Mbowe atikisa gereza la Lema

Jamani uko jela Lema anakaa room ya peke yake so mengi ya hayo mnayoyasema kama kuwa camerouned sidhani kama yanaweza mkuta
Ila ma sure ana mengi ya kusimulia
 
Ni vigumu sana kuacha asili nilidhani umebadilika kumbe ukivua gamba iko siku itarudia ukomavu ule ule.

Huyo hana tofauti na kina dada poa wa sinza,asipopewa posho havui ch**i na anaanza kuponda,akipewa tu hata kuivua anaona inamchelewesha anaichana,hivyo basi usimshangae.
 
Tatizo magamba wamezoea kujifungia ofisini ngoja waone wenzao wanavyozisaka taarifa toka jikoni
 
Mambo yanayoendelea gerezani ni aibu kuelezea ukitoka nje. Sidhani kama atakuwa tayari kuyaeleza hata kwa mke wake achilia mbali ndani ya bunge.
Yalishawahi kukupata nini, pole sana, una mtoto gani.
 
Aliacha kumtembelea Zitto akiwa Muhimbili anaona ni bora kumtembelea Lema akiwa gerezani?

Mhe. Freeman Mbowe alikuwa Jimboni kwake Kilimanjaro Zitto alipougua akiwa Dar es Salaam. Wasaidizi wake Makao Makuu Chadema ndio walishughulika ktk masuala ya kumpeleka India kwa matibabu zaidi. Mhe. Mbowe ameendelea kuwa karibu na Arusha kwa vile kulikuwa na kesi vile vile inamhusu. Kwa hiyo kumtembelea Mhe. Lema huko jela ni jambo la kawaida.

Mbona watu wengine mnaona upendeleo au uhasama mahali havipo?
 
Chadema wanajitahidi kwa kazi nzuri lakini tatizo lao hawajapata kiongozi ambaye ni 'unifying figure'. Wanaicheka CCM kwa mgawanyiko lakini na wao wenyewe ndiyo kitu kinachowanyemelea kwa sasa na wasishangae wakasambaratika hata kabla ya CCM. Kitendo cha Mbowe kutomtembelea Zitto akiwa hospitali eti tu kwakuwa alishindana naye kwenye kiti cha uenyekiti hakijengi bali kinabomoa.

Hapo kwenye red mkuu...
Tatizo letu ni pale tunapoongea hisia zetu kwa uhakika kama ndio ukweli wenyewe!
 
ZIARA ya Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, jana ilitikisa gereza kuu la Arusha huku uongozi ukihaha kuita askari wote waliokuwa mapumziko, kurudi kazini haraka kuimarisha ulinzi.

Mbowe alifika gerezani hapo saa 8.05 mchana kwa lengo la kumjulia hali Mbunge wa Arusha Godbless Lema ambaye mapema wiki hii, alikataa dhamana na kuamua kukaa gerezani kufuatia kuahirishwa kesi yake ya kudaiwa kuchochea maandamano bila kibali mjini humo hivi karibuni.

Katika ziara yake, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni , alimwomba Mbunge Lema kulegeza msimamo wake na kukubali kutoka gerezani kesho Jumatatu ili aweze kwenda Dodoma kuwawakilisha wananchi wake kwenye mkutano wa bunge unaonza kesho kutwa, Novemba 8.
.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuonana na Lema katika mahabusu ya gereza hilo lililopo eneo la Kisongo, Mbowe alisema amechukua hatua hiyo ili kumwezesha mbunge huyo kuhudhuria vikao vya bunge na kutumia nafasi hiyo kuueleza umma na jamii ya kimataifa adha anazokumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yake.

"Nimemwagiza atoke Jumatatu, tutakwenda pale mahakamani kumwekea dhamana na tutatoka naye pale hadi Viwanja vya NMC ambako atazungumza na wananchi wake kuwaeleza kilichotokea hadi kuchukua uamuzi wa kijasiri kwenda mahabusu," alisema Mbowe.

