Mbowe, Freeman; Lipumba, Ibrahim; Mbatia, James, Lyatonga, Augustino na Cheyo John. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe, Freeman; Lipumba, Ibrahim; Mbatia, James, Lyatonga, Augustino na Cheyo John.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 3, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wasalaam,

  Baada ya kelele nyingi za ushirikiano wa vyama vya upinzani vya siasa nimeona ni bora niwalete tena mbele yenu Wenyeviti wa Vyama vya Upinzani vyenye Wabunge ili tuweze kujiridhisha tena kuhusu ushirikiano wa vyama hivyo.

  Nafahamu fika kwamba vyama ni zaidi ya watu lakini pia mawazo ya watu na fikra zao zinaathiri au zinasaidia kwa kiasi kikubwa muonekano wa chama husika.

  Hawa wenyeviti kila mmoja ana lake zuri na baya; nitatoa mifano michache kwa kila mwenyekiti kwa zuri na baya lake;

  Freeman Mbowe:

  Baya: Inasemekana hana elimu ya kutosha (elimu ya chuo kikuu ndiyo inayozungumziwa hapa). anadaiwa kuihujumu NSSF kwa kutokulipa deni la kutengenezewa.

  Zuri: ni kiongozi ambaye ameweza kuivusha chadema kutoka kipindi kimoja hadi kingine kwa kushawishi vijana kushiriki katika uongozi na siasa za nchi. Ameweza kurudi bungeni kwa mara nyingine baada ya kumshinda mgombea wa CCM.

  Ibrahimu Lipumba:

  Baya: Ni mwenyekiti aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi ya wenyeviti wenzake wa vyama vyenye wabunge bungeni na ni mtanzania pekee aliyegombea mara nyingi nafasi ya uraisi na kushindwa. Ni mgombea pekee ambaye hajafanikiwa kufikisha idadi ya kura Milioni 2 kwa chaguzi zote alizoshiriki.

  Zuri: Ni profesa wa kwanza kugombea uraisi na profesa pekee aliyemshinda kwa kishindo profesa mwenzake kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa chama chake. Ni mwenyekiti mwenye mafanikio makubwa kuweza kuunganisha chama chake na chama cha mapinduzi kwa maslahi ya wazanzibari na kuacha maslahi ya bara pembeni mpaka kipindi kijacho.

  James Mbatia:

  Baya: ni mwenyekiti pekee ambaye kwa muda mrefu amekuwa na kashfa ya kuwa hayuko sawa kimaumbile (haijathibitishwa). Ni mwenyekiti pekee ambaye alishindwa vibaya kwenye kugombea ubunge kupitia jimboni. Ni mwenyekiti wa kwanza wa chama cha siasa kushindwa kwenye uchaguzi na kijana. Ni mwenyekiti wa kwanza wa chama cha siasa kushindwa uchaguzi na mwanamke.

  Zuri: Ni mwenyekiti pekee aliyeweza kushinda viti vingi vya wabunge mkoa wa kigoma pekee. Ameweza kujenga chama ambacho wanaokimbia CDM wanafikia kabla ya kurudi CCM.

  Augustine Lyatonga:

  Baya: ni mwenyekiti mzee kuliko wote. Amekuwa haeleweki kuhusu msimamo wake. Alitangaza hadharani kwamba anamkubali Kikwete na Chama chake kikasimamisha mgombea uraisi. Hakumpigia kampeni mgombea uraisi wake. Mwenyekiti pekee aliyewahi kucheza jukwaani kumsifia Kikwete na CCM.

  Zuri: ameweza kurudi bungeni baada ya muda mrefu nje. amefanikikwa kuwapa tumaini jipya wananchi wake wa Vunjo. Ni mshauri mzuri sana kuhusu hujuma na wizi wa CCM.

  John Cheyo:

  Baya: hajulikani kwa zuri lolote zaidi ya kwamba ni bwana mapesa. hachimbi visima kama Sabodo ingawaje watanzania wanaamini kwamba anapesa nyingi. ni mwenyekiti pekee aliyeamua kutumia chama kama taasisi ya kuendelea kupata ubunge. Kuna mikoa zaidi ya 10 ya tanzania hajawahi kufika tangu awe mwenyekiti kufanya siasa.

  Zuri: hajulikani anasimamia siasa za aina gani. ni msemaji mzuri kupinga baadhi ya masuala bungeni ambayo hana maslahi nayo.


  Ndugu WanaJF, baada ya hayo machache na yale mengi ambay wote mnayajua ni vizuri tukajiuliza hawa tunataka au tunategemea watuunganishe vipi?

  Huko Bungeni tunataka washirkiane vipi. Watatu kati yao wako bungeni wengine hawapo, je ni ushirikiano gani ulikuwa unahitajika?

  Nadhani kwa kupata mawazo ya wachangiaji tutapata angalau mwanga kuhusu wale wanaoongoza vyama vya upinzani tunavyovitaka vishirikiane!!:sad:
   
 2. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du Data zina ukweli? hasa Mbatia na Freeman napaogopa hapo p/se wataje na wengine mbona vyama bado vipo vingi?
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  duu... ukisoma vizuri hapa kuna mchanyato wa theolojia, saikolojia na intelijensia
   
 4. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni kweli vyama viko vingi ila imebidi niwalete kwenu wenyeviti ambao vyama vyao vina wabunge!
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Upuuzi tu....nyambafu
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Na ccm haina wabunge?.......CRAP!
   
 7. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Sema wewe kiazi nikisema mimi muhogo nitaambiwa nina mizizi.

  Hiyo post yake imekaa kikashfa kashfa kwa wenyeviti wa CUF, UDP, NCCR "huyu ndio kadhalilishwa kabisa"
   
 8. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na nyerere muungu wenu wa tanganyika alikaa ktk kiti cha uraisa kwa miaka 28 jee yeye mbona humtaji kua ni jambo baya? Au yeye ni mtakatifu baba askofu?
   
 9. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtabe, Mohamed na Birigita, nimeongeza neno 'upinzani' kuweka rekodi vizuri kwamba Raisi wenu hausiki.

  Kuhusu kumdhalilisha Mbatia hiyo umesema wewe Mohamed!! Each and every statement therein can be justified! Sijakurupuka!!

  Na kuhusu hao wengine sema ni kipi ambacho wamesingiziwa? mazuri au mabaya yao mengine unaweza ukawa unayajua!!

  The bottom line, hao ndio wanatakiwa waunganishe vyama vya upinzani vyenye wabunge!!
   
 10. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh huu mtego miye simo. Asante
   
 11. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duuuu :twitch:
   
 12. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  yangu macho
   
 13. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa BL unachimba kamanda?

  Duuuu haitoshi, tia neno!
   
 14. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh, mbona hapa kuna harufu ya Udini? Mbona Wagalatia ndio wengi? ili kuleta usawa, JK nae aingizwe na viongozi wa NRA nk.!
   
 15. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ehe! wewe umetokea dunia gani? hujui nyerere alishakufa na mwenyekiti aliye hai ni Dr Dr Dr JK. Watu wenye akili timamu hawalumbani na wafu, maana hawapo hai kujibu tuhuma dhidi yao. RIP...Mwl.JKN
   
 16. n

  niweze JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama jitihada na efforts zote unazofanya kutaka kujenga empty coalition ya CUF/Chadema au nia yako ya kutaka kusema upinzani hauna nguvu ni maneno empty hapa pia. Umeandika thread ndefu ambayo sijui kama kumweleza Mtanzania makosa ya Lupumba na Mbowe yanaweza kufananishwa na hiki chama cha CCM? Uzembe na ukaaji wa CCM madarakani umeleta mangapi? Nitaannza kichama na nitaishia personal kama wewe ulivyo elezea juu:
  Mafanikio na Matokeo ya Uongozi wa CCM e, Yanalingana na shutuma za huyu jamaa hapa juu?
  1. Ujamaa na kujitegemea = Umeskini na utajiri kwa viongozi wa CCM
  2. Azimio la Arusha = Umaskini na utajiri kwa viongozi wa CCM
  3. High Unemployment
  4. Kutolipa malipo kwa walio retire = Viongozi wa CCM Wanajengea majumba na kupeleka familia zao nje ya nchi
  5. Kuibiwa kwa funds za Kodi, TRA = Viongozi wa CCM wanajengea majumba na kupeleka familia zao nje ya nchi
  6. Mikataba hewa migodini na viwanda vya Taifa = Utajiri wa viongozi na umaskini kwa wananchi
  7. Mauaji: mahospitalini, kwenye maandamano, kutokana na umaskini kuto kuwa na kazi na chakula

  Sasa tuangalie JK, Mkapa, Mwinyi, Lowasa, Rostam, Sumaye kama Matendo Yao Yanafanana na Lipumba na Mbowe:
  1. Kikwete: kachaguliwa 2005 kwa kura nyingi ingawa Mw. Nyerere alimwona hafai na matokeo yake ndio haya
  - Wizi mkubwa wa mabilioni tangu achaguliwe
  - Hajui uongozi na vision of the country
  - Kuendeleza ufichaji siri mkubwa kwa CCM na Mafisadi wenzio
  - Ametumia muda mwingi kusafiri kama mfanyakazi wa ndege, kufanya deals za nchi na kuhakikisha Tanzania inafisika na yeye
  anatajirika
  - Kama kiongozi wa CCM na Kamati kuu wakakubali Dowans ilipwe bila aibu na shame on them. Nia kubwa ni "Kutajirisha familia ya
  Rostam na CCM" sio Wananchi
  - Wizi Mkubwa wa wazi wa Kura kupitia NEC. Tangu lini mgombea anajichagua yeye mwenyewe
  2. Matokeo CCM na Uongozi wa Mkapa na Mwinyi tukilinganisha na Lipumba na Mbowe
  - Wizi mkubwa wa Taifa letu na wao kuijiongezea utajiri bila shame on them. Sisi wananchi ndio tutawaprosecute them sio CCM
  - Umaskini mkubwa Tanzania
  - Serikali usio na mwelekeo
  - Uchumi mbaya
  - High unmployment
  - Wake Zao kuitia aibu Taifa kwa kuibia Taifa letu: Mama Mkapa na Mama Sitta Mwinyi

  Kutokana na Haya Nani ni Ameleta Maafa na Mauji ya Uchumi na Vitisho vya Polisi na Jeshi? Ni Lipumba au Mbowe? Tunajua Makada wa CCM na Watoto wa Viongozi wanataka kugeuza the Truth na This Time Nothing will Work maybe uneducated kwa sababu hao ndio bado wako nyuma, majority ya Tanzanians sio wajinga kama CCM ilivyo na ndio sababu tunaona mwamko wa siasa na opposition Tanzania.
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kushindwa na mwanamke ni baya?
   
 18. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  kumbe wewe ndo mhugo,aise muhogomchungu una ID nyingi sana. Alaf kumbe Birigita ni kiazi/kilaza teeh teeh!ujamtusi kweli?very ironic!
   
 19. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  bwn Albert,nakukubali,kama watu wasemavyo wanasheria wametulia hawakurupuki ni kweli. Na wewe ni kati ya maAdvocates wenye data. Nkianza na Mzee Cheyo,huyu mzee hana zuri kama ulivosema ila nawashangaa rais na Tendwa kuleta ushkaji na mzaha,mfano Udp ni chama cha Shinyanga,kimeshindwa kufanya kampeni nje ya mkoa na hakina mwakilishi nje ya mkoa huo kwa miaka mingi sana na kinavunja sheria kikatiba. Katiba mbovu ya mkoloni ya URT imesema chama hakitakuwa na lengo la sehemu moja bali cha kitaifa,jiulize ni lini ulisikia UDP nje ya mkoa kikifanya mikutano?ni uyo jamaa bungeni miaka yote. Pia,shutuma za Nccr hazijaanza leo,nliogopa sana nlipokuta wanafunzi wa kitivo cha sheria wakijadili na kueleza kuwa huyu jamaa kwa makusudi au bahati mbaya anazikimbia sifa za Mwanaume!naogopa kuona kiongozi wa kitaifa akiwa ivi. Watu wanaenda mbali na kusema kwamba kamwe hawezi kugombea kiti cha urais akiogopa kashfa isikuzwe,na kweli 2010 alikaa pembeni na kujichagulia kawe. Hapa weledi wanajiuliza,kama cdm kwa kumtumia mwanadada imembinua pale kawe,je nccr si mzizi mdogo kwenye mpingu wa cdm? Kuhusu Lipumba mi sina wasiwasi nae! Ni mwenyekiti ambaye anaweza kuliongoza taifa,ila mi niliona hofu mwaka 2008 mwezi agosti alipokuwa ktk semina ya wajumbe wa Cuf wa Mikoa yote Tanzania,nlimnukuu, "kwa mfumo wa nchi yetu,msitegemee lipumba kuwa rais wa Urt,najenga chama ili watakaokuja wapate pa kuanzia na hatimaye CUF ishike hatamu" hapa nlijiuliza je ana mpango kweli?mbona kila mwaka anagombea?mjumbe mmoja anayeitwa ustadh White aliyekuwa mjumbe kutoka Bukoba Kashai,aliniuliza,je hapa Mkuu anamaana gani?nlimpa majibu ambayo hata leo najua hata mi sikuwa na hamu nayo! Upande wa Mrema,ikumbukwe kuwa yeye analenga ruzuku na ni shushushu wa ccm. Mwaka 2004 nlikutana na Mmarekani mwenye asili ya kitanzania Mama Anitha Muyeya aliyekuwa karibu na Ikulu ya mkapa alinieleza ukaribu wa mzee mrema na ccm,nliogopa!uyu ni usalama wa taifa ambaye mpaka leo yuko kazini,kubali/kataa. Ila sasa mrema amechoka tumwache mzee aendelee na masuala yake. Kwa upande wa Mbowe,huyu jamaa ana elimu ya Diploma na ni mwalimu. Elimu hii inamtosha kufanya hata maamuzi magumu. Mtu mwenye Diploma nzuri akiamua kuitafuta digrii na PhD ni rahisi,sina wasi wasi na elimu yake. Kama rais wetu ana elimu ya digrii daraja la mwisho ambalo hata haruhusiwi kufanya masters mbona anaiongoza taasisi kubwa na hamna anayehoji elimu yake? Je hawa akina Mohammed wanaomkandia Mbowe mbona nao wana Diploma tena ya daraja la chini kabisa?!au wanadhani kuna siri hatuwajui?wakumbuke wanaishi Tanzania! Mwisho ningeomba bila ya kuangalia personality vyama vya upinzani viungane kumuondoa joka kuu,alaf wakae chini kuangalia nani anatupeleka tokea hapo. They should first chase the fox into the forest ,thats when they can come to warn the hen from wondering in the wilderness. With this,here I stand to be corrected!
   
 20. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #20
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ungekuwa hujakimbia darasa la kiswahili ungeelewa maana ya neno "muhogo" na "kiazi" na kwa taarifa yako mimi sina ID nyingi nimeamua kwa hiari yangu kuingia JF kwa jina langu halisi na sio under cover kama wewe. Nakuheshimu na napenda uniheshim Mkuu.
   
Loading...