Mbona Trump anapenda sana mipasho na mabishano .....

Mbona Trump anapenda sana mipasho na mabishano .....

thesym

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
3,867
Reaction score
4,859
Huyu jamaa tayari ameshachaguliwa raisi wa US lakini mambo anayofanya ni kama vile bado yupo kipindi cha kampeni.

Mabishano na vijembe kila baada ya masaa kadhaa kupitia huko twitter utadhani sio rais wakati huo mabaraza yote mawili chama chake kimeshinda, naona anashindwa kabisa kuapply yale aliyoyaandika kwenye kitabu chake the art of deal.

Capture.PNG
 
Huyo ni habari ingine

Napenda yake kiabiashara etc kwa muda mrefu, na vipindi vyake kwa TV.

Ha ha haaaaa
 
Bora hata ya huyo anakubali kushushuliwa kwenye mipasho yake. Wa kwetu ana madongo kama Mwajuma ndala ndefu na ukithubutu kumjibu unakuwa adui wa taifa unaishia kupelekwa sehemu "salama" isiyo salama.
Ukimjibu maana yake unataka battle na ni lazima upigwe battle, au wewe unataka upambane tu na mtu yeye katulia tu kama maiti
 
Urais haubadilishi Tabia binafsi

Sie tumekuwa na Mtu Mshamba asiejua kuvaa na Urais haujamfanya ajue Kuvaa japo Ana Watu wa Mavazi

Sie tumekuwa na Rais mpenda Chuchu hatari na uwepo wa Ulinzi na ubize na hadhi zake zote haukfanya aache Tabia yake hiyo

Sie tumekuwa na Rais Mlevi kiasi cha kupelekea mpaka baadhi ya Nyakati kuahirishwa kwa ziara rasmi za Rais kutokana na Uchovu wa Mipombe ya Kirusi aliyokuwa anafakamia mpaka Majogoo

Tumekuwa na Rais aliekuwa na Tabia ya kutokuwa Panctual na Tabia hiyo hakubadilisha japo kila kitu chake kiliwekwa kwny ratiba inayowezekana

Tumekuwa na Rais Mbishi aliekuwa hataki kushauriwa na yeyote kwa chochote japo kaajiri na kulipa Mishahara Washauri wake

Ndio sababu tunashauriwa kuchagua Mtu Mwenye Sifa za kuwa Rais kwa kuwa Urais wenyewe haubadilishi Tabia ya Mtu zaid ya Taasisi yenyewe ya Urais kuathiriwa na Tabia za Mtu anaeshikilia huo Urais
 
Urais haubadilishi Tabia binafsi

Sie tumekuwa na Mtu Mshamba asiejua kuvaa na Urais haujamfanya ajue Kuvaa japo Ana Watu wa Mavazi

Sie tumekuwa na Rais mpenda Chuchu hatari na uwepo wa Ulinzi na ubize na hadhi zake zote haukfanya aache Tabia yake hiyo

Sie tumekuwa na Rais Mlevi kiasi cha kupelekea mpaka baadhi ya Nyakati kuahirishwa kwa ziara rasmi za Rais kutokana na Uchovu wa Mipombe ya Kirusi aliyokuwa anafakamia mpaka Majogoo

Tumekuwa na Rais aliekuwa na Tabia ya kutokuwa Panctual na Tabia hiyo hakubadilisha japo kila kitu chake kiliwekwa kwny ratiba inayowezekana

Tumekuwa na Rais Mbishi aliekuwa hataki kushauriwa na yeyote kwa chochote japo kaajiri na kulipa Mishahara Washauri wake
Una tokea nchi gani Buda duuu Polen sanA
 
Back
Top Bottom