Alisema hawakusudii kufanya maandamano na kuliomba Jeshi la Polisi kutotafsiri mapokezi ya mbunge huyo kutoka mahakamani hadi NMC kama maandamano huku akionya kwamba wasithubutu kuingilia mipangilio hiyo, kwani Lema kama mbunge, ana haki ya kuzungumza na wapigakura wake.

"Tumechagua Jumatatu kwa sababu ya kupisha ujio wa ugeni mkubwa wa mwana Malkia wa Uingireza, Prince Charles unaotarajiwa kuanza hapa Novemba 9, mwaka huu na polisi wasithubutu kuingilia mipango hii, kwani inaweza kuvuruga hata makubaliano ya msingi tuliyofikiana nao kuhusu ugeni huo," alionya Mbowe

Alisema kama polisi wanadhani wanaweza kuingilia mapokezi hayo na mkutano wao wa hadhara na Arusha ibaki salama, basi wajaribu.

Alifafanua kuwa awali walipanga kuanza mikutano ya hadhara mjini Arusha kwa siku saba mfululizo kuanzia kesho kutwa na tayari waliwasilisha taarifa kwa Kamanda wa Polisi Wilaya (OCD), Zuberi Mwombeji, lakini baada ya majadiliano na uongozi wa jeshi hilo,walikubaliana kuahirisha kupisha ugeni wa Prince Charles.

Mbowe alisema majadiliano na makubaliano ya kuahirisha mikutano hiyo yalifikiwa kati yao na OCD pamoja na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa na akasisitiza kuwa utekelezaji utategemea ushirikiano wa jeshi hilo wakati wa mapokezi ya Lema na mkutano wa hadhara wa kesho.

Alisema katika mkutano huo, Chadema itatoa tamko kuhusu mateso yanayowakumba viongozi, wanachama na wapenzi wa chama hicho mkoani Arusha na sehemu mbalimbali nchini kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliopita.

Alisema kitendo cha Mbunge Lema kukubali kwenda gerezani kwa hiari kina ujumbe maalumu kwa dola inayotumia vitisho vya kubambikia wana mageuzi kesi na kuwafunga jela.

Wakati Mbowe akiingia gerezani hapo jana na msafara wa magari zaidi ya 12 na pikipiki kadhaa zilizopambwa bendera ya chadema, ulinzi uliimarishwa huku askari waliokuwa na silaha wakionekana kutanda kila kona. Mara baada ya kuwasili alilakiwa na uongozi wa gereza hilo.

Katika hatua nyingine, ujumbe mzito wa Jeshi la polisi ukiwa na makamishina wawili kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam jana ulimtembelea Mbunge Lema gerezani kuzungumza naye na kuwasilisha ombi maalumu ya kumtaka akubali kutoka mahabusu ili kurejesha amani na utulivu mjini Arusha.

Kwa mujibu wa Mbowe, Makamishina waliomtembelea Lema jana ni Peter Kivuyo, Simon Siro na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Leonard Paul
.
source mwananchi jumapili leo
 
Safi sana, umeharibu kwenye signature yako tu ambapo umepatia sehemu kidogo.
 
Tayari saa hizi nimeona zile Fuso za chadema zimeshaingia asubuhi hii tayari kwa mkutano wa kesho kumlaki Lema na kuongea na wananchi.
 
Lema kaumbuka na siasa zake uchwara.
Alikuwa anatishishia nyau. Chamtemakuni kakiona.
 
nimefurahi kusikia habari hii pia nina imani sana na Afande siro pia na lema naamini atakubali ili akawakilishe wananchi wake kule walikomtuma yaani bugeni
 
Mwaga mboga nimwage ugali.Serikali imeshikwa pabaya.
Ama serikali ikubali ama mwana wa malkia asilete zawadi.
 
Upuuzi mtupu.

CDM mnavuruga maisha na shughuli za kiuchumi za Wana-Arusha. Vurugu zenu na maandamano ya kijinga havina tija kwetu.

Tumetambua tulifanya kosa kubwa kuwapa dhamana ya kutuongoza. Hatutarudia kosa 2015.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom