Mbowe anaunguruma bungeni muda huu!

Mbowe anaunguruma bungeni muda huu!

wel said mkuu, unanikumbusha bunge la katiba. Ukawa walipoamua kususia bunge basi watu waliacha kulifuatilia na sasa watu wanataka Ukawa warudi ili waweze kulifuatilia tena.

Yani hii serikali ni kama redio ya betri kumi inavyopiga kelele na ghafla hunyamaza kimya pale unapochomoa betiri moja. Na upinzani ndo hiyo betri iliyotolewa.

Shikilia sindano hapo hapo mkuu ndo inaingia vizuri. R.I.P serekali ya jamuhuri ya Muungano ya ccm. Hivyo hivyo msijiguse wakati sindano inawaingia
 
Kaongea facts, lakini mahala si pake! Hili ni Bunge la Bajeti! Hizi siasa zinaturudisha nyuma sana.
 
naona anandeleza ulaghai tu, hamna chochote anachosema zaidi ya kuvumisha neno ccm. kila baada ya maneno kumi kuna neno ccm, ccm ccm.

kwani nani katuingiza sisi watanzania kwenye haya matatizo tuliyonayo leo? au wewe ulitaka atajwe nani?
 
mkuu embu niambie nini ameongea hapo cha maana, sana anajitetea kutoka kwao nje, anasema daftari la wapiga kura liboreshwe kama rasimu ilivyoelekeza chakushanga ambikiikimbia rasimu sasa hayo mapendekezo nani atayatetea tena????
kama kuna sheria ya nchi ameikiuka, mpeleke mahakamani! Habari ndio hiyo! Mtete au msitete, ujumbe umefika!
 
HOTUBAYA KIONGOZI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE.FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB)AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI YA WAZIRI MKUUKWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99 (9), ya Kanuni za Kudumuza Bunge Toleo la Mwaka 2013) _________________________________
  1. MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA MUSTAKABALI WA TAIFA
Mheshimiwa Spika,Nchi yetu ipo katika kipindi tete cha kikatiba na kisiasa. Mchakato wakutunga Katiba Mpya kwa ajili ya nchi yetu ulioanza kufuatia hotuba ya Mh. RaisJakaya Kikwete ya Mwaka Mpya 2011 uko katika hatari kubwa ya kuanguka nakuparaganyika. Sehemu kubwa na muhimu ya wajumbe wa Bunge Maalum, yaani wale wanaoundaUmoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamesusia vikao vya Bunge Maalum kutokanana kile wanachoona kama njama za kulitumia Bunge Maalum kama chombo chakupitishia matakwa ya kikatiba ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kutupa jalalanimatakwa ya wananchi kama yalivyoainishwa na Rasimu ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano ilivyoandaliwa na kuwasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko yaKatiba. Kwa sababu ya njama hizo, Bunge Maalum limegeuzwa kuwa uwanja wa matusi,vijembe, kauli za kibaguzi na vitisho dhidi ya wananchi wanaotaka mabadiliko yamsingi ya kikatiba na kisiasa, na ya muundo wa Muungano kati ya nchi mbilizinazounda Muungano huu, yaani Tanganyika na Zanzibar. Mheshimiwa Spika, Wakati akitangaza kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya katika hotuba yakeya tarehe 31 Desemba, 2010, Rais Kikwete alisema maneno yafuatayo ambayo, kwaumuhimu wake, tunaomba kuyanukuu kwa kirefu: “… Mwaka 2011, nchi yetu inatimiza miaka 50 ya Uhuru waTanzania Bara, miaka 47 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar na miaka 47 yaMuungano wa nchi zetu mbili. ... Kwa ajili hiyo ni vyema kuwa na Katibainayoendana na mabadiliko na matakwa na hali ya sasa. Katiba ambayo italipelekataifa letu miaka 50 ijayo kwa salama, amani, umoja na kuwepo maendeleo makubwazaidi.... “Ndiyo maana tukaamua kuanzisha mchakato huu na kwaajili hiyo, nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba ... itakayoongozwa naMwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbalikatika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano. Jukumu la msingi la Tumehiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wotebila kubagua, vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia,mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kotenchini, katika kutoa maoni yao juu ya wayatakayo kuhusu Katiba ya nchi yao. “Baada ya kukamilisha kukusanya maoni, Tume itatoamapendekezo yake yatakayofikishwa kwenye vyombo stahiki vya Kikatiba kwakufanyiwa maamuzi. Baada ya makubaliano kufikiwa, taifa letu litapata Katibampya kwa siku itakayoamuliwa ianze kutumika.... “Ni matumaini yangu kuwa mchakato huo utaendeshwavizuri, kwa amani na utulivu kama ilivyo sifa ya nchi yetu na mazoea yetu yakujadiliana bila kugombana.... Pasiwepo kutukanana, kudharauliana,kushutumiana, kubezana, kuzomeana wala kushinikizana. Naomba washirikiwaongozwe kwa hoja badala ya jazba. Tukiwa na jazba, hasira na kushinikizanakamwe hatutaweza kutengeneza jambo jema. Na inapohusu Katiba ya Nchi itakuwahasara tupu. Haitakuwa endelevu na kulazimika kufanyiwa marekebisho mengimwanzoni tu baada ya kutungwa.” Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza ahadi hiyo, Bunge lako tukufu lilitunga Sheria yaMabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania mnamo Novemba, 2011.Baadaye Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho mara tatu kati ya Februari 2012 naDesemba 2013. Aidha, Bunge lako tukufu lilitunga Sheria ya Kura ya Maoni, 2013.Vile vile, katika kipindi hicho hicho, Rais Kikwete aliteua Tume ya Mabadilikoya Katiba. Kama alivyoahidi Rais, Tume hiyo iliongozwa na mwanasheria aliyebobea naambaye aliwahi pia kuwa Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Katiba na Sheria naWaziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Jaji Joseph Sinde Warioba. Na kama alivyoahidi Rais, wajumbe wa Tume hiyowalitoka katika makundi mbali mbali ya jamii kutoka nchi zote mbili zinazoundaJamhuri ya Muungano. Wajumbe hao walijumuisha wanataaluma waliobobea,wanasheria, viongozi na watumishi wa umma waliolitumikia taifa katika nafasi zajuu, viongozi wa kidini na wawakilishi wa vyama vya siasa na wa asasi zakiraia.Mheshimiwa Spika, Kati ya Mei Mosi 2012 wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipoanza kazirasmi na tarehe 21 Machi, 2014, Tume hiyo ilipovunjwa rasmi, Bunge lako tukufuliliidhinisha jumla ya Shilingi bilioni 74.463 kwa ajili ya utekelezaji wamajukumu ya Tume. Katika kipindi hicho, Tume ilitembea nchi nzima kukusanya maoniya Watanzania juu ya Katiba Mpya waitakayo. Tume pia ilifanya rejea ya nyarakanyingi kama zilivyoorodheshwa katika kifungu cha 17(4) cha Sheria; pamoja nakupitia taarifa mbali mbali zilizoandaliwa na wataalamu walioteuliwa na Tumekwa ajili hiyo. Baadaye, kwa kuzingatia vyanzo hivi vya taarifa, tarehe 3 Juni 2013 Tumeilitoa Rasimu ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rasimuhiyo nayo ilipelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kutolewa maoni na wananchi,taasisi za kiserikali, asasi za kiraia, vyama vya siasa na watu mashuhuri.Aidha, Tume iliunda Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na ya kitaasisi ili kutoafursa kwa wananchi katika umoja wao kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Kwanza.Matokeo yake, Tume iliandaa Rasimu ya Pili ya Katiba ambayo iliwasilishwakatika Bunge Maalum na Mwenyekiti wa Tume, Jaji Warioba. Mheshimiwa Spika, Vyombo vya habari mbali mbali hapa nchini vimemnukuu Waziri wa Fedha Mh.Saada Salum Mkuya akisema kwamba, hadi kuahirishwa kwake, Bunge Maalumlimetumia zaidi ya Shilingi bilioni 27. Kama taarifa hizo ni za kweli itakuwana maana kwamba katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, mchakato wa KatibaMpya umetumia zaidi ya Shilingi bilioni 102. Hiki ni kiasi kikubwa mno chafedha katika nchi ambayo shughuli mbali mbali za maendeleo na huduma za jamiizenye umuhimu mkubwa kwa ustawi wa wananchi zimekwama kwa kukosa fedha. Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, licha ya matumizi haya makubwa ya fedha zaumma kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya; na licha ya maneno ya Rais kwamba wajumbewa Bunge Maalum wajadili Rasimu kwa hoja badala ya jazba, Rais Kikwete mwenyewendiye aliyeongoza mawaziri wake na viongozi wengine waandamizi na wajumbe waCCM wa Bunge Maalum katika kujadili Rasimu kwa “… kutukanana,kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana na kushinikizana.” Kauli na vitisho hivi vimetolewa hadharani sio ndani ya Ukumbi wa Bungetu, bali pia hata katika nyumba za ibada bila kujali athari zake kwa jamii yetuyenye imani tofauti tofauti za kidini. Wajumbe wanaounda UKAWA wamekataa kuwasehemu ya Bunge Maalum la aina hii na hawatarudi Bungeni hadi hapo dhima halisiya Bunge hilo itakapopatiwa ufumbuzi. Kama dhima hiyo itakuwa ni kutumia mwavuli wa Bunge Maalum ilikuendeleza mfumo wa kikatiba na muundo wa Muungano uliopo kwa sasa, basiwajumbe wa UKAWA hawatakuwa sehemu ya usaliti huo wa Watanzania. Hata hivyo,kama dhima ya Bunge Maalum itakuwa ni kujadili na kuboresha matakwa ya wananchikama yalivyodhihirishwa na Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume, basi wanachamawa UKAWA watakuwa tayari kurudi kwenye Bunge Maalum ili kuendelea na mjadala waRasimu hiyo.Mheshimiwa Spika, Madai ya Katiba Mpya yana historia ndefu ikianzia miaka ya mwisho ya1980. Mwaka 1990 Rais Ali Hassan Mwinyi aliunda Tume ya Rais ya Mfumo wa ChamaKimoja cha Siasa au Vyama Vingi iliyoongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu waTanzania, marehemu Francis Nyalali. Pamoja na mapendekezo mengine, Tume yaNyalali ilipendekeza kutungwa kwa Katiba Mpya kwa ajili ya nchi yetu. Tume hiyoilipendekeza pia muundo wa Muungano wa Serikali Tatu. Baada ya mfumo wa siasa wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1992, vyama vyaupinzani na makundi mbali mbali ya kijamii yaliendelea kudai kutungwa kwaKatiba Mpya. Hii ilitokana na kutoridhishwa na mfumo wa uchaguzi ambao haukuwahuru na wa haki, madaraka makubwa ya Rais, mfumo mzima wa usimamizi warasilimali za taifa pamoja na mapungufu mengi katika mifumo yetu ya utawala nauendeshaji wa Serikali. Kwa kiasi kikubwa, mapendekezo ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa naTume yanakidhi mahitaji haya ya mabadiliko ya kimsingi katika mfumo wa utawala,usimamizi wa rasilimali za taifa na uendeshaji wa Serikali. Ni wazi, kwa hiyo,kwamba Rasimu hii inatoa fursa muhimu ya kutibu majeraha yetu kama taifa. Kwa viongozi wa CCM, wakiongozwa na Rais Kikwete, kupotosha, kubeza nakukejeli mapendekezo haya ni kuthibitisha yale ambayo yaliwahi kusemwa naaliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Celina Kombani na baadaye kurudiwa naMwanasheria Mkuu Mh. Frederick Werema kwamba Serikali ya CCM haioni haja yakuwa na Katiba Mpya kwani iliyopo inatosha.Mheshimiwa Spika,Tangu mchakato huu wa Katiba Mpya ulipoanza mwanzoni mwa 2011, CCMilionyesha dalili zote za kutaka kuuteka na kuupotosha mchakato mzima. Suala lanafasi na ushiriki wa Zanzibar katika mchakato huu, na muundo wa Tume yaMabadiliko ya Katiba na utaratibu wa uteuzi wa wajumbe wa Tume yalikuwa masualayaliyoleta mvutano mkubwa. Baadaye suala la muundo, idadi na utaratibu wakuwapata wajumbe wa Bunge Maalum nayo yalileta mvutano mkubwa ndani na nje yaBunge lako tukufu. Hofu ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwamba CCM ingetumia mamlaka yaRais ya uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum kujaza makada wengi wa CCM katikaBunge hilo imethibitika kuwa ya kweli. Kwa utafiti wa Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni, kati ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum walioteuliwa na Rais Kikwete,zaidi ya wajumbe 160 ni wanachama na viongozi wa CCM waliochomekwa kwenye BungeMaalum kwa kutumia kivuli cha waganga wa kienyeji, taasisi za kidini, asasi zakiraia, taasisi za kitaaluma, watu wenye malengo yanayofanana, n.k. Ni dhahirihatua hizi hasi zimechangia kujenga mazingira ya kutokuaminiana na hivyo kuwekamsingi mbaya kwa mchakato wenyewe.Mheshimiwa Spika,Hata baada ya Bunge Maalum kuitishwa na kuanza kazi, CCM iliendeleakufanya hila za kuchakachua Kanuni za Bunge Maalum ili kupitisha hoja zaokirahisi. Hila hizo ziliposhindwa CCM ilitumia mabavu ya wazi kwa kulazimishaMwenyekiti wake wa Taifa atumie kivuli cha Urais kusisitiza msimamo wa CCM nakutisha Wajumbe wa Bunge Maalumu kwamba wakipitisha muundo wa Serikali Tatu,kama ilivyopendekezwa na Tume aliyoiteua yeye mwenyewe, basi Jeshi la Wananchiwa Tanzania litapindua Serikali. Hilo liliwezekana tu baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu kuchakachuaKanuni za Bunge Maalum ili kumwezesha Rais kuhutubia Bunge hilo baada yaMwenyekiti wa Tume, kama njia ya kumwezesha Rais kuijibu Tume na kupinga Rasimuyake hadharani na kulazimisha maoni na msimamo wa CCM.Mheshimiwa Spika, Kwa kadri ya ufahamu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, haijawahikutokea kwa Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kuchochea jeshi lake kufanyamapinduzi ya kijeshi ili kuzuia matakwa ya wananchi juu ya Katiba Mpyakutekelezwa. Haijawahi kutokea kwa Rais na Mkuu wa Nchi kuwaasa wajumbe waBunge la Katiba kujadili hoja badala ya jazba halafu Rais na Mkuu wa Nchi huyohuyo kugeuka na kukejeli na kubeza Tume aliyoiteua yeye mwenyewe na hivyokujenga mazingira ya wajumbe wa Bunge hilo “… kutukanana,kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana na kushinikizana.” Hapa ndipo CCM ilikoifikisha nchi yetu! Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inahoji, kama Rais Kikwete hakuwa tayarikukubali maoni ya wananchi katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba, kwa nini yeyena Serikali yake wameliingizia taifa hasara ya kutumia mabilioni ya fedha zawalipa kodi wa Tanzania kugharamia mchakato wa Katiba Mpya ambao ni wazi yeyena chama chake hawako tayari kukubali matokeo yake?Mheshimiwa Spika,Fedha zote zilizotumika kwa ajili ya gharama mbali mbali za Bunge Maalumhazikuidhinishwa na Bunge lako tukufu. Ukweli ni kwamba hadi sasa Bunge lakotukufu halijui bajeti yote ya Bunge Maalum, halijui fedha kiasi gani zimetumikakwa ajili ya matengenezo mbali mbali ya miundombinu ya Bunge hili, au kwa ajiliya posho, mishahara na stahili mbali mbali za wajumbe na watumishi wa BungeMaalum hadi lilipoahirishwa tarehe 25 Aprili, 2014. Aidha, Bunge lako tukufuhalina ufahamu wowote juu ya gharama za Bunge Maalum pale litakaporudi tarehe 5Agosti, 2014, kuendelea kujadili Rasimu ya Katiba Mpya.Mheshimiwa Spika, Bunge lako tukufu halina ufahamu huu kwa sababu, licha ya madai yaWabunge, Serikali hii ya CCM haijawahi kuleta makadirio ya matumizi kwa ajiliya shughuli mbali mbali za Bunge Maalum. Mwaka jana wakati Bunge lako tukufulinajadili makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwamwaka wa fedha 2013/2014, Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala iliagizakwamba bajeti ya Bunge Maalum “… iletwe Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa nakupitishwa.” Agizo hilo la Bunge sio tu lilipuuzwa mwaka jana kwa Serikali hiiya CCM kutokuleta bajeti hiyo, bali hata mwaka huu agizo hilo limepuuzwa kwanibajeti ya Bunge Maalum haipo katika makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaraya Katiba na Sheria! Mheshimiwa Spika, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inatamka wazi kwamba fedha zotezitakazogharamia mchakato wa Katiba Mpya zitatoka katika Mfuko Mkuu wa Hazinaya Serikali. Ibara ya 136(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniainatamka kwamba “fedha hazitatolewakutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali kwa ajili ya matumizi (isipokuwa) fedhahizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa yatokane na fedhazilizomo katika Mfumo Mkuu wa Hazina ya Serikali na idhini hiyo iwe imetolewana Katiba hii au Sheria nyingine yoyote; (na) fedha hizo ziwe kwa ajili yamatumizi ambayo yameidhinishwa ama na Sheria ya Matumizi ya Serikaliiliyotungwa mahususi na Bunge au Sheria iliyotungwa kwa mujibu wa masharti yaibara ya 140 ya Katiba hii.” Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 136(3) ya Katiba, “fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali hazitatolewakutoka Mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpaka matumizi hayo yaweyameidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na pia kwasharti kwamba fedha hizo ziwe zimetolewa kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwaajili hiyo kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.” Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa vifungu tajwa vya Katiba, fedha kwa ajili ya matumizimbali mbali ya Bunge Maalum zilitakiwa kuidhinishwa na Katiba au Sherianyingine yoyote. Masharti haya yalitekelezwa kwa Bunge lako tukufu kutungaSheria ya Mabadiliko ya Katiba iliyoidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katikaMfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali. Pili, fedha kwa ajili ya matumizi ya Bunge Maalum zilitakiwakuidhinishwa na ama Sheria ya Matumizi ya Serikali iliyotungwa mahususi naBunge au Sheria iliyotungwa kwa mujibu wa ibara ya 140 ya Katiba. Ibara ya 140inahusu Mfuko wa Matumizi ya Dharura unaoanzishwa kwa ajili ya mambo ya harakana dharura ambayo hayakutazamiwa kutokea na ambayo hayakupangiwa fedha zozoteza matumizi. Sharti hili halikutekelezwa. Tatu, hata kama fedha za matumizi ya Bunge Maalum zingeidhinishwa kamainavyotakiwa na Katiba, bado matumizi hayo yalitakiwa kuidhinishwa na Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Hili nalo halikutekelezwa. Ukweli nikwamba ingekuwa ajabu sana kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kuidhinisha matumizi yafedha za Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali wakati matumizi hayo hayakuidhinishwakwa mujibu wa Katiba. Kwa sababu zote hizi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kupatamajibu ya maswali yafuatayo:
  1. Je, bajeti ya matumizi ya BungeMaalum ni kiasi gani na kwa ajili ya matumizi gani?
  2. Je, ni kiasi gani cha fedha hizokimeshatumika hadi sasa na kwa ajili ya matumizi gani?
  3. Je, ni nani aliyejadili na kupitishabajeti hiyo?
  4. Je, ni Sheria gani iliyotungwa naBunge lipi iliyoidhinisha matumizi haya ya fedha za umma?
  5. Je, ni lini na kwa waraka ganiMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliidhinisha matumizi haya?
