Walikiona cha mtema kuni ni police wa magamba si umesoma hapo? Makamishna wameenda kumbembeleza akubali kutoka mahabusu ili Arusha iwe na amani! Mmekubali sasa eh? Lema kishawaambia labda mumtishie kingine sio jela wala kumuua! Kama haogopi kutishiwa kufa unadhani mtamtishia nini zaidi ya hapo? Lema kishapuliza kipenga hakuna kurudi nyuma!
MwaJ!! Mzima weweee!!
Niruhusu niogezee kuwa Watanzania wote!
Hatuna shida nyingine, tunahitaji kuona HESHIMA na Kuheshimiana kama kunakoonyeshwa na MAKAMISHNA kunarejea mtaani ... Kwani Huo sio UTU? Kwani Huo Sio UBINADAMU? Ni Hicho tu!! Watanzania Hatujali ni Chama gani kitachukua fursa ya Kurejesha
HESHIMA,
UPENDO na
MATUMAINI ya Taifa, Hayo maneno Matatu ni Msingi wa
Mwenge wakweli wa UHURU Limnara Likubwa Likiwa Limesimama pale ARUSHA. Hivyo basi, UTU kama UPENDO, UTU kama HESHIMA na UTU kama MATUMAINI ... vitaendelea Kuwa ni MSINGI UTAKO SIMAMIWA NA POLISI NA SEREKALI KAMA WALIVYOFANYA
MAKAMISHINA pale mjini ARUSHA ... Mbona Historia itakuwa imejirudia? Kivipi?
Arusha itakuwa imekuwa nuru ya matumaini mapya! Itakuwa imeonyesha dhana ya UTU kwa vitendo na makamanda makamishana hao kuingia kwanye historia. Kwani BILA UTU hakuna maisha wala Uhai. Hivyo watakuwa wametafsiri kwa vitendo dhana ya UTU na kuanzisha uwepo wa AZIMIO LA PAMOJA LA UTU WA TAIFA. .. Lazima Taifa likae na kukubaliana kuwepo kwa
AZIMIO LA UTU na UBINADAMU wa Taifa, ambalo litakuwa Limeanzia Gerezani KISONGO kati ya makamishana, Mwenyekiti Mbowe, G Lema na wengine wote. Litakuwa Azimio la Utu na ubindamu kushika hatamu katika mji wa Arusha na kuenea kote Tanzania. Kama Ule waraka wa G Lema unavyodai . Kawaraka kadogo lakini kamesheheni Vilivyo.
Lakini leo tunaongelea Kutaka AZIMIO LA UTU Lifanyike au Kuanzia Arusha... yaani AZIMIO LA UTU LA ARUSHA... Liwe AZIMIO lililofikiwa ARUSHA!!(AZIMIO LA ARUSHA) Haaaa ahaaahhh .. Kwani halikuwahi kuwepo? Kwani ile nyumba kando ya Limnara likubwa pale ARUSHA inakumbukumbu Gani? .. Si Ni AZIMIO LA ARUSHA LA MWAKA 1967.
Liilikwenda wapi? Tunauliza Azimio la UTU wa UBINADAMU wa Mtanzania la Mwaka 1967 ..Lilikwendawa WAPI? Majibu mnajua!!
Lilimezwa na AZIMIO la wapinaga UTU la ZANZIBAR ...Wakaja na AZIMIO LA
VITU BADALA YA
UTU ...Sasa misukumo ya Kijamii (MIZIMU) YA ARUSHA IMEFUFUKA!!! Inadai AZIMIO LA UTU NA UBINADAMU LIREJEE... HAPA INATAKIWA HEKIMA NA BUSARA KUBWA!!
Soma tena Waraka wa G Lema ... Kama una Muda kaulinganishe ... na WARAKA WA AZIMIO LA ARUSHA MWAKA 1967!!!
Nani haoni kuwa Waraka wa G Lema ni MTIZAMO WA SASA WA AZIMIO LILELI LA MWAKA 1967? ...Alafu tuache mambo ya UBISHI usiokuwa na Tija ya KIUTU NA KIBINADAMU!! ... kitu ni kilekile!!! Na mtu ambaye hakuwahi kujua maana ya azimio la arusha asome tu waraka wa G lema kwani ule ndio muhutasari wake!! Ndio maana ya kuwa na Kumbukumbu ya azimio la arusha ile nymba pale Arusha na alama ya Mwenge wa uhuru kila Kona ya Nchi ya Tanzania!! Na sasa serekali iwe tayari kurejesha ..DHANA YA UTU NA UBINADAMU KWENYE NYANJA ZOTE NA FUJO ZITAKOMA!!
NAFIKIRI HILI LIMEELEWEKA!!!
KUDHIBITISHA KUWA ... UTU ... Haupitwi na wakati! Na waasisi wa azimio la 1967 ...walitabiri ... NGUVU YA UTU KAMA MSINGI WA USTAWI WA JAMII YA TANZANIA ....
Itarejea!! Bora Makamishana HODARI wameliona hilo na SASA WAUNGWE MKONO NA VIONGOZI WA SEREKALI WA NGAZI ZA JUU!!
Wajitokeza HADHARANI ...
WAUNGE MKONA KUREJEA KWA AZIMIO LA UTU NA UBINADAMU ...wafuate kale kabarua kadogi ka G Lema (kwani hata zimio la 1967 kalikuwa ka kurasa moja). Hata kama hawataki kumtaja yeye kama Muanzisha Vuguvugu... Kikubwa zaidi wajaribu zaidi kumuelewa na wasimuumize kwa namna yeyote!! Kwani hiyo ndio ishara ya UTU Mpya, Tanzania na Nuru Mpya ya Ubinaadamu!!!