Mbona vitu vilivyoisha muda wa matumizi vinauzwa madukani??

mende 2014

JF-Expert Member
Apr 13, 2014
763
131
Nasikitika sana kuona wafanyabiashara kuuza vitu vilivyokwisha mda wa matumizi( Expire date).
Sijui wanauza bila kujua ama wanajua lakini wanauza tu kwa kuwa hawajawahi kuona kama kuna ufuatiliaji wowote?
Serikali itazame hadi mikoani kubaini tatizo hili maana wengi wataumia.
Vitu hivyo vinauzwa hadharani wala hawafichi.
 
Muuzaji ni jipu! wapo ambao wanauza kwa makusudi kabisa maana hataki kuingia hasara
wewe mnunuaji ni jipu! why usisome expire date??!
 
Mkuu.....
Kama umeshindwa kuweka taarifa na ushahidi wa hili bandiko lako, basi nawewe ni jipu. Kwasababu hakuna ulicho saidia au kuokoa kwa kuweka taarifa/ bandiko ambalo zaidi unaonekana kujiliza tu.
Hii ni sawa na kumlaumu mtu pembeni wakati amekukosea, na ukimuona unakaa kimya
 
Wewe usivinunue.

Yeye hatavinunua kwakuwa ana ufahamu tayari, lakini watanzania wenzetu ambao hawakubahatika kuwa na elimu ya kutambua hizo expiry dates wataangamia, ni vema sote tushirikiane tuchukue hatua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom