowe hukumsikiliza Dkt. Slaa, sasa umeizika CHADEMA!.

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2016
Posts
4,733
Reaction score
11,466
Mbowe hukumsikiliza Dr slaa sasa umeizika chadema,chadema hii ya sasa inayokubali uhuni huu unaofanywa na ccm na serikali yake!.Ingekuwa kipindi dr yupo hakika uenevu huu anaofanyiwa Lema wananchi wa arusha wasingeuvumilia.

Katika utawala huu msitegemee haki,uhuru kwa njia mnayofikiria kuwa vitapatikana.Chadema inayohitajika kwa sasa nichadema ya 2010_2015 chadema ambayo haikukubali uonevu wowote toka serikalini.

Nimeumia sana kitendo cha mheshimiwa lema kunyimwa dhamana leo hii tena bila sababu za msingi.Sasa naona mheshimiwa Mbowe umeifanyia mengi mazuri chadema sasa kaa pembeni umpishe either Lissu or Lema mwenyewe katika utawala huu wa mtukufu saana watu hawa ndio wataivusha chadema salama.
 
Hao unaosema wapewe ndo watakuja kuweka na msalaba kabisa.. jembe lilosimama kwenye ukweli lilishasepa.. waliobaki wengi misimamo yao ni haieleweki.. inatuvunja moyo wapinzani.. tukianzia kwa lowassa.. kugoma bungeni.. ukuta.. yani mambo hayasimami pahala pake..
 
Yaa huko sahii mkuu yaani ni kama huku CCM inavyo ongozwa ndivyo sivyo .. CCM tulikua mstari wa mbele kupinga vita rushwa lakini katika uongozi wa JPM sio muhimu kabisa .. Juzi tulitumiwa kupokea rushwa milioni 10 na tupo kimya kuhusu ili yaani
 
muombeni msamaha Zitto Kabwe arudi chadema mmpe uenyekiti.... bila hivyo laana ya uchagadema itawakula sana
 
Ndio maana Trump akapendekeza mtawaliwe tena akili mgando!!

Yaani bila Slaa, Mbowe, Lowassa na CHADEMA siku haiendi. Kisa umenunuliwa smartphone!!
P.mbv huoni lema uhuni anaofanyiwa,chadema haina siraha,wala dola lakini wananchi tupo nyuma yao.Ccm na serikali yake wakiweka moto nasi tutie moto kama ilivyo wao.
 
muombeni msamaha Zitto Kabwe arudi chadema mmpe uenyekiti.... bila hivyo laana ya uchagadema itawakula sana
Zitto hana ujasili kwa kipindi hiki,ndio maana aliitwa police mara mbili akanywea.Tunahitaji watu jasili zaidi wakiongea neno au kupanga jambo hawarudi nyuma,watu hao ni Lemma na Lissu.
 
Zitto hana ujasili kwa kipindi hiki,ndio maana aliitwa police mara mbili akanywea.Tunahitaji watu jasili zaidi wakiongea neno au kupanga jambo hawarudi nyuma,watu hao ni Lemma na Lissu.
Hivi sifa za wenye viti wa vyama ni kujua kusoma na kuandika? au?
 
Muanzisha uzi umefumuliwa marinda.
Msininukuu vibaya
 
Kuna kitu kina ukweli kidogo hapo. Mbowe chunguza kwa nini umekuwa soft katika kipindi hiki ambacho ndio hasa ule ujasiri wako ulikuwa unahitajika?
Mfano hilo swala la mikutano, Wabunge waandae hiyo mikutano yao majimboni na watoe mialiko kwenu viongozi mmoja mmoja wa kitaifa then unatia timu na kumwaga cheche zako wewe au mwingine yeyote tuone watafanya nini wakati mkutano sio wako na umealikwa? Au mamlaka gani yanazuia watu kualikana kama vile nyie sio raia?
Wakivamia mikutano hiyo basi kiwake na wananchi wajilinde, tuone kama hayo yakitokea kila pembe ya nchi huo uchwara kama utaendelea. Ebo!
 
Muanzisha uzi umefumuliwa marinda.
Msininukuu vibaya
Kweli mkuu nilifumuliwa na mama yako nae nikamfumua ndio maana alipokuzaa alik. .nyaa sana,kwani hajukwambia kijana.
 
Kuna kitu kina ukweli kidogo hapo. Mbowe chunguza kwa nini umekuwa soft katika kipindi hiki ambacho ndio hasa ule ujasiri wako ulikuwa unahitajika?
Mfano hilo swala la mikutano, Wabunge waandae hiyo mikutano yao majimboni na watoe mialiko kwenu viongozi mmoja mmoja wa kitaifa then unatia timu na kumwaga cheche zako wewe au mwingine yeyote tuone watafanya nini wakati mkutano sio wako na umealikwa? Au mamlaka gani yanazuia watu kualikana kama vile nyie sio raia?
Wakivamia mikutano hiyo basi kiwake na wananchi wajilinde, tuone kama hayo yakitokea kila pembe ya nchi huo uchwara kama utaendelea. Ebo!
Msaidieni Kulipa Madeni Arudi Kwenye Hali Ya Kawaida.Magufuli Sio Kikwete, Hanaga Unafiki Wa Kisiasa.Mbowe Hayuko Sawa Kiutu Uzima Tu
 
Ukiona kimya, ujue kuna bomu linasukwa, likilipuka, itakua ni zaid ya kupambana na serikali face to face kuhusu lema
 
Mleta mada ni mchochezi.
Hakika JPM anatekeleza kile alichotumwa na wananchi.
Lema ni mjinga sana. Badala ya kujenga hoja Bungeni na kuonyesha watanzania udhaifu wa serikali juu ya kuleta maendeleo yeye anakuja na usanii wa kuoteshwa ndoto kama enzi za kina kinjekitile.

Maneno ya ajabu ajabu anayoyatoa dhidi ya Rais wetu aliyechaguliwa kihalali na ambaye anaungwa mkono na watanzania walio wengi yanawasaidia nini wanyonge zaidi ya sifa binafsi za kisiasa.

Kwa sasa dunia nzima inatamani viongozi imara kama Magufuli.
Umeona Wamarekani wameshashtuka na kuamua kuondokana na siasa za usanii sanii na kucheka cheka jukwaani.

Lema amejitakia mana anafanya mambo ambayo sio matamko ya chama au vikao.
Sasa suala la kuota ndoto linahusiasa nini na chama ? Hapo chama kitamsaidiaje kuhusu ndoto zake za kipepo na ramli zake zisizo na kichwa wala miguu.
Tena alitakiwa apigwe viboko adharani kwa kuongea utumbo kinyume na matarajio na desturi za kiafrika.

Hata Dr. Slaa angekuwepo angeufyata mana Dr. Slaa ana misimamo mikali kuliko hata Trump. Haya anayoyafanya Magufuli yangeungwa mkono na Dr. Slaa kwa asilimia 1000. Jiulize wakati wa Mkapa uliwahi kumsikia Dr. Slaa na mbwembwe zake?
Tafakari usikurupuke!!
Huu ni utawala mwingine sio wa awamu iliyopita.Kila zama na kitabu chake. Watu jeuri wanaongozwa kijeuri. Hata enzi za Musa zilikua tofauti na enzi za Yesu. Musa alikata watu vichwa kwa maelfu lakini Yesu alikua mpole mpaka wakamuua.
Binadamu hana wema. Ndio maana marehemu Dr. Remy aliimba na kusema "wemaa, wema mmmmh"".

Kila mtanzania anajua kinachofanyika na kinachofanywa na Serikali hio ya awamu hii kinalenga kumkomboa mtanzania ndio maana hata wananchi wa jimbo la Lema hawako tayari kumuunga mkono.
JK alifanya yake wakina Lema wakamkejeli kila kona na kumjengea jina baya kila kona ya nchi. Wanachi wakashindwa kuonyeshwa mambo mema aliyoyafanya JK.
Sasa itakua ni jambo la ajabu kama tena JPM naye atarudia kosa lile lile la kuwaacha wakina Lema kutangaza mabaya tu kwa wananchi ili tu wajijenge kisiasa ;Yani akubali kubamolewa kisiasa ili wao wajijenge kisiasa, wakati yeye ndiye aliyechaguliwa.

Kama JPM anakosea wananchi waliomchagua wataona na uchaguzi ukifika watapila wenyewe. Yani Mwaka mmoja tu watu wanaanza kumwandama Rais kwa maneno ya ajabu ajabu.

Lema abadilike na afanye siasa za kistarabu. Aheshimu wengine ili naye aheshimiwe. Kuwa mbunge kusimfanye awadharau wengine na kuvunja sheria.
Mbowe ana busara sana ,amehudhuria vikao vya bunge kuwakilisha watu wa jimbo lake na sio kuanzisha vurugu kumtetea muota ndoto za vifo.
Bunge lipo kwa ajili ya vikao vya Lema vya kuwawakilisha wananchi wa jimbo lake na kutetea maslahi yao. Chaajabu Lema anatumia muda mwingi kupambana na serikali badala ya kuwakilisha kero za wananchi wake.
Kwa hali hii asitegemee watu wuunge mkono.
 
Tangu lini CCM wamepinga rushwa? Wangekuwa wanaipinga vijicent angeongoza bunge? Angeandika katiba ya samwel sita? Masansarusi ya stanbic yangekuwepo? Singa wa pap angevuta pale bot?Tuache unafiki
 
Zitto hana ujasili kwa kipindi hiki,ndio maana aliitwa police mara mbili akanywea.Tunahitaji watu jasili zaidi wakiongea neno au kupanga jambo hawarudi nyuma,watu hao ni Lemma na Lissu.
Nendeni mkachukue wafungwa wanaomaliza mda wao magerezani ambao wameshafungwa zaidi ya mara moja, nadhani kwa aina ya viongozi mnaotaka hawa watafaa sana.
 
Lowassa anaelekea kufanikisha mission yake ya kukisambaratisha Chadema
Nyumbu wakijakushtuka, sijui watakuwa wamebaki wangapi!!
DK Slaa alikuwa Nyati kwenye kundi la nyumbu.
Eti pamoja na wingi wao, Mahakamani walioenda kusikiliza kesi hawazidi 20!!!
 
Back
Top Bottom