Mbona hili John Tendwa halizungumzii

Mbona hili John Tendwa halizungumzii

Mm binafsi naona suluhisho ni hili! akifa mbunge kabla ya kipindi chake kuisha ateuliwe mwingine na chama husika bila ya kufanyika uchaguzi ili aendelee pale alipoishia yule marehemu na tuepuke gharama za chaguzi ndogo. tukisema kucheki afya ya mgombea kama mtoa mada anavyoshauri tutachemka tu! sababu hakuna ajuaye siku ya kufa, pia kuugua sio kufariki, anaweza akawa mgonjwa sana kisha akapona, vile vile mtu anaweza akawa mzima wa afya na akafariki ghafla kinyume na inavyotarajiwa! Masuala ya kifo ajuaye ni mola pekee!! mbona kikwete anatuchagulia wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na tunakaa nao hivyo hivyo kiroho ngumu!

Hii ndio suluhu ya gharama za uchaguzi anazolalamikia tendwa. Na mbunge anapofukuzwa uanachama ateuliwe mwingine toka cha husika.
 
Ww mwenyewe wakati mwajiri wako anakuajiri anajua kuwa ni mgonjwa, sasa na ww kwa nn hukuikataa hiyo ajira na umeamua kuichukua ?


mi ni mmachinga natembeza urembo na kupaka rangi kucha za dadazetu haka katekinolojia cha kichina kupitia simu ya mkononi ndicho kaniwezesha kuingia JF nikiwa juani nasubiria wateja maeneo ya kariakoo na posta
 
Hii ndio suluhu ya gharama za uchaguzi anazolalamikia tendwa. Na mbunge anapofukuzwa uanachama ateuliwe mwingine toka cha husika.

Usisahau kuwa pia Tendwa analalamika kuhusu haki ya wapiga kura je huoni hapo tutakuwa tunatoa nianya mingine ya kufukuzana ndani ya chama ikiwa mwenyekiti akiwa na mtu wake anataka kumuingiza kwenye ubunge ataamua kutengeneza majungu ili mbunge afukuzwe wapate fursa ya kumuingiza mtu wake. nafasi ya wanancgi katika kuamua mtu wa kuwaongoza na kusimamia maslai yao iko wapo ikiwa tutawaachia chama kuteua na akiteuliwa na chama atawajibika kwa chama au kwa wananchi? tunaona matatizo yanayotokea kwenye nafasi nyingi za kuteuliwa na raisi watu wanawajika kwa raisi na wanashindwa kuwajibika kwenye nafasi walizoteuliwa kwa kuogopa kuzipoteza na hivyo mara nyingi maamuzi mengi yanapindishwa na haki hatendeki na maendeleo yanachelewa au hayaji kabisa na. Na wengine wanavurunda kwa maksudi wakijua kabisa wao na marafiki wa waliowateua hivyo kwamba hawatawajibishwa
 
Nadhani una maana kwamba watanzania wenye hali hizo wasipate nafasi kama kigezo cha kuokoa gharama zinazoweza kujitokeza pale watakapopote maisha. Nadhani hapo umepotea, ujue kuna haki za binadamu, kufanya hivyo utakua unawanyanyapaa na ni kinyume na katiba ya nchi

unamwongeleaje mtu anayeshindwa hata kuhimili uzito wake mwenyewe akisimama?
 
Back
Top Bottom