Mbinu za kuboresha ndoa na afya yako.

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Ukizingatia kwamba, kuwa na ndoa imara ni kitu muhimu sana ili kuwa na afya na furaha, italeta mantiki kuelekeza nguvu zenu katika kuifanya ndoa yenu kuwa bora zaidi. Hapa chini kuna vidokezo kwa ajili ya kuifanya ndoa yako kuwa na afya zaidi:

Kwanza lea ndoa yako. Unajua mambo ayapendayo na asiyoyapenda, ndoto, hofu, wasiwasi, na matumaini ya mwenzi wako? Unajua kwa mapana ni nini mwenzi wako alifanya siku nzima ya jana? Unajua aina zipi za shinikizo mwenzi wako anazipata mahali pake pa kazi? Msingi wa ndoa nzuri ni urafiki imara.

Kama ndoa haijajengwa juu ya urafiki imara, itakuwa shida kuishi kwa pamoja kwa muda mrefu. Hakikisha unapata muda kila siku kukaa na mwenzi wako kwa siri ili kumjulia hali na matatizo aliyokabiliana nayo .

Katika vipindi hivi, weka kipaumbele kusikiliza na kujifunza kuhusu fikra, mawazo na hisia za mwenzi wako .

Pili kwa nguvu zote na kwa makusudi, chukua hatua kuboresha mapenzi kwa mwenzi wako. Gottman anasema, hiki ndicho kizuizi kikubwa cha dharau. Kumbuka mambo mazuri ya mpenzi wako.

Ulimpendea nini hadi ukaoana naye? Ni kitu gani kabla hujamuo kilikuvutia kwake kimaumbile? Kwa kurejesha mapenzi kwa mwenzio utakuwa umeboresha mwenendo bora.

Tatu, daima mheshimu mwenzi wako. Katika uhusiano ambao unaporomoka, heshima kamwe haipatikani.

Cha kusikitisha zaidi, wakati mwingine watu wanaishia kuwatendea wenzi wao vibaya zaidi kuliko ambavyo wangewatendea watu wasiowafahamu. Unamgombeza mkeo au mumeo mbele ya rafiki zako au familia?

Nne, mkubali mwenzi wako. Kumbuka kwamba kila mmoja wenu anahitaji kujisikia anakubalika kama binadamu.

Badala ya kumshambulia mkeo au mumeo, jaribu kusikiliza mawazo yake. Ni rahisi kutilia mkazo makosa ya mwenzio na kwa kufanya hivyo tunasahau mema anayofanya.

Tano, sameheaneni, mwenzio anapokuomba msamaha kwa dhati, usimkimbie au usiompe kisogo, wakati mwingine migogoro haikwepeki.

Majaribio ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika uhusiano yanapopuuzwa, uhusiano unaathirika.
Usifunge milango moja kwa moja kwa mkeo au mumeo anapojaribu kujirekebisha.

Sita, tulia. Unapokuwa umeudhiwa, pumua kwa nguvu. Watu wengi wanahitaji kama dakika 20 kutuliza miili yao baada ya kuudhiwa. Baada ya kutulia chukua nafasi yako, anza upya kulishughulikia tatizo lililo mbele yako, wakati umetulia na utakuwa tayari kumsikiliza mkeo au mumeo vizuri.

Saba, chukulia mambo kirahisi. Ijapokuwa mkeo au mumeo anaweza kufanya mambo ambayo yatakuudhi, kumbuka unaweza kukabiliana nayo.

Si busara kupambana na mkeo au mumeo katika mambo madogomadogo.

Nane, jitazameni upya na kujirekebisha. Uhusiano ni kama dansi. Wewe na mkeo lazima msonge mbele sambamba. Kumbuka kwamba uwe ni mwanamke au mwanaume una udhibiti kwa asilimia 50 wa mambo yote yanayotokea katika uhusiano wenu. Ndio maana wanasema, ndoa ikifa wote mmechangia.

Ni mara chache kupindukia, ambapo mmoja kati ya wanandoa ndiye mwenye mchango.
 
okay, okay okay imekaa njema hii na itasaidia ku re new mahusiano!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom