Mbinu za kupata mke au mume

Mbinu za kupata mke au mume

Kwa sasa inahitajika mbinu nyingi ili kupata mke au mume.Mkibaki kusubiri kuchumbiwa au kuchumbia,mtazeeka bika kuoa au kuolewa.Sasa jaribuni mbinu hizi:
1.Msikae ndani wiki nzima,toka nje,kama kuna matamasha nenda,mikutano mbalimbali nenda,kila aina ya mikusanyiko unayoweza kwenda basi wewe nenda
2.mikutano au vikao vya kidini,nenda bila kukosa labda kama umesafiri au unaimwa.Kwenye hivyo vikao jitahidi kuongea usikae kimya
3.Kusali ni muhimu sana,kwa hiyo dini yako.Viongozi wako wa kidini wafanye kuwa marafiki na uwe muumini mzuri,mwenye nidhamu kubwa maana huwa wanaombwa sana kuwatafutia wenza
4.Kwa kuzingatia bajeti yako toka kwenye pub mwisho wa wiki hata kama hunywi bia,nenda kanywe juice,kula nyama,ongea na watu,kubadilishana mawazo
5.Kuvaa vizuri,kila siku vaa vizuri bila kujali kama ni nguo za gharama,vaa kwa mpangilio na ni muhimu sana kuvaa viatu vizuri kila siku.
6.Dating sites jiandikishe na kujaribu bahati yako pia huko,hapa pia zingatia bajeti yako maana zingine ni za kulipia
7.Usiogope kuongea na marafiki zako kuulizia kama kuna mtu anatafuta mke au mume,na ukiwajua nenda kaongea nao kuonesha utayarifu wako kuoa au kuolewa
8.Tengeneza vigezo vyako vya mume au mke unayemtaka,ili iwe rahisi kuchagua
9.Shiriki mazishi kadri unavyopata nafasi na uwe umevaa kiheshima
10.Shiriki jogging mbalimbali ambazo hutangazwa na huko jichanganye na watu wa kila aina
11.Chagua timu ya mpira moja uishabikie na uwe unaenda viwanjani na uwe umevaa vizuri
12.Siku zote uwe msafi kwa mwili na nguo,usinuke mdomo,kikwapa na jasho kwani hiyo itakunyima mke au mme
13.Chunguza uwajue ni wanawake wepi au wanaume ambao hawajaoa au kuolewa,ukiwajua fanya urafiki nao mpaka umpate mmoja ambae unaweza kuongea nae
14.Jitahidi sana kutotembea na wanawake hovyohovyo au wanaume hovyohovyo,usimvulie kila mtu auone uchi wako
15.Jifunze sex vizuri,uwe na stamina,na mbinu nyingi za kujamiiana,ili unapopata mpenzi umpe manjonjo ya hatari
16.Fanya urafiki hapo mtaani unapokaa na wazazi ambao wana watoto wa kike na kiume ambao hawajaoa au kuolewa ili uwaambie upo tayari kuoa au kuolewa
17.Jitahidi sana kuongea kwa hadhari kila unapopata fursa kuongea
18.Sali kila siku kuomba Mola wako akupe mme au mke
19.Usisite kuja inbox kupata usaidizi uoe au uolewe na ni bure
Msikae ndani kusubiri,tokeni
20.Kwa wanawake jitahidi sana usizae nje ya ndoa
Kwa sasa na orodha ya wanaume 20 na wanawake 32 ambao wanatafuta wachumba,na kati ya hao kuna wanaume 12 na wanawake 17 wapo kwenye hatua kadhaa za mazungumzo ili kufikia uanuzi wa kuoana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Apo apo umesema tusali sana apo apo umesema tujifunze sex vizuri ukaongezea na mbinu za kujamiana... aisee
 
Tunaofelishwa na ponti namba 1 tukutane PM kwa kikao cha dharura
 
Kwa sasa inahitajika mbinu nyingi ili kupata mke au mume.Mkibaki kusubiri kuchumbiwa au kuchumbia,mtazeeka bika kuoa au kuolewa.Sasa jaribuni mbinu hizi:
1.Msikae ndani wiki nzima,toka nje,kama kuna matamasha nenda,mikutano mbalimbali nenda,kila aina ya mikusanyiko unayoweza kwenda basi wewe nenda
2.mikutano au vikao vya kidini,nenda bila kukosa labda kama umesafiri au unaimwa.Kwenye hivyo vikao jitahidi kuongea usikae kimya
3.Kusali ni muhimu sana,kwa hiyo dini yako.Viongozi wako wa kidini wafanye kuwa marafiki na uwe muumini mzuri,mwenye nidhamu kubwa maana huwa wanaombwa sana kuwatafutia wenza
4.Kwa kuzingatia bajeti yako toka kwenye pub mwisho wa wiki hata kama hunywi bia,nenda kanywe juice,kula nyama,ongea na watu,kubadilishana mawazo
5.Kuvaa vizuri,kila siku vaa vizuri bila kujali kama ni nguo za gharama,vaa kwa mpangilio na ni muhimu sana kuvaa viatu vizuri kila siku.
6.Dating sites jiandikishe na kujaribu bahati yako pia huko,hapa pia zingatia bajeti yako maana zingine ni za kulipia
7.Usiogope kuongea na marafiki zako kuulizia kama kuna mtu anatafuta mke au mume,na ukiwajua nenda kaongea nao kuonesha utayarifu wako kuoa au kuolewa
8.Tengeneza vigezo vyako vya mume au mke unayemtaka,ili iwe rahisi kuchagua
9.Shiriki mazishi kadri unavyopata nafasi na uwe umevaa kiheshima
10.Shiriki jogging mbalimbali ambazo hutangazwa na huko jichanganye na watu wa kila aina
11.Chagua timu ya mpira moja uishabikie na uwe unaenda viwanjani na uwe umevaa vizuri
12.Siku zote uwe msafi kwa mwili na nguo,usinuke mdomo,kikwapa na jasho kwani hiyo itakunyima mke au mme
13.Chunguza uwajue ni wanawake wepi au wanaume ambao hawajaoa au kuolewa,ukiwajua fanya urafiki nao mpaka umpate mmoja ambae unaweza kuongea nae
14.Jitahidi sana kutotembea na wanawake hovyohovyo au wanaume hovyohovyo,usimvulie kila mtu auone uchi wako
15.Jifunze sex vizuri,uwe na stamina,na mbinu nyingi za kujamiiana,ili unapopata mpenzi umpe manjonjo ya hatari
16.Fanya urafiki hapo mtaani unapokaa na wazazi ambao wana watoto wa kike na kiume ambao hawajaoa au kuolewa ili uwaambie upo tayari kuoa au kuolewa
17.Jitahidi sana kuongea kwa hadhari kila unapopata fursa kuongea
18.Sali kila siku kuomba Mola wako akupe mme au mke
19.Usisite kuja inbox kupata usaidizi uoe au uolewe na ni bure
Msikae ndani kusubiri,tokeni
20.Kwa wanawake jitahidi sana usizae nje ya ndoa

Uwe na fedha za uhakika au uwe tajiri, mbona wanawake utapata kila aina utakavyo.
 
Daah ndo nipo kwenye msoto huu, na nina hofu juu dada zetu maana wao wanawaza pesa tu ,kuumpata aliye tayali kwaajiri ya kujenga familiar ni mtihani kweli ,eeh MUNGU niongozee mja wako
 
Ningelikuja inbox kupata ushauri, lakini nilivyoangalia hiyo "avatar" yako nikajua naongea na shetani! Shetani anataka akukutanishe na maajenti wake kwa njia ya ndoa ili akupige!
noted
 
Mbona me naona wapo kibao na wanalilia kuolewa, Au useme kwa upande wa Wanawake wao wanasemaje?
nikwambie wanaume na wanawake ni wengi lakini,kupata mchumba unayemtaka ni shida
 
Watu weusi sisi tunawaza ushenzi muda mwingi mtu ambae yuko desperate na ndoa kuoa au kuolewa hasa wanawake mimi namuona kama mpumbavu hivi.

Tunashindwa kuwa desperate kuhusu hali zetu za maisha na taifa letu lilivyo tunawaza vitu vya kijinga tu ndio vinatuendesha.

Mtu anaona kama akikosa ndoa ni kama kanyimwa hewa anataka kufa huyu mtu hana tofauti na teja akikosa madawa ya kulevya.
una hakika kuwa ndoa ni ujinga?
 
With all due respect kuna namna tunakwama sana hii race yetu.

Nitakutolea mfano, miaka miwili nyuma nilikuwa kwenye mahusiano na mdada mmoja wa kijerumani, alikuwa ni doctor na ana miaka miwili tu toka amepata kazi.

Kuna wakati tulikuwa tunazungumza future yetu yule dada aliweka very clear kuwa hayupo tayari kuingia kwenye ndoa within five yrs kutoka pale sababu kubwa anahitaji time kudevelop carrier yake na maisha yake kwa ujumla (personal life) na ikitokea akafunga ndoa baada ya muda ule anahitaji kuenjoy maisha ya ndoa atleast miaka mitatu kabla hajafikiria kubeba ujauzito wa kwanza na by that time alikuwa na miaka 32 mi nikipiga hesabu zake hapo si chini ya miaka 8 hiyo mipango yake mpaka aje kunizalia nikaona mambo yasiwe mengi nikapita vilee.

Kiufupi wenzetu wanaplan na kuweka vipaumbele sana mipango ya maisha yao na ndoa mara nyingi inakuja baadae wakati kashaweka mambo yake sawa, sasa sisi wabongo hasa watoto wa kike kwanza ndoa wamechukulia kama kitega uchumi ama tool ya kutatua shida zao za kiuchumi ndio maana wengi wapo desperately, na expectations kibao.
kumbuka ndugu tunatofautiana kiutamaduni,umeongelea mjerumani hapo,kwa taarifa yako mimi ni mjerumani kwa baba na mama ni mnyamwezi,japo wazazi wangu ni marehemu,nimeishi ujerumani miaka zaidi ya 30 na kwa sasa nipo tanzania,najua somo la ndoa vizuri mno,na nina miaka 10 nasaidia kuwasogeza wanawake na wanaume kwenye ndoa,bila malipo
 
Back
Top Bottom