Mbio za sakafuni za Saed Kubenea kufika ukingoni mapema?

Mbio za sakafuni za Saed Kubenea kufika ukingoni mapema?

Matendo ya Saed Kubenea ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo yako mbioni kuwaingiza wananchi katika gharama ya uchaguzi mwingine wa kumtafuta Mbunge mpya wa Jimbo la Ubungo.

Wataalam wa mambo ya kisiasa wanatuambia demokrasia ni gharama hata hivyo gharama za demokrasia ambazo hazina mpango(justification) ni kama wizi wa mali ya umma. Matokeo ya matendo ya Saed Kubenea yako mbioni kuakisi wizi wa mali za umma(unjustifiable expenditure).

Ikumbukwe kuwa, Mbunge huyu wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam kwa tiketi ya CHADEMA kwa sasa ana kesi mahakamani ambayo matokeo yake yanaweza kutengua kikatiba Ubunge wake wa Jimbo la Ubungo.

Saed Kubenea anadaiwa mahakamani kama ilivyonukuliwa na Gazeti la Majira kutenda kosa Desemba 14, 2015, katika Kiwanda cha Nguo cha Took Garment Com Ltd, kilichopo Mabibo External kwa kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya, Makonda akisema ni kibaka, mpumbavu, mjinga na cheo alichonacho ni cha kupewa hali ambayo iliashiria uvunjifu wa amani na utulivu.

Katika macho ya kanuni za adhabu nchini, kosa la Kubenea linakaribisha kifungo gerezani cha kuanzia miezi sitta.

Katika sheria ya Kanuni za adhabu Sura ya Sita, kifungu cha 89(1)(a-b) kinasema;
89(1) Mtu ye yote ambaye:-
(a) atatumia maneno ya kinyaa, ya matusi au ya usafihi kwa mtu mwingine yeyote kwa namna ambayo huenda ikaleta uvunjifu wa amani; au
(b) atazozana au kwa namna nyingine yeyote ataleta fujo kwa namna ambayo huenda ikaleta uvunjifu wa amani. Mtu huyo amekosa kosa dogo na atakapoonekana na hatia atapasiwa kifungo cha miezi sita.

Katiba yetu ya mwaka 1977 kwenye kifungu cha 67(2)(c) inasema;
67(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.

Wananchi wa Ubungo kuingia kwenye Uchaguzi mwingine ambao sababu zake zingeweza kuzuilika kiutaratibu na kisheria liwe funzo kwa taifa!

Ni vizuri Mamlaka zinazowasimamia wawakilishi ambazo ni Tume ya Uchaguzi, Bunge na vyama vya siasa ziangalie utaratibu wa kuanzisha semina elekezi mapema iwezekanavyo baada ya uchaguzi ili wawakilishi wa aina ya Saed Kubenea waweze kupata darasa litakalo wawezesha kuelewa umuhimu wao katika taifa.

Wawakilishi wa aina ya Saed Kubenea lazima waelewe neno MHESHIMIWA kama kianzishi cha Jina kwa wabunge halikuwekwa kama pambio bali limewekwa kuonyesha umuhimu wa Mbunge katika jamii na taifa.

Huyu MHESHIMIWA tokea atangazwe kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, he keeps hitting the headlines for all the wrong reasons. Hawezi hata kujifunza kutoka kwa wabunge wa aina ya John Mnyika ambao wamefanikiwa katika ubunge siyo kwa sababu ya wrong reasons and character bali kwa sababu ya kuibua hoja za kitaifa na kuzisimamia kwa nguvu za hoja. Mnyika has always been exceptionally good at his job, he never puts a foot wrong.

Wananchi wanaingia gharama kubwa kumpata Mbunge lakini vile vile inatakiwa watu wa aina ya Saed Kubenea wawekewe chujio imara ili wasiweze kupenya na kuwa wabunge kwa sababu matendo yao hayaakisi/hayaendani na gharama za kumpata Mbunge kutoka kwa wananchi ambao ni walipa gharama za uchaguzi.

Waingereza wanasema, justice is blind, hii ina maana kuwa sheria hazina siasa na kwa maana hiyo, ni vizuri wananchi wa Jimbo la Ubungo wakaanza kujiandaa mapema kuingia kwenye Uchaguzi mwingine wa kupata Mbunge Mpya.
''kibaka, mpumbavu, mjinga na cheo alichonacho ni cha kupewa hali ambayo iliashiria uvunjifu wa amani na utulivu.'' haya ni maneno kutoka kwa mwehu kubinuka.
 
Hata akifungwa Ubungo ni ya upinzani CCM hawapati kitu
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi na siyo chama!

Hoja iliyoko ni wananchi wa Jimbo la Ubungo kuingia gharama nyingine ya pesa na kupiga kura kutokana na sababu ambazo zingezuilika!
 
Mkuu samahani lakini. Hivi yule mbunge aliyekula ya walipa kodi kama mil 10 hivi, karudi bungeni au? Au ile kisheria imekaaje na waliomchagua hawakubebwa milembe kweli na yale mafuso ya kipindi cha uchaguzi?
Mtake jina lake ili tuweze kumchambua!

Jamiiforums is where we dare to talk openly!
 
Hapo sasa ndio umesema nini? Kubenea tayari ni mbunge hiyo katiba au sheria sijui imesema kama aliyekuwa mbunge tayari ubunge qake unatenguliwa?
Soma vizuri hiyo thread usisome kwa ushabiki wa kisiasa na kujibu hoja ambazo hazina mshiko
 
Yaani KUBENEA ni namba nyingine,achana na yule mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,au yule Mzalendo KIBARAKA WA MWANDIGA!
Hao wote unao waona wanamponda kubenea ni uwoga tu wanajua kuwa shughuli ya kubenea pale jengoni itamnyima raha rais magufuli maana anaweza kuvunja rekodi ya rais kikwete ya kuvunja barazala mawaziri
 
Soma vizuri hiyo thread usisome kwa ushabiki wa kisiasa na kujibu hoja ambazo hazina mshiko
Kubenea ni mbunge na hayo yote ni majungu tu dhidi yake na hizo kesi atazishinda
 
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi na siyo chama!

Hoja iliyoko ni wananchi wa Jimbo la Ubungo kuingia gharama nyingine ya pesa na kupiga kura kutokana na sababu ambazo zingezuilika!
Hizo gharama n nyingi kuliko mabilioni waliyochota ya escrow?
 
Kubenea ni mbunge na hayo yote ni majungu tu dhidi yake na hizo kesi atazishinda
Hakuna ambaye amesema kubenea siyo Mbunge mwandishi ameelezea kesi inayomkabili na endapo atapatikana na hatia adhabu yake itakuwaje? Sasa hayo majungu yanatoka wapi hiyo kesi haipo?
 
Binadamu tunatofautiana kifikra na kimtazamo!

Ujanja ujanja na usanii umelipa tiketi ya kwenda bungeni!
Unaonyesha una chui binafsi zakimwandiga,kubenea ndiye mbuge utake husitake
 

Attachments

  • 1453347015994.jpg
    1453347015994.jpg
    34.8 KB · Views: 32
Hakuna ambaye amesema kubenea siyo Mbunge mwandishi ameelezea kesi inayomkabili na endapo atapatikana na hatia adhabu yake itakuwaje? Sasa hayo majungu yanatoka wapi hiyo kesi haipo?
Hizo ni ndoto za alinacha
 
Hakuna ambaye amesema kubenea siyo Mbunge mwandishi ameelezea kesi inayomkabili na endapo atapatikana na hatia adhabu yake itakuwaje? Sasa hayo majungu yanatoka wapi hiyo kesi haipo?
Mtakesha mkiwanga lkn kubenea ni mbunge n ataenelea kuwa mbunge
 
Kuna swali limeiulizwa la msingi kabisa kwa mtoa maada, kwamba sheria ulizozisema mbona hakuna inayomnyang'anya mbunge ubunge wake.
Akipatikana na kosa kifungo kisichozidi miezi 6 na Ili akose sifa ya kuwa mbunge ahukumiwe na kufungwa kifungo cha zaidi ya miezi 6.
Tueleweshe vizuri la sivyo point yako ni ya kishabiki.
 
"kibaka, mpumbavu, mjinga na cheo alichonacho ni cha kupewa"...
Hapa Kubenea (kama kweli alisema) atakua amekosea hapo tu kwenye kibaka lakini mengine yote ni sawa kabisaaa.

Mkuu kwani umesahahu Bunge la katiba na wizi wa simu? Huyu dogo alihusishwa direct na aliyeibiwa..so Kb hajakosea kumuita hivyo.
 
Mbona hamuongelei gharama za uchaguzi mnaotaka urudiwe Zanzibar? Wakae bila mbunge hadi 2020 maana inaelekea Makonda anatosha kufanya kazi za mbunge.
Mambo ya Zanzibar wanayafahamu vizuri Wazanzibari!

Zanzibar ni nchi yenye mipaka yake, Rais wake, Bunge lake na mahakama zake.

Matatizo ya Zanzibar yanatatuliwa kizanzibari!
 
Mh, nawe umejiridhisha na "post" yako hiyo! Yupi mbunge wa kuaminika huyo mwongo/mchonganishi/mfitini, sifa alizo nazo Kubenea! Wana Ubungo mmeingizwa mjini kwani ahadi za Mbunge wenu zimejaa laghai lukuki. Kimbelembele tu kitamweka pabaya.

TAFAKARI CHUKUA HATUA

Kumbe unafanya unajimu!!!! Basi sawa, Time will tell!
 
Mambo ya Zanzibar wanayafahamu vizuri Wazanzibari!

Zanzibar ni nchi yenye mipaka yake, Rais wake, Bunge lake na mahakama zake.

Matatizo ya Zanzibar yanatatuliwa kizanzibari!
Mwaka huu kitaeleweka tu. Miaka yote mnang'ang'ania muungano, ila mwaka huu kwa sababu ya uchaguzi mpo tayari kusema Zanzibar wako kivyao. Mpo tayari kuitenga Zanzibar na Tanganyika
 
Kwenye post ya mtoa mada naomba kuelrweshawa yafuatayo..
1. Hukumu inasema kikizidi kifungo cha miezi 6. lakini adhabu ya Kubenea endapo atapatikana na kosa inasema kifungo kisichozidi miezi sita... UFAFANUZI TAFADHARI KWA ANAYEJUWA ataachishwaje ubunge kwa kofingu hicho
2. Adhabu inatamka mtu hatateuliwa au kuchaguliwa kugombea ubunge kama keshafungwa. Sasa kubenea yeye ni mbunge tayari na sijaona panaposema akishakuwa mbunge halafu akafungungwa nini kinatokea
 
Back
Top Bottom