Mbowe ana hekima sana!

Mbowe ana hekima sana!

Yaani ukilogwa ukapitia kwa bahati mbaya kwenye mkutano wa CDM na ukafanikiwa kuwakuta kati ya hawa (Mnyika, Mbowe na Dr Slaa) wakihutubia lazima ubadilike. hawa jamaa hotuba zao hua zinaingia mpaka moyoni na kujikuta mtu unatoa machozi
 
Hekima iko wapi hapo? naona uchochezi wa uvunjifu wa amani tu.
 
Ndio maana watu huuliza je CDM wamejiwekea Backup yoyote endapo kitafutwa?

Vyama vya upinzania vilivyo muhimu karibu vyote vina ndoa na CCM sijui kwa CCJ ambayo katiba yake kidogo inafanana na katiba ya TANU na sijui kama huko nako hamna mapandikizwa
Mimi nadhani uwepo wa Back up hautasaidia, maana itakuwa ni kama kuanza upya kuwabadilisha watu kutoka CHADEMA na kwenda huko kwingine. Hapo tunaweza kupotea kabsia kwenye ramani ya siasa za Tanzania. Cha msingi hapa ni kwamba kama chama kikifutwa ambacho ndiyo chombo chetu cha kutolea dukuduku na kudaia haki zetu, basi tutazidai haki zetu nje ya chama. Hapa yatakuwa ni maandamano yasiyo na mwisho.
Itabidi tu tufanye hivyo, maana hatutakuwa na namna nyingine. Tunazitaka haki zetu za msingi kama watanzania, tunataka mabadiliko, chombo chetu cha kutusaidia kuyafikia mabadiliko kimefutwa, tunafanyeje? Tutaandamana hadi huyo Tendwa na Kikwete wake wakimbie nchi, kama si kukamatwa na kufungwa kama wenzake akina Mbaraka na Morsi.
 
Hekima iko wapi hapo? naona uchochezi wa uvunjifu wa amani tu.
Ingeshangaza sana kama ungeona hekima katika kauli hiyo ya mbowe ilihali wewe umezoea hotuba za mbayuwayu na kong'ota. Umezoea hotuba za .... za kuambiwa changanya na za kwako, .... waliopata mimba ni kiherehere chao. Nawajua wafanya biashara ya madawa ya kulevya kwa majina. Uwepo wa foleni kubwa ni dalili za nchi kukua kiuchumi.

Yaani ni aibu hata kumwambia mtu kwamba hayo yamesemwa na Rais. Lakini utakuta CCM ndiyo wanapiga makofi na vigelegele tena wakichombeza .... waambie hao!! Hivi unategemea maneno gani ya hekima kutoka kwa watu kama akina kibajaji, Serukamba, Nkamia na msululu mrefu wa wana magamba ambao ndiyo wameaminiwa na chama?

Kaa chini tafakari mtu ambaye ndiyo mnampigia chapuo kwa nafasi ya uraisi (Magufuli) ndiyo huyo anawaambiwa wasioweza kulipa nauli ya kivuko wapige mbizi! Pana hekima hapo? Na maneno kama hayo, wanaCCM ndiyo huwa mnayashangilia. Hivi utaona neno lolote la hekima katika kauli ya Mbowe, kwa mtu uliyezoea mipasho kama hiyo?

Hizi hapa kwenye video ndiyo hekima za CCM.

 
Last edited by a moderator:
Nawaomba sana viongozi wa cdm wazidi kufafanua kuhusu hili swala kwa wananchi mana ccm wanalipotosha sana. Mungu ibariki tz pamoja na Tanzania.
 
Naomba ku-declare interest, mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini nina mapenzi na cdm kwa wakati huu. Wakikengeuka nami nageuka.

Kuna watu ukiwasikiliza na/au kusoma maandiko yao unafarijika kwamba tz bado tunao watu wenye upeo na uzalendo na wanaofahamu aina ya tanzania tuitakayo. Katika orodha hiyo ya watu wachache, MBOWE yupo. Mbowe ni kiongozi, akizungumza masikio yanasikia na moyo unapokea. Watu wa aina hii ni wachache, ni mfano wa Mwalimu

Kabla ya kuanza kuongea Mh.Mbowe ukimya mkubwa hutawala....Sauti yake ya base ndogo hutoka kwa utaratibu huku ukipambwa na busara ya hali ya juu katika matamshi yake....huwa hayupo kubishana bali kueleza kile anachokiamini na ambacho chama cha demokrasia wanakusudia kufanya!
Nampa Heko sana....
 
Hekima iko wapi hapo? naona uchochezi wa uvunjifu wa amani tu.

Hekima ni nini kwako???? au heshima sio hekima??
Au ulitaka aseme LIWALO NA LIWE....ANAEUA ALBINO AUAWE.....WAPIGWE TU,TUMECHOKA.....?
 
Hakika Mhe.Mbowe ni charismatic leader na hata CCM wanamkubali lakini kwasababu za kiitikadi wanajifanya kumpinga, wao watamsema kwa uzuri akimsifia Mwenyekiti wa chama chao pekee!
 
Wananchi sio woga tena mbele wa wanaCCM kama mwigulu na pinda anavyodhani
 
Kwa hizo kauli za wanaCCM kweli chama kinahitaji halftime/mapumziko, ikiwezekana mechi ndo imeisha hivyo wakafanye mazoezi tena hivi kweli kocha wao laikufany miaka zaidi ya kumi ilopita, ndo maanaaaa vichaa wakapata rungu
 
kumbe ukiwa muuza dawa za kulevya na kuendesha kumbi za muziki na kuuza pombe unakuwa na busara,

Halafu kumbe ukipanga na kusimamia mauaji ya watu unakuwa na busara kweli tanzania daima hakuna waandishi,

Samahani je ukiwa MUUZA WANYAMA WA HIFADHI YA TAIFA NA UUZWAJI NA USAFIRISHAJI WA DAWA ZA KULEVYA NI CREDIBILITY YA KUWA TOP OFFICIAL NDANI YA CCM
 
Hekima ni nini kwako???? au heshima sio hekima??
Au ulitaka aseme LIWALO NA LIWE....ANAEUA ALBINO AUAWE.....WAPIGWE TU,TUMECHOKA.....?
Bora umwambie. Hawa wanzetu wana shida sana katika tafakari ya maneno ndiyo maana ukiangalia top leadership yao yote ni ya aina hiyo hiyo. Ni watu wa kuropoka tu. Katika safu ya uongozi ya CCM mtu anayejiheshimu ni Dr. Bilal tu. Hawa wengine wote ni mipasho kwenda mbele. Sasa watu waliozoea mipasho ya hivyo kamwe hawawezi kuona hekima katika maneno haya ya Mbowe.
 
kama isingekuwa makeneza angalau kidogo lakini makengeza.

Ili upinge maneno ya Mbowe, inabidi uuvae uendawazimu kwanza. by j4 sidhani kama kichwa chako kipo sawa sawa... Kuna gololi itakuwa imelegea tu!
 
mizengo kayanza pita pinda....
we piga tu...ninasema tutawapiga tu
ninatoa amri piga tu.
hekima ni majaliwa sio jamani.
 
Katika hali hii ambayo wengine wanaona ni uchochezi (Mafisadi) huku wengine wakiona ni ukombozi (wazalendo), Naamini taratibu taratibu taifa litaelekea katika siasa ambazo zitaacha kutumia vyombo vya dola na badala yake maamuzi ya wananchi yataheshimiwa. Hapo ndipo kilele cha maendeleo kilipo.
 
Back
Top Bottom