Mboni amtolea machozi mzee wa ruksa...!!

Mboni amtolea machozi mzee wa ruksa...!!

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,069
Reaction score
34,839
HOSTI wa Kipindi cha ‘The Mboni Show‘ kinachorushwa kupitia Kituo cha Runinga cha EATV, Mboni Masimba Jumapili iliyopita aliangua kilio mbele ya Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi walipokuwa kwenye hafla ya kufuturisha kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


Mtangazaji huyo alimwaga machozi wakati akiwakaribisha wageni waalikwa pamoja na kutoa shukrani zake kwa wote waliomsaidia kufanikisha shughuli hiyo.
Baada ya kutoa shukrani alionekana kuwa mwenye furaha kwa kumtambulisha baba yake mzazi, mzee Masimba ambaye hajulikani kwa watu kama ilivyo kwa mama yake.



Aidha, mtangazaji huyo alimwita mama yake, bila ya kutarajiwa akaanza kumuomba msamaha mzazi wake huyo kwa kumsumbua na kumuahidi kwamba amejirekebisha.
“Nakuomba msamaha mama yangu, Mboni si yule tena nimebadilika, nisamehe sana,“ alisema Mboni kisha akaangua kilio kujutia makosa yake.



Baada ya tukio hilo, Mboni alisikika akiomba dua kwa Mwenyezi Mungu ili ampe mume mwema. Mtangazaji huyo alirudia mara kwa mara kipengele hicho cha kuomba mume kiasi cha baadhi ya wageni waalikwa kusema kwamba ni kweli anahitaji mume kwani umri wake unahitaji kuwa na familia.

Mbali na matukio hayo, Mboni alitambulisha vituo viwili vya watoto yatima ambavyo anavihudumia kupitia kampuni yake ya The Mboni. Mbali na Mwinyi wageni wengine walikuwa ni Shehe wa Mko wa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Asha Rose Migiro pamoja na Khadija Mwanamboka.
Wengine ni Shay-rose Bhanji na baadhi ya wanamuziki wa The Kilimanjaro ‘Wana Njenje’ Steve Nyerere na watu wengine maarufu.


MBONI AMTOLEA MACHOZI MZEE WA RUKSA...!! - GUMZO LA JIJI
 
Ameshakuwa sasa. At least that's a step forward one can bank on.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Msamaha unaombwa Nyumbani, tena unawafuata wazazi unafunga safari kabisa, sio unawaita wazazi kwenye tukio lako na media ipo halafu unajifanya kuomba msahama huo ni utovu wa adabu, na kukosa maamaadili na mwongozo sahihi wa kufanya mambo
 
Msamaha unaombwa Nyumbani, tena unawafuata wazazi unafunga safari kabisa, sio unawaita wazazi kwenye tukio lako na media ipo halafu unajifanya kuomba msahama huo ni utovu wa adabu, na kukosa maamaadili na mwongozo sahihi wa kufanya mambo

tehe teheh humu ndani nako kuna visa? watanzania wanapenda sana camera
 
Kama umebadilika kama unavyosema mama ni bora, maana habari zako hazikuwa nzuri mitaani!!
 
Kamlilia mamake au Mzee Mwinyi?????!!!!

Tuwe na weledi katika uandishi ili kujitofautisha na magazeti ya udaku.

Au ndo kutaka kuipa habari uzito kwa kutumia jina la mz Mwinyi?????
 
Back
Top Bottom