Mheshimiwa Spika, Majibu ya maswali haya ni muhimu ili kuliepusha taifa letu na balaa laufisadi na wizi mkubwa wa fedha za umma kama ilivyotokea mwaka 2005. Mwaka huo,kama inavyojulikana, mabilioni ya fedha za umma yaliibiwa kutoka katika akauntiya kulipa madeni ya nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kugharamiakampeni za Uchaguzi Mkuu za CCM na mgombea wake wa Urais. Makada wa CCM na viongoziwaandamizi wa CCM na Serikali yake walishiriki katika ufisadi huo. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali hii ya CCM itoe kaulirasmi mbele ya Bunge lako rasmi kuhusu giza hili lililogubika fedha za matumiziya Bunge Maalum. Hii ni muhimu sio tu kwa sababu ni muhimu kuwa na uwazi katikamatumizi ya fedha za umma, bali pia ili kuzuia wizi na ufisadi wa fedha za ummakwa kutumia kivuli cha mchakato wa Katiba Mpya ambao tayari umevurugwa na CCM,Serikali yake na viongozi wake waandamizi. Mheshimiwa Spika,Katika mazingira ambayo Bunge Maalum limegeuzwa na CCM kuwa uwanja wakuwazomea, kuwatukana, kuwatisha, kuwadhalilisha na kuwabagua kidini na kiasiliyao, wajumbe wa Bunge hilo wanaotetea maudhui ya Rasimu ya Katibailiyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Katika hali ambayo CCM imejazamakada wake ndani ya Bunge Maalum kwa kutumia kofia na vivuli mbali mbali vyakitaasisi ili kuhakikisha agenda yake ya kuendeleza mfumo wa kikatiba na muundowa Muungano uliopo inatekelezwa. Katika mazingira ambayo CCM inatumia wingi wake huo kupindua Rasimu yaKatiba iliyoandaliwa na Tume kufuatana na maoni ya wananchi. Katika hali ambayowajumbe wa CCM katika Bunge Maalum wamebadilisha Kanuni za Bunge Maalum ilikuwawezesha kuchakachua maoni ya wananchi kama yalivyoakisiwa na Rasimu yaTume, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kuweka wazi msimamo wa wajumbewake na wanachama wa UKAWA kwamba haitakuwa busara kwake kuendelea na mjadalawa Bunge Maalum wenye lengo la kupitisha mapendekezo ya kundi la viongozi waCCM. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na wanachama wa UKAWA haiko tayarikuendelea kushiriki katika Bunge Maalum ambalo limejaa kauli za kibaguzi,kashfa, vijembe na matusi dhidi ya wajumbe wa UKAWA na dhidi ya wajumbe wa Tumeya Mabadiliko ya Katiba, hasa Mwenyekiti wake Jaji Joseph Sinde Warioba.Mheshimiwa Spika,Mjadala wowote utakaoendelea kuanzia sasa katika Bunge Maalum hautakuwana uhalali wowote mbele ya macho ya Watanzania. Ni mchakato wa CCM,unaoendeshwa kwa fedha za umma na wanaCCM, kwa faida na matakwa ya CCM.Kinachoendelea sasa katika Bunge Maalum hakitajibu matatizo mbali mbali yaMuungano ambao umeigeuza Zanzibar kuwa koloni la Tanganyika na ambaoumeivalisha Tanganyika joho la Jamhuri ya Muungano na ambao unatishia mahusianokati ya wananchi wa nchi hizi mbili. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kwa niaba ya wanachama wa UKAWA,itaendeleza harakati za kudai Katiba Mpya yenye kujibu haja, matakwa namatumaini ya Watanzania walio wengi nje ya Bunge Maalum ambalo limetekwa nyarana CCM. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni itaendeleza harakati, nje ya BungeMaalumu, zitakazowezesha kubadilishwa kwa muundo wa Muungano kwa kuivuaTanganyika koti la Muungano, kuipatia Zanzibar mamlaka kamili ndani ya Muunganona kujenga mahusiano ya hadhi na haki sawa baina ya Tanganyika na Zanzibar. Kama ilivyoonekana wazi wakati wa mjadala katika Kamati mbali mbali zaBunge Maalum, licha ya kujaza makada na washirika wake, CCM haiwezi kupitishamatakwa yake ndani ya Bunge hilo kwa vile haiwezi kupata theluthi mbili yaidadi ya wajumbe wa kuiunga mkono kama inavyotakiwa na kifungu cha 26(1) chaSheria ya Mabadiliko ya Katiba na ibara ya 98(1) ya Katiba. Hii ndio sababupekee iliyosababisha kuahirishwa kwa Bunge Maalum hadi mwezi Agosti ijayo bilaya kupiga kura ya maamuzi juu ya Sura za Kwanza na Sita za Rasimu zinazohusumuundo wa Muungano. Kama CCM haijaweza kupata idadi ya wajumbe inayotakiwa na Sheria naKatiba ndani ya Bunge Maalum inayolitawala, itakuwa ni ndoto kupata idadiinayotakiwa na Sheria wakati wa kura ya maoni ya kuhalalisha Katiba Mpyaisiyotokana na matakwa ya wananchi. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inawatakaWatanzania wote wenye nia njema na nchi yetu, kujiandaa kwa ajili ya kura hiyoili kuhakikisha kwamba ndoto na matumaini yao kuhusu Katiba Mpya hayapotezwikutokana na hila za CCM na washirika wake. 2. KAULI ZA UCHOCHEZI NA UBAGUZI NJE YA BUNGE MAALUM MheshimiwaSpika, Pamoja na kuhamisha mjadala wa Bunge Maalum la Katibausijadili Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba nabadala yake kujadili Rasimu ya Katiba ya Chama kimoja, CCM, nje ya BungeMaalum, imeendeleza kauli za kichochezi na kibaguzi zinazoweza kuvunja amani. Katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdrahamani KinanaUnguja wa tarehe 4 Mei 2014, “Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW),Salmin Awadh Salmin ambaye ni Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba, amesemawawakilishi wa CCM wanajiandaa kuwasilisha hoja binafsi kwenye Baraza hilo ilikuwapa nafasi wananchi waulizwe iwapo wanataka kuendelea na Serikali ya Umojawa Kitaifa.” Madhumuni ya mchakato huo ni kuvunja serikali ya Umoja waKitaifa ambayo iliamuriwa iwepo na kura ya maoni ya Wazanzibari wote naimesaidia kuleta amani na utulivu Zanzibar. Aidha, kauli ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, BaloziSeif Idd katika mkutano huo wa CCM kuwa Mhe. Ismail Jussa Ladhu, Mwakilishi waMji Mkongwe kuwa siyo raia wa Zanzibar ni ya kibaguzi, kichochezi na yenyekupandikiza chuki dhidi ya jamii watu wenye asili ya Kihindi. Ni kauliinayopaswa kulaaniwa na kilampenda amani popote alipo. MheshimiwaSpika, Kambi rasmi ya Upinzani inapenda kumwuliza Mheshimiwa WaziriMkuu, kama hii sasa ndiyo Sera Mpya ya CCM na serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kuivunja Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na kuibua hisia zaubaguzi? Jeshi la Polisi lilishiriki katika mauaji yaliyotokeaZanzibar Januari 2001 na kwa mara ya kwanza kusababisha wakimbizi zaidi ya 2000kutoka Zanzibar kwenda Kenya. Kauli za kuchochea kuivunja serikali ya Umoja waKitaifa Zanzibar zinatonesha vidonda na zinapandikiza mbegu ya chuki na vuruguinayoweza kusababisha maafa makubwa. MheshimiwaSpika, Ikumbukwe Baraza la Wawakilishi kwa pamoja lilipeleka warakakwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kupendekeza “kuwepo kwa mamlaka huru yaZanzibar, mamlaka huru ya Tanganyika na mamlaka ya Muungano na iwekwe wazimaeneo, uwezo, nguvu, utendaji na mipaka ya kila mamlaka.” Kwa Kiswahili rahisi, mamlaka huru ya Zanzibar, mamlaka huruya Tanganyika na mamlaka ya Muungano maana yake Serikali ya Zanzibar, Serikaliya Tanganyika na Serikali ya Muungano. Kwa CCM na Serikali ya Muungano kuwabana Wawakilishi waZanzibar kubadilisha msimamo wao wakati wa Bunge maalum la Katiba ni kuendelezataswira kuwa mambo ya Zanzibar yanaamuliwa Dodoma na kwa hiyo kuendeleakuudhoofisha Muungano. MheshimiwaSpika, Katika mizunguko ya mikutano ya CCM na maandamano yapikipiki kuhusiana na mchakato wa Katiba ndani ya Tanganyika na Zanzibar,kumeendelea kutolewa kauli za kutukana, kudhalilisha na hata kubeza viongozimbalimbali wa vyama vingine na hata wasio na vyama wanaotofautiana kimsimamo aukimtazano na CCM. MheshimiwaSpika, Viongozi wa juu wa CCM na serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania wanawajibika kukemea kauli hizi lakini hawafanyi hivyo na badala yakekuonekana ama kuzitoa, kuzikoleza au kuzishabikia bila kutathmini nafasi nawajibu wao wa kuliunganisha Taifa. Kitendo hiki siyo tu ni fedheha kwa Chama Tawala, bali niushuhuda wa aina gani ya viongozi tulio nao. Vikiruhusiwa kuendelea vitendo vya CCM vitaliingiza taifaletu katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na hata maafa.
wtNU09GRklDRTkuMBgAAAAMbXNPUE1TT0ZGSUNFOS4wAvGZtJYAIf8LTVNPRkZJQ0U5LjAYAAAADGNtUFBKQ21wMDcxMgAAAAdPbbelACH5BAEAAAAALAAAAAABAAEAAAICRAEAOw==
3.MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU WA2015. MheshimiwaSpika, Iliyoonekana awali dhamira njema ya kupata Katiba aliyokuwa nayo RaisJakaya Kikwete ilikuwa itupatie Katiba Mpya kwa Watanzania katika Mwaka 2014.Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inalitaka Bunge Maalumu kujadili Rasimu yaKatiba Mpya na Maudhui yake kama iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko yaKatiba na si vinginevyo. Ni bahati mbaya kwamba, Rasimu ya Katiba Mpya imewekwa kando na mjadalawa katika Bunge Maalumu umejikita katika Mapendekezo ambayo hayamo katikaRasimu. Hali hii inapoteza uhalali wa Bunge Maalumu la Katiba, si tu kwa kuwalinakwenda kinyume na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kifungu cha 25 lakini kwa sababulinakwenda kinyume na Matakwa ya wananchi ambayo kwa ujumla wao yako katikaRasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa na Tume. Mheshimiwa Spika, Ni bahati mbaya zaidi kwamba baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu laKatiba hasa kutoka kundi la walio wengi wamejivika jukumu lililokuwa la Tume yaMabadiliko ya Katiba wakidai kupokea maoni mbadala ya wananchi, kitendo hiki nikinyume na Sheria na ukiukwaji wa kiasi kikubwa wa haki ya wananchi ambao kwaujumla wao walitoa maoni yao kwa Tume ya Katiba. Mheshimiwa Spika, Nchi yetu inapaswa kuingia katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa naUchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Mwaka 2015. Ndoto ya Watanzaniailikuwa kutumia Katiba Mpya katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Kama tutakwenda katika uchaguzi mkuu wa Mwakani bila Katiba Mpyatutaliingiza Taifa katika mgogoro mkubwa wa kikatiba yaani “Constitutionalcrisis” ambao utakuwa rahisi kuzaa machafuko haswa kipindi cha uchaguzi. Katiba inayotumika sasa, Katiba ya Mwaka 1977, ina mapungufu mengi nahaiwezi kutupatia uchaguzi ulio huru na wa haki katika mazingira ya sasayanayojengwa na uzoefu wa chaguzi nne zilizopita chini ya mfumo wa vyama vingi. Mheshimiwa Spika, Ni dhahiri vilevile kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kufikia chaguzizilizo mbele yetu bila kukamilisha upatikanaji wa katiba mpya yenye maridhiano.Kwa vyovyote vile, uhalali wa Katiba itakayokuwepo wakati huo wa uchaguzi ndiyonjia pekee ya kutokugeuza chaguzi za mbele kuwa kichocheo cha mpasuko mkubwazaidi. Tukienda katika Uchaguzi Mkuu Mwakani tukiwa katika mazingiratuliyonayo leo tutakwenda tukiwa tumegawika kama Taifa pengine kuliko wakatimwingine wowote katika historia ya nchi yetu. MheshimiwaSpika, Kuna uwezekano mkubwa wa Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015 kuwachanzo cha machafuko makubwa ya kisiasa hapa nchini ikiwa Serikali itaendeleakupuuza mapendekezo ya marekebisho ya Sheria na Kanuni mbalimbali za Uchaguzizilizolalamikiwa kwa muda mrefu. Miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa na vyama vya siasa nipamoja na daftari la kudumu la wapiga kura, marekebisho ya Sheria ya Uchaguziya Mwaka 1985 ambayo imepitwa na wakati na hivyo kutokidhi mahitaji ya kisiasaya sasa, na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi. MheshimiwaSpika, Kutokana na kutofanyika kwa marekebisho hayo, chaguzizimekuwa zikifanywa kiholela bila utaratibu unaoeleweka kwa kutumia mwanya waudhaifu au upungufu uliopo katika sheria na kanununi mbali mbali za uchaguziili mradi udhaifu au upungufu huo unakipa Chama cha Mapinduzi ushindi. MheshimiwaSpika, Mara kadhaa Serikali ilipoulizwa kuhusu marekebisho yasheria na kanuni mbalimbali za uchaguzi imekuwa ikijibu kwamba tusubiri KatibaMpya ambayo itatatua kero hizo. Ni kweli kwamba mchakato wa Katiba Mpyaunaendelea, lakini umegubikwa na wingu zito la mivutano jambo ambalo nikiashiria kimojawapo kwamba tunaweza tusipate Katiba Mpya kwa muda uliopangwa. MheshimiwaSpika, Kwa kuwa kuna dalili na viashiria vya kutopata katiba mpyakabla ya uchaguzi mkuu wa 2015, na kwa kuwa hatutakuwa tayari kuingia katikauchaguzi mkuu kwa kutumia katiba ya sasa ambayo ndio chimbuko la matatizo yaki-uchaguzi tuliyo nayo sasa; Hivyo basi Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali kueleza mbele ya Bunge hili ina mpango gani wa kuwekautaratibu wa mpito (transitional arrangements) kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015ikiwa uchaguzi huo utafanyika kabla ya Katiba Mpya kupatikana. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri kwa dhati kabisakwamba, taratibu za mpito za kushughulikia masuala yote ya Uchaguzi Mkuuziendelee kufanyika ili kama uchaguzi mkuu utafika kabla ya kuwa na katiba mpyabasi kuwe na “fall-back position” ili kuinusuru nchi kuingia katika mtanzikoambao unaweza kuwa chanzo cha machafuko ya kisiasa. Mheshimiwa Spika, Hatuwezi kuingia uchaguzi wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa kwa utaratibuuliopo leo. Hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi Mkuu mwakani na Tume ya Uchaguzi kamailivyo leo ambayo haijawekewa vyombo vya kikatiba ikiwemo mifumo ya utendajiambayo itahakikisha uhuru wa Tume unalindwa na haki kutendeka kwa wadau wote. Hatuwezi tena kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani wakati Matokeo yaUchaguzi wa Rais hayawezi kuhojiwa Mahakamani na hoja ya mgombea huruhaijapatiwa majibu. Hatuwezi kuingia katika uchaguzi ujao na daftari la wapiga kuralililopo leo. Hatuwezi kulikubali daftari jipya litakalotengenezwa kama wadau wotehatutashirikishwa kikamilifu katika hatua zote za upatikanaji wake ikiwemomifumo itakayotumika. Mheshimiwa Spika, Naomba kurudia, Ni kweli, kama ilivyo kawaida, Serikali na CCM inawezakupuuza tahadhari hizi na kulazimisha kwenda katika chaguzi hizi katikamazingira ambayo hayana muafaka kama inavyoonekana sasa katika Mchakato wakatiba Mpya. 3.1 UCHAGUZI WASERIKALI ZA VITONGOJI, VIJIJI NA MITAA Mheshimiwa Spika; Mwezi Machi2014 Waziri Mkuu Mizengo Pinda alizungumza na vyombo vya habari na kuelezakwamba ameona dhahiri hatari ya kusogezwa mbele kwa Uchaguzi wa Vitongoji,Vijiji na Mitaa kutoka Oktoba mwaka 2014 mpaka mwaka 2015.Waziri MkuuPinda alieleza kwamba Uchaguzi huo ungesogezwa mbele kutoa nafasi kwa kazizingine kuendelea hususan mchakato wa mabadiliko ya katiba. Waziri Mkuu Pindaalieleza kwamba angemwomba Rais Jakaya Kikwete kusogeza mbele uchaguzi huo.Hata hivyo,wakati kauli hizo zikitolewa Kambi Rasmi ya Upinzani inazo taarifa kwambamaandalizi ya uchaguzi huo yanaendelea chini kwa chini kwa ajili ya uchaguzihuo kufanyika Oktoba mwaka 2014. Maandalizi hayo ni pamoja na mapitio ya Kanuniza Uchaguzi tajwa. Mheshimiwa Spika; Kambi Rasmiya Upinzani inataka Waziri Mkuu alieleze Bunge iwapo aliwasilisha maombi husikakwa Rais na nini majibu juu ya hatma ya uchaguzi husika. Serikali inayotawaliwana CCM inapaswa kuhakikisha kwamba inaheshimu maoni ya wananchi juu ya uchaguziwa vitongoji, vijiji na mitaa ambapo wametaka mabadiliko makubwa ya taratibu zauchaguzi huo kupitia mchakato wa mabadiliko ya katiba. Kambi Rasmiya Upinzani inatambua kwamba Uchaguzi wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa na mfumomzima wa Serikali za Mitaa sio mojawapo ya mambo ya Muungano. Hivyo, kwakuzingatia rasimu kuwa iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katikaBunge Maalum imependekeza muundo wa Muungano wa Shirikisho lenye Serikali tatu,masuala ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa yanapaswa kuingizwa katika Katiba zaNchi Washirika za Tanganyika na Zanzibar. Hivyo, KambiRasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kufanya maamuzi na mabadiliko ya Kisheriakuwezesha uchaguzi huo kufanyika mapema baada ya mchakato wa mabadiliko yaKatiba kukamilika ili kuhakikisha kwamba Uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki. Mheshimiwa Spika; Izingatiwekuwa chini ya sheria zetu, kanuni za chaguzi hizo hutungwa na Waziri mwenyedhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Na kwa mujibu wamuundo wa sasa wa utawala wa Tanzania pamoja na kuwa na waziri wa nchi anayehusikana TAMISEMI, mwisho wa siku mwenye dhamana kamili ya “Wizara” hii ni WaziriMkuu, ambaye kwa sasa ni Mheshimiwa Mizengo Pinda. Itakumbukwakwamba mwaka 2009 katikati ya mwezi Agosti baada ya kimya cha muda mrefu,kilichoambatana na shinikizo toka kwa wadau kutokana na serikali kucheleweshakutoa kanuni tofauti na ahadi yake, hatimaye Waziri Mkuu Pinda kupitia Tangazola Serikali (GN) namba 304 ya tarehe 21 Agosti 2009 alitoa kanuni na maelekezokuhusu taratibu za uchaguzi husika yaliyotolewa kwa nyakati mbalimbali. Mheshimiwa Spika; Ifahamike kwamba mwanya huu wa kisheria wa Wazirikutunga kanuni ulitumiwa vibaya mwaka 2004 na kufanya kanuni hizo kutungwakupendelea chama kinachotawala kwa kuweka mianya ya hujuma za kiuchaguzi.Matokeo yake ni uchaguzi uliopita wa vitongoji, vijiji na mitaa kutokuwa huruna haki kutokana na mapungufu mengi ambayo hata serikali yenyewe iliyakiri.

