Ni kweli diwani wa hapo Gairo ni wa Chadema, lakini cha ajabu aliwekwa kwa nguvu ya pesa na mbunge Shabiby, baada ya chaguo la mgombea wa CCM wa udiwani, kuwa siyo mtu 'wake' Shabiby.
Huyo mwarabu/mkaguru Shabiby ameigeuza Gairo kama himaya yake ya kisultani, kila analolitaka kwa wanaccm wenzake ni lazima liwe, wakimgomea tu, basi anajigeuza 'ukawa' ili kuwakomoa wanaccm wenziwe!
Suala hilo liko wazi kabisa, hata viongozi wa juu kabisa wa CCM, JK na Kinana, wanalijua vizuri sana hilo jambo, lakini kwa kuwa nao wanamgwaya sana huyo mwarabu, wamebaki kumkodolea macho tu, bila kumchukulia hatua zozote za kichama!