tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Hawa polisi mbona kama wanamtetea Dogo janja kwanini wamsemee yeye tu na si kumskiliza na aliyejeruhiwa? Wanasema alivamiwa, alivamiwa kivipi mtu yupo kwenye gari lake? mbona wanajaribu kufukia vitu. Wanadhani hatujui chanzo cha DOgo janja kumpiga risasi huyo dogo?
Alafu siku hizi kumbe watanzania tunaruhusiwa kumiliki silaha za moto?
Soma pia:Kama serikali inafuata sheria na katiba kwanini Polisi na usalama wanateka watu
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linafanya uchunguzi wa kina kufuatia tukio la kujeruhiwa kwa risasi kijana mmoja katika eneo la Sombetini jijini Arusha usiku wa kuamkia Agosti 24, 2025.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema kuwa kijana aliyejeruhiwa ametambuliwa kwa jina la Bakari Daud (18), mkazi wa Sombetini, ambaye alipigwa risasi mguuni saa 5:30 usiku.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa Bakari, akiwa na mwenzake, alidaiwa kutaka kumvamia Abdulaziz Abubakari (30), maarufu Dogo Janja mkazi wa Levolosi, wakati akishuka kwenye gari.
“Katika hali ya kujihami, Abdulaziz alitumia silaha aliyokuwa nayo na kumjeruhi Bakari,” imeeleza sehemu ya taarifa ya Jeshi la Polisi.
Aidha, watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo, huku hatua za kisheria zikiendelea kuchukuliwa.
Kamanda wa Polisi amewataka wananchi kuepuka kujihusisha na matukio ya kihalifu na badala yake kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya usalama ili kuepusha madhara.