Mathalani upigaji kura haukuwa wa siri, fujo katika mikutano ya uchaguzi,matayarisho kuwa hafifu, kuingiliwa na maafisa na watendaji wa kata na vijijiambao walifikia hatua ya kuwatisha wananchi na kutotoa taarifa za muhimu zauchaguzi, kukosekana kwa daftari la wapiga kura na uchaguzi kusimamiwa nachombo kisicho huru cha kiserikali moja kwa moja(Wizara ya TAMISEMI).


Kutokana namapungufu hayo CCM ilishinda kwa asilimia 96 na kupata mtaji haramu wa kisiasaambao ilianza nao kama hujuma katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na kufanyauwanja wa ushindani wa kisiasa usiwe sawa. Na hivyo, CCM ikashinda kwatakribani asilimia 80 katika uchaguzi mkuu mwaka mmoja baadaye. Lakini zaidikutokana na hujuma hizo wananchi wakalazimishwa kuongozwa na viongozi wavitongoji, vijiji na mitaa katika maeneo mengi wasio kuwa na uhalali wakukubalika ambao wamekuwa kikwazo cha maendeleo na pia kusababisha migogoroambayo ingeweza kuepukwa.

Mheshimiwa Spika;
Ilitarajiwakwamba marekebisho ya haraka yangefanyika , hata hivyo hakuna hatua za maanazilizochukuliwa kati ya mwaka 2005 mpaka 2008. Kesi iliyofunguliwa na vyama vyaupinzani mwaka 2004 kuhusu kanuni na taratibu za uchaguzi wa vitongoji, vijijina mitaa mpaka sasa ilibaki katika kizungumkuti. Kwa upande mwingine, Serikaliilikuwa ikiitisha mikutano na vyama na kuiahirisha bila maamuzi ya msingikufikiwa kuhusu marekebisho yanayostahili kufanywa katika sheria na kanunizinazosimamia chaguzi husika, hali ambayo imeanza kujirudia tena kati ya mwaka2011 na 2014.


Mheshimiwa Spika; Mwaka 2009,mwezi Februari ndipo serikali imesaini makubaliano na wadau kuhusu uchaguzihuu. Kwa kisingizio cha ufinyu wa muda, masuala ya msingi yaliyopaswa kufanyiwamarekebisho mengi hayapo kama sehemu ya makubaliano hayo. Kwa mara nyinginetena, serikali ilichelewesha muda na baadaye kutumia kisingizio cha mudakukwepa kufanya mabadiliko ya msingi ya kisheria ya kuhakikisha uchaguzi huuunakuwa huru na wa haki.

Kama ilivyotarajiwa kutokana na makubaliano hayo, yafuatayo iliamuliweyasifanyiwe marekebisho kutokana na sababu mbalimbali zilizotolewa na serikaliikiwemo ufinyu wa muda. Kuhusu kilio cha miaka mingi cha wadau cha kutakauchaguzi usimamiwe na Tume ya uchaguzi kama ilivyo katika baadhi ya nchinyingine duniani; makubaliano yaliweka bayana kuwa uchaguzi utaendeleakusimamiwa na serikali kupitia waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa. Ndiomaana kanuni ziliendelea kutungwa na waziri badala ya chombo huru. Katikakanuni hizo umri wa kugombea; umebaki kuwa miaka 21 badala ya kushuka mpaka 18.Wagombea binafsi; hawakuruhusiwa.


Mheshimiwa Spika; Mwito waVyama vya siasa kutaka viwezeshwe kutoa elimu ya uraia nao haukuzingatiwa.Serikali iliendelea kuweka msimamo kupitia maelekezo ya taratibu za uchaguzihusika kuwa jukumu la kutoa elimu ya uraia litaendelea kuwa la serikali. Hoja yakutaka uchaguzi wa madiwani uende sambamba na chaguzi zingine za mitaa nayohaikuwepo katika kanuni zilizotolewa na Waziri Mkuu Pinda. Uchaguzi wa madiwaniuliendelea kuwa na uchaguzi mkuu mwaka 2010; hii ni kwa sababu suala hililinahitaji marekebisho ya kisheria na serikali ilishatamka wazi kwamba mudaumeshakwisha wa kufanya marekebisho husika.

Haya ni masuala nyeti ambayo wadau wengi walipenda yafanyiwe marekebisho lakinihakuna mabadiliko yoyote ambayo Serikali iliyafanya kuhusu masuala hayo katikakanuni zilizotungwa ambazo Waziri Mkuu Pinda alizitangaza.

Mheshimiwa Spika;
Matokeo yakeni kuwa Waziri Mkuu Pinda na ofisi yake kuandaa Kanuni na taratibu za uchaguziwa vitongoji na mitaa zilizo kinyume na misingi ya chaguzi huru na haki ambayoni mhimili wa utawala bora. Ama kwa hakika mambo haya yanahitaji kutazamwa kwakina na kwa haraka na wadau wowote ili kuepuka hali hiyo kujiridua na hivyochaguzi za ngazi hiyo kugubikwa navurugu zenye kutishia amani na demokrasia.

Mheshimiwa Spika;
Kasoro hizoni pamoja na kanuni kuelekeza kwamba karatasi za kura kutokuwa na majina ya wagombea na kwamba mpiga kuraalilazimika kuandika mwenyewe. Hali ilichochea kuchelewa ama kuvurugika kwamchakato wa upigaji na uhesabuji wa kura katika maeneo mengi. Mheshimiwa Spika, Katika nchiambayo takribani nusu ya wananchi wake hawajui kusoma na kuandika na sehemukubwa ya wanaojua bado si kwa kiwango kizuri, uamuzi wa kutunga kanuni ambazozinalazimisha kwamba wapiga kura waandike wenyewe majina kamili ya wagombeaulitoa mianya ya kuvurugika kwa uchaguzi na ukijirudia tena utasababisha atharizaidi.

Mheshimiwa Spika,
Baadhi yaupungufu Ofisi ya Waziri Mkuu iliukirimnamo 11 Septemba 2009 kupitia barua yenye kumbukumbu Na. HB.114/126/01 kwambamaelekezo ambayo iliyatoa yalikiuka kanuni. Mathalani,maelekezo yalisema wajumbe wa Halmashauri ya vijiji wanawake wa viti maalumwatakuwa si chini ya 25%. Wakati ambapo Sheria Na. 19 ya mwaka 2009 inatamkakwamba idadi ya wanawake viti maalum katika halmashauri ya kijiji inatakiwakuwa si chi ya theluthi moja ya wajumbe ambayo kwa vyovyote vile sio chini yawanawake nane(8). Mheshimiwa Spika, Kwa upandemwingine maelekezo ya uchaguzi yaliyotolewa na Waziri Mkuu Pinda yalipingana nakanuni ambazo ofisi yake imezitoa kuhusiana na dhamana ya wagombea. Kanunizitaka mgombea awe amedhaminiwa na chama cha siasa. Hata hivyo, katikamaelekezo Ofisi ya Waziri Mkuu imekwenda mbali zaidi kwa kuongeza manenomengine ambayo hayapo kabisa kwenye kanuni ya kwamba mgombea lazima aweamedhaminiwa na ‘ngazi ya chini kabisa ya chama chake’. Maelekezo hayoyalipingana kabisa na katiba za vyama shiriki ambazo zinaeleza bayana ni ngazizipi zenye mamlaka ya kudhamini wagombea. Maelekezo hayo potofu yalitumikakuwawekea pingamizi wagombea wengi wa upinzani na kusababisha waenguliwe. Mheshimiwa Spika, Izingatiwekuwa mfumo wa utawala wa nchi yetu unaanzia katika vitongoji, vijiji na mitaaambayo ina mamlaka kadhaa ya kiutendaji na kimaamuzi. Kuruhusuuchaguzi huu kuvurugika ama kuleta viongozi wabovu, kama taifa tutakuwatumeweka msingi legelege wa utawala na demokrasia na athari zake zitaonekanakatika kukwama kwa jitihada za kimaendeleo. 3.2 TUMEHURU YA UCHAGUZI NA MABORESHO YA DAFTARI LA WAPIGA KURA. MheshimiwaSpika, Katika mwaka wa fedha 2013/2014, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni ilieleza kwa kirefu jinsi ambavyo serikali ina dhamira ovu dhidi yaDaftari la Kudumu la Wapiga Kura, na hivyo inapoka haki za kikatiba za wananchiwaliotimiza masharti ya kupiga kura ambao inakataa kuwaandikisha ili wasipigekura. Aidha Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilionyesha bayanajinsi ambavyo ilijitahidi kumuuliza Waziri Mkuu maswali bungeni juu ya sualahili, na Waziri Mkuu mara zote alionekana kutoa majibu ya jumla ambayohayakukidhi haja ya tatatizo. MheshimiwaSpika, Ikumbukwe kwamba tangu uchaguzi mkuu wa 2010, kumefanyikachaguzi ndogo takribani nne za Ubunge katika Majimbo ya Igunga - Tabora, Arumeru Mashariki - Arusha, Kalenga – Iringa, na Chalinze mkoaniPwani. Aidha, zimefanyika chaguzi za marudio za madiwani takribani 90katika kata kadhaa hapa nchini kwa sababu mbalimbali. Katika chaguzi hizi,daftari la Kudumu la Wapigakura halikufanyiwa marekebisho na hivyo kuwanyimawananchi wengi waliokuwa na sifa ya kuandikishwa na kupiga kura haki yakushiriki katika chaguzi hizo. MheshimiwaSpika, Licha ya wapiga kura waliotimiza masharti ya kupiga kurakunyimwa haki hiyo ya kikatiba kwa kutoboresha Daftari la Kudumu la WapigaKura; jambo hili pia limesababisa migogoro isiyo ya lazima baina ya vyamavilivyoshiriki katika chaguzi hizo na tume ya uchaguzi. Katika chaguzi zote hizo za marudio; wastani wawaliojitokeza kupiga kura hawakufika asilimia 30 na hivyo kusababishamanung’uniko kuwa Tume ya Uchaguzi inashirikiana na Serikali na Chama ChaMapinduzi kuzuia walio wengi kutokupiga kura kwa maslahi ya CCM. Hadi leo, siyo Tume wala Serikali imeweza kutoa sababu zamsingi za wapiga kura wengi kiasi cha wastani wa asilimia 70 kutokuwezakujitokeza na kupiga kura achilia mbali wale ambao hawajaandikishwa kabisa. MheshimiwaSpika, Kwa kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani imeshasema vya kutoshakuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura; na kwa kuwa Serikalihaionyeshi umakini, kujali na dhamira ya dhati ya kuboresha Daftari la Kudumula Wapiga kura kwa kuwa chaguzi zote za marudio zilizofanyika baada yamwaka 2010 zimefanyika bila daftarti la wapiga kura kufanyiwa maboresho, jamboambalo limewanyima wananchi wengi haki ya kupiga kura; na kwa kuwakufanya chaguzi bila kuboresha daftari la wapiga kura kunafanya chaguzi hizo kukosa sifa ya kuwa huru na za haki; hivyo basi; Kambi Rasmi yaUpinzani inaitaka Serikali kufanya mambo yafuatayo kabla yauchaguzi mkuu ujao:
  1. Kutoa Ratiba Rasmi yaMaboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Bunge hili.
  2. Kuleta marekebisho ya Sheria yaUchaguzi ili kuondoa ukomo wa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura (wa mara mbili kwa kipindi cha miaka mitano) na badala yake daftari hilo liwehuru wakati wote kuandikisha wapigakura wapya wanaotimiza masharti ya kupiga kurana kuingiza marekebisho ya taarifa za wapigakura wengine,
  3. Kutenga Bajeti Maalumu kwa ajili yaMaboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na
  4. Kupanga Ratiba yenye kutoa muda wakutosha wa Uhamasishaji wa wananchikujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
3.3 UANDIKISHAJIWA WATU KWENYE DAFTARI LA URAIA UNAOFANYWA KINYEMELA NA MABALOZI WA NYUMBA KUMIWA CCM Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni imepata taarifa kwamba mabalozi wa nyumba kumi wa CCM wanafanya zoezi la uandikishaji wawananchi kwenye kitu kinachoitwa Daftari la Uraia. Uandikishaji huu unafanyikakinyemela na unaonekana kuwa na barakaza Serikali kwa kuwa fomu za usajili zinatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mheshimiwa Spika, Taarifatulizozipata ni kwamba Daftari hilo ndio linategemewa kutumika katika uchaguziwa Serikali za Mitaa na pia litatumika katika uandikishaji wa wananchi kwenyeDatari la Kudumu la Wapiga kura. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmiya Upinzani imeshtushwa sana na usajili huu kwa kuwa haufanywi na NIDA walatume ya Taifa ya Uchaguzi ambazo ndizo Mamlaka halali kisheria kufanya usajiliama kwa lengo la Vitambulisho vya Taifa au kwa ajili ya Wapiga kura.Tumeshtushwa zaidi kwa sababu kwa taarifa tulizopata, usajili huo unafanyikakibaguzi kwa kuwaruka wananchi ambao ni wa vyama vya upinzani. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmiya Upinzani inamtaka Waziri Mkuu atoe maelezo mbele ya Bunge hili kuwa ni nanialiyeamuru usajili huo ufanyike na ni kwa malengo gani. 3.4 UANDIKISHAJIWA WAPIGA KURA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA BIOMETRIC (BIOMETRIC VOTERREGISTRATION) MheshimiwaSpika, Katika hotuba yangu nilipowasilisha bungeni makadirio yamapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2013/2014nilisema kwamba; “kuna mchakato wa maandalizi ya siri unaoendeshwa naTume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wa kuandaa utambuzi wa wapiga kura kwa kutumiamfumo wa “biometric” kwa maana ya kumtambua mpiga kura kwa alama za mwili kamaalama za vidole na au mboni ya jicho kama sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuuujao wa 2015”. Kwa mujibu wa taarifa tulizokuwa nazo wakati ule, nikwamba tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilishaanza maandalizi mengi ya msingibila kushirikisha wadau, hasa vyama vya Siasa, isipokuwa CCM. MheshimiwaSpika, Nilieleza pia kuwa teknolojia hii kwa siku za karibuniimetumika katika chaguzi nchini Ghana na Kenya. Kote huko, ilifeli, nachupuchupu iingize mataifa hayo katika vurugu kubwa za uchaguzi. Mataifa hayayalilazimika kurudia mfumo wa upigaji na kuhesabu kura kwa mkono, haliiliyosababisha hofu kubwa. MheshimiwaSpika, Niliweka bayana pia kwamba, si kwamba Kambi Rasmi yaUpinzani haiafiki matumizi ya teknolojia mpya kurahisisha na kuboresha mfumomzima wa uchaguzi katika nchi yetu, bali inatambua athari kubwa zinazowezakutokea siku za usoni kama suala lililo “sensitive” namna hiihalitafanywa katika misingi ya uwazi na ushirikishwaji wadau muhimu kama vyamavya siasa katika hatua zote la tangu awali kabisa. MheshimiwaSpika, Kutokana na sababu hizo, tuliitaka Serikali kutoa maelezoya kina kuwa ni sheria gani iliyotungwa na bunge inayoruhusu uboreshaji wadaftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo huu wa “biometric” na pia ni bajetiipi inatumika kutekeleza mpango huo. Aidha, tulihoji ni kwa ninimpango huo unafanyika kwa siri bila wadau wa siasa nchini kushirikishwa nakutoa baraka zao juu ya mpango huo. MheshimiwaSpika, Pamoja na tahadhari zote tulizotoa hususan ushirikishwajiwa wadau katika kwanza kuifahamu hiyo “Biometric Voter Registration – BVR” nakuiridhia, Tume bado imeendelea kutenga wadau hususan Vyama vya Upinzani nakuendelea kushirikiana na Serikali ya CCM katika kuielewa BVR, kutengenezamifumo yake ikiwemo zabuni za ununuzi wa vifaa na mifumo yake ya uendeshaji. MheshimiwaSpika, Kumekuwepo na ucheleweshaji mkubwa wa utekelezaji wa mfumohuu. Miongoni mwa sababu kuu ni kunyukana kwa makundi ndani ya Serikali, Tumeya Uchaguzi na wazabuni katika kugombea fursa za kuuza mifumo hii mipya ya BVR. Vigogo ndani ya Serikali wamekuwa sehemu ya kucheleweshampango huu kwa zaidi ya mwaka sasa. Japo kwa mwonekano wa haraka kutoka kwaPPRA yaani Mamlaka ya Uthibiti wa manunuzi ya Umma, Taifa litaaminishwa kuwarufaa kadhaa kuhusiana na kandarasi ya BVR inatokana na ushindani miongoni mwaWazabuni, ukweli unaofichwa ni kuwa nyuma ya wazabuni hawa wako Vigogo waSerikali na Familia zao MheshimiwaSpika, Mazingira haya ni viashiria tosha vya uwepo wa uwezekanowa ufisadi mkubwa tena wa kutisha katika mfumo huu wenye malengo maovu makuu mawili:
  1. Lengo la kutengeneza mfumo wenyeusiri mkubwa utakaowezesha uchakachuaji wa kitaalam wakati wa uchaguzi
  2. Lengo la baadhi ya vigogo kutengenezamabilioni ya fedha kupitia mradi huu
Mheshimiwaspika, Kwa kuzingatia unyeti wa zoezi hili kwamba linawezakuiingiza nchi katika machafuko makubwa, Kambi rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali iweke wazi mchakato mzima wa wazabuni na gharama halisi za mfumo huusambamba na Makampuni yote yaliyohusika na ambayo bado yana wahusika katika zabuni hii ikiwemo sifa ya kila mzabuni. Kama serikali itashindwa kuweka wazi swala hili, basiKambi rasmi ya Upinzani itatangaza mgogoro na zoezi zima hadi hapo uwazi(transparency) na ushirikishwaji utakopokuwa dhahiri. 3.5 UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI WA KISIASA NA KIUTENDAJI MheshimiwaSpika, Utawala bora ni pamoja na kutenda mambo kwa haki na kwakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa kwa ajili ya utekelezaji mzuri washughuli kiutawala. Aidha, kudumisha demokrasia kunachagiza sifa za utawalabora. MheshimiwaSpika, Kwa muda unaozidi mwaka mmoja sasa, kumekuwa na zuiola vyama vya upinzani kufanya shughuli zake katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwakisingizio cha vurugu za zilizotokea mwaka jana wakati wananchi wakikataa bombala gesi kujengwa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. MheshimwaSpika, Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania Rais ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza hali ya hatari katika nchi aukatika sehemu ya nchi. Kwa kuzingatia hali iliyopo Mtwara na Lindi kwa sasa niwazi kuwa inaonekana kuna hali ya hatari ambayo imetangazwa kimya kimya kwavyama kuzuiwa kufanya shughuli za kisiasa huku kukiwa na ushahidi kuwa Chamatawala - CCM wanaendelea kufanya mikutano yao katika maeneo hayo kama kawaida. MheshimiwaSpika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kwaamba huu niubaguzi wa wazi kabisa baina ya CCM na vyama vingine vya upinzani na niukiukwaji mkubwa wa misingi ya utawala bora katika nchi. Hivyo, inamtakaWaziri Mkuu kutoa kauli hapa Bungeni kuwa ni nani aliyetangaza hali hiyo yahatari katika mikoa ya Lindi na Mtwara kiasi cha kuzuia shughuli za siasakatika mikoa hiyo na ni sheria ipi imetumika kukandamiza haki ya demokrasia kwakipindi kirefu hivyo cha muda wakati vurugu zilizotokea Mtwara na Lindi zilishakwisha. MheshimiwaSpika, Ni vyema ikaeleweka kuwa hitaji la kumtaka kiongozi wakisiasa kuchukua hatua za uwajibikaji wa kisiasa, pale jambo linalosababishwana uzembe wa ama yeye binafsi, watumishi walio chini ya mamlaka yake na hatamfumo anaousimamia, siyo jambo la chuki binafsi; bali ni kielelezo cha uongoziunaojali na kujutia, madhila yaliyosababishwa. MheshimiwaSpika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikipiga keleleikiwataka mawaziri na watendaji wengine waandamizi wa Serikali hii kuwajibikakwa kujiuzulu kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa kusimamia vyema kazi zaSerikali lakini kumekua na uzito mkubwa kuukubali utamaduni huu wa uongozi jamboambalo limesababisha maovu kuendelea kufanyika na hivyo kuathiri ustawi waTaifa. 3.6 OFISI YAMSAJILI WA VYAMA VYA SIASA MheshimiwaSpika, Kwa nyakati mbalimbali kuanzia wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2005 tumekuwatukieleza kwamba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Mamlaka zinginezinazohusika za Serikali zimeshindwa kushughulikia matumizi ya fedha haramukwenye siasa na fedha za umma zinazochotwa kifisadi kwa ajili ya kufadhilikampeni za CCM. MheshimiwaSpika, Ufisadi huo ulihusisha makampuni mbalimbali ambayo yalitumika kupitishiafedha zilizokwenda kwa baadhi ya wagombea na viongozi wa CCM. Aidha, Ufisadihuo ulifikia kilele chake pale ilipoelezwa hadharani namna ambavyo Fedha hizozilifadhili pia Kampeni za chama chenyewe cha CCM na mgombea wake wa UraisMheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Kama sehemu ya kudhibiti hali hiyo tukataka vile vile Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali (CAG) aanze kukagua hesabu za vyama vya siasa. Hatimaye pamoja nasheria kumpa CAG uwezo wa kukagua hesabu za vyama vya siasa jukumu hilohalikutekelezwa kwa muda mrefu kwa sababu ambazo zilitokana na serikalikushindwa kutimiza wajibu wake kwa makusudi au kutokuona umuhimu wake. Mheshimiwa Spika; kila wakativyama vilivyotaka kukaguliwa CAG alivijulisha hakuwa na rasilimali za kuwezakutekeleza jukumu hilo.

Ni kwabahati mbaya hata Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na mashirika ya ummailipofuatilia utekelezaji wa jukumu hilo ilishindwa kubainisha wazi kuwakikwazo kilikuwa ni serikali na si vyama vya siasa. Tunashukurukwamba hatimaye sasa CAG amekagua hesabu za vyama vya siasa na tunatumainikwamba amefanya hivyo kwa vyama vyote. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmiya Upinzani inataka hakikisho kutoka kwa Waziri Mkuu kwamba zoezi hilo litakuwaendelevu na hakutatokea tena taarifa kutoka kwa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza Serikali (CAG) kwamba ameshindwa kukagua mahesabu ya vyama vyote vya siasakwa madai ya kukosa fedha au ufinyu wa bajeti. Aidha,ukaguzi huu ni lazima uweke mkazo katika kufuatilia matumizi yote sio ya ruzukupekee kwa kuzingatia kiwango cha matumizi makubwa ya fedha yanayofanywa hususanna CCM katika uendeshaji wa chama na katika kampeni za chaguzi ziada ya ruzukuambayo chama hicho na vingine vinapokea. Historia yamapato yasiyojulikana vyanzo vyake wakati wa uchaguzi haipaswi kujirudiatunapoelekea kampeni za nchi nzima za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Kura yaMaoni ya Mabadiliko ya Katiba na Uchaguzi Mkuu wa Udiwani, Ubunge na Urais wamwaka 2015. Mheshimiwa Spika, Msajili waVyama vya siasa ana wajibu pia wa kudumisha mahusiano na vyama alivyovisajili.Tunatambua kwamba Baraza la Vyama vya siasa ni kati ya vyombo vyenye kuwezeshakukutana na kujadiliana. Hata hivyo, vipo vyombo vingine vyenye wajibu wakuvikutanisha vyama vya siasa kuwezesha majadiliano yenye kuleta muafaka katikamasuala mbalimbali. Kati yavyombo hivyo ni pamoja na Taasisi ya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)kilichoanzishwa na Vyama vyenye wabunge na kinachoshirikisha vile vile vyamavisivyo na wabunge kwa lengo la kuvikutanisha bila kujadili tofauti za kisiasakatika masuala yenye maslahi mapana kwa Taifa. Mheshimiwa Spika, Taasisi kamaTCD zipo pia katika baadhi ya Nchi nyingine na kwa kutambua wajibu wa Taasisihizo Serikali zao huzipatia ruzuku toka fedha za umma kuziwezesha kutekelezawajibu unaochangia katika kukuza demokrasia na mustakabali mwema wa kisiasakatika nchi hizo. Mheshimiwa Spika, Kwakuthamini nafasi ya TCD katika muktadha huo Rais aliagiza kwamba Taasisi hiyoiweze kupatiwa ruzuku kutoka kwa Serikali. Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikasaini Hati yaMaelewano (MOU) na TCD hata hivyo utekelezaji wa makubaliano hayo umekuwa ni wakusuasua. Jambo hili Waziri Mkuu unalifahamu kwa undani, hivyo wakati umefikasasa wa kutoa kauli Bungeni sababu za utekelezaji huo kukwama. Mheshimiwa Spika, Aidha, nivizuri Vyama na wadau wa demokrasia wakaelezwa wazi kupitia majumuisho yaMapito ya Utekelezaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu kiasi cha ruzuku kilichotolewakwa mwaka wa fedha 2013/2014 nje ya mchango wa matukio. Pia, kiwangocha ruzuku kinachokusudiwa kutolewa kwa mwaka wa fedha 2014/2015 badala yakusubiri tu mahitaji ya kuvikutanisha vyama yanapotokea masuala yanayohitajimaridhiano ndio umuhimu wa TCD unapoonekana. Kwa upandemwingine Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nayo inapaswa kuongezewa wataalamuna fedha iweze kuwa Kituo-Rasilimali kwa Vyama Vya Siasa (Political PartiesResource Centre) ili ilishiriki kikamilifu katika kuvijengea uwezo vyama nakuchangia katika maendeleo ya kisiasa yenye mchango katika uchumi wa nchi naustawi wa wananchi. 4. GHARAMA ZA UENDESHAJI WA SERIKALI MheshimiwaSpika, Nitazungumzia gharama za uendeshaji wa Serikali katikamuktadha wa Rasimu ya Katiba inayotokana na maoni ya wananchi ambayoinapendekeza mfumo wa Serikali Tatu. Katika mjadala wa sura ya 1 na 6 ya Rasimu ya Katiba hojakubwa iliyokuwa ikitumiwa na CCM na mawakala wao kupinga maoni ya wananchi yamfumo wa Serikali tatu na kupenyeza ajenda yao ya Serikali Mbili ilikuwa nikwamba mfumo wa Serikali tatu utaongeza gharama za uedeshaji wa Serikali na kwamaana hiyo utaongeza mzigo kwa wananchi ambao ni walipa kodi. MheshimiwaSpika, Licha ya Tume ya mabadiliko ya Katiba kufanya utafiti wakina na kupendekeza Serikali ndogo ya Shirikisho na taasisi chache za Muunganoambazo gharama zake ni ndogo kuliko mfumo wa Serikali mbili tulio nao sasa,bado CCM na mawakala wao wameendelea kueneza propaganda miongoni mwa wananchikuwa Serikali tatu zitakuwa mzigo mkubwa kwa wananchi jambo ambalo si kwelihata kidogo. MheshimiwaSpika, Jambo la kushangaza sana Serikali hii hii inayopingaSerikali Tatu kwa kisingizio cha gharama kubwa ndio inayoendelea kugawa mikoana wilaya za nchi yetu kila kukicha na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji waSerikali mara dufu kuliko ambavyo ingekuwa kwa uendeshaji wa Seriakali yaShirikisho la Serikali Tatu zinazopendekezwa kwenye Rasimu ya Katiba. MheshimiwaSpika, Kama Serikali ingekuwa inajali gharama basi ingekuwainafanyia kazi mapendekezo ya Kambi ya Upinzani tangu mwaka 2010 ambapotuliishauri kupunguza matumizi ya kawaida na kuongeza fedha katika miradi yaMaendeleo. Aidha, Serikali ingeacha kuendelea kugawa mikoa na Wilayakwani kwa kufanya hivyo ni kuongeza gharama za uendeshaji wa Serikali. Ni jambola ajaba kabisa kwamba kwa jinsi Serikali hii isivyojali gharama za uendeshajiwa Serikali, hata Kata ya Mbagala sasa inapendekezwa kuwa Wilaya Mpya!!! Ofisi ya Waziri Mkuu imeshindwa kumshauri Rais juu yaugawaji wa Mikoa na Wilaya, matokeo yake kila kukicha tunajenga Makao Makuu yaWilaya na Mikoa wakati fedha hizo tungeweza kuzielekeza kwenye miradi yaMaendeleo na huduma za jamii kama vile shule, hospital ink. MheshimiwaSpika, Ili kudhihirisha kwamba Serikali haina uchungu na gharamaza uendeshaji wa Serikali na kwamba inatumia kivuli cha gharama ili kupingamaoni ya wananchi ya Serikali Tatu katika Rasimu ya Katiba. Katika bajeti ya shilingi trilioni 19.6 kwa mwaka huu wafedha 2014/2015, shilingi trilioni 14.2 sawa na asilimia 72.4 ni matumizi yakawaida (ya uendeshaji wa Serikali) wakati shilingi trilioni 5.4 sawa naasilimia 27.5 tu ndio bajeti ya Maendeleo. Fedha za maendeleo zilizotengwahazifikii asilimia 35 ya bajeti yote kama ambavyo Mpango wa Maendeleo wa Miakamitano unavyoelekeza. 5. MATUMIZI MABAYA YA VYOMBO VYA HABARI VYA UMMA MheshimiwaSpika, Vyombo vya Habari vya Umma ni mali ya wananchi wote bilakujali itakadi zao za kisiasa wala imani zao za kidini. Vyombo hivi vinatumiakodi ya wanachi na hivyo vinawajibika kutoa habari kwa wananchi wote bilaubaguzi wowote. MheshimiwaSpika, Licha ya wajibu wa kutoa habari kwa usawa na bilaupendeleo kuwa ni wajibu wa kikatiba, vyombo vya habari vya ummakwa mfano Kituo cha Televisioni cha Taifa (TBC1), Redio ya Taifa (TBCTaifa), na hata Magazeti ya Serikali husan Daily News na Habari Leo, vimekuwavikitumika kutetea misimamo na mitazamo ya upande mmoja wa Chama cha CCM, nakuvinyima fursa vyama vyenye mitazamo tofauti. Hii ni kwa sababu Serikali na hata baadhi ya viongozi waCCM wamekuwa wanaingilia masuala ya uhariri wa vyombo hivyo, kiasi chawasimamizi wa vyombo kudhani wanaendesha vyombo vya CCM. Haya ni matumizi mabayaya kodi za wananchi zinazoendesha vyombo hivyo, na ni dhuluma kwa wananchiwanaopaswa kuhudumiwa na vyombo hivyo kwa usawa bila kujali tofauti zakiitikadi, za kijamii au za kidini. MheshimiwaSpika, Vyombo vya habari vya Umma vimekuwa na tabia ya kutoahabari chanya kwa upande wa Serikali na CCM lakini vimekuwa vikitoa habari hasikwa upande wa Upinzani na mara nyingine kutotangaza kabisa habari chanyazinazotokana na kazi nzuri ya Upinzani. Jambo hili liliwahi kulalamikiwa naKambi Rasmi ya Upinzani lakini bado ubaguzi katika kutoa habari unaendelea. MheshimiwaSpika, Mfano hai wa ubaguzi unaofanya na vyombo vya habari vyaumma ni pale ambapo Kituo cha Television cha Taifa (TBC1) na Redio ya Taifa,TBC –Taifa vilipokatikasha matangazo yake ya moja kwa moja ya Bunge Maalumla Katiba wakati Mjumbe wa Bunge Maalum anayetokana na chama cha UpinzaniMheshimiwa Tundu Lissu alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maoni ya Wachache. MheshimiwaSpika, Sababu iliyotolewa kwamba kulikuwa na matatizo ya kiufundihaina mashiko kwa kuwa kituo cha Television cha Taifa kiliendelea kurushamatangazo mengine jambo linalothibitisha kwamba kulikuwa hakuna tatizo lakiufundi. MheshimiwaSpika, Kambi Rasmi ya Upinzani ilipata taarifa kwamba watendajiwa TBC1 na TBC Taifa walipata maelekezo kutoka kwa Waziri wa Habari, VijanaMichezo na Utamaduni kwamba wakatishe matangazo ya moja kwa moja ya BungeMaalum wakati Mheshimiwa Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya wachache. Tunaitaka Serikali ilieleze Bunge hili ni kwa niniinaelekeza vyombo vya habari vya umma kufanya kazi kwa ubaguzi ilhali vyombohivyo vinatumia fedha za walipa kodi wa nchi hii. 6. UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI 6.1UWEKEZAJI MheshimiwaSpika, Kwa mujibu wa Ripoti ya Ufanyaji Biashara yaBenki ya Dunia ya mwaka 2014 inaonesha kuwa Tanzania imeporomoka kutoka nafasi ya 136 mwaka 2013 hadinafasi ya 145 kati ya nchi 185 zenye mazingira bora ya kibiasharaa[1]. Mheshimiwa Spika, Ripoti hiyo,imetaja nchi nane bora Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazofanya vizuri kuwa nipamoja na Mauritius ya 20, Rwanda ya 32, Afrika Kusini ya 41, Botswana ya 56,Ghana ya 67, Zambia ya 83, Morocco ya 87 na Namibia ya 98. Mheshimiwa Spika, Kwa taifa lenyerasimali na utajiri wa kutosha kama la kwetu ni jambo la fedheha na la kushtuakwa kuwa bado tumejikuta tukishika mkiakatika masuala ya kibiashara hata katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki hukumara nyingi tukijisifu kwa takwimu zisizo za kweli au za kutoka kwenye vyanzovisivyo na sifa na vingine vya kutengeneza kwa malengo hayo. Na hii ni kwasababu tumeshuka kwa nafasi 9 hali ambayo siyo nzuri kwa uchumi wa nchi. Hayani matokeo ya kushindwa kwa Sera na mifumo mibovu ya uwekezaji ya Serikali ya CCM ambayo kwamuda wa miongo mitano sasa inashikilia dola. Mheshimiwa Spika, Kama hiyohaitoshi ripoti hii inaeleza maeneo yenye changamoto ambayo yanachochea nakuchangia kushuka kwa ufanyaji wa biashara ni pamoja na upatikanaji wa mikopo,rushwa, mfumo wa utoaji na upatikanaji vibali, mazingira ya biashara mipakani,ulipaji kodi na usajili wa ardhi na mali. Mheshimiwa Spika,Pamoja na kuwaKituo cha Uwekezaji (TIC)kimeanzishwamwaka 1997 ambapo ni takribani miaka 17 iliyopita na kinatakiwa kuwa sehemu moja ya kurahisisha masuala yaufanyaji biashara nchini bado changamoto ya urasimu katika ufanyaji biasharaunatajwa kama kikwazo nchini[2]. Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi yaUpinzani bungeni inaitaka serikali kuhakikisha kuwa huduma katika kituohicho zinaboreshwa na pia rushwainatokomezwa katika masuala ya kupata vibali na hati mbalimbali za biashara ilikujenga mazingira mazuri ya uwekezaji yenye tija kwa taifa kuliko sasa ambapobado wawekezaji wengine wanashindwa hata kulipa kodi ya ardhi waliomilikishwaili kuwekeza nchini[3]. 