Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,703
Dhuluma imeota mizizi ndani ya CHADEMA. Nilitamani ninyamaze lakini kunyamaza hata pale haki ya WALEMAVU wanyonge inapoporwa ni kushiriki uporaji wa haki hiyo. Uporaji huu wa kumteua Bi Catherine Ruge kuwa mbunge wa viti maalumu kuchukua nafasi ya marehemu Elly Macha ni dharau, dhuluma na kashfa kwa walemavu wote bila kujali itikadi za vyama.
Naamini kwa dhuluma hii na kumkosea heshima Marehemu Daktari Elly Macha hata jeneza na mwili wake unazunguka huko kaburini kwa kukosa amani. Ni juzi tu CHADEMA kilijizatiti kupora haki za kinamama katika ubunge wa bunge la Afrika Mashariki watanzania tukalaani hatimaye tukazima jaribio hilo. Leo tena Mbowe huyuhuyu kwa kushibisha matamanio yake anatuletea "mlemavu" wake tata.
Hongera Bi Ruge japokuwa ulemavu wako siuoni labda mwenyekiti anaujua ulemavu wako kiundani zaidi. Je ulemavu wako ni nini ili watanzania wajue, maana ulemavu wa marehemu Elly Macha ulikuwa wa macho na tulikuwa tunauona? Hivi CHADEMA na UKAWA haina WALEMAVU wanaoonekana ukiachana na ulemavu anaouona Mbowe kwa mlemavu huyu Catherine? Bado naamini laana ya Dr Slaa na Chacha Wangwe inaiandama CHADEMA?
Je kama CHADEMA kimeweza kuwatenda WALEMAVU ubaya huu, watawatenda vipi BAWACHA na watanzania kwa ujumla? SITANYAMAZA nasikia harufu ya RUSHWA hapa.
Remy Cameroon