Mbona hili John Tendwa halizungumzii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona hili John Tendwa halizungumzii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kitalolo, Jan 20, 2012.

 1. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Baada ya fukuza fukuza ndani ya vyama vya siasa, tulishuhudia baadhi ya watu wasiohusika na migogoro hiyo wakijaribu kulizungumzia swala hilo kwa jinsi walivyoona inafaa, na baadhi yao walionyesha kutokukubaliana na halia hiyo kwa madai kuwa ikiwa fukuzafukuza ndani ya vyama itaendelee itaigharimu sana serekali kurudi kwenye uchaguzi mioni mwao alikuwa msajili wa vyama vya siasa John Tendwa.

  baada a kutathimini kwa kina kuhusu kifo cha aliyechaguliwa kuwa mbunge wa arumeru mashariki Jeremia sumari nikajikuta nikipata sali ambalo nafikiri kwa kigezo cha John tendwa Basi inabidi serekali ilitolee maamuzi ili kuizuia serekali kurudi kwenye uchaguzi na hivyo kuingia gharama zitokanazo na uchaguzi baada ya kifo cha mbunge baada ya kuchaguliwa. Hoja hapa ni nini? inasemana kuwa tangu wakati wa kampeni Mh. Sumari alikuwa kiumwa hata kushindwa kuhudhuria mikutano ya kampeni lakini ccm kwa kulijua hili iliendela na mchakato wa kampeni bila kuzingatia afya ya mgombea, na sasa kwa mujibu wa John tendw ni kwamba serekali itaingia gharama za uchaguzi kutokana na kifo cha sumari je serekali na ccm hawakuona afya ya mh. wakati wa mchakato wa kumchagua mgombea na wakati wa kampeni na hivyo ili kuinusuru serekali na kuingia gharama za uchaguzi zitakazotekea baada ya ya kifo hivyo basi kumteua mtu mwingine?

  Au waheshimi Tendwa na werema mtusaidi kupeleka hoja bungeni na itungwe sheria itakayolazimisha kuchunguza afya ya mgombea ili ikithibitiswa kuwa ni mgonjwa basi asiteuliwe kugombea nafasi ya uongozi kwa kuepeka kuja kushindwa kuwatumikia wananchi waliomchagua, na ikiwa ugonjwa ukampelekea mahuti basi, tutakuwa tumeiokoa serekali na gharama zisizotarajiwa za kurejea uchaguzi.

  Haswa ikizingatiwa kuwa tumekwishaona dalili za baadhi ya viongozi wanaotangazwa kuwa wako mstari wa mbele kuichukua ikilu 2015 afya zao hata ukiwatazama tu kwa macho wanaonyesha kuwa ni dhaifu na kuna mashaka ikiwa watafika hiyo 2014 sasa ikiwa watafika maana sisi sio miungu je tuwape dhamana ya kuingoza hii nchi? na je ikitokea kutokana na afya zao baada ya kupewa uongozi wa nchi mauti ikawakumba je serekali haitaingia gharama za kurejewa kwa uchaguzi kwa mujibu wa tendwa kwamba kufukuzana kwenye chama kutaipelekea serekali kurejea uchaguzi na hivyo kuingia gharama, kama ndivyo je ccm haioni iko haja ya kutunga sheria ya dharura kama ilivyotungwa ile ya uspika kwamba sasa ni zamu ya wanawake seria hiyo itumike kumzuia mgombea mwenye afya yenye mgogoro kugombea nafasi yoyote ili kuepuka kurudiwa kwa uchaguzi na kuiingizia serekali gharama na pesa hizo zitakazopatikana zikatumika kulipana posho watakapokuwa wanaudhuria vikao vya bunge?
  Na endapo ikatokea kiongozi kufariki baada ya uchaguzi iwe ni kwa mapenzi ya Mungu tu?

  Hii pia itakuwa faida ya ccm kwani itakuwa imetumia njia rahisi kuwaengua baadhi ya magamba vinganganizi vinavyowania kuiteka ikulu 2015 .

  Nadhani mko aware kwamba gamba moja ambalo linatanganza nia kwa nguvu kuelekea ikulu hali ya afya yake sio nzuri kihivyo hata kwa kumwangalia tu anaoneka ni dhaifu sana na aliyepoteza uwezo wa kimwili.

  Think deep
   
 2. S

  STRONG GIRL Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hapo umeronga, na isiwe kwa wagojwa tu, uwekwe mfumo ambao pia utasaidia kuondoa gharama za uchaguzi hata kama mtu kafa kwa ajali
   
 3. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  umeonaehee ila kila mahali iyo sheria isimwonee hata wa chama kimoja maana mi nashangaa eti igunga ndiko walikojifunzia gharama za uchaguzi? mbona wamefungua kesi kibao mahakani kupinga baadhi ya majimbo yaliyochukuliwa na upinzania kama Arusha? Je ikiwa mahakama itayatengua matokeo ya ubunge wa Arusha kutakuwa na gharama za kurejewa kwa uchaguzi?
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  nkubaliana na wewe ila nina hofu na kambi ya ccm.
  ni nani atakaekuwa mzima?
  ukiwapima ccm wote ni wagonjwa.hapo wapinzani watapeta kiulainiiiiiii
   
 5. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi nikijuacho ni kuwa kila mtu anaumwa au ni mgojwa mtarajiwa. hata wewe mleta hi thread. kwa hiyo sioni logic. Ila hii fukuzafukuza katika vyama kama walivyofanya chadema-arusha, nccr-kafulila na cuf wawi kwa hamadi si busara hata kidogo. This is a wastage of our resources. natamani sheria ingebadilishwa leo hii ili tuziokoe kodi zetu. kwa kweli ni ujinga.
   
 6. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hilo ndilo tatizo sugu tuko baadhi yetu tunajijua kabisa kuwa tu wagonjwa sasa kwanini tukagombee nafasi za uongozi huku tukijua kuwa tutakuja kulazimisha kurudiwa kwa uchaguzi .
  inawezekana kweli hata mimi ni mgonjwa ila sigombei nafasi yoyote niko najitahidi kuimarisha afya yangu niweze kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha

  Turudi nyuma tujiulize gharama zilizotumika kwenda kumtibu mzee st Thomas ili hali alipokuwa anaondoka mwenyewe alisema "UGONJWA HUU SITAPO NAOMBA WATANZANIA MNIOMBEE KWA MUNGU" Je hakukuwa na haja ya kumwacha hapa nyumbani ili kupunguza garama maana naamini kuna gharama zililipwa kule hosp na gharama za kuusafirisha mwili kuurejesha nyumbani, fedha hizi serekali ingeweza kuongeza safari za muheshimiwa kwenda kuombea misaada nje na kuwashawishi wawekezaji kuja kuwekeza kwenye nchi maskini. sijui na hao wawekezaji inakuwa waje kuwekeza wakati tunawaambia nchi hii ni maskini
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nadhani una maana kwamba watanzania wenye hali hizo wasipate nafasi kama kigezo cha kuokoa gharama zinazoweza kujitokeza pale watakapopote maisha. Nadhani hapo umepotea, ujue kuna haki za binadamu, kufanya hivyo utakua unawanyanyapaa na ni kinyume na katiba ya nchi
   
 8. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  katiba ya double standard? ni wapi kwenye katiba kunaposema kuwa akifukuzwa wa upinzani inakuwa gharama kwa serekali akifukuzwa wa magama hakuna gharama? chunguza kwa makini nini ninachomaanisha hapo. au kuna sehemu kwenye katiba kunaposema kuwa sasa uspika ni zamu ya mwanamke?
  Kunya anye bata akinya kuku kaharisha ehee

  kwni vyama vya upinzania havina katiba inayoweka bayana misingi na mipaka ya mwanachama bila kujali kuwa ni kiongozi wa ngazi yoyote au ni mwanachama tu?
  sasa kwanini tuziingilie katiba za vyama wakati wanatekeleza katika kidemokulaishia? Hii ndiyo hoja yangu ya msingi hizo nyingine si-hasa tu
   
 9. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Haki gani hizo unazoongelea? ukienda kusoma Russia, India etc lazima uwe tested for HIV, TB, etc ukikutwa positive kesho yake unapindishwa ndege kurudi Bongo.

  Ukiwa short listed kufanya interview kwenya balozi za UK, USA lazima kwanza uwe tested for HIV, ukiwa positive hata interview hiyo hufanyi.

  Kwanini basi mtu anye aspire high post of this country asiwe tested for chronic diseases like HIV/AIDS, cancer, diabetes, nitaacha BP kwasababu tutakosa wagombea, if the question is to serve money?!
   
 10. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  yes say it again
   
 11. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mm binafsi naona suluhisho ni hili! akifa mbunge kabla ya kipindi chake kuisha ateuliwe mwingine na chama husika bila ya kufanyika uchaguzi ili aendelee pale alipoishia yule marehemu na tuepuke gharama za chaguzi ndogo. tukisema kucheki afya ya mgombea kama mtoa mada anavyoshauri tutachemka tu! sababu hakuna ajuaye siku ya kufa, pia kuugua sio kufariki, anaweza akawa mgonjwa sana kisha akapona, vile vile mtu anaweza akawa mzima wa afya na akafariki ghafla kinyume na inavyotarajiwa! Masuala ya kifo ajuaye ni mola pekee!! mbona kikwete anatuchagulia wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na tunakaa nao hivyo hivyo kiroho ngumu!
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ww mwenyewe wakati mwajiri wako anakuajiri anajua kuwa ni mgonjwa, sasa na ww kwa nn hukuikataa hiyo ajira na umeamua kuichukua ?

   
 13. k

  kiche JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ngwendu mimi sikubaliani kufukuzana kwa visa,ila kama mtu kweli ameenda tofauti na utaratibu wa chama na jitihada zimefanyika kurekebisha zimekwama naamini ni sahihi kuchukua hatua,ni upumbavu kushindwa kuchukua hatua,naomba kukuuliza je wewe unashauri kifanyike nini wakati kila jitihada zimeshindikana????
   
 14. T

  TUMY JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nasoma hiyo makala uliyoiandika ila sikuweza kuisoma yote kwani imenichefua sana, Hivi ina maana kwamba mtu akiumwa basi ni kosa, ama ina maana mtu akiumwa ni dalili kwamba atafariki kwa hiyo asishirishwe kwenye jambo lolote, ni wangapi wameumwa wakapona wewe umeumwa mara ngapi na bado ukapona na sasa una andika makala zako za ajabu huku JF:

  Chunga sana kauli zako.
   
 15. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchaka mchaka you are right ila hoja ya Bobuk ni ya msingi. Kabla mtu hajapitishwa kugombea nafasi itabidi wapimwe afya zao and iwe lazima! In case mtu akifa baada ya kushika wadhifa then ateuliwe mbunge wa chama husika ila when disputed results are revoked by a court of law the winner of the case becomes the MP. Hii iatapunguza gharama.
   
 16. Mwamikili

  Mwamikili JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 416
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hili ni kweli kabisa ndio maana tunataka katiba mpya sio viraka itakayojumuisha haya yote, hata kwenye kampeni hakuudhulia sana ki vile, hii tanzania mbona watu wapo wengi sana na wanaafya zao! kwani lazima watu wale wale kila siku!!
   
 17. T

  Tewe JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Kila chama kina miiko na maadili yake na kila anayeomba uanachama lazima akubaliane na miiko na maadili ya chama.
  Kila anayekwenda kinyume lazima aadhibiwe kwa mujibu wa taratibu za chama husika kutochukua hatua kwa waasi ndani ya vyama kutafanya vyama visitawalike.
  Kwenye utawala wa sheria adhabu haikwepeki chamsingi watu wazingatie mipaka yao na wakuu wa vyama waache ubabe wazingatie sheria na hekima kutatua migogoro kwenye vyama vyao na ili kukwepa ghalama anapokufa mbunge aliyeshika nafasi yapili aapishwe bila kujali anatoka chama gani
   
 18. k

  kiche JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi nashangaa watu wanapotetea mtu kuvuliwa uanachama kisa eti atapoteza ubunge!!!kama hivyo ndiyo sahihi basi nadhani tunyamaze kupiga kelele kuhusu watu wanaovuja pesa za serikali na kuwataka wawajibishwe!!pale tunaongea mpaka mapuvu yanatoka mdomoni eti sheria zimevunjwa!!!vipi kuhusu kwenye chama pindi sheria zinapovunjwa!!!?kama sheria zipo ni bora zifuatwe,ni ndoto kutegemea kupata maendeleo wakati sheria zinapondwa!si kwenye siasa tu bali kila kwenye eneo la uwajibikaji.

  Kuhusu suala la afya na usalama wa wabunge wetu na ili kuepuka gharama ni bora watu wangekuwa wanakaguliwa afya wakati wa uchukuaji fomu na iwepo sehemu ya kujaza,hapa sioni tatizo,mbona tunapotakiwa kuajiriwa uwa tunapima afya kwanza kabla ya kuingia kazini,hapa tatizo lipo wapi?kitu kingine wabunge wasijiendeshe wenyewe hasa kwenye safari ndefu,mi navyojua wabunge wanapewa pesa za dereva,je kama mbunge anaamua kujiendesha hizo pesa anazipeleka wapi??kwangu mimi hapo si uadilifu hata kidogo.
   
 19. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  u are taliking nothing, kwani mtu akiumwa ni lazima afe? nani alijua kwamba sumari angekufa
   
 20. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  Sio tu tendwa hata JF wanapaswa kutazama upya akili za waanzisha thread, manake andiko lako mtoa mada inaonyesha mukichwa hutumiki vizuri. Kila mtu atakufa na sifa za kugombea ni haki za msingi za kibinadamu na hata kama unaumwa unayohaki ya kugombea labda kama akili haiko vizuri.
   
Loading...