6.2 UWEZESHAJI WAWANANCHI (EMPOWERMENT) Mheshimiwa Spika, Ni dhahiri kuwauwekezaji wa miradi mbalimbali hapa nchini umeweza kufungua milango ya fursa zaajira kwa wananchi. Ni malalamiko ya muda mrefu juu ya miradi ya uwekezajinchini, kutotoa kipaumbele kwa nafasi za ajira hasa kwa wazawa. Malalamiko hayosi tu kuwa yamejenga uhasama kati ya wazawa na wageni, lakini pia yamechangiakwa kiasi kikubwa kukwama kwa programu mbalimbali za serikali ambazo zinalengakujenga uwezeshaji wa kiuchumi wa wananchi wa maeneo husika. Mheshimiwa Spika, Taarifa ya uwekezaji iliyotolewa na Kituo chaUwekezaji Tanzania (TIC) inaonyesha kuwa kulikuwa na ongezeko la ajira kwenye makampuni ya uwekezaji mwaka 2009kufikia 83,879 kutoka 83,473 mwaka 2008. Hata hivyo idadi kubwa ya ajirailikuwa kwa Watanzania ambao sio wataalamu[4]. Mheshimiwa Spika, Pia idadi yawafanyakazi ambao sio Watanzania iliongezeka kutoka 752 mwaka 2008 mpaka 815jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 ambayo inaruhusuwawekezaji kuleta wataalam nchini pale ambapo teknolojia inayotumika hainawataalam kama hao nchini. Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzaniinaitaka serikali kutoa kauli na maelekezo mahsusi kuhusu uwepo wa idadi kubwaya wafanyakazi ambao si wataalam nchini jambo ambalo linawanyima fursa vijanawengi wanaohitimu katika taasisi zetu za elimu. Mheshimiwa Spika,Suala lauwezeshaji wananchi kiuchumi pia halimaanishi kuwa Serikali itoe fungu la fedha kwa ajili ya shughuli za uwekezaji. Badalayake, ina wajibu wa kutoa fursa – hata za upendeleo ikibidi - ; kwakulinganisha na washindani wageni. Ni dhahiri wakipata haki ya miliki,wawekezaji Watanzania wana uwezo wa kutosha wa kuvuta mitaji kutoka makampunimakubwa na hata mashirika na taasisi za fedha za kimataifa. Aidha, ielewekevilevile kuwa hata wawekezaji wengi wageni wanaoaminika na serikali hii,hutafuta mitaji toka taasisi za fedha zakwao na Kimataifa baada ya kupewa vibali vya kuvuna rasilimali zetu kwa bei yakutupa na Serikali ya CCM. Mheshimiwa Spika,Inashangazakusikia kauli za viongozi waandamizi waSerikali zinazovunja moyo wawekezaji hao badala ya Serikali kuwa chombo chauwezeshaji wa wazawa katika uwekezaji. Mheshimiwa Spika, Wawekezajiwazawa ambao walionesha nia au wameendelea kuonesha nia ya kuwekeza katikamiradi mbalimbali, wameendelea kukashifiwa, kudharauliwa na kudhalilishwa nakauli tata za viongozi kuwa hawana uwezo. Kwa mfano,kauli ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kuwa Watanzaniahawawezi na hawana uwezo wa kuwekeza kwenye gesi na mafuta, hivyo wawekezekweye viwanda vya matunda, juisi, nyanya, nk ni kauli ambayo ilistahili kukemewa kwa nguvu zote na Serikali na yeyekuwajibishwa moja kwa moja aidha kwa kujiuzulu au kufukuzwa kazi. Lakini chakushangaza, Viongozi Wakuu wa Serikali walikaa kimya na wengine hatakushangilia. Huu ni ushuhuda wa wazi kuwa kauli kuwa “Sekta Binafsi” ni “engine”ya kukua kwa uchumi kwao inamaanisha sekta binafsi ya kigeni. Kambi rasmi yaUpinzani Bungeni inawashangaa zaidi wafanyabiashara hawa wanaotukanwa hadharanikuwa ndiyo wafadhili wakubwa wa CCM hiyo hiyo inayowabeza. Mheshimiwa Spika, Kauli hizi za viongozi waandamizi wa Serikaliza kuudhi hazitakiwi kufumbiwa macho kwa kuwa wapo katikautumishi wa umma kwa maslahi ya Watanzania. Ni dhahiri kuwa, wawekezaji wazawawana wajibu wa kuona kuwa Watanzania hawaachwi nyuma na badala yake wanashirikipia moja kwa moja katika sekta mbalimbali za uwekezaji. MheshimiwaSpika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inawasihi Watanzaniawote wenye nia na dhamira ya dhati ya kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini,kutokata tamaa kuhusiana na uwezo wa Watanzania kushiriki moja kwa moja katika kuendelezarasilimali hizi. Na wala isifike mahala Watanzania wakaaminishwa amakudanganywa kuwa ni dhambi kuwapendelea wazawa katika uwekezaji wa gesi asiliana mafuta, bali uamuzi kama huo uchukuliwe kuwa ndiyo njia mojawapo nzuri yakushirikisha wazawa moja kwa moja katika kunufaika na rasilimali zao hizo. 6.3UNUNUZI WA SAMANI ZILIZOTENGENEZWA NCHINI MheshimiwaSpika, Kwa mudamrefu sasa kumekuwa na msisitizo kuhusu ofisina taasisi za serikali kununua samani zinazotengenezwa nchini. Ni dhahiri kuwa nchi zilizoendelea hazikufanikiwa kupiga hatua bilakushirikiana na wafanyabiashara wa ndani hivyo samani za ndani zikinunuliwa kwawingi pato la taifa litaongezeka kwani lita – stimulate sekta nyingine zauchumi ikiwemo ajira. Serikali lazima sasa ieleze ni wizara, taasisi na ofisi zake ngapi zimeanzakutekeleza tamko la Serikali la kuanza kutumia samani zilizozalishwa na viwandavya ndani ya nchi? 7.0 MAPENDEKEZOYETU YA NYUMA NA AHADI ZA SERIKALI 7.1RERA (Real Estate Regulatory Authority) MheshimiwaSpika, Katika hotuba ya Kambi ya Upinzani kwa mwaka wa fedha2011/2012 tuliitaka serikali kuanzisha chombo kitakachoweka uratibu nausimamizi wa sekta ya majengo makubwa ya biashara ambayo inayokuwa kwa kasikubwa. Mamlaka hii siyo tu itasimamia haki za wapangaji, balihata mapato ya Serikali na ubora wa majengo haya na huduma zake. Tulipendekezamamlaka hii ya udhibiti iitwe ”Real Estate Regulatory Authority.” Tunarudia tenakusisitiza ushauri wetu huu kwani Serikali inapoteza mapato bila sababu yamsingi kwa jeuri na kiburi cha kutokubali ushauri uliotoka upinzani. 7.2 Uundwaji wa Tume Huru za Kimahakama MheshimiwaSpika, Kumbukumbu za taarifa rasmi za Bunge zinaonyesha kwambakatika hotuba ya KUB mwaka 2011/2012 tuliishauri Serikali kuhusu kuunda tume ya kijaji ya uchunguzi wa vifo vya raia. Mheshimiwa Waziri Mkuupamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali walikubali na wakaahidi kutekeleza hilo,lakini toka mwaka huo hadi sasa hakuna chochote kilichotekelezwa na Serikali. MheshimiwaSpika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kwamba Serikali hainadhamira yeyote ya kulitafutia ufumbuzi wa kudumu suala hili ambalo wananchiwamekuwa wakililalamikia kuhusu jamaa zao kuuawa na vyombo vya dola. Ni ukweliuliowazi kwamba tangu kipindi hicho vimeripotiwa vifo kadhaa, majina ya watuwaliouawa yanapatikana katika taarifa ya haki za binadamu ya mwaka 2013, uk.22. MheshimiwaSpika, Maadam ahadi ni deni na wananchi wanaendelea kuuwawa,tunaomba kwa mara nyingine tena kauli ya Waziri Mkuu kuhusiana na kadhia hii. 8.0 MAPITIO YA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUUKWA MWAKA WA FEDHA 2013/14 Mheshimiwa Spika, Naomba sasakuangalia fedha za maendeleo kwa baadhi ya mafungu kwenye ofisi ya Waziri Mkuu.Kwa mujibu wa Randama, inaonyesha kuwa kwa mwaka wa fedha 2013/14 Ofisi yaWaziri Mkuu, Fungu 37, Tume ya Taifa ya Uchaguzi; Fungu 61 na Mfuko wa Bunge,Fungu 42 kwa pamoja zilitengewa jumla yaTshs. 54,729,392,000/- kwa fedha za maendeleo. Hadi Machi 2014 kiasi ambachotayari kilikwishatolewa ni Tshs. 17,263,036,286/- sawa na asilimia 28.4 yabajeti. Mheshimiwa Spika, Kwa bahatimbaya ni kwamba kwa upande wa Tume ya Uchaguzi hakuna fedha yoyote ya maendeleoiliyotolewa hadi kufikia hiyo Machi 2014. Kwa mwakahuu wa fedha 2014/15 kwa mafungu hayo hayo inaonekana zimetengewa jumla yashilingi 29,953,134,000/- zikiwa ni fedha za ndani na fedha za nje. Mheshimiwa Spika, Mwonekano wamatumizi ni dhahiri kwamba uwezo wa Serikali kutoa fedha za maendeleo si mkubwana jambo hili limepelekea uwepo wa bajeti kubwa lakini utekelezaji wake nimdogo sana. Mfano unaonekana kwenye Wizara hii inayoongozwa na Kiongozi waShughuli za Serikali. Je, hili ni kuwadanganya Watanzania au Serikaliinajidhalilisha yenyewe au kuna fedha zingine zinazotumika bila kupitia kwenyemfumo wa kuidhinishwa na Bunge?Mheshimiwa Spika, Kamati yaBunge iliishauri Serikali katika vikao vyake iwezeshe Tume ya Uchaguzi iliiweze kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Katika maelezo ya Utekelezajiwa hoja hiyo, Serikali ilieleza kwamba kwa mujibu wa sheria za Uchaguzi, Tumeya Taifa ya Uchaguzi inatakiwa kuboresha daftari mara mbili kati ya uchaguzimmoja na unaofuata. Aidha, Tumeitaandikisha watu wote watakaokuwa wametimiza umri wa kupiga kura katikauchaguzi Mkuu Oktoba, 2015. Awamu ya kwanza ya uandikishaji itafanyika mweziSeptemba hadi Desemba, 2014 na awamu ya pili itafanyika kati ya April na Agosti2015. MheshimiwaSpika,
Serikaliinasema tayari imekwishatoa kiasi cha Tshs. Bilioni 39 kwa ajili ya maandalizihayo. Fedha hizi hazikuwa katika bajeti ya Tume na hakuna maelezo yeyote ya niwapi Tume au serikali ilichota fedha hizi. Kwa msingi huu, ni dhahiri ukaguziwa matumizi kama haya utakuwa wa utata mkubwa kwa CAG na ni ushuhuda mwinginewa usiri mkubwa unaoendesha Tume ya Uchaguzi. Aidha, Serikaliimeshindwa kutoa mchanganuo wa kina wa namna fedha hizo zilivyotumika ili Watanzaniana wadau wa Demokrasia waweze kujiridhisha kwa kazi zilizofanyika na thamani yafedha hizo zilizokwishatolewa. Mheshimiwa Spika, Randamainaonyesha kuwa kwa mwaka wa fedha 2014/15 Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefanya makadirio ya Jumla ya kiasicha shilingi 761,462,903,911.00 (US$476 Million) kwa ajili ya uboreshaji waDaftari la Kudumu la Wapiga Kura, Uendeshaji wa Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuumwaka 2015. Kati yafedha hizo shilingi 296,551,542,711.00 (US$185.3 Milion) zimeombwa kwa ajili yakuboresha Daftari la kudumu la wapiga kura na kiasi cha Sh. Bilioni 144(US$90million) kwa ajili ya uendeshaji wa kura ya maoni na kiasi cha Sh.323,277,260,150.00 (US$202 Million) kwa ajili ya uchaguzi mkuu, 2015. Mheshimiwa Spika, Baada yakufanya uchambuzi wa kina, imebainika kwamba mchanganuo nuliotolewa na Serikalikatika Randama, unatofautiana na ukokotoaji halisi kwa kiasi cha shilingibillion 2.4 Tofauti hiini kubwa mno na inatia mashaka kuhusu kama kweli Serikali iko makini katikakutayarisha bajeti zake au pengine kuna mchezo mchafu uliofichika katikataarifa hii. Kumbuka kuwa kuna shs bilioni 39 tayari zimekwishatumika kwamujibu wa taarifa ya Waziri wa Nchi, Sera na Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuuambazo chanzo chake hakina maelezo yeyote. Mheshimiwa Spika,Jambo lakutia mashaka ni kwamba randama hiyo hiyo fungu 61 jedwali no. 9 pamoja najedwali no.10 fedha hizo zinazoombwa hazijaonekana katika majedwali hayo. Kambi Rasmiya Upinzani inaitaka Serikali kutoa maelezo kwani mfuko mkuu wa Serikali(consolidated fund) unaweza kuwa unatumika vibaya kutokana na ukweli kuwamatumizi yake hayakaguliwi na Mkaguzi wala kamati za hesabu za Serikali. Mheshimiwa Spika, Baada ya kusema hayo, kwa niaba ya Kambi Rasmiya Upinzani, Naomba kuwasilisha. Freeman A. MboweKUB naMsemaji Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu 06 Mei, 2014

[1]Ripoti ya Benki ya Dunia(2014). Ufanyaji Biashara. Toleo la 11

[2]Tanzania Investment Act, 1997

[3]Report on Assessment and Evaluation of Ownership of Farms above 50 Acres inTanzania Mainland, September 2013, Ministry of Lands, Housing and HumanSettlement.

[4]http://letstalklandtanzania.com/s/tag/human-settlements/http://www.tic.co.tz/media/TIR2012%20Main%20Report%20for%20Web.pdf(23/02/2014) Tanzania Investment Report Tanzania Investment Report, Foreign Private Investment and InvestorPerception 2012, issued by TIC



 
Mwanamakambako, kisaikolojia tu unaonekana bado hujaamka bado upo usingizini unafikirishwa na wanasiasa. Be yourself ndugu kisha chukua hatua
 
Naishi Mtaa wa Kibulang'oma, Kata ya Lizaboni, Wilaya na Manispaa ya Songea Mjini, Mkoa wa Ruvuma, nchi ya Tanzania

Sijapata kuona MNGONI -------- na mbumbumbu kama wewe...hakika unatuabisha wakazi wa mkoa wa Ruvuma.
 
naona anandeleza ulaghai tu, hamna chochote anachosema zaidi ya kuvumisha neno ccm. kila baada ya maneno kumi kuna neno ccm, ccm ccm.

Sijawahi kumuona mwana ccm yeyote mwenye uchungu na taifa kwa nyie mliopo sasa. Mmekutana wote wala rushwa na matapeli wakubwa hivyo hakuna ukweli utakao ongelewa wala rushwa mkaukubali.
 
Kwa shule zenu za kata kamwe hutakaa uelewe kazungumzia nini

Naona wewe wakishua mwenzangu ila ungekua na akili kidogo kama ungeelewesha nini nilichotaka kujua sasa sijui umepata nini hapa,au unataka kuandika tu uonekane,kaazi kwelikweli
 
Back
Top Bottom