bunge la tanzania
______________
majadiliano ya bunge
_____________
mkutano wa nne
kikao cha arobaini na sita tarehe 13agosti, 2011
(mkutano ulianza saa tatu asubuhi)
dua
spika (mhe. Anne s. Makinda) alisoma dua
mhe. Freeman a. Mbowe:
mheshimiwa spika, kikuletwa power station kijiji cha chemka,kata ya masama rundugai - wilaya ya hai, inayomilikiwa na tanesco imefungwa siku nyingi na mali zake zikiwemo nyumba, ardhi, mashine na miundombinu ziko katika hali mbaya. Nahitaji kujua ni lini station hii itafunguliwa/kufufuliwa. Aidha, ni vipi uwezekano wa station hii kukabidhiwa halmashauri ya wilaya ya hai kwa ajili ya kuendelezwa/kufufuliwa kwa kushirikiana na rea?
mheshimiwa spika, umeme wilaya ya hai. Miradi ya wilaya hii imekwama katika hatua mbalimbali. Bajeti ya wizara haionyeshi fungu lolote kwa mradi wowote wa wilaya ya hai. Miradi iliyo katikati itafanywaje? Miradi ambayo haijaanza itaanza lini? Miradi ya wilaya ya hai ambayo imekwama ni kama ifuatavyo:-
(a) miradi ya umeme iliyofika nusu.
(i) losaa kitongoji cha mungu amaye - mradi unaendelea, nguzo tayari zimewekwa bado waya.
(ii) bomangombe kingereka - mradi unaendelea, nguzo ndogo 60 pamoja na transfoma mpya tayari bado waya.
(iii) fiderisi - nguzo 17 zimewekwa, mradi unaendelea bado waya.
(iv) masama mashariki monjulu - mradi mdogo nguzo 30, bado waya.
(v) kware korongoni - nguzo 30 zimewekwa, mradi unaendelea bado waya.
(vi) kawaya - nguzo 12 tayari zimewekwa, mradi unaendelea bado waya.
(vii) bomangombe uzunguni - nguzo 17 zimeshapelekwa bado hazijasimamishwa, bado waya.
(viii) mroma ufishi - nguzo 10 zimewekwa, mradi unaendeleam bado waya.
(ix) kitifu kwa sadala - nguzo 24 tayari mradi unaendelea bado waya.
(x) tema masama mashariki - nguzo 28 tayari, mradi unaendelea bado waya.
(xi) lemira kati - nguzo 19 tayari mradi unaendelea, bado waya.
(b) miradi ya tanesco iliyo kwenye mpango
(i) machame ndernyi a nguzo 10 pamoja na waya na transifoma.
(ii) machame ndernyi b - nguzo 10 pamoja na waya.
(iii) uswaa mbweera - nguzo 24 na waya.
(iv) kia junction - nguzo 15 na waya.
(v) kwa sadala - nguzo 24 na waya.
(vi) bomangombe gezaulole - nguzo 12 na waya.
(c) miradi iliyokwama kupitishwa kutokana na tanesco kushindwa kumudu gharama
(i) lemira isuki kirumbiu - nguzo 40, transfoma moja na waya.
(ii) tema juu - transfoma moja ipo nguzo na waya bado.
(iii) uboro - nguzo 30, transfoma na waya.
(iv) mbosho parish - nguzo 60 zilihitajika zimepelekwa nguzo 30 na waya, bado nguzo 30 na waya.
(v) bomangombe magadini - nguzo 40 transfoma moja na waya.
(vi) kwa somali - nguzo 30 transfoma moja na waya.
(vii) mungushi kambi ya maziwa kuelekea sanya juu - nguzo 40 transfoma moja na waya.
(viii) chemka ngulu - nguzo 30 na waya.
(ix) longoi nguzo nne - nguzo 70 transfoma na waya.
(x) ngosero - nguzo 80 transfoma na waya.12
(xi) bomangore kwa kiriwe - nguzo 60 transfoma na waya.
(xii) roo secondary - nguzo 40 transfoma na waya.
(xiii) mashua - nguzo 60 na waya.
Mheshimiwa spika, maeneo mengi yenye miundombinu ya umeme sasa imechakaa sana na nyaya za umeme nyingi ni wazi (yaani hazikoinsulated) na kwa hali ya uoto wa sehemu za milimani nyaya hizi hupita katikati ya migomba na miti. Mimea hii sehemu nyingine husababisha
short circuit na hivyo kuongeza tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara. Aidha, mara
kadhaa nyaya hizi zimesababisha vifo au majeraha makubwa kwa wananchi. Ni lini tanesco
itaanza ukarabati wa miundombinu hii?
mhe. Magdalena h. Sakaya: