Mbona Hii Line Haisomi Kwenye Simu Wakuu, Msaada.

Mbona Hii Line Haisomi Kwenye Simu Wakuu, Msaada.

NDUKI

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2013
Posts
3,440
Reaction score
2,452
Heshima kwenu wadau.

Hope mko poa kabisa, nahitaji msaada wenu ili kujua tatizo la hii line ya tigo mbona haisomi kwenye simu wakuu.

Ni line iliyokuwa ikitumika siku zote kwenye simu aina ya HTC desire 816 dual sim, sasa juzi nilikuwa MOI pale nikapata tatizo la mtandao ukawa haupatikani nikasema nizime simu kisha niwashe net haikurudi, nikasema nibadili line kwenye slots 1 and 2, nilivyorudisha line ndio ikagoma haikusoma tena mpaka sasa.

Ni line ya tigo nikasema niiweke kwenye simu nyingine inaonekana kama kawaida ila kwenye hii HTC haionekani nimejaribu kuweka slot 1 and 2 lakini wapi, nini tatizo wakuu. Line nyingine ni Airtel inaonekana bila shida. Tatizo liko wapi wakuu. Shukran sana wadau.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom