- Source #1
- View Source #1
Katika pitapita zangu huko mtandaoni nimekutana na hii video kuwa Mbowe amekiri kuwa CHADEMA ni chama chake binafsi, kuna uhalisia gani kwenye video hii wakuu?
- Tunachokijua
- Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambaye alikuwa ni moja kati ya waasisi wa chama hicho mwaka 1992 na mwaka 2005 alikuwa mgombea wa urais kupitia tiketi ya CHADEMA, lakini pia mwaka 2010 hadi 2020 alikuwa mbunge wa jimbo la Hai mwaka.
Mbowe alichaguliwa kuwa Mwenyekiti (rejea ukurasa wa 18) wa CHADEMA kuanzia mwaka 2004 hadi hivi sasa 2024, akipokea kijiti hicho kutoka kwa Bob Makani ikiwa ni jumla ya miaka ishirini (20) mpaka sasa akiitumikia nafasi hiyo.
Mnamo tarehe 19 Novemba 2024 Mbowe alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia juu ya mwenendo wa mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Kumekuwapo na video inayosambaa mtandaoni ikimuonesha Mbowe akisema CHADEMA si chama cha Lissu wala mnyika bali ni cha Mbowe.
Je uhalisia wa video hiyo ni upi?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa kutoka kwenye uhalisia wake kwa kukata vipande vidogovidogo kutoka kwenye video halisi na kuviunganisha jambo liloleta maana ambayo haikutolewa na Mbowe.
Tazama video halisi kupitia kiungo hiki kuanzia dakika ya 59:15:00 mpaka 1:00:00
View: https://www.youtube.com/live/9kQEVPB0RAk?si=VjntRm2QFsRm8e7P
Sehemu inayotaja hiki ‘chama si cha Lissu wala mnyika ni cha mbowe’ sehemu ya neno ‘Mbowe’ imekatwa (zingatia sehemu hiyo ina hali ya kuruka kwa picha na sauti) imekatwa kutoka sehemu nyingine ya video na kuunganishwa katika kipande hicho cha video hatimaye kupotosha maana halisi.
Aidha Mkurugenzi wa mawasiliano na mambo ya nje wa CHADEMA John Mrema kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X amethibitisha kuwa video hiyo imepotoshwa huku akiambatanisha video halisi inayotokana na Mkutano wa Mbowe na waandishi wa habari.