Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,209
Nimesoma kauli ya Mbowe kama ilivyonukuliwa katika gazeti la Tanzania daima, kwa kweli nimefarijika sana. Na nimejiridhisha kwamba Mbowe ni kiongozi wa ukweli. Maneno haya ya Mbowe, hayawezi kusemwa na kiongozi mwingine yeyote anayeheshimika ndani ya CCM. Wakati Mbowe akitoa kauli yenye hekima ya hali ya juu, kule upande mwingine tungeshuhudia mwenyekiti wake akiongea mipasho. "Za kuambiwa....", "Ukitaka kula ukubali kuliwa" etc. Sasa msome Mbowe hapa: Ndipo ujue kuwa uwingi wa degree za darasani si kipimo cha hekima.
"Sitamuogopa rais, lakini nitamheshimu, sitaogopa polisi lakini nitawaheshimu, sitaogopa Jeshi lakini nitaheshimu Jeshi. "Kuanzia sasa sitamheshimu mtu yeyote asiyeheshimu ubinadamu wa mtu mwingine.
Uchaguzi wa juzi wa kata, tumeshinda kwa mapambano ya damu. Watu wetu wamepigwa kila mahali, wamekatwa mapanga na mashoka na vijana wa CCM, Green Guard. "Katika hali kama hiyo siwezi kucheka na polisi, ndiyo maana juzi tumetangaza kuwapatia vijana wetu mafunzo ya ukakamavu ili tujilinde na vitendo hivi. Hatujaanzisha jeshi, tulichokisema na kukisimamia ni hiki.
"Wananchi wa Songea, huu ni mkutano wangu wa kwanza kuhutubia hadharani tangu nilipokoswa koswa kuuawa kwa bomu, risasi za SMG na risasi za bastola kwenye tukio la Soweto, Arusha siku ya kuhitimisha kampeni.
"Lakini napenda niwaambie kitu kimoja, miye kama kamanda wenu mkuu, sitaingiwa hofu. Sasa tuna usongo zaidi na wametuongeza charge (nguvu) ya kuing'oa CCM katika chaguzi zijazo, maana tunajua tunasimamia haki, ukweli na matumaini ya Watanzania wote," alisema.
Huku akiwatoa machozi baadhi ya waliohudhuria mkutano huo wa juzi, baada ya kuona kitabu kimojawapo chenye picha za watu aliouawa na kuteswa na vijana wa Green Guard ya CCM, Mbowe aliuita ushindi wa kata nne za jijini Arusha kuwa ni wa damu zilizomwagika za wanachama wake.
"Kama kuna mtu alifikiri kuwa kumuua au kutaka kumuua Mbowe atamtia hofu...huyo mtu ameshindwa. Kwa kweli siku ile mimi na wengine tuliokuwa walengwa kabisa wa lile tukio tulinusurika kwa mipango ya Mungu tu. Ni kwa sababu tunaongozwa na Mwenyezi Mungu, tutaendelea kupigania haki hadi kieleweke.
"Huko Serengeti, kwenye Kata ya Machila, watu wetu wake kwa waume wametekwa nyara, wakapelekwa na kufichwa kwenye nyumba ya CCM, wengine wamebakwa, wengine wamewekewa chupa sehemu za siri, kwa sababu tu ya CHADEMA," alisema.
Mbowe alidai kuwa amesikitishwa na upotoshaji mkubwa unaofanywa kwa makusudi na CCM na serikali kwamba chama chake kimeanzisha jeshi, kiasi cha kuvisukuma vyombo vya dola kuanza kuwakamata viongozi wa juu wa chama hicho.
"Hatuwezi wala hatuna mpango wa kuanzisha jeshi kama ambavyo polisi wanataka kupotosha kwa kusoma habari zinazoandikwa na magazeti ya CCM na kutangazwa na TBC. "Nani hajui kuwa CCM wana kikundi kinaitwa Green Guard ambacho kiko nchi nzima, kinapiga
wananchi, kinaumiza wapinzani na ushahidi tunao wa kutosha, kinapewa mafunzo ya kijeshi na ushahidi tunao.
"CHADEMA tumeshalalamika na kulia mara chungu nzima kuwa si sahihi vitendo hivi kuendelezwa, hakuna anayetusikiliza, si polisi wala si serikali. Wote wamekaa kimya. Wakati mwingine vitendo hivi vinafanywa mbele ya usimamizi au macho ya polisi, kila siku wanaoumizwa ni
CHADEMA. Sasa tukasema basi, kuendelea kulialia ni uendawazimu," alisema.
Mbowe alisema walichokiamua ni kufanya ulinzi shirikishi au ulinzi jamii kama ambavyo polisi wamekuwa wakiasa na kusihi kila siku.
"Tulichokisema wala si kitu kipya kabisa. Kimo ndani ya katiba yetu. Naomba mtu yeyote hapa anayeweza kusoma apande hapa juu asomehii katiba ya chama hapa, inazungumzia Red Brigade. Tunachofanya sasa hivi ni kuwapatia vijana ukakamavu.
Hatuanzishi jeshi, wala hatutakuwa na mabomu, wala bunduki, shoka, wala mapanga kama walivyo wenzetu, lakini kama ni mchaka mchaka au karate tutapiga. "Mtu yeyote mwenye nia mbaya na nchi yake hawezi kutangaza hadharani, na sisi kwa kuwa nia yetu ni njema na yenye lengo la kujilinda ndiyo maana tulitangaza mchana kweupe," alisema Mbowe.
Source: Tanzania daima