Mbowe anusurika kifo mara tatu

Mbowe anusurika kifo mara tatu

Elineema J Mosi

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2013
Posts
808
Reaction score
148
Mwnyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema amenusurika kuuawa katika matukio matatu yanayotokana na harakati zake za kisiasa.

Akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mji wa Meatu mkoani Simiu jana, Mbowe alisema hata kama atauawa hatasikitika na kwamba Watanzania wasimlilie.

Mbele ya umati huo akiwemo mbunge wa Maswa, John Shibuda, Mbowe alisema kuna watu ndani na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakifanya kila mbinu kuwaangamiza viongozi na makada wa chama hicho.

Mbowe alisema viongozi wa CHADEMA akiwemo yeye mwenyewe wamekumbana na misukosuko mingi, ikiwemo yenye kuhatarisha maisha yao kutoka kwa wanasiasa wasioipenda nchi, lakini kwa neema ya Mungu wamenusurika.

"Leo hii hata kama nikiuawa, naomba Watanzania msinililie. Mbele ya jeneza langu, nizikeni huku mkisema Bwana Alitoa na Bwana Ametwaaa, Jina Lake Lihimidiwe.

"Leo CHADEMA sio ya Slaa wala ya Mbowe bali ya Watanzania iliyojengwa kwa misukosuko mingi na mkono wa Mungu.

"Mmeshuhudia namna viongozi wake walivyonusurika kuuawa na kufungwa, na watu kufunguliwa na kesi mbalimbali.

"Kwa hiyo yeyote awe kiongozi wa CHADEMA au watawala anayetamani kuibomoa chadema hataweza kamwe," alisema.

Kiongozi huyo alisema wale wote wanaofanya hivyo, wajue kuwa wanapambana na mkono wa Mungu na wamelenga kuwaumiza Watanzania.

"CHADEMA ina baraka za Mungu na ndio maana imeshinda na kupita katika majaribu mengi ya watawala ambao wameshindwa kuifuta au kuibomoa," alisema.

Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wako katika ziara ya mikutano ya mabaraza ya wazi kujadili rasimu ya Katiba mpya ambayo itaendeshwa nchi nzima kwa nia ya kukusanya maoni ya Watanzania.

Chanzo: Tanzania Daima

MY TAKE:
Hii inaonyesha siasa za Africa ni ngumu na nizakidhalimu maana watu wanaviziana h ata kwa kuuwana.
 
Aisee. Halafu vipuuzi puuzi kama Makamba January na Jerry Slaa vinatukana. Ipo siku yao
 
Abarikiwe sana Mwenyekiti Mbowe... Ingawa anaongoza mapambano ya CDM kuingia ikulu, lakini ni wazi kwamba ameongoza vyema harakati za upinzani nchini. Hata kama CDM haitaingia ikulu, au hata kama yeye hatashuhudia ikiingia ikulu, lakini historia itabaki kuwa alikuwa mmoja wapo wa viongozi mahiri wa upinzani aliyewahi kutokea Tanzania hadi sasa...
Nchi inakuwa na raisi mmoja tu kwa wakati mmoja, lakini inakuwa na viongozi wa vyama vya upinzani kadhaa wakati wowote... Kwa sasa, na kwa historia ya nchi hii, Mbowe ndiye kinara kati ya wenyeviti wa vyama vya upinzani zaidi ya 18. Pamoja na kuwapo na wenye elimu kubwa sana zaidi yake, Mbowe amewapiku wote na kudhihirisha kipaji kikubwa cha kuongoza alicho nacho.

Namuombea maisha marefu na afya njema, ili siku moja apate nafasi ya kushuhudia kwa macho yake mabadiliko yale ambayo amekuwa akitapigania.

Viva Mwenyekiti wa ukweli...
 
sasa Mbowe anadanganya watu ili aonewe huruma? yeye kama amenusurika kufa Ponda naye atasemaje?
 
Afadhali wakoloni walikuwa wanaua waafrika kwa sabb walikuwa si ndugu zao. Kwa sasa tunauana sisi kwa sisi. Ama kweli nimeamini maneno ya P.W. Botha kwamba mwafrika wape risasi na bunduki,watauana 2
 
Hii inaonyesha siasa za Africa ni ngumu na nizakidhalimu maana watu wanaviziana hata kwa kuuwana.

Sasa Africa na hiyo habari hapo juu vinahusianaje?
Siasa za Jembe ne Nyundo ndo hatari, maana hata ile itikadi ya wakulima na wafanyakazi haizungumziwi kabisa siku hizi.
Ni mwendo wa madawa ya kulevya na biashara haramu tu!
 
No.
Hiyo inaonesha kuwa demokrasia ya kweli bado kujengeka Afrika nzima kwa ujumla.
Sio Tanzania tu. Demokrasia iliyopo kwa sasa ni ya kinadharia sana. Hili halihitaji uthibitisho kwa sababu tanzania ni uthibitisho tosha sana ikifuatiwa na nchi jirani ziizungukayo.
 
Abarikiwe sana Mwenyekiti Mbowe... Ingawa anaongoza mapambano ya CDM kuingia ikulu, lakini ni wazi kwamba ameongoza vyema harakati za upinzani nchini. Hata kama CDM haitaingia ikulu, au hata kama yeye hatashuhudia ikiingia ikulu, lakini historia itabaki kuwa alikuwa mmoja wapo wa viongozi mahiri wa upinzani aliyewahi kutokea Tanzania hadi sasa...
Nchi inakuwa na raisi mmoja tu kwa wakati mmoja, lakini inakuwa na viongozi wa vyama vya upinzani kadhaa wakati wowote... Kwa sasa, na kwa historia ya nchi hii, Mbowe ndiye kinara kati ya wenyeviti wa vyama vya upinzani zaidi ya 18. Pamoja na kuwapo na wenye elimu kubwa sana zaidi yake, Mbowe amewapiku wote na kudhihirisha kipaji kikubwa cha kuongoza alicho nacho.

Namuombea maisha marefu na afya njema, ili siku moja apate nafasi ya kushuhudia kwa macho yake mabadiliko yale ambayo amekuwa akitapigania.

Viva Mwenyekiti wa ukweli...

Siku nikikutana na Mheshimiwa Mwenyekiti F.Mbowe(MB),Nitamwambia maneno haya,bravo.
 
thats wonderful words mkuu.
 
mbowe ni zaidi ya kiongozi ndani ya chadema....viatu vyake vime mtosha..Glory glory Chadema.
 
Hakika hapa alimshika Shibuda makalio na maccm wake. Hongera mwenyekiti kwa kumuambia Shibuda ukweli, pamoja na wale waliotabiri kifo cha chadema.
 
Shibuda (Yuda Iskarioti huyo) alikuwepo akipanga usaliti wake!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom