SI KWELI Mbegu za mwanaume zinamnenepesha mwanamke sehemu zake za mwili

SI KWELI Mbegu za mwanaume zinamnenepesha mwanamke sehemu zake za mwili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Katika pitapita zangu za mtandaoni nimekutana na madai yakisema kuwa mbegu za mwanaume zinamnenepesha mwanamke sehemu zake za mwili je ni kweli?

1785760168776.png
 
Tunachokijua
Kumekuwa na dhana kwamba kumbe za mwanaume zinapomwagwa ndani ya mwili wa mwanamke zinaweza kuchangia kuongeza sehemu za mwili wake ikiwemo mapaja (Hips), makalio pamoja na matiti.

JamiiCheck imefuatilia vyanzo mbalimbali na makala za kiafya na kubaini kuwa madai hayo hayana uthibitisho wa kisayansi na kwamba hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mbegu za mwaname na kuongezeka kwa sehemu za mwili wa mwanamke.

Makala ya Planned parenthood inaelezea kuwa ni kweli kuwa baadhi ya wasichana wanapoanza kufanya ngono kuna baadhi ya mabadiliko yanaweza kutokea na hivyo kudhani kwamba chanzo cha mabadiliko hayo ni tendo hilo.

Mwanamke anaweza kupata mabadiliko wakati wa ujauzito ikiwemo kuongezeka kwa matiti, uzito pamoja umbo na hii ni kwa sababu ya maandalizi kukipokea kiumbe kipya.

Ufafanuzi wa Daktari

JamiiCheck imewasiliana pia na Daktari ambaye amefafanua pia kuwa madai hayo hayana ukweli na ni dhana tu iliyojengeka miongoni mwa watu wengi kwa sabab wanapokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi ni kawaida miili yao kubadilika.

Dkt. Benard Kivuma kutoka Ifakara, Morogoro anaendelea kufafanua kuwa mabadiliko hayo yanaweza kusabababishwa na sababu nyingine kama mabadiliko ya mtindo wa maisha, lishe, kiwango cha mazoezi au hali ya kisaikolojia.

Kwa kuwa mabadiliko haya hutokea wakati wako kwenye mahusiano, watu wengi huamini kwamba ni mbegu ndiyo chanzo.

Lakini kuna statement huwa tunatumia inayosema: correlation is not equal to causation…. Kwa sababu vitu viwili vinatokea kwa wakati mmoja, haimaanishi kwamba kimoja ndicho kimesababisha kingine.
Back
Top Bottom